Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Pigeni kelele tu ndugu zangu. Tukimaliza kuondoa ubalozi wa vatican tuondoe na wa Iran vile vile. Hii si ni Islamic state?
Itakuwa ni visasi tu lakini tatizo letu ni huu wa Vatican ambao haupo kihalali na unatuletea umaskini badala ya neema.
 
Mag3 sio lazima uchangie kwenye huu uzi wala hata wewe hautunyimi usingizi usipochangia hizi pumba zako si uende kwenye chit chat au jukwaa la mapenzi

Boko Haram,
Ajabu ya Rahman.

Mie sioni wapi nimeshabikia maneno ya Sheikh Ilunga.

Maswali niloulizwa nimejibu kuwa sina ujuzi nayo huo
ni uwanja wa maulamaa.

Kweli hilo ndilo la kuleta kisirani na kutukanana?
Lakini kama tusemavyo Waswahili.

Heri nusu shari kuliko shari kamili.
 
Itakuwa ni visasi tu lakini tatizo letu ni huu wa Vatican ambao haupo kihalali na unatuletea umaskini badala ya neema.

Vatican inakuletea umaskini???
Ni kweli hayo?
Vijana wenu wangapi wamesoma na kutibiwa kwenye taasisi za kikatoliki? Pamoja na kupata ilm ya madrassa, Mzee wako Mohamed Said ilibidi akaongezee elimu ya maana kwenye shule za kikatoliki. Elimu hiyo ndio ilimuwezesha kufika mpaka chuo kikuu, leo hii unasema inawaletea umaskini?? Simfahamu Mohamed Said lakini nafikiri hajawa maskini...
 
Naona umerudia ujinga wenu!.Watu walikuwa wameketi wanasoma umeingia wewe golo umeharibu kila kitu.Mohammed amekasirika anasema
Mag,

Naona unahamaki nyingi na lugha yako siipendi.
Mimi si mtu wa shari.

Kuanzia sasa sikujibu..
Mohammed kaa pembeni upumzike.Mimi mwanzo nilifikiri hizo nukuu zote mbili ni kutoka kwako.Kumbe moja ni kutoka kwa wakoloni.Ajabu iko wapi wakati wewe umewataja wote wawili,babu yako na Kasanga Tumbo huku wakoloni wakimtaja Kasanga Tumbo peke yake.
Madhumuni ya Mohammed ni kusahihisha historia.Kwanini tusome kejeli za wakoloni pekee kwa kuwaita waliogoma ni foolish tu kumbe kulikuwa na wengi walioshiriki na kufanikisha huo mgomo.Sisi tutafaidika na nini kwa kusoma kejeli za wakoloni pekee.
Jamani tukubaliane huyu mchochezi ama kwa makusudi au kwa hila, lengo la kumwaga ngano zake ni kuleta machafuko ya kidini nchini na amini usiamini, hata Waislaam wengi hawamuungi mkono..
Wanaotaka kuleta machafuko ni nyinyi watetezi wa mfumokristo.Kwanini hamko tayari kukubali kasoro za kuwepo ubalozi wa Vatican hivyo ukafungwa au kuvunjwa NECTA na waislamu wakaingizwa.Hata machafuko yakija basi si kutokana na Mohammed bali ung'ang'anizi wa mfumo kristo Tanzania kitu ambacho kwenye nchi nyingi zenye mchanganyiko wa kiimani hakipo.Ushawishi wa mfumokristo unafanya hata mahakama zikose heshima.
 
Tumechoka na hadithi zenu za kuku na yai.
Pesa itoke serikalini tunakochangia sote halafu sifa mjitafutie nyinyi.Umeambiwa Vatican hata benki yake haina wachilia mbali visima vya mafuta na mashamba ya mazao ya kibiashara sasa hizo pesa wanatoa wapi kutusaidia.Hii ni taasisi ya kinyonyaji tu na kimafia.Waondoke Tanzania.
Masheikh wangapi wametobolewa macho kwenye hizo hospitali za kikatoliki na wangapi wamewekewa glucose wakafa huku wamekwenda kutibiwa magonjwa ya sukari.
Mohammed Said najua unayajuwa haya na kwa bahati umeingia na id yako halisi.Ukiumwa usiende hospitali zao utakutana na akina Nyambala na Jasusi.Njoo tukupatie tiba za kisunna inshaAllah utapona.
 

