Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Hayo ndio makosa makubwa yaliyo kwenye kitabu cha Mohamed Said anayoyatetea kwa nguvu huku akikwepa baadhi ya hoja nzito!

Kimantiki Mohamed amewalisha maneno Nyerere na Sykes

Amewaamulia yeye, lakini ukikisoma kitabu chake chote mpaka ganda lake hakuna aliponukuu mahojiano ya Nyerere au Sykes! Zaidi imewekwa hisia au lengo la Mohamed Said tu.

Hii ndio hatari inayotukumba watanzania!

Nilieleza katika moja ya post zangu hapo juu kuwa ili ufahmu historia ya AA,TAA na TANU nilazima utulie sana na uangaze kuanzia ideology yao,

Kwa wazee wetu hawa wanaukombozi wa Tanganyika, ideology yao ileile ya AA iilitoka ikibadilika kibaiolojia hadi TANU na uhuru kamili ndani ya mapito yao kulikuwa na mageuzi mengi sana, kwanza kutoka uanaharakati na kuingia uanasiasa. Hapa ndipo palipo anza kuzaliwa makundi ya kisiasa kama ilivyo kwenye siasa za leo, na moja ya uchaguzi mgumu ni ule wa kura tatu wa 1953 uliomwingiza Mzee Nyerere kuwa rais wa TAA na kumbwaga mpinzani wake kisiasa Mzee Sykes!

Sasa Mohamed Said huenda anatumia makovu hayo ya kisiasa kufarakanisha watu,

Asilo lizingatia Mohamed ni kuwa wahusika hawakutoa neno lolote juu yao mpaka wanaingia kaburini zaidi ya hisia za mashabiki wao tu ambazo leo yeye Mohamed Said anatumia kupotoshea watu kwa minajri yake.

Nimeeleza kidogo kuwa moja ya makosa katika *ngano* za Mohamed Said ni kuakisi kuanzia miaka ya 1950,

Sasa kwamwanahistoria usie makini unaeziangaza harakati za ukombozi kwa miaka hiyo ya 1950 nilazima utaibuka na dhana yako sio ya historia husika,
 

Kaka! kweli umekisoma kitabu chote cha Mohamed Said.
 
hapana yericko,hapo unakosea moja wa moja baina ya hao watu wawili,ndugu julius na ndugu sykes,,

nikuulize swali,unaenda kuwahoji watu wawili kuhusu kufanyika kwa tukio fulani,kati ya hao watu wawili mmoja baina yao alilifanya hilo tukio kwa mikono yake na mwingine alishuhudia kwa macho yake wakati tukio hilo likifanyika,na hao watu ni watu ambao walikuwa wanafahamiana kias flani,

unataka kuniambia baada ya kuwahoji na wote wawili wakakaa kimya je ukimya wa yule mfanyaji au mtendaji wa lile tukio unalandana na ukimya wa yule shuhuda wa hilo tukio??

Hapo utapata kuona ukimya wa nyerere ni dhidi ya kusutwa kwa yale anayoulizwa na ukimya wa sykes ni dhidi ya kuyaokoa mengine yasiyostahiki kutokea kwa maslahi ya taifa hili,huku akijua tu ya kwamba ukweli siku zote utadhihiri tuh na hauwezi potea kamwe,na leo ni kweli mwenye macho haambiwi ona na mwenye maskio haambiwi sikia,ile hoja ya huyu nguruvi haina mashiko,tafadhali turudi kwenye mantiki kuu.
 

Kwa kesi ya kitabu cha Mohamed Said, wenye dhamana ya mwisho walikuwa ni Mzee Nyerere na Mzee Sykes tu si vinginevyo,

Kwa hilo siasa haihitajiki bali ukweli pekee kutoka kinywani mwa Mzee Sykes na Mzee Nyerere sio kulishwa maneno!
 
Sio tu kuwalisha maneno bali amefikiri kwa niaba yao, kaamua kwa niaba yao na wakati mwingine kahukumu kwa niaba yao! Mara kwa mara ataandika Mwalimu hakutaka hili lifanyike hivi, Mwalimu hakujibu hili kwa sababu hii, Mwalimu kakaa kimya kwa sababu hii,..., ni shutuma kwa kwenda mbele.

Waislamu wenyewe anaojidai kuwatetea amewagawa makundi mawili: Wale waliofanyakazi na Mwalimu au BAKWATA hao hawana nafasi kwake. Hawazungumzii kabisa kama akina Rashid Kawawa. Mzee wetu huyu hana tofauti na Sheikh Ponda isipokuwa kwa mbinu anazotumia kuwafikishia ujumbe Waislam.

