Jasusi,
Nilifika George Washington Memorial hapa Washington na nikaona
ile video inayoonyesha mapambano yake na Waingereza.
Nilichukua muda mrefu katika makumbusho haya na kwa hakika huyu
shujaa anastahili kuenziwa na Waamerika.
Nimepita George Washington Bridge nikielekea New Jersey kutoka New
York nimeona sanamu ya Washington na farasi wake na nikaonyeshwa
sehemu alipowachenga Waingereza wakati wa vita vya ukombozi.
Lakini Washington anaenziwa kwa kile alichowafanyia wananchi wake.
Nyerere ataenziwa na hakuna awezae kuzuia hilo.
Lakini juu ya kuenziwa kwake atakumbukwa halikadhalika kwa yale aloacha
nyuma.
Jamii moja imeneemeka nyingine hohehahe na hata kuandika historia yao
walikuwa wanatishwa
''G.Washington ataenziwa kwa kile alichowafanyia wananchi wake, lakini Nyerere ataenziwa hilo halina ubishi'' Hapa Mohamed unakubali kuwa ataenziwa hata kama hakuna alichowafanyia wananchi wake. Logically hilo halipo. Utamuenzi vipi mtu kama hakuna alichokifanya?
Sijui kama G.Washington alikuwa perfect human being na pengine hilo ndilo unalotaka kuwaeleza watu.
Nimesoma historia ya G.Washington it's not all roses! there is the dark side of him.
Wamarekani wanasema , wait a minute let us take the positive and forgive the negative.
Mohamed, jamii ya Tanzania imetengenezwa kwa mchangayiko. Hilo tu linatosha kumpa Nyerere credit.
Kuna Wahindi, Waarabu, Waafrika n.k. Kwahiyo si sahihi kusema jamii zipo mbili moja ilineemeka na nyingine kudhalilika.
Tukienda mbali, hadi mwishoni mwa miaka ya 1990 sehemu kubwa ya wafanyabiashara na watu waliokuwa na ahueni miongoni mwetu walikuwa ni waarab na wengi kwa ukweli waislam. Sijui kama hiyo haikuwa neema kwa jamii moja.
Lakini basi unawaweka wapi watu kama wahindi na waarab ambao katika standard ya maisha ya kitanzania wana hali njema kiasi ukilinganisha na wamatumbi.
Jamii ulioikusudia kuneemeka ni wakristo. Hili nalo logically halina mashiko wala mantiki.
Ukitembea Tanzania watu wanapigika accross the board.
Hakuna kituo cha mafuta cha kidini wala mifuko ya sukari yenye nembo ya dini.
Inflation ambayo ni 19% inakula kila mahali na kwa kila mtu.
Hakuna kitu ambacho kimewekwa mahususi kwa kuangalia jamii fulani.
Hata kama tutaziangalia jamii kwa mtazamo unaoutaka, swali linabaki kuwa kwanini basi Shia, Bohara na Ismailia wafanikiwe zaidi ya wamatumbi. Je nao ni sehemu ya kundi la neema aliloliacha Nyerere!
Nasema haya kwasababu ukiangalia jamii za waarabu, wahindi, Shia, Bohara, Ismaili ukweli ni kuwa wana unafuu mkubwa sana kuliko jamii za wakristo uliowalenga hapa. Sasa wao nao ni kundi dhalilili au ni kundi la neema.
Ninakuhakikishia kuwa kuna mwislam leo amekaa mahali anamwangalia mkristo na kufikiri ni jinsi gani anaweza kumsaidia.
Nilikuwa Peramiho mission kuliko na kanisa la zamani sana.
Nilienda Machame pia. Kweli kama ukristo ni neema basi kuna wakristo A class na F class.
Mohamed, Tanzania ninaoijua mimi ni ile ya Mzee John kufiwa na mwanawe na gari la maziko kutolewa bure na Ustadhi Muhsin.
Ni ile ya Mzee Bakari kumkopesha kibaba cha unga Mzee Joseph.
Ni Tanzania ile niliyoiona Heathrow Mama akiwa na watoto na akiongea kiswahili, halafu wakatokea watu na kuuliza unakwenda wapi na kuanzia hapo mama akapata msaada kwa mtoto aliyekuwa mgonjwa.
Si mama mwenye watoto au waliotoa msaada walioulizana wewe ni kabila gani au wewe ni dini.
Kilichowaunganisha ni Utanzania.
Hii habari ya kupika na kuzua hadithi ili kufurakanisha jamii haisadiii na wala haikubaliki kwa mwenyezi mungu.
Labda waislam wanisaidie wapi katika Kuran, hadithi na sunna imeelezwa kuwa kuna nyakati za farki ili awaye apate thawabu.