Insha Allah.

M
 

Ami,
Mimi ningetegemea majalada ya Waingereza ningepitwa na mengi.

Ikiwa una kitabu changu soma historia ya Dockworkers Union kama
nilivyoieleza mie kisha kasome kama alivyoiandika Illife.

Mbingu na ardhi.

Ndiyo yale TANU imeasisiwa Pugu.

Mie babu yangu ndiye alikuwa mfadhili akitoa fedha zake nyingi katika
harakati toka TAA hadi wanaunda TRAU 1955.

Jamaa kakasirika yeye hana historia ya kueleza popote.
Kilichobaki ni matusi.

Tumbo na babu yangu wakielewana sana.
Wamejenga nyumba mtaa mmoja, mjengo mmoja na zinatazamana.

Walipoletewa taarifa na wapashaji habari kuwa watakamatwa wote
wawili walikwenda "underground."

Tumbo akaweza kutoroka akenda Mombasa.

Babu yangu alijificha kwa muda akipanga mipango ya biashara zake
kisha akaibuka.

Makachero hawakujua alikuwa wapi juu ya jitihada zao zote.

Yapo mengi.
 

Mag3,

Mambo ya Ukimwi yametoka wapi tena mbona unajidhalilisha kiasi hicho.

Mungu ametupa akili kwa ajili ya kufikiri siyo kufugia nywele sasa ili bandiko lako la wakoloni sijui umeliokota wapi ngano tupu, mkoloni kuwaita wazee wetu wajinga ndiyo unaona ushahidi wa mgomo wa wafanyakazi mie nilidhani na wewe ulikuwemo kwenye huo mgomo wa wajinga.

Siku ingine usipende kuokota maneno na kuyaleta JF kuanzia leo tunakuogopa kama Ukimwi.

Vipi leo hauchutami.
 
Huo uamuzi wako hata hauninyimi usingizi, mangapi umeshindwa kujibu? Maelezo yangu yameelekezwa kwa Watanzania wenye uelewa mpana zaidi wanaoufuatilia huu mjadala. Utasemaje wewe si mtu wa shari huku unashabikia mahubiri ya Sheikh Ilunga?

Watanzania siyo wajinga wewe wachukuwe hizo pumba zako za mkoloni ndiyo wakubali.

Unatafuta pakutokea sasa wapi Mohamed Said kashabikia mahubiri ya Ilunga kakwambia hilo suala la maulamaa yeye hana Ilm nalo.
 
Itakuwa ni visasi tu lakini tatizo letu ni huu wa Vatican ambao haupo kihalali na unatuletea umaskini badala ya neema.
Vatican inakuleteaje umaskini wewe? Kwani ni hela zetu za kodi zinazomlipa balozi? Si wanalipa wao? Ubalozi wa vatican upo kihalali Tanzania kama vile ulipo Marekani.
 

Kumbe hata wakoloni hawakumtambua Salum Abdallah, babu yake Mohamed, kama kiongozi wa mgomo uliotikisa taifa? What then, was Abdallah's role?
 

kimsingi una confuse vatican city na Holy see - which is actually the ecclessiatical government of vatican ambayo ina diplomatic ties na nchi 180 na inatambulika vema. nyie tz mkiwafukuza what difference does that make kwanza kwa uwekezaji walionao bongo what you are proposing is next to impossible.
Nakupa assignment, fanya research kidogo kujua signing ceremony ya EU ilifanyika vipi na mahala gani utajua mamlaka ya vatican.
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1364433069731.jpg
    20.7 KB · Views: 53
Kumbe hata wakoloni hawakumtambua Salum Abdallah, babu yake Mohamed, kama kiongozi wa mgomo uliotikisa taifa? What then, was Abdallah's role?

