Rudi kinyumenyume:
Kwamba ratio vyuoni ikoje kati ya Waislam na Wakristo
Sekondari ratio ikoje na shule ya Msingi ration ikoje
Halafu unakuja huku uraiani kwenye maeneo yenye Waislam wengi (Pwani, Lindi, mtwara, Tanga, Kigoma)
mwamko ukoje kuhusu Elimu, vipi kuhusu shule za Seminari za Kiislam zipo kwenye hali gani.
Tena nenda hatua moja zaidi linganisha Maua Seminary, Marian girls, St Anthony nk nk ziko kwenye hali
gani na kina nani wana watoto huko.
Unaweza kuchepuka kidogo ukaangalia pia Wachaga, Wahaya, Wanyakyusa kule wanapotoka na mwamko wao
kwenye Elimu halafu piga hesabu mumo ratio ikoje kwa Waislam na Wakristo.
Halafu mbona umechagua nafasi za appointment. Hujafikiria pia madaktari. Nenda Muhimbili utafute akina Kimario
Edward, Swai John, Mwakingwe nk uone wako wangapi halafu linganisha idadi yao na akina Pazi nk.
Au na kwenye udaktari kuna Waislam wananyimwa fursa ya kutibu watu na uhaba woote wa madaktari nchi hii?
Tuambie nani huyo anawanyima watanzania fursa ya kupata matibabu tumlaani.