Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Views 84164 si haba,ujumbe umewafikia wengi sana,na wengi wanazidi nufaika kwa Elimu hii kubwa kupata kutokea katika historia ya nchi yetu,sisi na walio wengi wanaofuatlia mjadala huu hatuoni uchochez uko wapi,

Na hawa wanaopinga na kukejeli hawaeleweki hasa hoja zao za msingi ni zipi..
 
Hayo ni kweli kabisa kwanza unatakiwa hujue Waislam kumpiga Nyerere hawajaanza kupitia kitabu cha Mohamed Said, wameanza kumpinga toka alipowakamata Masheikh na kuwaweka ndani baada ya uhuru.
Ritz,si kweli haya unayosema.

Kwanza naomba uweke sentensi sawa. Usitumie waislam maana kila mtu anaweza kuwa mwislam na uislam hauna hati miliki au application.Uislam ni imani na dini.
Ningeshauri useme ''baadhi ya waislam''.

Baada ya kusema hayo naomba nikuthibitishie kuwa baadhi ya waislam walimpinga Nyerere kabla ya uhuru.
Namnukuu Mohamed Said Mwakapopo aliyesema '' AMNUT ilianzishwa na waislam ili kumpinga Nyerere na kulikuwa na majaribio mawili ya kumuondoa katika madaraka ya uongozi wa TANU mwishoni mwa miaka ya 1950''.

Maana ya hii ni kuwa kabla ya uhuru, baadhi ya waislam kama AMNUT walishampinga Nyerere na hata kutaka kumuonodoa katika uongozi kwa kwa sababu ya Ukristo wake.

Baadhi ya Waislam walimuunga mkono na hawa ndio wengi waliotupatia uhuru wakiwemo akina Rehani Waikela, Sheikh Amir, Abdul Sykes,Bibi Titi Mohamed, Rashid Mfaume Kawawa, Chifu Abdallah Fundikira, Mzee Ngozi wa Moshi, Mzee Chaurembo, Mshume Kiyate, Mzee Kitundu, Mzee Mwapachu kwa uchache wa kuwataja.

Lakini pia lazima uelewe kuwa Uislam ni jina na mwislam ni muumini wa Uislam.
Si kila mwislam ni muumini ingawa ,muumini lazima awe mwislam.
Hivyo basi atumie jina la uislam kumpinga Nyerere si lazima awaye awe mwislam.

Ahsante
 

Nguruvi,

Mimi ukitaka kuninasibu kwa majina ya wazee wangu ni haya: Mohamed Said Salum Abdallah Samitungo Muyukwa Mwekapopo.

Vizazi saba hivyo nyuma.
Chunga spelling ya hayo majina.

Chifu Abdallah Said Fundikira alikuwa anaweza kwenda
nyuma vizazi kumi na tatu.
 
Ahsante, nimeandika kumbe ulishaandika.
Nikushukuru pia kuibua hili kwasababu kuna contradictions nyingi sana miongoni mwa baadhi ya watu.

Ritz anasema ''waislam'' in general walianza kumchukia Nyerere miaka mingi.Pengine walichukia na mfumo wake wa siasa ikiwa ni pamoja na chama alichoasisi akiwa rais na wazee wa Tandamti wakiwa wameshaondolea, hapa nina maana CCM.
Fair enough!

Mohamed Said anasema waislam walinong'oneza wamchague mtu wa CCM katika uchaguzi. Fair enough!

The question is, where do they stand on the issue.
Do they have the common ground! or it's a matter of shoot any moving object.
 
mzee kwenye sarcasm you are not very good at it... nice try though

MM,

Hapana siko sarcastic.

TANU iliundwa St. Francis College.

Hizi hadithi za Abdu Sykes na stori za mikutano ya siri nyumbani
kwake kuunda TANU miaka ya 1950s kabla hajakutana na Nyerere
ni ngano za Waswahili wakishalewa kahawa.

Wasikushughulishe.
Historia ya uhuru ishaandikwa na Chuo Cha Kivukoni.
 
kumbe habari yenyewe ya waikela ni uzushi.

Z,

Usipoteze muda wako hapa JF katika sijui historia ya uhuru.
Hawa Waswahili wakishalewa kahawa wanatunga ngano.

Historia ishaandikwa na Kivukoni College na hiyo ndiyo historia
ya kweli.
 
Adui wa waislam wa Tanzania ni nani? na kwa nini?
 
Duh! unatokwa mapovu bure! mbona maneno ya "kukiri"hukuambiwa wewe. Nilikuwa naongea na Ritz alipokuwa akibisha kwamba wewe hutumii misikiti na uislam kwa manufaa yako na chuki za kueneza uchochezi ambao utaleta maafa muda si mrefu. Jaribu kurudia tena maongezi yangu na Ritz. Kwa umri wako ukiwa una jaa gesi utapata kiarusi bure wakati tunahamu kuendelea kusikia ngano zako za Tandamti na Gerezani!
 
