Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

nyerere_in_india_1981-2.gif
 
Jasusi,

Nilifika George Washington Memorial hapa Washington na nikaona
ile video inayoonyesha mapambano yake na Waingereza.

Najua ushafika hapo na unayajua vyema makumbusho hayo.

Nilichukua muda mrefu katika makumbusho haya na kwa hakika huyu
shujaa anastahili kuenziwa na Waamerika.

Nimepita George Washington Bridge nikielekea New Jersey kutoka New
York nimeona sanamu ya Washington na farasi wake na nikaonyeshwa
sehemu alipowachenga Waingereza wakati wa vita vya ukombozi.

Lakini Washington anaenziwa kwa kile alichowafanyia wananchi wake.

Nyerere ataenziwa na hakuna awezae kuzuia hilo.

Lakini juu ya kuenziwa kwake atakumbukwa halikadhalika kwa yale aloacha
nyuma.

Jamii moja imeneemeka nyingine hohehahe na hata kuandika historia yao
walikuwa wanatishwa.

Najua hili linakuhusu.
Leo nilikwenda mazikoni makaburi ya Kisutu.

Nimefika katika kaburi la mzee wako Abdu Sykes na mwanangu ndiye aliyesoma
dua.

Pembeni yake liko kaburi la mama yetu, mkewe mama yake Kleist Bi. Mwamvua
Mrisho Mashu.
Mohamed,
Kumbuka kuwa hakuna binadamu aliye kamili. Washington ametawala wakati utumwa umetamalaki. Hata yeye alikuwa anamiliki baadhi ya watumwa. Ilichukua miaka, mpaka enzi za Lincoln, ambapo utumwa ulisimamishwa hapa Marekani. Lakini huyu anasifika kama baba wa taifa, pamoja na madhaifu yote yaliyokuwepo. Sasa badala ya kumlaumu Nyerere kwa kushindwa kuondoa hali ya hohe hahe kwa baadhi ya jamii, tujikite sisi tuliopo tuziondoe hizo kasoro, na yeye tumpe sifa zake kwa jitihada alizofanya kukabiliana na kasoro hizo badala tu ya kumbeza. How does that sound?
 
Zingatia sheria za jf ili usikumbane na lungu la Mods,

Kuniita Yericko X ni kinyume na miiko na maadili ya jf.

Kwaheshima ya jukwaa na wanaotufuatilia hapa, nakusihi ulifute hilo neno hapahapa nakuwaomba radhi wasomaji wetu kisha tusonge mbele ndugu.

Hivi ni kwanini hawa watu wanakuita Jericko X? maana ake nini? ni tusi au kebehi? kama ni kinyume na kanuni kukuita hivyo basi ni bora kanuni za JF ziheshimiwe nakubaliana nawe JN!
 
Duuh!!!! Mohamed Said,24/7 unakuwa humu, sasa huko makaburini unakwenda na tablet???

"Najua hili linakuhusu.
Leo nilikwenda mazikoni makaburi ya Kisutu."
 
Last edited by a moderator:
Wimana,

Mvaaji ndiye ajuae wapi kiatu kinabana.
Labda nikuongezee.

Huku kwetu jeshi la polisi linachukuliwa
kama ''armed wing of the Church.''

Unajua ndugu yangu kwa hali yako kama
Mkristo hujaonja kubaguliwa.

Siku hiyo hapakuwa na maandamano hapa
Dar es Salaam kote.

Huyo alokamatwa ananihusu na ninajua mie
nikisemacho.

Asante MS
Huko Tarime Wakurya wanapata madhila makubwa sana. Wanapigwa Risasi hovyo na makaburu kwa kushirikiana na
Serikali. Gereza la Tarime utawakuta wao ndio wengi. Kweli wanabaguliwa sana tena sana na mfumo Kristo.

Kule Moshi Wakatoliki na Walutheri wanabaguliwa sana, tena utawakuta wengi wao ndio wako gereza la Moshi.
Wanabaguliwa sana sana na Mfumo Kristo.

