Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Sawa ni la kitoto, ila naludia tena nitafutie mwislam mwenye vyeti vyake amekosa kazi kwa sababu ya dini yake.acha upotoshaji unapata faida gani kuongea uongo?

Nina mdogo wangu kamaliza chuo cha ardhi leo mwaka wa tatu hana kazi kaishapeleka CV zake Wizara ya Ujenzi hajapata kazi wale aliowaacha chuo saizi wamepata kazi hapo Wizara ya Ujenzi.
 
Sawa ni la kitoto, ila naludia tena nitafutie mwislam mwenye vyeti vyake amekosa kazi kwa sababu ya dini yake.acha upotoshaji unapata faida gani kuongea uongo?

Mgashi,

Hatutanii haya mambo ni kweli.
Itatufaa kitu gani sie kuzua uongo mzito kama huu.

Ndugu zanguni tunakusihini hebu nanyi fanyeni uchunguzi.
Mkiujua ukweli tutasaidiana kuondoa fitna hii.

Tukijaamka mambo yeshavurugika tutakuwa tumechelewa.
 
Nina mdogo wangu kamaliza chuo cha ardhi leo mwaka wa tatu hana kazi kaishapeleka CV zake Wizara ya Ujenzi hajapata kazi wale aliowaacha chuo saizi wamepata kazi hapo Wizara ya Ujenzi.

Bahati nzuri ni mdogo wako. Sasa naomba unisaidie yafuatayo:
  1. Kuna ushahidi gani kuwa kakosa hapo Wizarani kwa sababu ya Uislam wake?
  2. Kama huna ushahidi basi nakuruhusu uongee bila ushahidi (walau kwa sasa) kwa kutoa maelezo kwanini unadhani (maana huna ushahidi) kanyimwa kwa Uislam wake na hao waliopata (huna ushahidi wote ni Wakristo) wamepata kwa Ukristo wao.
 
Nina mdogo wangu kamaliza chuo cha ardhi leo mwaka wa tatu hana kazi kaishapeleka CV zake Wizara ya Ujenzi hajapata kazi wale aliowaacha chuo saizi wamepata kazi hapo Wizara ya Ujenzi.

Mimi namfahamu Kijana mmoja mtaani kwetu akiitwa Eliace aliyekaa miaka kama mitatu na nusu bila kupata kazi na alikuwa na shahada ya Computer Science. Amefariki mwaka jana hajaona Salary slip zaidi ya Temporally job za hapa na pale. Na mifano inaendelea.....!

Naomba na huyo umuingize kwenye kumbukumbu zako pia.
 

Mgashi,

Usifananishe matatizo hayo na historia ya dhulma dhidi ya Waislam.
Hivyo ni vitu viwili tofauti sana.

Athari ya ubaguzi wa dini inakwenda mbali na ni hatari zaidi.

Inawezekana wewe ni mtu muadilifu na huamini kama tuna
wabaguzi ndani ya jamii yetu.

Zungumza na Waislam na fanya utafiti wako mwenyewe bila
hofu.

Utapata ukweli.
 

Plato...

Hilo linawezekana sana lakini kweli kitu hicho ndiyo kitaondoa tatizo
la Waislam liwe halipo?
 

Magembe,

Tutazungushana sana hapa JF.

Serikali ina kila kitu kutoka kwa
Waislam juu ya matatizo haya.

Tatizo ni hofu ya kukubali hilo.

Kwao ni bora takataka ukaziweka
chini ya busati.
 

Nguruvi,

Huna haja ya kuamini utafiti huu.
Inatosha wewe ukubali kuwa ni uongo.

Muhimu kwa Waislam ni serikali ijue
hata kama na wao watasema ni uongo.

Kubwa zaidi ni Waislam ambao ndiyo waathirika
na wao wafahamu.
 
Magembe,

Tutazungushana sana hapa JF.

Serikali ina kila kitu kutoka kwa
Waislam juu ya matatizo haya.

Tatizo ni hofu ya kukubali hilo.

Kwao ni bora takataka ukaziweka
chini ya busati.


Mzee Mohamed haya umeyasema sana. Nimeuliza swali kwa specific context ya mdogo wake Ritz na nataka jibu specific na si generalization. Sasa nahotaka ni Ritz anipe majibu yangu maana kamtaja mdogo wake jambo ambalo ni zuri kwa mjadala kwa kuwa anamtaja mtu wa "nguoni mwake." Ritz nasubiri majibu.
 
