Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Tulia, nenda taratibu...au umechoka? Kutetea uongo hakika kunachosha. Umeonaje hizo namba hapo juu? Uzuri wa hesabu ni kuwa hakuna kudanganya hapo na hakuna porojo kama hizi unazotaka kuzileta. Wanaofuatilia huu mjadala wanajua ninavyotetea utaifa badala ya udini na mashambulizi yangu yote yameelekezwa kwa waongo, wazushi na wachochezi bila kuangalia imani zao. Naamini yaliyoandikwa humu hatatokea mtu ayafute, yapo na yataendelea kuwapo ili siku zijazo wenye kutaka kujua yaliyoongelewa wasisubiri simulizi za barazani, hapana, waingie humu wayasome kwa macho yao. Pumzika kijana.

Hata hivyo naona mengi yamesemwa kuhusu vurugu za Mwembechai mwaka 1998 wakati wa Benjamin Mkapa na mwalimu wako Mohamed Said amekuwa akiyarudia mara kibao akimnukuu Prof. Njozi. Je unaweza kuniambia kwa nini hataji chanzo cha vurugu hizo kuwa maandamano ya waumini wakidai uchunguzi wa yaliyotokea Mwembechai mwaka 1993 wakati wa Hasan Mwinyi ambapo pia waumini wa Kiislaam walipoteza maisha. Kwa nini hataji tofauti za wenyewe kwa wenyewe zilizosababisha vurugu kutokea? Mzee Rukhsa anarukwa huku hata jina lenyewe la Rukhsa lilitokana na matamshi yake wakati huo?
 

Ritz, kwa kweli binafsi napenda kitabu hiki kisomwe; tena ningekuwa na uwezo hata ningewanunulia watu wengine. Sijui kama umekisoma au la lakini kama umekisoma - kama mimi nilivyofanya - utaona kuwa ni kitabu ambacho kinapaswa kusomwa na kila Mtanzania kwani kinaelezea vizuri ni jinsi gani madaia ya "dhulma" dhihdi ya Waislamu yalivyoanzishwa, kutetewa na kuendelezwa kwa miongo mitatu sasa.

Lakini kuna sababu nyingine kwanini kitabu hiki kinapaswa kusomwa na kila Mtanzania - kinadokeza michango ya watu mbalimbali katika harakati za Uhuru. Kuna watu wengi ambao Mohammed SAid anawataja (wengine wametajwa na wengine) ambao kwa kweli tusingeweza kuwafahamu bila yeye kuwataja. Watu hawa kwa kiasi wametudokeza kwa umakini mkubwa jinsi Nyerere alivyopendwa, kuheshimiwa na Waislamu na Watanganyika wengine wakati wote wa uhuru. Hii inanipa sasababu ya tatu.

Kitabu hiki kingeweza kuitwa "Nyerere - Shujaa kati ya Mashujaa" au "Nyerere - Rafiki wa Waislamu" na bado kingekuwa kweli. Kitabu hiki kinamuonesha Nyerere kama kiongozi makini, mtu thabbiti kimaamuzi na mwenye uwezo wa kuongoza ambao mfano wake haujatokea bado. Ukisoma kitabu hiki utaona mara moja kuwa Nyerere HAJAWAHI kuwa na tatizo na Waislamu, hajawahi kusema jambo lolote mbele ya umma au hata kwa watu wake wa karibu ambalo lilimuonesha kwenye mtazamo mbaya dhidi ya Waislamu.

Kwa wale wasiojua kitabu kinathibitisha kitu ambacho Nyerere amekuwa nacho toka utoto - urafiki wa karibu wa Waislamu. Rafiki yake wa utotoni - wakati Nyerere hata hajawa Mkristu Mkatoliki bado - alikuwa ni Muislamu na huyu ndiye alieacha impression kubwa kwa Mwalimu naamini. Ndio maana Nyerere hakuwa na shida kabisa ya kuwaamini Waislamu, kuchanganyika nao na kupatana nao. Wengi wanafikiria Nyerere alikutana na Waislamu alipokuja Dar kwa mara ya kwanza!
 
