Hayo ni kweli kabisa kwanza unatakiwa hujue Waislam kumpiga Nyerere hawajaanza kupitia kitabu cha Mohamed Said, wameanza kumpinga toka alipowakamata Masheikh na kuwaweka ndani baada ya uhuru.
Ritz,si kweli haya unayosema.
Kwanza naomba uweke sentensi sawa. Usitumie waislam maana kila mtu anaweza kuwa mwislam na uislam hauna hati miliki au application.Uislam ni imani na dini.
Ningeshauri useme ''baadhi ya waislam''.
Baada ya kusema hayo naomba nikuthibitishie kuwa baadhi ya waislam walimpinga Nyerere kabla ya uhuru.
Namnukuu Mohamed Said Mwakapopo aliyesema '' AMNUT ilianzishwa na waislam ili kumpinga Nyerere na kulikuwa na majaribio mawili ya kumuondoa katika madaraka ya uongozi wa TANU mwishoni mwa miaka ya 1950''.
Maana ya hii ni kuwa kabla ya uhuru, baadhi ya waislam kama AMNUT walishampinga Nyerere na hata kutaka kumuonodoa katika uongozi kwa kwa sababu ya Ukristo wake.
Baadhi ya Waislam walimuunga mkono na hawa ndio wengi waliotupatia uhuru wakiwemo akina Rehani Waikela, Sheikh Amir, Abdul Sykes,Bibi Titi Mohamed, Rashid Mfaume Kawawa, Chifu Abdallah Fundikira, Mzee Ngozi wa Moshi, Mzee Chaurembo, Mshume Kiyate, Mzee Kitundu, Mzee Mwapachu kwa uchache wa kuwataja.
Lakini pia lazima uelewe kuwa Uislam ni jina na mwislam ni muumini wa Uislam.
Si kila mwislam ni muumini ingawa ,muumini lazima awe mwislam.
Hivyo basi atumie jina la uislam kumpinga Nyerere si lazima awaye awe mwislam.
Ahsante