Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mag3, Mtu kama wewe ni wakupuuzwa tu unasema mwaka 1961 ulikuwa unasoma hukuwai kuwasikia hawa wazee wa Kariakoo Mohamed Said ni muongo hawa wazee hawakuwepo umekuja kuwasikia kwa Mohamed Said wewe si ndiyo muongo waheed.
Ritz soma tena post yangu unayoinukuu... hivi wengine mkoje? Post yenyewe iko humu na haijafanyiwa editing bado tu unataka kudanganya kuhusu niliyoandika, duh! Mimi nimeingia Dar es Salaam kwenye miaka ya sitini ndio nikaanza kuwasikia hao wazee wake Mohamed Said wakati huo kenyewe bado katoto kadogo tu kanasimuliwa hadithi mabarazani.

Ritz, acha kushabikia mambo usiyoyajua...je unajua kuwa hao wazee wake unaowapigia debe nao kuna wakati waliitwa wakuja? Ngoja nikupe somo kidogo;
 

Actually anachobandika hapa Mohamed si maneno ya Sivalon. Anachobandika ni tafsiri yake kuhusu kile alichokisema Sivalon. Hawawezi kuweka maneno ya Sivalon au Bergen verbatim. Kuna bango alibandika hapa Ritz akituhadaa kuwa ni kauli za van Bergen lakini nina hakika ni kauli za Mohamed akielezea tafsiri yake ya kile alichokisema Bergen. Mohamed amekiri kuwa anayo maandishi ya Bergen lakini hawezi kuyaweka hapa kwa sababu yataharibu muktadha wa kile anachotaka watu waamini.
 
Sasa kwa nini wewe hufanyi mahojiano na hao wengine ukaandika.
Nimuhoji Nyerere ili aseme nini?

Nini ambacho sikuwa nakijua kuhusu harakati za kuunda TANU hadi
nende kwa Nyerere?

Mohamed,
This seems to be the crux of your problem. Hukuweza kumhoji Nyerere kwa sababu hukutaka kwa kuamini kwamba unajua kila kitu kuhusu yeye. Umetoa shutuma lukuki juu yake, kuanzia hotuba aliyoandikiwa na Sykes kusoma UNO, kununuliwa chakula na wazee wa Kariakoo, etc. etc. Haikuwa issue ya Nyerere aseme nini, lakini kwa sababu ulishajivika joho la utafiti it was imperative that you get a word from someone you turned into a subject of your ridicule. By not doing that reveals that you had an agenda which was not based on seeking the truth, because you believed you already have the truth, but now your agenda was to propagate that truth you believe you know, no matter how erroneous. Mbona ulienda kwa family ya Sykes? Mbona uliwatafuta mpaka wazee wa Tanga? And Nyerere was just around the corner?
 
Huo Ustaarabu umeutoa wapi? na ktk utamaduni upi wa Mtanzania, au uislaam maana hata Mwenyezi Mungu kazungumzia haya, mtume (SAW) kawazungumzia haya unayoyakataa sasa unachotaka kusema wewe mwenye maadili ni kipi haswa?...Hii akili ya kuogopa kuzungumza na wanawake kwa sababu ni wanawake inaonyesha wazi wewe aidha unawaweka chini kama sii sawa na wanaume ktk kufikiri na kujenga hioja, hivyo binafsi yangu nampongeza sana Bibie kuwepo nasi hapa kijiweni na tunaelimishana wala sii kubishana - Ni ktk kukubali kutokubaliana kwa msingi mmoja tu - Hoja hujibiwa!
 

Jasusi,

Hakika sikuwa na haja na Nyerere.

Na kweli nilikuwa na agenda na agenda yangu ilikuwa kukijibu
kitabu cha Kivukoni College.

Na kweli nilikuwa na uhakika wakati naandika kitabu.

Yote ulosema ni sawa kabisa.