Therefore, there is absolutely no shred of truth in his assertions and claims?
nkungu, a house without foundation? Sounds silly, right? Nobody I know who is worth their salt as a contractor or builder would build any structure without a foundation!
 
Last edited by a moderator:
Therefore, there is absolutely no shred of truth in his assertions and claims?

None whatsover, once you make up statistics or you fake them you can not claim any credible conclusions based on those statistics. Hakuna dhulma dhidi ya Waislamu. Labda utuambie - kama unaamini ipo dhulma - ushahidi wake ni nini?
 
Kama Umma mkubwa wa waislam uko nje ya BAKWATA ambayo inakutana na wakrsito kusuluhisha mgogoro huu, basi tutegemee vurugu na baadaye vita nchini kwetu.
Nkungu, hii ni moja ya sababu ambazo 100K wapo hapa kusoma. Mohamed anaongea kama yeye ndiye waislam. Mohamed hana statitistic za kuthibitisha madai yake.

Kama umemsoma vizuri yeye ni mmoja wa vinara wanaoleta tension kati ya waislam na Wakristo.
Anaongea mawazo yake na kusema hayo ndiyo mawazo ya waislam!
Hapo amesema waislam hawawaikubali BAKWATA alitakiwa alete proof ya hilo kwanza.

Nafahamu hana proof kwasababu mtu aliyeshindwa kutete data za research zake ambazo ni nusu ukurusa hawezi kuja na reasonable and sound proof ya madai kuhusu waislam. Ninakuhakikishia hawezi.

Mtu aliyesimama kuhubiri data za kupika na za uongo kwa miaka 15 hana credibility au moral authority ya kuongea kuhusu watu wangapi ni BAKWATA na wangapi siyo, wangapi mapagani na wangapi makafir. Credibility haimpi fursa hiyo

Mwaka 1981 alisema Warsha ilifanikiwa kuleta mapinduzi ndani ya Bakwata.
Katika old guards aliyebaki alikuwa ni Adam Nasibu. Mwaka 1982 anatumbia Bakwata ilikuwa na nguvu sana.

Licha ya kuchanganya hadithi ni lazima watu wajiulize hawa warsha waliweza vipi kushindwa tena na Bakwata ikiwa Bakwata haikuungwa mokono na wengi!!

Hivi vikundi unavyosikia ni ''wengi'' ni vya watu wachache. Leo hii kuna vikundi vinavyafanya kazi katika mitaa.
Utasikia kamati ya haki, kamati ya mali, n.k. Kwa maneno mengine hata katika vikundi husika bado hawakubaliani.
Kwa ujumla ni kuwa hakujawa na organaizesheni unayoweza kusema ni true representative katika hao wengi wa Mohamed.

Kama ipo, Mohamed asimame hapa na kusema ni ipi hiyo.
Kwa vile ameshasema Bakwata haitakiwi na waislam(na wala sina sababu za kuitetea) basi atueleze ni taasisi gani inayoweza kusimama kama mwamvuli wa vikundi vyote nje ya Bakwata?

Lakini swali muhimu sana ni kuwa kama Bakwata ambao hawana wafuasi kwa mujibu wa Mo wanatafuta maridhiano na wenzao wakristo, je hilo ni sahihi au la! na kwanini.
Tunauliza haya kwasababu ndiyo mambo muhimu sana katika kuleta mustakabali wa taifa.

Mustakaabli haupatikani pale wengine wanaona wenzao ni enemy na kuhubiri chuki katika kivuli cha uongo na uzushi.

Hizi tension za kwamba kuna ugomvi wa waislam na wakristo zinachagizwa na vikundi vya watu fulani.
Angalia familia, majirani na ndugu wa Tanzania halafu jiulize lini watu hao wamefarakana kwasababu tu ya tofauti zao za dini.

Hata hivyo kuacha makundi haya yaeneze uongo na uzushi kuna pelekea hali hiyo kutokea.
Ni kwa sababu hizo, watanzania kwa umoja wao wasimame na kukemea wahuni wanaotumia dini katika kutafuta uluwa wao wawe wakristo, waislam, budha au wajadi.
 