Kabla sijasahau.
Huku mtaani Vijana wanaonewa sana, wao tu ndio wanakamatwa na kutiwa magerezani. Serikali hii ya kibaguzi
inabagua na kuwadhalilisha Vijana wa nchi hii. Inawaonea kwa sababu wao ni Vijana, Kisa? Kwa sababu ya
mfumo Kristo, ambao hauwapendi Vijana.

Halafu naona nimechanganya kule Moshi si Wakatoliki na Walutheri wanaoonewa ni Wachaga!

Huu mfumo Kristo huu!
 
Jasusi,

Nilifika George Washington Memorial hapa Washington na nikaona
ile video inayoonyesha mapambano yake na Waingereza.

Nilichukua muda mrefu katika makumbusho haya na kwa hakika huyu
shujaa anastahili kuenziwa na Waamerika.

Nimepita George Washington Bridge nikielekea New Jersey kutoka New
York nimeona sanamu ya Washington na farasi wake na nikaonyeshwa
sehemu alipowachenga Waingereza wakati wa vita vya ukombozi.

Lakini Washington anaenziwa kwa kile alichowafanyia wananchi wake.

Nyerere ataenziwa na hakuna awezae kuzuia hilo.

Lakini juu ya kuenziwa kwake atakumbukwa halikadhalika kwa yale aloacha
nyuma.

Jamii moja imeneemeka nyingine hohehahe na hata kuandika historia yao
walikuwa wanatishwa
''G.Washington ataenziwa kwa kile alichowafanyia wananchi wake, lakini Nyerere ataenziwa hilo halina ubishi'' Hapa Mohamed unakubali kuwa ataenziwa hata kama hakuna alichowafanyia wananchi wake. Logically hilo halipo. Utamuenzi vipi mtu kama hakuna alichokifanya?

Sijui kama G.Washington alikuwa perfect human being na pengine hilo ndilo unalotaka kuwaeleza watu.
Nimesoma historia ya G.Washington it's not all roses! there is the dark side of him.
Wamarekani wanasema , wait a minute let us take the positive and forgive the negative.

Mohamed, jamii ya Tanzania imetengenezwa kwa mchangayiko. Hilo tu linatosha kumpa Nyerere credit.
Kuna Wahindi, Waarabu, Waafrika n.k. Kwahiyo si sahihi kusema jamii zipo mbili moja ilineemeka na nyingine kudhalilika.

Tukienda mbali, hadi mwishoni mwa miaka ya 1990 sehemu kubwa ya wafanyabiashara na watu waliokuwa na ahueni miongoni mwetu walikuwa ni waarab na wengi kwa ukweli waislam. Sijui kama hiyo haikuwa neema kwa jamii moja.

Lakini basi unawaweka wapi watu kama wahindi na waarab ambao katika standard ya maisha ya kitanzania wana hali njema kiasi ukilinganisha na wamatumbi.

Jamii ulioikusudia kuneemeka ni wakristo. Hili nalo logically halina mashiko wala mantiki.
Ukitembea Tanzania watu wanapigika accross the board.

Hakuna kituo cha mafuta cha kidini wala mifuko ya sukari yenye nembo ya dini.
Inflation ambayo ni 19% inakula kila mahali na kwa kila mtu.

Hakuna kitu ambacho kimewekwa mahususi kwa kuangalia jamii fulani.
Hata kama tutaziangalia jamii kwa mtazamo unaoutaka, swali linabaki kuwa kwanini basi Shia, Bohara na Ismailia wafanikiwe zaidi ya wamatumbi. Je nao ni sehemu ya kundi la neema aliloliacha Nyerere!

Nasema haya kwasababu ukiangalia jamii za waarabu, wahindi, Shia, Bohara, Ismaili ukweli ni kuwa wana unafuu mkubwa sana kuliko jamii za wakristo uliowalenga hapa. Sasa wao nao ni kundi dhalilili au ni kundi la neema.

Ninakuhakikishia kuwa kuna mwislam leo amekaa mahali anamwangalia mkristo na kufikiri ni jinsi gani anaweza kumsaidia.
Nilikuwa Peramiho mission kuliko na kanisa la zamani sana.
Nilienda Machame pia. Kweli kama ukristo ni neema basi kuna wakristo A class na F class.

Mohamed, Tanzania ninaoijua mimi ni ile ya Mzee John kufiwa na mwanawe na gari la maziko kutolewa bure na Ustadhi Muhsin.