Mimi sikwenda kwa famili ya Sykes mimi nakua namuona Bwana Abdu.
Nakua namuona Bwana Ally Kipata pale sikwenda kokote.

Sasa ni zamu yenu na nyie kuandika huo ukweli ambao manona
mimi nimeuacha.

Hebu kisome tena kitabu changu kuhusu hotuba ya UNO.

Hotuba ya UNO chanzo chake ni TAA Political SubCommittee ya 1950
walipotoa mapendekezo ya katiba kwa Gavana Twinning.

Document hii nimeeleza kuwa imepotea haipo kokote si CCM Library wala
Nyaraka za Taifa.

Pole sana ndugu yangu naona hii hotuba imekuchoma sana.

Lakini ukweli utabaki kuwa ilipoundwa TAA Political Subcommittee Nyerere
alikuwa hayupo na inawezekana ndiyo maana hata kitabu cha Kivukoni
hawakuwa na habari na huo waraka.

Laiti kama nisingeutaja hapa JF wengi wasingeujua.
 


Jasusi,

Kama iko chuki basi si mie chanzo chake.

Chuki hii chanzo chake ni dhulma na wala
si kwa Wakristo bali kwa wale madhalim awe
Muislam awe Mkristo.

Soma kitabu changu utakutananao humo.
 

Wewe kumbe Dar es Salaam umekuja mie Dar es Salaam ndio kwetu nimezaliwa unaponiambia niache ushabiki kwa mambo nisiyoyajua nakushangaa unataka niongolee habari za wapi Kilimanjaro au Mbeya.

Tatizo lako mtu mzima halafu muongo.

Unanipa somo gani hizo ngano za wazungu kwako ndiyo somo.
 

Mag3,

Sisi tukisomeshwa Qur'an barazani achilia kuhadithiwa
historia barazani na wazee wetu.

Hayo uloweka ni maandiko ya Wazungu nayajua sana.
Umekuja 1960!

Mimi wazee wangu wako hapo takriban miaka 100.
 
Nguruvi..huyu bwana kwa kujigfananisha na Irving Wallace amesema mengi kuhusu uandishi wake...

MM,

Ndiyo maana kama ukisoma ile post utaona nimeanza mbali
toka kwa Mark Twain hadi kwa Irving Wallace.

Nimekuchagulia hao wawili tu kwa makusudi.
Nilitaka msomaji ajuaye mambo haya asome katikati ya mistari.
 

J,

Ukisoma historia ya uhuru wa Tanganyika utajua chanzo cha
tatizo la udini.
 
I trust you as a story teller of our times, unfortunate we will never let you ruin another generation. History isn't synonymous to ngano hence not every story teller is a historian.

N,

Merry go round!
 

Mag3,

Kitabu kiko sasa miaka 15.
 
J,

Ukisoma historia ya uhuru wa Tanganyika utajua chanzo cha
tatizo la udini.

kikundi cha wazee wachache wa Dar-es-Salaam ambao waliamua kuanzisha fitna ya kidini dhidi ya Baba wa Taifa mtu ambaye hakuwa amewatendea lolote baya. Wazee hawa walipitisha hisia hizi za udini dhidi ya Nyerere kabla ya Uhuru na baada ya uhuru kwa watoto wao ambao leo wameamua kuandika historia mpya ya Tanganyika kwa msingi wa kidini - kama wazee wao. Lakini kundi kubwa la wapigania uhuru walikataa hili na watoto wao wanaendelea kuukataa udini na hivyo kambi mbili zimesimikwa rasmi.
 
Mohamed Said,

Hebu tuwekee orodha ya Masheikh waliokamatwa na Nyerere wengine wakafungwa wengine wakawekwa kizuizini.
 



Anytime you find someone more successful than you are like Mohamed Said, especially when you're both engaged in the same business -(literature) you know they're doing something that you aren't

Wewe pia si naskia ni mwandishi???
Andika cha kwako basi uitangazie dunia kile unachokifaham na kile chenye ukweli na uhalisia..
 