Hata awapambe vipi WAKIMBIZI wake hawa, historia ya NCHI hii haitabadilika.
 
kwa kesi ya kitabu cha mohamed said, wenye dhamana ya mwisho walikuwa ni mzee nyerere na mzee sykes tu si vinginevyo,

kwa hilo siasa haihitajiki bali ukweli pekee utoka kinywani mwa mzee sykes na mzee nyerere sio kulishwa maneno!


basi na ingeleta mantiki kama julius angekanusha,hivi yericko mimi nakuja kwako nakushutumu na kukuletea picha za kukufumania na tukio fulani la aibu na nakuambia kabisa hizi ni picha zako mimi nimeshazitangaza kwa jamii,nawewe unajua kabisa zile picha si za kweli na ni za kutengeneza tuh ili niharibu reputation yako,kweli utathubutu kukaa kimya na usiseme chochote??

Sasa sembuse hili la mustakabali wa taifa na jins tunavomjua julius kweli angethubutu kukaa kimya hivi hivi bila kumchukulia hatua huyu mwenye choko choko??

Nadhani jibu kichwani mr big brother yericko unalo,thanks.
 

Kabla sijakujibu nikuulize swali:

Unafiki au kudhani ni kwanini Mzee Sykes hakujibu chochote juu ya mlishwayo na Mohamed Said mpaka anapoingia kaburini?
 
Nadhani Kitabu cha Mohamed Said kilitoka 1998. Atusaidie mwenyewe kilianza kusambazwa hapa nchini mwezi gani. Marehemu Nyerere alifariki October 14, 1999. Hatujachukulia mda aliougua. Jamani tumtendee haki mzee wa watu siyo kusema tu hakujibu.
 
kabla sijakujibu nikuulize swali:

Unafiki au kudhani ni kwanini mzee sykes hakujibu chochote juu ya mlishwayo na mohamed said mpaka anapoingia kaburini?

thanks brother yericko,namimi naomba nikujibu ndugu yangu,
muhusika mkuu na mwenye kesi ya kujibu na kutolea maelezo alikuwa ndugu julius,pili pili asozila yeye sykes zimuwashie nini??
Mantiki alishajitosheleza yeye na ukweli ule,na muhusika limemchoma na kaamua kukaa kimya,yumkin sykes alikaa kimya ili amskie muhusika je,atakubali ama atakanusha?kama tujuaavyo,wale wote ni bin adam,na muda wao wa kufa ulipowadia wote wakafariki,lakini ukweli uliobakia wenye macho tumeuona,wenye maskio tumeuskia,na wenye akili tumeuzingatia na kuufikisha kwenye jamii,na ni ukweli huu tutazid kuwasimulia watoto wetu,wajukuu wetu na vitukuu,thanks a lot,nikuongeze??
 
Kaka! kweli umekisoma kitabu chote cha Mohamed Said.

Sina tatizo na uchambuzi wako.

Huenda umesimama hapo ulipo kwa kuwa umeshindwa kuona katika
yale niliyosema sababu za Abdu kunyamaza kimya pale TAA ilipoanza
kukashifiwa.

Kashfa ambazo hazikuishia kwa TAA bali zilitambaa hadi kwake yeye
kwa kuambiwa uongozi wake kati ya 1950 - 1954 hakuwa akiongoza
chama cha siasa bali chama cha "starehe."

Na hapa sitaki kusema kuwa maana ya maneno hayo kwa ukamilifu
wake ni kuwa yalikuwa yanakwenda nyuma hadi kwa baba yake
aliyeasisi African Association.

Kama wanaukumbi mtakumbuka nilishasema kuwa kulikuwa na mradi
wa kuandika historia ya TANU na kazi hiyo alipewa Abdu akisaidiwa na
Dr. Kleruu.

Mradi huu Nyerere aliuhujumu kwa kuwa yale aliyokuwa akiandika Abdu
hayakumpendeza Nyerere.

Abdu alianza kuandika kwa kuianza historia ya TANU na kuasisiwa kwa
African Association.

Hapa sitaki kueleza mengi kuhusu mafanikio ya TAA hadi kuwezakuja
kuundwa kwa TANU.

Nyerere hakupenda historia ile kwa sababu yeye alitegemea ile historia
ya TANU ingekuwa historia yake.

Haikuwa hivyo ilikuwa historia iliyokwenda nyuma hadi 1929 African
Association ilipoasisiwa.

Haya ninayoeleza huyo ni marehemu Abdu Sykes anazungumza wakati
wa uhai wake.

Ndiyo maana baada ya hapo Abdu akamnyamazia Nyerere na yeyote
kuhusu historia ya TANU.

Ndiyo maana hata Lady Judith Listowel alipomhoji Abdu mwaka 1962
Abdu hakufunguka.

Ndiyo maana ilipoandikwa historia ya TANU na Kivukoni College historia
ilianza na kumalizikia na Nyerere.