Ni ile ya Mzee Bakari kumkopesha kibaba cha unga Mzee Joseph.

Ni Tanzania ile niliyoiona Heathrow Mama akiwa na watoto na akiongea kiswahili, halafu wakatokea watu na kuuliza unakwenda wapi na kuanzia hapo mama akapata msaada kwa mtoto aliyekuwa mgonjwa.

Si mama mwenye watoto au waliotoa msaada walioulizana wewe ni kabila gani au wewe ni dini.
Kilichowaunganisha ni Utanzania.

Hii habari ya kupika na kuzua hadithi ili kufurakanisha jamii haisadiii na wala haikubaliki kwa mwenyezi mungu.
Labda waislam wanisaidie wapi katika Kuran, hadithi na sunna imeelezwa kuwa kuna nyakati za farki ili awaye apate thawabu.
 
Jasusi,
Naogopa hata kusema.

Unajua nini Mohamed? Mimi ni great admirer wa black Americans. Ukisoma historia yao, waliyopitia, jinsi walivyomudu na ku "overcome" kwa kutumia lugha yao wenyewe, there is much to admire. Imagine kama viongozi wao wangeanza kwa ku demonise George Washington, na viongozi wote wa wazungu ambao kwa hakika waliwatesa bila kiasi hawa Wamarekani weusi--kila jumapili kulikuwa na tukio la mweusi kutundikwa mtini na kunyongwa na wazungu wakishuhudia na kupiga makofi kama mojawapo ya spectacle--sijui kama juhudi zao za kugombea haki ambazo walithibitishiwa na katiba zingezaa matunda. Lakini viongozi wao, hasa Martin Luther King jr. waliwashauri waelekeze macho yao "the eye on the prize" kama walivyosema wenyewe. Badala ya kutizama nyuma waliangalia mbele. Leo, White House, ambako mweusi alikuwa ni mpishi, mfagiaji, mfungua mlango na msafisha viatu, inakaliwa na mweusi, akipigiwa saluti na watu weupe. Nadhani hapa kuna somo kwetu sote. Badala ya kutizama nyuma na kulaumu, tuangalie mbele na kujiuliza ni vipi tunaweza kulikwamua taifa letu na dhuluma ambazo kila kukicha zinaongezeka. Leo, Tanzania tumefikia mahali mtu anakamatwa, anachomwa jicho, anang'olewa jino bila ganzi na kupigwa bila sababu, na serikali haifanyi chochote. Polisi hao hao ambao tunawategemea kulinda amani wamekuwa ndio wavunjaji wakubwa wa amani yetu. Hapo ndipo tulipofika leo Watanzania.
 
Nimekusoma.

Umenishushia gunia la chumvi mgongoni.
Ntakujibu Insha Allah.
 
Leo, Tanzania tumefikia mahali mtu anakamatwa, anachomwa jicho, anang'olewa jino bila ganzi na kupigwa bila sababu, na serikali haifanyi chochote. Polisi hao hao ambao tunawategemea kulinda amani wamekuwa ndio wavunjaji wakubwa wa amani yetu. Hapo ndipo tulipofika leo Watanzania.

Unaweza kuita huu ni Ugaidi?
 
Wakati mwingine huwa napata hisia kwa Mzee MS haishi nchi hii.

Vijana wa Kiislam wananyanyaswa kwa sababu ya Uislam wao, Uh Mzee huijui hii nchi pengine au una lako jambo.
Huku mtaani anaweza kuingia Polisi na kuwakamata Vijana kadhaa kisa kwa nini wanapiga soga usiku, Vijana Wenyewe
wanaita "Pira". Na humo atakamatwa Mngoni, Mjita, Muislam, Mkristo n.k.

Lakini wakati huo huo utawakuta vijana wa Kingoni, Kijita, Kikristo na Kiislam wakipiga soga mitaa ya kwao Oiysterbay
na polisi wakawapa salamu ya heshima na kuondoka zao!

Tokea nikiwa mdogo sikuwahi kusikia iwe kutoka kwa marafiki zangu ama majirani kwamba mtu amekamatwa usiku
kutokana na dini yake. Nililo na hakika nalo kesho asubuhi wataamka Vijana wenzao kwenda kuwawekea dhamana!