Jasusi,
Siwezi nikavutana na wewe kuhusu wakoloni kumtambua au kutomtambua babu yangu katika
mgomo ule.

Si muhimu.

Ila nitakueleza kitu kimoja kuwa babu yangu ndiyo alikuwa mwenyekiti muasisi wa TRAU.
Duka la babu yangu lilikua moja ya maduka yaliyokuwa yakitoa posho kwa wagomaji.

Jasusi,
Hebu soma hii ''excerpt'' kutoka moja ya makala zangu zilizochapwa kwa mwezi mzima na gazeti la
Mwananchi kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika:

SalumAbdallah katika mkutano ule wa siri kuzungumzia kuunda TANU alitoa mchango washilingi ishirini kumsafirisha Katibu wa TAA Jimbo la Mafharibi Germano Pacha kuja Dar es Salaam.

Wakati ule hizozilikuwa fedha nyingi. Mwaka 1955 muda mfupi baada ya kuundwa TANU, SalumAbdallah alichaguliwa kama mwenyekiti muasisi wa Tanganyika RailwayAfrican Union (TRAU)chama cha wafanyakazi wa Reli kilichokuwa na nguvu sana wakati wa kupiganiauhuru na kikitoa mchango mkubwa kwa TANU.

Katibu wa TRAU alikuwa ChistopherKassanga Tumbo.

Mwaka 1960 TRAU chini ya uongozi huu iliiitsha mgomo uliodumusiku 82. Kwa miezi takriban miezi mitatu si treni, meli na mabasi ya relweyalitembea.

Inasemekana hapajatokea mgomo ambao ulitayarishwa kwa ufundi naustadi kama mgomo wa relwe wa mwaka 1960.

Mwishowe serikali ya kikoloni ilisalimu amri na wafanyakaziwa relwe wakasitisha mgomo na kurudi kazini madai yao yote yakiwa yamekubaliwa.

Mgomo huu miezi michache kabla ya Tanganyika kuwa huru ulimtisha sana Nyererekwani alitambua kuwa kulikuwa na uongozi wa vyama vya wafanyakazi uliokuwa nanguvu sana na aliogopa baada Tanganyika kuwa huru vyama hivi chini ya viongozikama hawa vitampa shida katika utawala wake. Katika mambo kama haya kunakuwa namikasa mingi.

SalumAbdallah alikuwa na binti yake mwalimu wa shule ambae kijana mmoja katika relwe alimpenda naakapeleka possa kwake kwa nia ya kutaka kufunga ndoa.

Bahati mbaya kabla SalumAbdallah hajajibu posa ile mgomo ukawa umetokea.

Sasa Yule kijana kwa bahatimbaya hakugoma kwa hiyo akawa katika kundi lililojulikana kama vibaraka.

SalumAbdallah alihamaki sana kuwa yule kijana ambae alitegemea atajakuwa mkwe wakekaisaliti TRAU.

Salum Abdallah akamwagiza mshenga wa yule kijana aje achukemajibu ya posa yake.

Mshenga hakujua nini kinamsubiri. Siku ya siku ilipofikaakajikusanya yeye na wenzake kwenda kupokea jibu la posa yao wakiwa na uhakikakuwa jibu litakuwa zuri na kitakachobaki ni kupanga siku ya harusi.

SalumAbdallah alitoa kiti chake cha uvivu akakiweka sawasawa na mlango mkubwa wanyumba yake anasubiri ujumbe ufike.

Toka mbali Salum Abdallah anamuona mshengana wapambe wake wale wanakuja na kanzu zao na kashda na ndani ya ujumbe kunamasheikh wawili watatu wa kuheshimika.

Walitegemea chai nzito kwani SalumAbdallah hakuwa mtu mdogo katika jamii.

Naam, hapakuwa chai wala salaam kamailivyo kawaida wala Salum Abdallah hakumpa nafasi mchenga kusema chochote.Alinyanyuka na posa ya yule kijana akawatupia miguuni waiokote.