Mwanakijiji,
I am glad you mentioned Dau. Firstly I hear he is Mohamed's financier and secondly I hear he is implementing at NSSF an Islamization policy, i.e. no hiring of Christians there.
 
Ntamahalo,

Nilipokuwa katika teens nikipenda kuimba nyimbo za wakati wangu.

Kulikuwa na nyimbo moja ''Have You Heard the News?''
Elvis Presley.

Unazo taarifa?
Tumegonga 100,000.

Wanafata nini hapa?

nimegundua kuwa tunajadili na mtu asiyeelewa. Hivi wewe kwa mawazo yako unadhani kwa nini views zimefika 100,000?
1. je ni kazi yako nzuri wamevutiwa nayo?
2. Je ni kuvutiwa na uchambuzi wa Yericko Nyerere ambaye kwa kiasi kikubwa anakuumbua kwa kupindisha historia ya Tanganyika +Zanzibar =Tanzania?
3. Wachangiaji waliowengi kwnye uzi huu wako upande wako au wa mleta mada?

nijibu haya, na wengine pia mnaweza kuyajibu hayo maswali ili kumsaidia kuelewa huyu Improper Islamist
 

wewe nawe bingwa wa nini hapo kwenye red?
 
Mohamed Said tunaomba kitabu chako chapisho la nne,ufanye marekebisho,mtu mzima kula"humble pie"is not a crime.
it is quite evident maybe unknowingly kitabu kina one two many errors.Do justice to your adopted country kabla natives hawaja ku skin alive
 
Last edited by a moderator:

Mag3,

Una lolote la maana unachekesha sana unataka kuwasemea wafuatiliaji wa huu uzi huwezi kuwashikia akili kaa kimya kinachokusumbua wewe ni husda na chuki dhidi ya Uislam na Waislam.

Waislam tunakusoma na tumeona kejeli na dhihaka zako unasema mashambulizi yako mpaka unatukana unatetea utaifa uangalii imani ya mtu.

Kusema kuwa Mohamed Said kuwataja Wazee wa Kiislam wa Kariakoo kwako ni matusi makubwa hapa unatetea utaifa upi kwa nini upendi hawa wazee watajwa kama siyo dini yao? kuwatukana hawa Wazee kwako siyo tatizo ebu jichunguze kila unachokiandika wanaokuunga mkono ni Wakirsto wenzako jiulize kwa nini.

Halafu mimi nafurahi sana unavyoangaika na muuza kahawa kama mimi mwenye elimu ya madrasa anavyokushughulisha kuanza kuhesabu posts zake...haa haaa haa.

Hesabu na Like zangu usije kusahau.

Wewe ni mmoja kati ya maadui wakubwa wa Uislam michango yako ndiyo imekuweka uchi kazi kwako kuchutama au kukimbia.
 
Mwanakijiji,
I am glad you mentioned Dau. Firstly I hear he is Mohamed's financier and secondly I hear he is implementing at NSSF and Islamization policy, i.e. no hiring of Christians there.

I once heard such allegations against Dr. Dau. Zitto Kabwe akiwa mwenyekiti wa kamati ya POAC, alikuta DAU anaikopesha serikali ya J.K MABILIONI ya fedha za wavuja jasho bila kuwa na mkataba maalum wa namna ya kuzirejesha. Akawaambia waandae mikataba hiyo, kilichofuatia ni kamati yake kupigwa stop, kwani kwa jicho la ndani, imeingilia harakati za ISLAMIZATION POLICY in a country.
 

Mzee Mwanakijiji,

Nafasi ni yenu sasa bahati nzuri wewe na wenzako ni waandishi wazuri sana jikusanyeni Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mag3, Jasusi, na wengine ambao mtawaona wanafaa muandike kitabu mkiite hayo majina "Nyerere ni Shujaa kati ya Mashujaa" au "Nyerere Rafiki wa Waislam"

Mkifanya ivyo nadhani mtamnyamazisha kabisa Mohamed Said na kitabu chake.

Anzeni huo mchakato sasa hivi.
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa naamanisha South African Indian, Sheikh Ahmed
Deedat.
Makosa ya aina hii huwa yanfaywa na kila muandishi na kila msemaji.Lakini kwa watu wa mfumo akifanya Mohammed Said wanakuwa wamepatia sehemu ya kuikandamiza historia halisi ya Tanzania na kutaka ionekane eti ni ngano.
 