Haya yanafaa kwenye mihadhara yenu na sio hapa!
 

SASA hii kali,yaani chief Fundikira aliweza kwenda nyuma vizazi kumi na tatu,hii kwa afrika mbona haiwezekani,maana hicho kizazi cha kwanza si itakuwa kabla vasco da gama hajapita maeneo haya-hii data ni suspect
 
Z,

Usipoteze muda wako hapa JF katika sijui historia ya uhuru.
Hawa Waswahili wakishalewa kahawa wanatunga ngano.

Historia ishaandikwa na Kivukoni College na hiyo ndiyo historia
ya kweli.
Aah! Mohamed, ustaadh, yamekuwa haya tena!
 

Angalia kiarusi usijekupata wewe na siku hiyo ndiyo utatambua kuwa MUNGU yupo.
 
Angalia kiarusi usijekupata wewe na siku hiyo ndiyo utatambua kuwa MUNGU yupo.
Yote poa tu, kwani kwa nchi maskini kama hizi zetu ambako hatuna kawaida ya kupima afya zetu mpaka tuumwe haitakuwa ajabu. Sasa nikitambua kuwa mungu yupo itabadili maumivu na madhara ya kiharusi?hao wanaoumwa sasa hivi ni kwakuwa hawajatambua uwepo wa mungu? mbona unaleta mambo ya watoto!
 

Katika Waislam wanafiki hawakosi ndiyo hao Bakwata na wengine ndiyo wanaweza kumsifu Nyerere lakini Waislam wengi wanamlaani Nyerere fanya uchuguzi wako katika Misikiti yote ya Tanzania huko ndipo wanapopatika Waislam.
 
Last edited by a moderator:

Umefanya vizuri kutuwekea hii orodha ya kina Waikela na Masheikh waliomuunga mkono Nyerere na kutupatia uhuru.

Jiulize baada ya uhuru Nyerere aliwageukia hawa hawa Masheikh waliomuunga mkono na kuwaweka kizuizini hapa ndipo Waislam walipoanza kumchukia Nyerere.

Nguruvi3, hakuna Muislam ambae anaweza kumuunga mkono mtu dhalimu ambaye amewadhalilisha Masheikh wetu Uislam unatufundisha kuwa kitu kimoja tena tushikamane kwenye kamba moja kupinga dhulma dhidi ya Uislam na Waislam.

Waislam wanaomuunga mkono Nyerere ni wanafiki tu wakiongozwa na Bakwata.

Kama uamini na wewe fanya utafiti wako kupitia misikiti ya Tanzania na hili jambo ni la muda wala alitokani na kitabu cha Mohamed Said.
 

Kuna mzee mmoja alikuwa naye anajifanya ATHEIST akapatwa na maradhi ya moyo kalazwa hospital TMJ jamaa wamenda kumuangalia yupo analia tu anasema Mungu nisaidie nipone...nilishangaa sana kumbe dawa ya ATHEIST ni maradhi.
 
Kuna mzee mmoja alikuwa naye anajifanya ATHEIST akapatwa na maradhi ya moyo kalazwa hospital TMJ jamaa wamenda kumuangalia yupo analia tu anasema Mungu nisaidie nipone...nilishangaa sana kumbe dawa ya ATHEIST ni maradhi.
Ritz unapata tabu na huyu jamaa anakupotezea muda ni hizi safari zinampa kichwa na viroba achana nae tuendelee na darasa la mzee MS
 
SASA hii kali,yaani chief Fundikira aliweza kwenda nyuma vizazi kumi na tatu,hii kwa afrika mbona haiwezekani,maana hicho kizazi cha kwanza si itakuwa kabla vasco da gama hajapita maeneo haya-hii data ni suspect

Kwa akili yako unaamini Vasco da Gama ndiyo mtu wa kwanza kuzunguka dunia.
 
Kuna mzee mmoja alikuwa naye anajifanya ATHEIST akapatwa na maradhi ya moyo kalazwa hospital TMJ jamaa wamenda kumuangalia yupo analia tu anasema Mungu nisaidie nipone...nilishangaa sana kumbe dawa ya ATHEIST ni maradhi.
Ritz, wewe ni msomi achana na hizi story za kawaida sana. Mbona zipo nyingi sana hizo! nikupe nyingine hii; Jamaa mmoja alikuwa anaumwa sana akajua hana ndugu na akifa atazikwa na Manispaa, akahofu sana, mara sheikh mmoja akapita pale wodini, jamaa yule akamwita na kumwambia sheikh, "unajua miminilikuwa mkristo lakini usiku nimeota kuwa dini ya kweli ni uislam naomba kuanzia sasa hivi na mbele yako ni silim" Siku ya tatu akafa na kuzikwa kwa heshima zote za kiislam!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…