Mohamed Said,
Nashukuru kwa kunifahamisha kisa hiki.
Ritz,
Unataka kumjua Judith Listowel.
Tuanze na cheo chake.
Huyu anaitwa Lady Judith Listowel.
Alikuwa mke wa Listowel ambae alikuwa gavana Ghana.
Huyu mama alikuwa ''entertainer'' wakati wa ujana wake na aliachana na
mambo haya alipoolewa na huyu Listowel ambae alilkuwa anatoka katika
koo za juu ''upper class'' za Kiingereza.
Judith Listowel asingelimjua Ally Sykes ila alipojulishwa kwake na Peter
Colmore.
Ally Sykes na Peter Colmore ''two of a kind'' wana kisa kirefu.
Nina makala nzima kuhusu watu hawa ukipenda naweza kukuwekea hapa.
Mie nikimjua Colmore toka utoto wangu kwa kuwa ofisi yake ya Dar es Salaam
ilikuwa nyumba ya tatu kutoka kwetu.
Akija kutoka Nairobi alikuwa pale.
Ilikuwa ni nyumba yake cum office.
Ally Sykes na Peter Colmore walikuwa marafiki toka 1942 wakiwa watoto kabisa
Nairobi na wakaja kufanya biashara pamoja na wote wakatajirika kufru kiasi Peter
Colmore aliwezakununua ndege yake binafsi na Rolls Royce Nairobi katikia miaka ya
1950.
Ally Sykes haitaji maelezo anafahamika.
Lady Judith Listowel alipotaka kuandika kitabu chake ''The Making of Tanganyika''
Listowel akendaNairobi kwa Colmore na Colmore akamuagiza kwa Ally Sykes Dar es
Salaam.
Hii ilikuwa 1962.
Nina mdogo wangu wakati huo ana miaka 8 yeye alimwona Judith Listowel kwa
macho yake mwenyewe na anasema alinipa hela na akafanya kituko kidogo.
Alikudua nguo mbele yake akatoa fedha katika nguo yake ya ndani.
Huyu mdogo wangu anasema alishtuka lakini Lstowel akamwabia asiogope.
Listowel alipokuwa Dar es Salaam akifanya utafiti wake mwenyeji wake alikuwa
Ally Sykes na Ally Sykes ndiye akimzungusha na gari yake huko na huko.
Binafsi nimesoma barua za mkono ambazo Listowel alimwandikia Ally Sykes akimuuliza
kuhusu hili na lile katika historia ya Tanganyika.
Abdu Sykes alipokutana na Listowel nyumbani kwake Magomeni Mikumi Abdu hakufunguka
kuhusu mchango wake katika kuasisi TANU.
Kisa nini?
Kisa kilikuwa Abdu na Kleruu walipokuwa wanaandika historia ya TANU baada ya uihuru
palitokea msuguano kidogo kwa kuwa Nyerere hakupenda historia ya TANU ianze nyuma
yake na kuasisiwa kwa African Association 1929.
Abdu hakusema lolote la maana kwa Listowel katika utafiti ule.
Nadhani haya yanatosha.