Na zaidi kumwekea Nyerere maneno kama yale ya hotuba ya kuaga ambayo Mohamed anasema Nyerere alitamka kuwa hamjui Abdul Sykes. Alipotakiwa kuweka ushahidi Mohamed kageuza kibao kutaka ushahidi wa video hata wa maandishi hautaki. Nilidhani akiwa mtafiti hapa ndipo alipotakiwa kuthibitisha lakini ameshindwa! failure.

Ameshindwa kama alivyoshindwa katika madai ya namba za mitihani. Na hapa pia kamwekea Kighoma Malima maneno ya kutosha tu wakati hana ushahidi wa maneno hayo.

Anasema Mapinduzi ya ZNZ yaliletwa na Nyerere, hajawahi kwenda kumhoji Naosr Moyo, Jumbe au Mwinyi.
Tunachosubiri ni maajaliwa ya manani toleo la nne laitakuwa na maneno ya wazee hao wakiwa hawawezi kujitetea.
 
vipi hapo kwenye rangi? mafuta yameisha? maana lugha ya mfumo kristo (lugha ya malkia) haitaki ubabaishaji.
 
Mimi nakupongeza kwa hilo na ni dalili ya kuwa umejiamini unazungumza ukweli.Allah subhaanahu wa taala azidi kukuthibitisha kwa hilo na akulipe ujira uliio mkubwa.
Kwenye mustwalahul hadithi (sayansi ya uchambuzi wa hadithi za Mtume S.A.W) wapokezi wakiwa majhuli (wasiofahamika) inakuwa sababu ya hadithi zao kutiliwa shaka na kutupwa.Wewe bila kujua itakuwa umefuata njia hii.
Usikatishwa tamaa na watu kama Mzee Mwanakijiji.Ukweli wanaujua lakini wamekusudia kuupindisha.Mohammed elewa kuwa kuibuka kwa ukweli ukaficha uongo ni ahadi ya Allah subhaanahu wa taala .Hivyo hata wakijipinda kiasi gani hawatoweza kufuta ahadi hiyo.Huwa inatokea kila zama na kila eneo mpaka ukweli uwe juu ya uongo na haki juu ya baattil.
 

Ami,

Ahsante sana ndugu yangu.

Ngoja nikuongezee.

Abdu Sykes alikuwa na sahib wake Ahmed Rashad Ali.
Huyu ni ndugu yake Prince Sudi kwa mama mmoja.

Babu yake Ahmed Rashad alipata kuwa waziri katika serikali ya Sultan katika 1800s.

Nimemueleza Mzee Rashad katika kitabu changu tafasiri ya Kiswahili.

Rashad Ali na Abdu na Abdu Sykes wamejuana 1939 paleArab Association na nyumba
hii ipo na nembo yake hadi leo.

Ukiwa Dar iangalie Mtaa wa Jamuhuri na Chagga iko kwenye kona.

Ahmed Rashad wakati wa kudai uhuru alikuwa mtangazaji maarufu Radio Free Afrika
Cairo.

Rashad alikuwa akimwambia Abdu kwa nini Nyerere anasema yeye ndiye aliyeasisi
TANU ilhali sote tunajua TANU is your baby na we uko kimya.

Abdu alikuwa akijibu kumwambia Rashad ikiwa Nyerere anataka kuchukua credit ya
kuunda TANU mwacheni.

Na Abdu mpaka anaingia kaburini hakusikika hata akisema kuwa juhudi zakupata umoja
wa Waafrika zilianzwa na baba yake Kleist 1929 na yeye akaziendeleza hadi kuunda TANU
1954.

Mwaka 1950 Abdu alipokwenda kukutana na uongozi wa KAU Nairobi ukiongozwa na Jomo
Kenyatta Rashad alikuwapo.

Nina mengi sana ndugu yangu.
Namshukuru Allah kwa kunijalia hidaya hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…