Wewe Mwanakijiji ni mgumu sana kuelewa na kurudi nyuma katika uadui na uzushi wako.
Ndio maana tumesema huu uzi umekuwa mrefu bila sababu kwa vile kila wakati unataka upewe jibu la zamani.
Tumekwambia na kukunakilia sehemu Nyerere alipokuwa na ugomvi na waislamu mpaka ikabidi alie.
Dalili ya ugomvi ni nini kama si kulia mwishowe?.
Sifa yako ni mwindaji mzuri sana na mdowezi asiyekata tamaa utadhani fisi.
Fisi ni mara chache sana kupotea moja kwa moja anaposhindwa kunyang'anyiana mzoga na Simba.
 
Makosa ya aina hii huwa yanfaywa na kila muandishi na kila msemaji.Lakini kwa watu wa mfumo akifanya Mohammed Said wanakuwa wamepatia sehemu ya kuikandamiza historia halisi ya Tanzania na kutaka ionekane eti ni ngano.

Correction hakufukuzwa... Aliondoka mwenyewe

When Sheikh Deedat left the country he left Christianity dented and confidence amongMuslims on their religion strengthened.

Nikweli makosa yanatokea kwa kila mwandishi, kitu kikubwa ni mwandishi kukiri kama amekosea na kurekebisha alipokosea.
 
Hilo hawatoweza inshaAllah na nafasi ya kufanya hivyo haipo.Wangefanya kabla ya chapisho ya la historia ya Mohammed Said ingekuwa na mantiki lakini wakifanya sasa hivyo vizazi wanavyotaka kuvibadili fikra watawacheka kwani watajua kwamba ni sarakasi tu.
Wanachoweza kufanya kwa nionavyo mimi ni hapo baadae kuitisha maandamano yatakayolindwa na polisi eti kulaani kitabu cha The life and Times of Abdulwaheed Sykes,author Mohammed Said.

Walipotaka kufungia radio imani kila jambo hapa JF likitokea basi wanalaumiwa hao radio mwishowe wakafungia.Na sasa kila waislamu wakijitetea kwa dhulma wanazofanyiwa inaelezwa kuwa chanzo ni historia ya Mohammed Said.Hii ni kama kwamba waislamu ni mazezeta sana wa kuona dhulma.
Kazi aliyofanya Mohammed inajitegemea na naamini sio kama wanavyosaema watu wa mfumo,hakuwa na lengo la kumchochea yeyote.Isipokuwa tu waislamu wamepata nguvu kuona dhulma dhidi yao ni za maksudi baada ya kusoma matukio ya kihistoria ya kweli aliyoandika bwana Mohammmed.Hivyo ni uwiyano ndiio uliowapa waislamu nguvu kujitetea jambo ambalo sasa watu wa mfumo wameona kwanza wavuruge historia ili dhulma zao ziendeleea kirahisi.
Kwa uwezao wa Allah hili halitorudi nyuma.
 
Mkuu Ritz
Sina uhakika na takwimu sahihi za Ratio ya waislamu na wakristo kwenye mawizara lakini kweli nameobserve kwa haraka haraka kwenye sehemu nyingi makazini (both private and Public sector) wakristo wengi sana kulingana na waislamu.

But hii inamaanisha kuwa kweli ilikuwa systematic plan ya kuwajaza wakristo makazini?

Inamana haiwezekani pia ikawa hii ni matokeo ya sababu nyingine lukuki zisizo zakupangwa ambazo kwa njia moja au nyingine matokeo yake ndo haya.

Mfano hivi wakristo wakisema Zanzibar kuna mfumo Muslim ambao uko systematic kusuppress wakristo kwakutumia kigezo cha Ratio ya kila eneo waislamu kwa wakristo ni 3:1, kuanzia Uongozi, serikalini, mpka idadi ya wakazi.