Last edited by a moderator:
Nina mdogo wangu kamaliza chuo cha ardhi leo mwaka wa tatu hana kazi kaishapeleka CV zake Wizara ya Ujenzi hajapata kazi wale aliowaacha chuo saizi wamepata kazi hapo Wizara ya Ujenzi.
nimemaliza chuo cha ardhi mwaka 2009, kulikuwa na tatizo la vyeti, hivyo ilikuwa ngumu kidogo kupata ajira serikalini, hata hivyo vyeti ndo vimeanza kutolewa mwaka jana. lakini nina ushahidi wa wanzanibar tuliokuwa nao wamepata ajira wote, wengine pale pale chuo cha adhi, wengine huko kwao znz, ila pia course za chuo cha ardhi zina fursa nzuri ya kuweza kujiajiri. wengi tulivyoona ajira zinachelewa tukaamua kujiajiri wenyewe. mdogo wako alisoma course gani?
darasa letu waliopata kazi serikalini ni hao wazenji tu, wawili kwao zenji na mmoja kabaki chuo upande wa estate.
waliobaki wote wapo kwa firm au kitaa kama mimi,
 
Nina mdogo wangu kamaliza chuo cha ardhi leo mwaka wa tatu hana kazi kaishapeleka CV zake Wizara ya Ujenzi hajapata kazi wale aliowaacha chuo saizi wamepata kazi hapo Wizara ya Ujenzi.

na unafikiri hajapata kazi kwa sababu ya Uislamu wake? Mbona na miye nina mdogo wangu wa kike kamaliza kazi sasa mwaka wa nne na hajapata kazi katika fani aliyosomea (mambo ya Diplomasia) imembidi afanye kazi ya benki kama teller... sasa niseme ni sababu ya UKristu wake (maana huko alikokuwa anaomba kunaongozwa na mtu mwenye jina la Kiislamu)...
 

Mie siwezi kukusemea wewe kuhusu dada yako...mdogo wangu kaambia kabisa nyie watu wa madrasa mnamatatizo sana.
 
Nguruvi,

Huna haja ya kuamini utafiti huu.
Inatosha wewe ukubali kuwa ni uongo.

Muhimu kwa Waislam ni serikali ijue
hata kama na wao watasema ni uongo.

Kubwa zaidi ni Waislam ambao ndiyo waathirika
na wao wafahamu.


Suala siyo kuamini utafiti wako; suala ni ukweli wa utafiti huo. Utafiti hauwi kweli kwa sababu mtu kasema 'nimefanya utafiti". Unapofanya utafiti kuna njia zinazokubalika kisayansi kwa kufanya utafiti hasa wa kukusanya takwimu. Siyo kila mtu anaweza kutoa takwimu zikakubalika; ili zikubalike ni lazima ziwe zimekusanywa kwa kufuata protocol ambayo hata watu wengine wakijaribu kurudia basi waweze kupata matokeo yanayokaribiana na yale.

Kwa mfano mtu anaposema asilimia 85 ya wanafunzi wote Chuo Kikuu walikuwa Wakristu ni lazima aweze kuonesha alijuaje ni asilimia 85? Je, kama alihesabu kwenye darasa lake moja na akakuta kati ya wanafunzi 100 85 ni Wakristu (wana majina ya Kikristu) je anaweza ku-extrapolate kuwa 'kwa vile darasa langu lina wanafunzi 85 Wakristu basi Chuo kizima kina asilimia 85 ya Wakristu"? Lakini pia itabidi atuwekee kwenye utafiti wake maana yake nini anaposema "Mkristu". Je alimuasign kila mwenye "jina la Kikristu" kuwa ni Mkristu na mwenye jina la "Kiislamu" ni Muislamu? Au aliwauliza watu dini zao?

Lakini cha kushangaza - sijui kama kinashangaza kwako - mtu anasema ati "Wakristu 85% na 15% Waislamu". Hivi kweli hakuna Wahindi na watu wasio na dini yoyote au wenye imani za jadi? Kwenye pointi hii tu unaweza kuona kuwa hizo takwimu haziwezi kuwa zimefanywa na wasomi.

Kama huo utafiti ambao umeweka "Research Data" upo tuelekeze tuupate vipi ili na sisi wengine tuupitie na kuweza kuona ulivyofanya ili tukiridhika na methodology yake (na labda hata conclusion yake) tuweze kusema kweli kuna "systematic discrimination" nchini.

