Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Wewe Mzee unataka kutudanganya kweupe!.Huu mjadala umekuwa mrefu kutokana na wewe kurudia maswali na Mohammed kujaribu kujibu kila kitu na kukitolea ufafanuzi.Bado wewe unarudia suala hilo hilo kuwa anakwepa kujibu.
Ungekuwa unabishana na mimi
 

Mohamed Said,

Kuna watu wamekuja Dar es Salaam miaka ya 1960 haya mambo watayajua wapi.

Ukimueleza habari za marafiki zake Abdulwahid Sykes kina Kitwana Lunga, Said Ali Maswanya, Ally Said, watakuambia ngano.
 
Wewe Mzee unataka kutudanganya kweupe!.Huu mjadala umekuwa mrefu kutokana na wewe kurudia maswali na Mohammed kujaribu kujibu kila kitu na kukitolea ufafanuzi.Bado wewe unarudia suala hilo hilo kuwa anakwepa kujibu.
Ungekuwa unabishana na mimi

Huyo mzee sisi tushamuwia radhi na kumpuuza tokea mda mrefu sana..

Mbaya zaidi ana kuja kwa style ya mbuni ya kuficha kichwa huku mwili wake wote kauacha wazi,saiz tunachofanya ni kuendelea kumpuuza tuh..
 
Wewe Mzee unataka kutudanganya kweupe!.Huu mjadala umekuwa mrefu kutokana na wewe kurudia maswali na Mohammed kujaribu kujibu kila kitu na kukitolea ufafanuzi.Bado wewe unarudia suala hilo hilo kuwa anakwepa kujibu.
Ungekuwa unabishana na mimi
aisee nimeamini ujinga ni utumwa.
 
Waislam wa nchi hii nendeni shule acheni kulalama,hamuwezi kupewa nyadhifa mnazozitaka kama mtaendelea kuishia darasa la pili C,somesheni watoto wenu katika shule sahihi ambazo zina walimu waukweli ili baadae waje kuuokoa uislam kwa hoja za msingi wasije wakaja kuwa kama nyie
 

Umepotea njia..
 

Nguruvi,

Mimi siye niliyshindwa kuhusu hotuba ya muago ya Nyerere.
Ndani ya kitabu changu hilo la yeye kusahau cheo cha Abdu
nimelisema.

Na usidhani nyie ndiyo wa kwanza kushangazwa na hilo.
Sasa leteni video tuisikize na ilikubalika lakini hadi leo haijaletwa.

Vipi utanilaumu mimi?
Leteni hiyo video tuisikize mnikamate uongo.

Namba za mitihani sijashindwa.
Wakujibu si nyie ni Wizara ya Elimu.

Sasa tuje kwa Aboud Jumbe.

Mimi nilikuwa mhariri wa kitabu chake Partnership.
Inakutosha au nikuongezee?

Tuje kwa Hassan Nassor Moyo.
Alikuwa jirani yangu kwa miaka 15.

Inatosha au nikuongezee?
 

Umepanda daladala ya Temeke wakati wewe unaeleka Boko.
 

Nguruvi,

Mimi siye niliyshindwa kuhusu hotuba ya muago ya Nyerere.
Ndani ya kitabu changu hilo la yeye kusahau cheo cha Abdu
nimelisema.

Na usidhani nyie ndiyo wa kwanza kushangazwa na hilo.
Sasa leteni video tuisikize na ilikubalika lakini hadi leo haijaletwa.

Vipi utanilaumu mimi?
Leteni hiyo video tuisikize mnikamate uongo.

Namba za mitihani sijashindwa.
Wakujibu si nyie ni Wizara ya Elimu.

Sasa tuje kwa Aboud Jumbe.

Mimi nilikuwa mhariri wa kitabu chake Partnership.
Inakutosha au nikuongezee?

Tuje kwa Hassan Nassor Moyo.
Alikuwa jirani yangu kwa miaka 15.

Inatosha au nikuongezee?

Unasema kuhusu mapinduzi ya Zanzibar...

Mimi nimemuhoji Kamanda wa Majeshi ya Wamakonde Mohamed
Omar Mkwawa.

Soma ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru'' cha Dk Harith Ghassany.
Ipo na picha yangu nimeshika video camera pwani ya Kipumbwi.