Akawaambia, "Katafutenimke kwa vibaraka wenzenu, nyumba yangu haingii kibaraka."

Sasa Jasusi mimi nitashughulishwa na nini kama Waingereza hawamtambui babu yangu?
Leo hii babu yangu huyu hapa anasikilizwa na waliokuwa hawamjui sasa wanamjua na
mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Kumbe hata wakoloni hawakumtambua Salum Abdallah, babu yake Mohamed, kama kiongozi wa mgomo uliotikisa taifa? What then, was Abdallah's role?


Jasusi,
Siwezi nikavutana na wewe kuhusu wakoloni kumtambua au kutomtambua babu yangu katika
mgomo ule.

Si muhimu.

Ila nitakueleza kitu kimoja kuwa babu yangu ndiyo alikuwa mwenyekiti muasisi wa TRAU.
Duka la babu yangu lilikua moja ya maduka yaliyokuwa yakitoa posho kwa wagomaji.

Jasusi,
Hebu soma hii ''excerpt'' kutoka moja ya makala zangu zilizochapwa kwa mwezi mzima na gazeti la
Mwananchi kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika:

SalumAbdallah katika mkutano ule wa siri kuzungumzia kuunda TANU alitoa mchango wa shilingi ishirini kumsafirisha Katibu wa TAA Jimbo la Magharibi Germano Pacha kuja Dar es Salaam.

(Wasomi wa Makerere waliokuwa walimu pale Tabora walipojua kuwa ''this is for real'' akina Salum Abdallah wamedhamiria kuunda
chama cha siasa wakaingia uoga wakawa hawaji tena katika ile mikutano ya siri iliyokuwa inafanyika Town School).

Wakati ule hizo zilikuwa fedha nyingi. Mwaka 1955 muda mfupi baada ya kuundwa TANU, SalumAbdallah alichaguliwa kama mwenyekiti muasisi wa Tanganyika RailwayAfrican Union (TRAU)chama cha wafanyakazi wa Reli kilichokuwa na nguvu sana wakati wa kupigania uhuru na kikitoa mchango mkubwa kwa TANU.

Katibu wa TRAU alikuwa ChistopherKassanga Tumbo.

Mwaka 1960 TRAU chini ya uongozi huu iliiitsha mgomo uliodum usiku 82.

Kwa miezi takriban miezi mitatu si treni, meli na mabasi ya relwe yalitembea.

Inasemekana hapajatokea mgomo ambao ulitayarishwa kwa ufundi na ustadi kama mgomo wa relwe wa mwaka 1960.

Mwishowe serikali ya kikoloni ilisalimu amri na wafanyakaziwa relwe wakasitisha mgomo na kurudi kazini madai yao yote yakiwa yamekubaliwa.

Mgomo huu miezi michache kabla ya Tanganyika kuwa huru ulimtisha sana Nyerere kwani alitambua kuwa kulikuwa na uongozi wa vyama vya wafanyakazi uliokuwa nanguvu sana na aliogopa baada Tanganyika kuwa huru vyama hivi chini ya viongozi kama hawa vitampa shida katika utawala wake. Katika mambo kama haya kunakuwa na mikasa mingi.

SalumAbdallah alikuwa na binti yake mwalimu wa shule ambae kijana mmoja katika relwe alimpenda naakapeleka posa kwake kwa nia ya kutaka kufunga ndoa.

Bahati mbaya kabla Salum Abdallah hajajibu posa ile mgomo ukawa umetokea.

Sasa Yule kijana kwa bahati mbaya hakugoma kwa hiyo akawa katika kundi lililojulikana kama vibaraka.

SalumAbdallah alihamaki sana kuwa yule kijana ambae alitegemea atajakuwa mkwe wake kaisaliti TRAU.

Salum Abdallah akamwagiza mshenga wa yule kijana aje achukue majibu ya posa yake.

Mshenga hakujua nini kinamsubiri.

