Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Ulikuwa umeishawahi kusikia habari za hawa wazee, Sheikh Suleiman Takadir, Mzee Fundi Muhindi, Idd Tosiri, Idd Faiz, Dr William Mwanyisi, Dr Vedasto Kyaruzi, Stephen Mhando, Dossa Aziz, Ally Sykes, H.K. Viran, Liwali Juma, Abdulkarim Karimjee, George Magembe, Erikah Fiah, Mufti Sheik Hassan Bin Amir, Jumbe Tambaza,Mshume Kiyate, Rajabu Diwani, Makisi Mbwana, Sheikh Haidari Mwinyimvua, Tewa S Tewa, Denis Phombeah, Dome Okochi, Patrick Aoko, John Rupia, Joseph Kimalando.

Wapo wengi sana hawa wote ni watu wa kutunga.
 
Hawa ni mashujaa waliotanguliza utanganyika wakafanya kazi na watanganyika wenzao bila kujali tofauti ya dini wakafanikiwa kuuleta uhuru. Akaja Mohamed Said na uovu wake akawavisha joho la uislam kwa masilahi yake binafsi akawapamba na kuwapandikiza maneno na chuki dhidi ya shujaa mwenzao Nyerere, ati kwa kuwa maiti/marehemu hana kauri. Mohamed akatumia majina ya wazee hawa kuwachochea watu wasiofikiri kama Ritz ili wawachukie watanzania wenzao kwa misingi ya dini.
 
Duh! Ritz, lazima utakuwa unatania! unamaana serikali hii inayoundwa na chama chako kitukufu cha CCM chini ya ustaadh Jakaya Mrisho Kikwete!

Baada ya kupatikana uhuru kilichofuatia ni kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa Mashekh waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa Nyerere.

Miongoni mwao waliokamatwa ni Abdillah Schneider Plantan, Sheikh Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Hassan bin Amir, Shariff Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba, Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela, Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar, Abdalah Mwamba, Sheikh Hashim Haji, Sheikh Nurdin Hussein, Salum Abdallah Popo, Sheikh Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Mafta, Rajabu Kiguu, na wengine wengi.

Halafu mnataka Waislam wamuite Nyerere baba wa taifa.
 
Hapana Ritz, kama ni swali muulize hili; Kusema kweli sasa tumechoka na porojo, hadithi na histohisia, tunataka solution..."way forward" kuondokana na hiyo kadhia...

Mag3,

Umechoka wewe na nani? Kama mmechoka kaeni pembeni kuna watu zaidi ya 90,000+ wanaofuatilia huu munakasha wewe ni nani JF?

Wewe tumishakuzoea juzi ulisema kuwataja hawa wazee wa Kariakoo kwako ni matusi makubwa.

Sasa unalia lia nini eti umechoka kama umechoka sisi tufanyaje tukubebe?
 
Last edited by a moderator:

Hao waliotofautiana na Nyerere kina Kamaliza, Kambona na wengineo mbona wana majina ya Kizungu (nadhani labda ni Wakristo kwa jinsi tunavyochukul;iana siku hizi).

Ni watu wenye low understanding na wenye kutukuza udini tu ndio wanaoweza kukaa na kuandika Vitabu kuchunguza Makabila na Dini za watu ili kutafuta sababu za kutukuza dini na makabila yao kwa manufaa ya waliowatuma.
 
Kwani walisingiziwa?
 

Nadhani Kambona na Kamaliza walikuwa WaKristo (kwa jinsi tunavyochukuliana siku hizi kupitia majina ya kizungu kuwakilisha Wakristo na ya Kiarabu kuwakilisha Waislamu) walitofautiana sana tu na Nyerere.

Huyo 'mwanahistoria' mwenye mawazo ya chini sana ambaye unataka aje kuandika kuhusu udini na kabila la Nyerere ili kumtweza atabaki Mohammed Said tu. Kama wataibuka wengine labda itakuwa kujaribu kuupinga upotoshaji wa Sheikh Said kama alivyofanya Yeriko Nyerere.
 
Waulize watu wa usalama wa taifa, ukishindwa muulize mzee chauchochezi Mohamed Said mmanyema.

Hawa wazee kwako hawana hadhi yeyote lazima utoe majibu hayo bahati nzuri watu wanatusoma.
 

Wimana,

Hiyo nukuu ya ''fear'' nadhani huyo ni Kwame Nkrumah.
 

kwenye red mambo gani???
 

Winama,

Kwa hakika kitabu changu si cha kubezwa kwa walokisoma kila
mmoja kimemuathir sana.

The East African walifanya ''serialisation'' mara tatu kuanzia wiki
ya pili ya December 1998.

John Iliffe na James Brenan wanahistoria na waandishi maarufu
wamekifanyia ''reviews'' katika Cambridge Journal of African History.

Baada ya kitabu hiki nimezungumza Vyuo Vikuu vya Johannesburg,
Ibadan, Kenyatta, Zanzibar University, Ohio, Northwestern nimealikwa
Islamic Propagation Centre International Durban, Zentrum Moderner
Orient (ZMO), Berlin, Ujerumani na kwingi tu humu nchini.

Kitabu hiki hivi sasa kinasomeshwa vyuo vingi vinavyofunza history ya
Africa Ulaya na Marekani.

Kitabu hiki kinakwenda sasa toleo la tatu.

Hiki kitabu kingelikuwa cha kipuuzi kisingepata haya yote na kingelikufa
zamani.

Winama,

Nakuhahakikishia ndugu yangu mimi sina sababu ya kusema uongo haya
yote niliyoandika ni kweli tupu.

Lakini uamuzi ni wako bora umenisoma na ukajua kuwa walikuwapo mashujaa
na wazalendo ambao wewe kabla ya kunisoma hukubahatika kuwasoma popote.

Hili kwangu linatosha sana.
 
Zanzibar nako kuna mfumo gani vile?
Usiwaguse wazanzibari watakutoa macho!

Kabla Nyerere hajaingia Zanzibar wazanzibari walikua wamepiga hatua kimaendeleo kushinda nchi zote za Afrika mashariki.
Ndio wa kwanza kuwa na Train.
Ndio wa kwanza kuwa na umeme.
Ndio wa kwanza kuwa na State TV
Ndio wa kwanza kupata rubani wa Boeing na mara ya kwanza kutua gulf Air Zanzibar abiria walipatwa na mshangao kusikia rubani alipokaribia kutua akiongea kiswahili fasaha.
Kuna mengi tu ambayo wazanzibari walitupita watanganyika lakini wivu wa Nyerere na mfumo wake akaihujumu Zanzibar.
 

Gwalihenzi,

Unanionea bure.
nilichofanya ni kuandika yale yalotokea.

Sina uwezo wa kumchochea yeyote.
 
Mzee ms,
Umekuwa kila ukiulizwa ukiilejea mifano hiyo hiyo na kusema ni mifano michache kama ya oic na ujenzi wa chuo.
Tupe na madhila mengine c kuludia mifano hiyo hiyo kila siku.

Mgashi,
Narudia majibu kwa kuwa maswali nayo ni hayo hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…