Iko picha ya Mzee Omar Mkwawa pia.

Unadhani mambo yale yalikuwa ya akina Moyo na Karume?

Mpate Mzee Aboud Mmasai, Jimmy Ringo mratibu toka TANU Office
Tanga.

Mpate Mzee Baramia.

Mpate Jumanne Abdallah aliyekuwa akitoa ulinzi kwa vijana wa Kimakonde
katika pori la Sakura.

Mpate Kassim Hanga na Oscar Kambona.

We unadhani utakaa hapo la laptop yako upambane na mimi katika haya.
Unataka nikuwekee mimi nilimjua vipi Hanga?

Akija mtaani kwetu nyumbani kwa Mama Abdu Mgunya kucheza bao.

Na siku alipoletwa Mnazi Mmoja kuadhiriwa na Nyerere kwenye mkutano
wa hadhara mimi na wenzangu tupo pale tunalaani maana kiwanja chetu
cha mpira kimetekwa hatuwezi kucheza.

Halafu wale walokuwa pale nawaju kwa majina.

Yule Mzee Omari Londo.
Yule Hamza Aziz nk. nk.

Na wao wananijua mtoto wa Said Salum mjukuu wa Baba Popo.
Soma kwanza ndiyo ujishauri kama una afya ya kuvaana na mimi.

Mimi sijaparamia historia hii ni historia ya mji wangu ya wazee wangu.
Naijua ndani nje.
 
shikamoo Mohamed Said
niliwaambia huyu 'mume' ni mkubwa
huyu anayoyasema ameyafanyia utafiti
hakukurupuka kama kina Yericko na wenzake
Kuendelea kupaki ndani ya huu uzi ni kujidhalilisha
hamna jipya zaidi ya kubwabwaja
Nimepatwa na uvivu hata kuendelea kuchangia
kama nilivyokuwa nafanya mwanzo
baada ya kuona hakuna jipya
kwa kina yericko na wenzake
hongera Mohamed Said umefanya jambo
ambalo athari yake itadumu milele
 
Last edited by a moderator:

shabash!!!! wewe mzee unatisha. Marshallah
 
Kwabahati mbaya unafurahia masimulizi ya kuremba bila kuzama kitafakuri, ni vigumu kutambua ukweli ulipo
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mohamed,Leo saa tatu na robo usiku ipo documentary moja nzuri ITV inayomhusu Mwalimu. Usiikose. Pole pia kwa radio yako kufungiwa miezi sita.

Hiyo Documentary imejikita wapi wakati yupo TAA, TANU, CCM au baada ya kustaafu.
 
shabash!!!! wewe mzee unatisha. Marshallah

Mfumo,

Unajua wazee wetu walikuwa na matumaini makubwa sana na Nyerere.
Nyerere alipendeka mno wala hapana mfanowe.

Wazee waliweka kila kitu pembeni wakashughulika na umoja wa Watanganyika.
Walikuja kusikitishwa na yale yalokuja kutokea baada ya uhuru mwaka 1961.

Nyerere akavunja Baraza la Wazee wa TANU 1963 mwenyekiti akiwa Mzee Idd Tulio
Kafa Iddi Tulio TANU haina habari.

Kazikwa na ndugu zake Waislam.

Idd Tulio alihiudhuria mkutano wa kwanza wa TANU pale Arnautoglo na mkutano wa
Tabora wa Kura Tatu.

Ana mengi.

1964 ikafuatia wazee kutupwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Mwaka 1968 taasisi yao kipenzi EAMWS iliyokuwa ikiwaletea maendeleo Waislam Nyerere
akaivunja.

Wazee hawa wameingia kaburini na kinyongo kikubwa dhidi ya Nyerere.
Leo ukimtaja Nyerere katika msikiti kibwagizo kinachofuatia ni ''laana ya Allah iwe juu yake.''

Tumefika vipi hapa?

Mimi nasema haya ili wahusika wajue ukweli ya hali huku mitaani.
Ikiwezekana turekebishe haya mambo.

Tumefikafika vipi katika hali hii?
Mimi siko hapa kujistarehesha au kuingia ubishi na watu.

Naeleza historia ya wazee wangu ili wale wasioijua wawajue na nini ulikuwa mchango
wao katika kuitafuta amani ya kweli.

Tusijidanganye hali si shwari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…