Son of Alaska
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 2,812
- 1,061
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mohamed,Jasusi,
Nilifika George Washington Memorial hapa Washington na nikaona
ile video inayoonyesha mapambano yake na Waingereza.
Najua ushafika hapo na unayajua vyema makumbusho hayo.
Nilichukua muda mrefu katika makumbusho haya na kwa hakika huyu
shujaa anastahili kuenziwa na Waamerika.
Nimepita George Washington Bridge nikielekea New Jersey kutoka New
York nimeona sanamu ya Washington na farasi wake na nikaonyeshwa
sehemu alipowachenga Waingereza wakati wa vita vya ukombozi.
Lakini Washington anaenziwa kwa kile alichowafanyia wananchi wake.
Nyerere ataenziwa na hakuna awezae kuzuia hilo.
Lakini juu ya kuenziwa kwake atakumbukwa halikadhalika kwa yale aloacha
nyuma.
Jamii moja imeneemeka nyingine hohehahe na hata kuandika historia yao
walikuwa wanatishwa.
Najua hili linakuhusu.
Leo nilikwenda mazikoni makaburi ya Kisutu.
Nimefika katika kaburi la mzee wako Abdu Sykes na mwanangu ndiye aliyesoma
dua.
Pembeni yake liko kaburi la mama yetu, mkewe mama yake Kleist Bi. Mwamvua
Mrisho Mashu.
Zingatia sheria za jf ili usikumbane na lungu la Mods,
Kuniita Yericko X ni kinyume na miiko na maadili ya jf.
Kwaheshima ya jukwaa na wanaotufuatilia hapa, nakusihi ulifute hilo neno hapahapa nakuwaomba radhi wasomaji wetu kisha tusonge mbele ndugu.
Wimana,
Mvaaji ndiye ajuae wapi kiatu kinabana.
Labda nikuongezee.
Huku kwetu jeshi la polisi linachukuliwa
kama ''armed wing of the Church.''
Unajua ndugu yangu kwa hali yako kama
Mkristo hujaonja kubaguliwa.
Siku hiyo hapakuwa na maandamano hapa
Dar es Salaam kote.
Huyo alokamatwa ananihusu na ninajua mie
nikisemacho.
Hivi ni kwanini hawa watu wanakuita Jericko X? maana ake nini? ni tusi au kebehi? kama ni kinyume na kanuni kukuita hivyo basi ni bora kanuni za JF ziheshimiwe nakubaliana nawe JN!
''G.Washington ataenziwa kwa kile alichowafanyia wananchi wake, lakini Nyerere ataenziwa hilo halina ubishi'' Hapa Mohamed unakubali kuwa ataenziwa hata kama hakuna alichowafanyia wananchi wake. Logically hilo halipo. Utamuenzi vipi mtu kama hakuna alichokifanya?Jasusi,
Nilifika George Washington Memorial hapa Washington na nikaona
ile video inayoonyesha mapambano yake na Waingereza.
Nilichukua muda mrefu katika makumbusho haya na kwa hakika huyu
shujaa anastahili kuenziwa na Waamerika.
Nimepita George Washington Bridge nikielekea New Jersey kutoka New
York nimeona sanamu ya Washington na farasi wake na nikaonyeshwa
sehemu alipowachenga Waingereza wakati wa vita vya ukombozi.
Lakini Washington anaenziwa kwa kile alichowafanyia wananchi wake.
Nyerere ataenziwa na hakuna awezae kuzuia hilo.
Lakini juu ya kuenziwa kwake atakumbukwa halikadhalika kwa yale aloacha
nyuma.
Jamii moja imeneemeka nyingine hohehahe na hata kuandika historia yao
walikuwa wanatishwa
Jasusi,
Naogopa hata kusema.
Duuh!!!! Mohamed Said,24/7 unakuwa humu, sasa huko makaburini unakwenda na tablet???
"Najua hili linakuhusu.
Leo nilikwenda mazikoni makaburi ya Kisutu."