Waarabu-watanzania wa hapa tanzania, 95% ni waislamu, ingawa wao ni minority katika nchi lakini ni matajiri sana kulingana na watanzania wengi, na wakitaka kuwapeleka watoto wao shule sehemu yoyotr dunia wanaweza...

Hata wahindi-watanzania wengi hapa tanzania ni wahindi waislamu, na 90% ni well off.

Je mbona hawa pia idadi yao ni ndogo sana mawizarani and yet wao ndo wanashikiria uchumi wa nchi and infact wao pia wanaendeshs hii nchi kwasababu wanapower kubwa ya kuinfluence policy ya nchi hii. ?

Umewataja masheikh walikamatwa na Nyerere, lakini na mimi nauliza je kulikuwa hakuna wakristu pia waliokamatwa katika kipindi hiko? Au utaniambia walikamatwa kuzuga tu ili isionekane ni mpango wa kuwakandamiza waislamu.

Je Nyerere aliwakamata hao Masheikh bila ya sababu? Je kams alikuwa na sababu inamana we unaona sababu ya Nyerere haina mashiko ila ya Masheikh ndo inamashiko?

Nashindwa kuelewa inakuwaje Nyerere huyu mnaesema alikuwa anatatizo na waislamu kiasi akaanza mkakati kuwakandamiza, kuchagua waziri wake wa Mambo ya ndani (kama sijakosea) muislamu ambaye baadae akaja kuwa Raisi wa inchi tena baada ya kuwa Raisi wa ZNZ.

Kwa jinsi picha nayopata ya huyo Nyerere mlivyomdisplay inamana alikuwa na nguvu kiasi kwamba angetaka Mwinyi asingekuwa Raisi, na wasingefanya lolote..

Lakini akakubali the Most Powerful person kwenye nchi awe Muislamu, mmoja ya wale wale ambao ameweka mkakati kuwakandamiza na kuhakikisha wanabakia second class citizen...

Haikuishia hapo bado aka wamentor na kuwaweka undet his wings vijana wengie wakislamu ambao wengi wao currently ndo viongozi waandamizi wa nchi...

Huyu huyu Nyerere ambaye anatatizo na waislamu ambaye mnasema ni mdini na mcatholic kwanza kabla ya yote, akakubali kuingia compromise kuwatosa Wayahudi kwa kusupport taifa la waislamu tupu Palestina...

Haikuishia hapo,
Sasa hivi viongozi waandamizi karibia wote ni waislamu, with the Most Powerful person kwenye inchi hii Raisi, hadi Mkuu wa usalama wa Taifa ni muislamu, unafikiri wajasikia kama kuna kundi la waislamu (kwassbbu haiwezekani ikawa waislamu wote kama watu Bakwata tu hawajumuishwi kwenye waislamu) linalolalamika kuna systematic dhulma against waislamu? Mbona bado mnalalamika mnaonewa, mnakandamizwa. Kams kweli kipo kweli waislamu wote hawa si wangefuta huu mtandao once and for all.

Haya matatizo kwenye mfumo yapo nchi kwetu, inatakiwa kama nchi tuyaadress na kutafuta ufumbuzi.

Lakini ukiyaangalia kikundi zaidi, hatutafika kokote na atutapata kwasababu kwenye ubishani wa imani hakuna mshindi kamwe.

Waislamu wanatakiwa wajiassemble na kukaa chini, waadress matatizo yso within wao kwao bila ya kupoint finga kwa dini nyingine ndo sababu ya matatizo yao,(kwasababu dini nyingine haitakubali kama wao ndo sababu ya hayo matatizo ambapo watarudi kwenye mabisho tena ambayo hayana mwisho) then watafute ufumbuzi wa hayo matatizo. Wafanye mikakati kama kujenga shule zaidi za kiislamu, vyuo, mahospitali na kila kitu, uone kama kuna mtu atawasumbua.

Kama wahindi wanavyofanya, wao wametengeneza kanchi kao ndani ya Tanzania ambapo wanajitegemea kwa kila kitu, wanashule zao, hospitali zao, misikiti yao, vyuo vyao, nk.

Pia nahaidi kuvitafuta vitabu Smith. P. Fr. Sivalon. J, Bergen Jan Pvan hivi nipate undani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…