Kuna wakati nilikwambia kwamba inawezekana hao watu unaopiga soga nao wanapenda kukupa habari unazozipenda.

Mitaa yetu hii, Nyumba moja wapangaji kama Umoja wa Mataifa (Kila kabila na dini mumo humo). Huko kwa wahangai
kaji halikadhalika mchanganyiko wa kila kabila na dini. Tunakula pamoja, tunataniana pamoja, tunacheza pamoja, tuna
shabikia "Premier league" na Simba/Yanga pamoja, tunaishi nyumba moja, tunatega kwenda nyumba za Ibada
pamoja, tunazika pamoja, tunaimba pamoja. Halafu muda fulani wakamatwe wa Dini fulani na wengine waachwe!!

Ukistaajabu ya Firauni utayaona ya ......................!
 
Unajua nini Mohamed? Mimi ni great admirer wa black Americans. Ukisoma historia yao, waliyopitia, jinsi walivyomudu na ku "overcome" kwa kutumia lugha yao wenyewe, there is much to admire. Imagine kama viongozi wao wangeanza kwa ku demonise George Washington, na viongozi wote wa wazungu ambao kwa hakika waliwatesa bila kiasi hawa Wamarekani weusi--kila jumapili kulikuwa na tukio la mweusi kutundikwa mtini na kunyongwa na wazungu wakishuhudia na kupiga makofi kama mojawapo ya spectacle--sijui kama juhudi zao za kugombea haki ambazo walithibitishiwa na katiba zingezaa matunda. Lakini viongozi wao, hasa Martin Luther King jr. waliwashauri waelekeze macho yao "the eye on the prize" kama walivyosema wenyewe. Badala ya kutizama nyuma waliangalia mbele. Leo, White House, ambako mweusi alikuwa ni mpishi, mfagiaji, mfungua mlango na msafisha viatu, inakaliwa na mweusi, akipigiwa saluti na watu weupe. Nadhani hapa kuna somo kwetu sote. Badala ya kutizama nyuma na kulaumu, tuangalie mbele na kujiuliza ni vipi tunaweza kulikwamua taifa letu na dhuluma ambazo kila kukicha zinaongezeka. Leo, Tanzania tumefikia mahali mtu anakamatwa, anachomwa jicho, anang'olewa jino bila ganzi na kupigwa bila sababu, na serikali haifanyi chochote. Polisi hao hao ambao tunawategemea kulinda amani wamekuwa ndio wavunjaji wakubwa wa amani yetu. Hapo ndipo tulipofika leo Watanzania.
tena umenikumbusha mkuu!
huyu absalom kibanda huyu ni mkristo au muislam?
mnisamehe kwa kuuliza hilo, sijawahi kuwa na tabia ya kuuliza ila udini ulioingia sasa inabidi niulize.
 
tena umenikumbusha mkuu!
huyu absalom kibanda huyu ni mkristo au muislam?
mnisamehe kwa kuuliza hilo, sijawahi kuwa na tabia ya kuuliza ila udini ulioingia sasa inabidi niulize.

Tupe tafsiri ya neno udini.
 
UDINI ni ubaguzi wa jamii zenye imani tofauti,
na wewe naomba unipe tafsiri ya neno mfumo kristo.

Kama aliofanya Nyerere kuwaweka ndani Masheikh na wengine kuwafukuza nchini.

Matunda ya mfumo kirsto mfano wake ni huu uzi.

Hapa tulipofika ni kazi ya mfumo kirsto.
 
Kama aliofanya Nyerere kuwaweka ndani Masheikh na wengine kuwafukuza nchini.

Matunda ya mfumo kirsto mfano wake ni huu uzi.

Hapa tulipofika ni kazi ya mfumo kirsto.
embu fafanua namna huo mfumo kristo unavyofanya kazi,
 
embu fafanua namna huo mfumo kristo unavyofanya kazi,

Kusoma hujui hata picha nayo uoni.

Tembelea ofisi zote za serikali wizara zote za serikali angalia "Ratio" ya Waislam na Wakirsto waliojiriwa ndiyo utajua mfumo kirsto
 
Back
Top Bottom