Ndiyo maana unaona nilipokuja kuandika katika Africa Events kuwa Abdu
Sykes ndiye muasisi wa TANU mwaka 1988 toleo zima la gazeti lilikusanywa
likachomwa moto.

Humu nimeandika mengi kuhusu harakati za uhuru naamini mengi kwa
wanaukumbi ni mambo mageni.

Narudia kusema tena.
Simlazimishi mtu kuamini niliyoandika hata kidogo.

Ninachosema ni kuwa hiyo ndiyo historia ya wazee wangu kama
nilivyopokea kutoka kwao.
 

Ndugu yangu umetoa hoja vizuri nami nakusoma.
Ghafla hamaki zimekupanda unaanza matusi tena
neno lenyewe unaliwekea HERUFI KUBWA.

Maana ya herufi kubwa kwenye maandishi ni kuwa
"unapiga kelele."

Huna haja ya kukasirika ndugu yangu hapa tunaelimishana.
 
Kwa tuliowahi kufanya kazi na Nyerere hilo si la kushangaza. YEYE ALIITWA HAAMBILIKI kwa sababu alikuwa mjuvi wa kila kitu. Nakumbuka nikiwa wizara ya Fedha kitengo cha bajeti wakti wa vuguvugu la kuhamishia makao makuu kwenda Dodoma kama wataalamu wa uchumi tuliandika paper nzuri sana tukielezea uchumi wa nchi na mwelekeo wake kwa wakti huo na kujiongezea mzigo wa kuhamisha makao makuu kwenda Dodoma. Nakumbuka siku hiyo alituita na kututukana kama watoto wadogo tusio na taaluma kisha akapitisha maamuzi yake ambayo mpaka leo Tz inawagharimu na makao makuu hayajafanikiwa. Kifupi alikuwa HAAMBILIKI kwa lolote wala chochote.
 

Mkuu niwe mkweli nisimamie weledi wa mambo.

Sio kwamba yote yaliyo katika kitabu chako ni batili la hasha, yapo mengi mazuri kama ilivyo kwenye kitabu cha Kivukoni.

Leo hii mimi nikitaka kuandika historia hii, yapo nitakayonukuu katika kitabu chako na cha kivukoni!

Kinachoondoa nguvu ya kitabu chako ni kuweka hisia zako ama za mitaani kuwa ndio uhalisia wa Mzee Nyerere na Sykes.

Hata post yako hii hapo juu unasema wazi kuwa Mwalimu Nyerere alihujumu mpango wa Dr Kreluu na Addu wa kuandika historia ya TANU, lakini tukisema uthibitishe hili utakuja na ushahidi kutoka kwenye kitabu chako hichohicho tunachokipinga kuwa ni cha kufikirika.

Hayo ni sehemu ya mapungufu makuu katika andiko lako mkuu!
 
 

Sina la kuongeza.
Nadhani wanaotusoma wameelewa hoja zetu sote.

Insha Alla tuwaachie wao.
 

Naheshimu mawazo yako.

Narudia tena mimi humu ukumbini kazi yangu kubwa ilikuwa
kueleza historia ambayo si wengi walikuwa wanaifahamu.

Alhamdulilah nimejitahidi kadri ya uwezo wangu.

Sina uwezo wa kuwafanya waniamini ila ninachoamini ni kuwa
hawa wasomaji ni watu wenye akili na uwezo wa kuchambua
mambo.

Hawa ndiyo walengwa wangu na hakika ujumbe umewafikia.
 

Ngano...
 
Nadhani Kitabu cha Mohamed Said kilitoka 1998. Atusaidie mwenyewe kilianza kusambazwa hapa nchini mwezi gani. Marehemu Nyerere alifariki October 14, 1999. Hatujachukulia mda aliougua. Jamani tumtendee haki mzee wa watu siyo kusema tu hakujibu.

Wakati mwingine hunijia huruma kwa kuwa mimi najua mengi katika haya
kupita hawa ninaojadiliananao.

Kuna habari nyingine huwa siona sababu ya kuziweka hapa na ni nyingi.

Nyerere si kama hakujibu.
Alikubali kuandika maisha yake na humo ataeleza upande wake wa historia.

Kazi hiyo alimpa Prof. Haroub Othman.
 

Ndugu yangu umefanya haraka.
Ushahidi uko hapo.

Nastaajabu vipi hukuuona.
Angalau basi ungeuliza kiungwana.

Mzee ushahidi uko wapi?
Insha Allah ningekujibu.

Umenitukana na kuniita muongo bila ya
sababu, mchochezi nk.

Angalia hizo footnote gazeti la Majira
ndilo lililomnukuu Kadinali Pengo.

Ikiwa wewe ni mjuzi katika mambo haya
utaelewa kwa nini ilikuwa muhimu nibandike
hicho kipande.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…