Mzee Said naomba utuambie huu utafiti wa "Research Data" ulifanywa na nani na upo wapi ili tupitie mtiririko mzima wa utafiti huo?
 

Ushahidi kaambiwa kabisa wakati anapeleka CV zake kaambiawa kabisa nyie watu wa madrasa mnamatatizo.

Dogo katafuta kazi online kapata Japan saizi yupo huko.

Sijui unataka ushahidi gani tena.
 
Plato...

Hilo linawezekana sana lakini kweli kitu hicho ndiyo kitaondoa tatizo
la Waislam liwe halipo?

Na lipo sio moja, kuna mengi. Lakini duara ni kubwa sana ukitaka tu-breakdown matatizo ya nchi hii kulingana
na Rangi, Dini, Kabila na eneo hutakosa la kukuunga mkono.

Tuseme hivi:
Hakika Wahindi na Waarabu katika nchi wana afueni sana, lakini Wamatumbi kama sisi wengi wetu dhoofu hali.
Walioko jela wengi weusi, wanaokula mlo mmoja tu kwa siku wengi weusi n.k n.k.

Waislam wengi tu (Ismailia, Bohora) wana afueni na mambo yao Alhamdulillah yamewanyookea kwenye Elimu na hali. Lakini Waislam wa Kilwa, Rufiji, Kisarawe hali si hali. Halafu rudi kwa Waislam wa Machame mambo yao si mabaya kulinganisha na hao wengine ingawa si mazuri sana kama Ismailia/Bohora!

Njoo kwenye kanda, Kusini si bora sana Kielimu na Kiuchumi kuliko Kaskazini na Nyanda za juu kusini. Lakini hapohapo Kaskazini Manyara wako nyuma kuliko Arusha na Kilimanjaro. Hata mkoa wa Kilimanjaro, Moshi iko mbele kuliko Same.

Unataka na makabila?
Wanyakyusa wako vizuri kielimu kuliko Wagogo. Lakini Wanyakyusa wa Rungwe wako vizuri zaidi ya wale wa Chunya!

Sasa Humo kwa Weusi utakuta Wakristo, Waislam, Wachaga, Wanyakyusa, Wasukuma n.k.
Kwa Kanda utakuta Weusi, Weupe, Wakristo ,Waislam, Wasukuma, Wadengereko n.k
Kwenye dini utakuta kuna Weupe, Weusi, Wasukuma, Wachaga , Wadengereko nk n.k
Na kwenye kabila Hao woote juu pia wamo.

Ndio maana nakushauri toka kwenye hiyo level nenda level ya juu zaidi. Hata miongoni mwa watoto wa familia moja kuna tofauti itakuwa Taifa?
Yatazame matatizo ya Nchi hii kwa upana wake utagundua mengi na hapana shaka tutatoka hapa tulipo kama Taifa.
 

Mkuu inatakiwa uzame sana katiks historia uitambue historia ya Vatican.

Vatican city ni nchi iliyondanu ya Nchi kamili iitwayo Italia,

Inatambuliwa na umoja wa mataifa na inabalozi wake katika umoja huo, vivyo hivyo ina balozi zake karibu kila nchi duniani.

Rejea mkataba wa mwaka 1929 ulioitambua rasmi kuwa vatican city.

Papa ni mkuu wa Vatican City na ni mkuu wa kanisa katoliki duniani
 
Miye dadangu alisema kaambiwa ati "Nyie Wakristu muda wenu umepita sasa ni zamu yetu"...

Hakuna aliyekukatalia kumbe sasa kuna tatizo la udini serikalini nashukuru kusikia hayo maneno kutoka kwako zamu ya Wakirsto imeishapita baada ya kuwekwa na Nyerere.
 
Ushahidi kaambiwa kabisa wakati anapeleka CV zake kaambiawa kabisa nyie watu wa madrasa mnamatatizo.

Dogo katafuta kazi online kapata Japan saizi yupo huko.

Sijui unataka ushahidi gani tena.
uongo ni dhambi
kwenye CV aliweka dini yake?
 
Hata wewe binafsi kuna nyakati umejaribiwa kukiri au kusema usichokiamini usembuse kutoka kwa huyo anayekuhusu?
boKwamba siku hiyo hakukuwa na ri, wataka kutuaminisha kuwa matamshi na hamasa za kuandamana Polisi walizitungae na kujipa kazi ya kuwakamata, vyombo vya habari-Tv na magazeyi zilionyesha picha za maktaba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…