Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
- Thread starter
- #781
Wanajamvi, tuendelee kuangalia mtitiriko wa ngano kwa macho mawili.
Huko nyuma Mohamed amesema kuwa alipoandika kitabu chake Nyerere alikuwa hai na alikaa kimya bila kusema lolote pengine Mohamed akichukulia kuwa huo ni ushahidi wa Nyerere kukubalina na kitabu chake au udhaifu wa Nyerere kuzikabili hoja zake.
Huko nyuma Mohamed amesema baada ya kusoma kitabu chake, Profesa Haroub Othman kipenzi cha Nyerere kabla, alibadili mawazo na kumwendea Nyerere kumueleza aandike jambo kuhusu yasemayo kwasababu kukaa kimya kunatoa taswira na hisia tofauti. Nyerere alikaa kimya hadi anaingia kaburini
Kuna mambo tunajifunza kutoka kwa Abdu Sykes na Nyerere. Wote wanakitu wanafafana katika baadhi ya mambo.
Wote wawili walikaa kimya kuhusu historia ya TAA,TANU na hata majengo waliyotumia katika harakati.
Wote walikaa kimya hata pale walipopata shinikizo la kutakiwa kusema jambo.
Wote hawakupenda kuongelea yaliyotokea.
Wote hawakuandika vitabu kuhusu maisha yao binafsi ya kisiasa na harakati zao katika uhuru
Wote walikaa kimya hadi walipoingia kaburini kwa nyakati tofauti.
Hakuna anayeweza kujua hekima zao kukaa kimya hadi wanaingia kaburini.
Inatosha kusema kuwa huenda ni kuchelea kuligawa taifa au tu ni kwasababu hawakupenda kuzifanya jitihada zao kama silaha za vizazi vijavyo kwani hilo halikuwa lengo la kazi yao. Narudia, hakuna ajuaye kwanini walikaa kimya.
Wanapotokea watu na kuyatumia majina yao kufikia malengo yao au kukidhi haja zao za kibinadamu na hali, si kuwatendea haki hata kidogo zaidi ya kuudharau na kuudhalilisha mchango wao.
Hakuna mahali Mohamed amemkariri Abdu Sykes akidai kuwa harakati zake zililenga kuwakomboa Waislam
Hakuna mahali Mohamed amemkariri Nyerere akisema kuwa harakati zake zilikuwa kumkomboa Mkatoliki.
Ushujaa wa kudai wasichokisema hawa manguli waliobobea, sisi makapuku tunaupata wapi na kwanini na faida ta nani?
Kinachofikirisha zaidi ni kuwa Abdu Sykes na Nyerere wana mfafano(similarity) katika jambo hili.
Vipi mmoja wao apewe sifa za ukimya na mwingine abebe rungu zito la hukumu ya historia kwa ukimya ule ule?
Kwanini Nyerere ahukumiwe kwa kutojibu kitabu cha Mohamed, na Sykes asikuhumiwe kwa kutojibu kitabu cha kivukoni?
Kwanini Nyerere ahukumiwe kwa kutoandika kitabu cha historia kama alivyoshauriwa na Prof Othman lakini Sykes asihukumiwe kwa kutokubali shikizo la rafiki zake?
Kwanini Nyerere ahukumiwe kwa ukimya hadi alipoingia kaburini, na Sykes apewe sifa kwa ukimya wakati anaingia kaburini?
Hadi hapo tunaona kuwa hukumu ya Nyerere ilishaandaliwa kabla hajasomewa mashtaka, na mashtaka hayakuandaliwa kwa makosa yake bali kwasababu tu ni Nyerere mkatoliki kwa mintaarafu ya Mohamed Said.
Flip flop katika mambo ya kihistoria ni kitendo cha kutisha.
Historia ni dead subject iliyo katika facts. Ukiifanyia ''doctoring'' hukawii kukwama.
Tunaona double standard, gross interpretation and misrepresentation iliyochagizwa na prejudice.
Hayo ndio maajabu ya Allah.
Anatetea marehemu bila uwepo wao , leo historia ya Nyerere na Sykes inahadithiwa vyuoni Marekani.
Bondia anaweza pigwa kwa knockout, unanimous decision au technical knockout.
Hayo ndio makosa makubwa yaliyo kwenye kitabu cha Mohamed Said anayoyatetea kwa nguvu huku akikwepa baadhi ya hoja nzito!
Kimantiki Mohamed amewalisha maneno Nyerere na Sykes
Amewaamulia yeye, lakini ukikisoma kitabu chake chote mpaka ganda lake hakuna aliponukuu mahojiano ya Nyerere au Sykes! Zaidi imewekwa hisia au lengo la Mohamed Said tu.
Hii ndio hatari inayotukumba watanzania!
Nilieleza katika moja ya post zangu hapo juu kuwa ili ufahmu historia ya AA,TAA na TANU nilazima utulie sana na uangaze kuanzia ideology yao,
Kwa wazee wetu hawa wanaukombozi wa Tanganyika, ideology yao ileile ya AA iilitoka ikibadilika kibaiolojia hadi TANU na uhuru kamili ndani ya mapito yao kulikuwa na mageuzi mengi sana, kwanza kutoka uanaharakati na kuingia uanasiasa. Hapa ndipo palipo anza kuzaliwa makundi ya kisiasa kama ilivyo kwenye siasa za leo, na moja ya uchaguzi mgumu ni ule wa kura tatu wa 1953 uliomwingiza Mzee Nyerere kuwa rais wa TAA na kumbwaga mpinzani wake kisiasa Mzee Sykes!
Sasa Mohamed Said huenda anatumia makovu hayo ya kisiasa kufarakanisha watu,
Asilo lizingatia Mohamed ni kuwa wahusika hawakutoa neno lolote juu yao mpaka wanaingia kaburini zaidi ya hisia za mashabiki wao tu ambazo leo yeye Mohamed Said anatumia kupotoshea watu kwa minajri yake.
Nimeeleza kidogo kuwa moja ya makosa katika *ngano* za Mohamed Said ni kuakisi kuanzia miaka ya 1950,
Sasa kwamwanahistoria usie makini unaeziangaza harakati za ukombozi kwa miaka hiyo ya 1950 nilazima utaibuka na dhana yako sio ya historia husika,