Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

 
 

Jasusi,

Mbona wengi tumesoma shule hizo si ndiyo Waingereza
wakishirikiana na Wamishionari katika elimu?

Sasa tungesoma wapi wakati shule ndiyo hizo za serikali
na misheni?

Si jambo la kushangaza.

Nimepata kuandika paper kuhusu matatizo ya elimu kwa Waislam wa
Tanzania: TheQuestion of Muslim Stagnation in Education in Tanzania
- A Muslim Riddle
(Paper presented at the Conference of the Global
World of the Swahili
Intercultural Dialoguemon the Indian Ocean Zanzibar,
February 20 - 23, 2003).


NB: Nimeshangazwa jana kuna mtu kaniletea link na nimeiona hii paper ikinasibishwa
na BBC.j
 
Tawire baba! Mohamed amelenga kuwa na Bosnia na Herzegovina, Nigeria na Somalia. Yeye anasimulia hazina zilizoachwa wakati anataka kurithisha kizazi maafa.

Imesemwa katika hadithi za dini kuwa katika shughuli ngumu kufanya ni biashara kwasababu punje moja katika pishi ya mchele inaweza kukutia matatani. Inasemwa mizani iwe ya haki.Ni biashara ndiyo ugumu wa biashara!
 
WC,

Unataka tubishane kwa kitu ambacho waliasisi wazee wangu
na mie kuijua historia yake?

Hivi wewe utaijua AA kuliko mimi mjukuu wa waasisi hawa?
Hivi wewe utaujua undani wa TANU kunishinda?

Huo ni muhali.
Mohamed Said, nani anakupa mamlaka ya kumiliki "historical knowledge"? kwanini uamini kuwa wewe ni mtu pekee mwenye uwezo na akili ya kufahamu historia ya AA na TANU ati kwa sababu wazee wako walihusika?Nakusihi acha kiburi na majivuno ya jinsi hiyo!
 
Mzee Mwanakijiji;5976827]Historia - na ulinukuu maneno ya Sykes huko nyuma - akisema TANU iliasisiwa 1954.
Tena akasema ''.......I was one of the founder of TANU 1954''hakusema founder of TANU mwaka 1948 au mwingine. Abdul Sykes hakuwa mjinga wa kutaja mwaka! alimaanisha alichokusudia akifahamu kuwa historia ndivyo ilivyokuwa na yeye hakuwa na uwezo wa kuibadili isipokuwa itajieleza yenyewe Ni historia hiyo anayoieleza Mohamed ndiyo ismeayo kuwa kulikuwa na mhausiano ya vyama vya kisiasa vya Tanganyika na Zanzibar kuanzia zama za AA. Hii kama tutaifanya Mohamed itakavyo basi yupo atakayeandika kuwa muungano wa mwaka 1964 ulianza miaka ya 1940 na kwamba CCM ambayo ni zao la TANU na ASP nayo ilianza miaka ya 1930. Hapo ni laghai tu kwenda kwa mbele. Sidhani kama utaeleweka maana utakuwa umeondoa dhana nzima ya uzulu na umanyema hata kama mantiki inalazimisha hali iwe hivyo. Wataalam wasaikolojia wanasema ukitaka kumshinda mtu kwanza kabisa hakikisha unamfanya duni na dhalili.

Mohamed anadhani kuwa asemayo ni kuwajenga vijana wa kiislam. Anapingana na kanuni za asili kuwa hadi hapo atakapoamua kuwaambia ukweli, zao la uchochezi na ulaghai halina siku za usoni.

Leo mwanafunzi aitwaye Halima au Najmira hata kama ameshinda kulala mhula mzima basi anafaa kwa masomo na kazi. Kwamba certificate si uwezo ni jina la imani ya mtu
Mohamed amewafanya wajsikie duni bila sababu .
 
By Mohamed Said WC,Unataka tubishane kwa kitu ambacho waliasisi wazee wangu
na mie kuijua historia yake?Hivi wewe utaijua AA kuliko mimi mjukuu wa waasisi hawa?
Hivi wewe utaujua undani wa TANU kunishinda?Huo ni muhali
Mohamed, knowledge haingii akilini kwa njia za kurithi. Knowledge ni kitu kinatafutwa. Hatujui mtoto wa G.Washington, Churchil, Gandhi, Mandela, Nyerere, Reagan nao watasemaje.

Hili ndilo tatizo kubwa sana, kwamba ukizaliwa Dar unajua kiswahili. Utashangaa anatoka mtu bara anakuwa mwalimu wa kiswahili hapo hapo uswahilini. Hii kutokana na kuamini kuwa maarifa yanaingizwa kichwani kwa njia za osmosis.

Mtu anadhani historia ya Nyerere lazima mtoto wake aifahamu sana, utashangaa watu wanaoandika historia ya Mwalimu wengine walimuona akipita kwa mbali au gazetini. Vipi umewahi kusikia watoto wangapi wa Mkwawa, Mwinyigumba na wengine wakijinasibu kwa maeneo au sifa za baba zao.

Mtu anaamini kuwa kwakuwa babu yake alikuwa karani shirika la reli au bandari basi yeye ni lazima awe mkuu wa shirika hilo kwasababu anaufaham zaidi hata kama hajawahi kukanyaga darasa stahiki.
 
Mzee Mwanakijiji,

Naona unataja tu majina ya viongozi Waislam kama ushahidi wa maandiko yako.

Wewe ni muandishi mahiri usiishie kutaja tu majina zama zaidi mpaka Wizara zote za serikali na mashirika uje na "Ratio" Waislam na Wakirsto kina nani wamejaa serikalini hapo ndiyo tutafahamu nani anafaidika na matunda ya uhuru.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said, nani anakupa mamlaka ya kumiliki "historical knowledge"? kwanini uamini kuwa wewe ni mtu pekee mwenye uwezo na akili ya kufahamu historia ya AA na TANU ati kwa sababu wazee wako walihusika?Nakusihi acha kiburi na majivuno ya jinsi hiyo!

Gwalihenzi, nionyeshe mahali mzee MS amesema yeye ndiye mwenye"historical knowledge"peke yake ya AA na TANU baba ficha upumbavu wako onyesha busara zako angekuwa na majivuno asinge jadiliana na vilaza kama wewe huku jf
 
 
 
 
 
its unfortunate tht we even do discuss abt muslims and christianity stuff. hivi vitu tumeletewa didnt we have any identity b4 this white guys came to Africa? lets stick to our own beliefs sidhani kama tutakuwa na matatizo.period.
 
 

Nguruvi,
Mfano wako si sawa.

Ujuzi nilionao katika historia ya TANU hauendani na urithi.

Nimeijua kwa kuona, kusikia kutoka wenye TANU yao na
kwa kutafiti.

Hizo ni daraja tatu za uelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…