Unajua nini Mohamed? Mimi ni great admirer wa black Americans. Ukisoma historia yao, waliyopitia, jinsi walivyomudu na ku "overcome" kwa kutumia lugha yao wenyewe, there is much to admire. Imagine kama viongozi wao wangeanza kwa ku demonise George Washington, na viongozi wote wa wazungu ambao kwa hakika waliwatesa bila kiasi hawa Wamarekani weusi--kila jumapili kulikuwa na tukio la mweusi kutundikwa mtini na kunyongwa na wazungu wakishuhudia na kupiga makofi kama mojawapo ya spectacle--sijui kama juhudi zao za kugombea haki ambazo walithibitishiwa na katiba zingezaa matunda. Lakini viongozi wao, hasa Martin Luther King jr. waliwashauri waelekeze macho yao "the eye on the prize" kama walivyosema wenyewe. Badala ya kutizama nyuma waliangalia mbele. Leo, White House, ambako mweusi alikuwa ni mpishi, mfagiaji, mfungua mlango na msafisha viatu, inakaliwa na mweusi, akipigiwa saluti na watu weupe. Nadhani hapa kuna somo kwetu sote. Badala ya kutizama nyuma na kulaumu, tuangalie mbele na kujiuliza ni vipi tunaweza kulikwamua taifa letu na dhuluma ambazo kila kukicha zinaongezeka. Leo, Tanzania tumefikia mahali mtu anakamatwa, anachomwa jicho, anang'olewa jino bila ganzi na kupigwa bila sababu, na serikali haifanyi chochote. Polisi hao hao ambao tunawategemea kulinda amani wamekuwa ndio wavunjaji wakubwa wa amani yetu. Hapo ndipo tulipofika leo Watanzania.
Leo, Tanzania tumefikia mahali mtu anakamatwa, anachomwa jicho, anang'olewa jino bila ganzi na kupigwa bila sababu, na serikali haifanyi chochote. Polisi hao hao ambao tunawategemea kulinda amani wamekuwa ndio wavunjaji wakubwa wa amani yetu. Hapo ndipo tulipofika leo Watanzania.
tena umenikumbusha mkuu!Unajua nini Mohamed? Mimi ni great admirer wa black Americans. Ukisoma historia yao, waliyopitia, jinsi walivyomudu na ku "overcome" kwa kutumia lugha yao wenyewe, there is much to admire. Imagine kama viongozi wao wangeanza kwa ku demonise George Washington, na viongozi wote wa wazungu ambao kwa hakika waliwatesa bila kiasi hawa Wamarekani weusi--kila jumapili kulikuwa na tukio la mweusi kutundikwa mtini na kunyongwa na wazungu wakishuhudia na kupiga makofi kama mojawapo ya spectacle--sijui kama juhudi zao za kugombea haki ambazo walithibitishiwa na katiba zingezaa matunda. Lakini viongozi wao, hasa Martin Luther King jr. waliwashauri waelekeze macho yao "the eye on the prize" kama walivyosema wenyewe. Badala ya kutizama nyuma waliangalia mbele. Leo, White House, ambako mweusi alikuwa ni mpishi, mfagiaji, mfungua mlango na msafisha viatu, inakaliwa na mweusi, akipigiwa saluti na watu weupe. Nadhani hapa kuna somo kwetu sote. Badala ya kutizama nyuma na kulaumu, tuangalie mbele na kujiuliza ni vipi tunaweza kulikwamua taifa letu na dhuluma ambazo kila kukicha zinaongezeka. Leo, Tanzania tumefikia mahali mtu anakamatwa, anachomwa jicho, anang'olewa jino bila ganzi na kupigwa bila sababu, na serikali haifanyi chochote. Polisi hao hao ambao tunawategemea kulinda amani wamekuwa ndio wavunjaji wakubwa wa amani yetu. Hapo ndipo tulipofika leo Watanzania.
tena umenikumbusha mkuu!
huyu absalom kibanda huyu ni mkristo au muislam?
mnisamehe kwa kuuliza hilo, sijawahi kuwa na tabia ya kuuliza ila udini ulioingia sasa inabidi niulize.
UDINI ni ubaguzi wa jamii zenye imani tofauti,Tupe tafsiri ya neno udini.
UDINI ni ubaguzi wa jamii zenye imani tofauti,
na wewe naomba unipe tafsiri ya neno mfumo kristo.
embu fafanua namna huo mfumo kristo unavyofanya kazi,Kama aliofanya Nyerere kuwaweka ndani Masheikh na wengine kuwafukuza nchini.
Matunda ya mfumo kirsto mfano wake ni huu uzi.
Hapa tulipofika ni kazi ya mfumo kirsto.
embu fafanua namna huo mfumo kristo unavyofanya kazi,
Unaweza kuita huu ni Ugaidi?