Siku ya siku ilipofika akajikusanya yeye na wenzake kwenda kupokea jibu la posa yao wakiwa na uhakika kuwa jibu litakuwa zuri na kitakachobaki ni kupanga siku ya harusi.

SalumAbdallah alitoa kiti chake cha uvivu akakiweka sawasawa na mlango mkubwa wa nyumba yake anasubiri ujumbe ufike.

Toka mbali Salum Abdallah anamuona mshengana wapambe wake wale wanakuja na kanzu zao na kashda na ndani ya ujumbe kuna masheikh wawili watatu wa kuheshimika.

Walitegemea chai nzito kwani SalumAbdallah hakuwa mtu mdogo katika jamii.

Naam, hapakuwa chai wala salaam kamailivyo kawaida wala Salum Abdallah hakumpa nafasi mchenga kusema chochote.Alinyanyuka na posa ya yule kijana akawatupia miguuni waiokote.

Akawaambia, "Katafuteni mke kwa vibaraka wenzenu, nyumba yangu haingii kibaraka."

Jasusi,
Mimi nitashughulishwa na nini kama Waingereza hawamtambui babu yangu?
Historia ya KIvukoni haimjui watakuwa hao Waingereza adui zake?

Leo hii babu yangu huyu hapa anasikilizwa na waliokuwa hawamjui sasa wanamjua na
mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

c.c. Pasco:
Huo hapo juu kuhusu posa ya kibaraka ndiyo uleeeeee ''wazimu'' mke wangu Bi Zena
Bint Farijallah alosema ananipenda sana lakini ananiogopa huenda na mimi nimerithi
''wazimu.''
 

Twende taratibu,

Kwanza umesema kuwa ati Vatican City ndio wana diplomatic ties na nchi 180. Huo ni uongo kwani walio na diplomatic ni Holy See wakimwakilisha papa kwa waumini wao. Labda nikuulize ushawahi kusikia balozi wa Vatican asiyekuwa cardinal, mkatoliki na pia sio mwakilishi wa Holy See???

Pili unadai kanisa Lina uwekezaji mwingi uongo mwengine. Wangelikuwa wawekezaji wangeliwakataza Kanisa lisiwe linachukua kodi zetu kila mwaka. Pili kwa uchumi upi ambao Vatican unao hadi wawe wawekezaji ? By the way uchumi wa Vatican ni Mdogo kuliko wa Tanzania sasa jiulize wewe hizo pesa unazodai wamewekeza wamezitoa wapi? Nipo njiani ila nikifika ofisininitakuwekea wanavyosema wataalamu wa Sheria kuhusu Vatican na diplomatic ties
 
Rapheri,

Si kweli kuwa sitaki kuona michango ya Mwanakijiji.
Nimeacha kumjibu kwa kuwa kanitukana.

Mzee Said uwe mkweli kwanza; ulinitukana nikakurudishia heshima hiyo hiyo! Nilisema wakati ule ukitaka kujadiliana kwa heshima utajadiliana kwa heshima. Binafsi sitatiziki kabisa na wewe kutokujibu hoja zangu kwa sababu najua hauna majibu na pale ambapo unadhania unayo huwezi kuyatoa kwa ukweli kwani utaonesha udhaifu wa hoja zako na ulaghai wa kileunachokiita ni historia ya "wazee wako" ambayo mimi nimeiita ni 'histohisia'!
 

Sijui nani alikufundisha mantiq! asije kuwa mwalimu yule yule wa Mohammed Said.
 
Kuanza ku argue kuwa dini gani ina nguvu zaidi na wakati dini hizo zimeletwa na wavamizi wa Africa ni ujinga mtupu.
 
Kuanza ku argue kuwa dini gani ina nguvu zaidi na wakati dini hizo zimeletwa na wavamizi wa Africa ni ujinga mtupu.
I was thinking the same thing,ni sawa na uende nchi zilizotawaliwa na waarabu waislam na si wazungu,halafu uulize kwanini mokoni huyu wa kiislam utamaduni wake umekubalika kuliko mkoloni yule wa kikristo/kizungu nk.
 

Mdondoaji, unajaribu kisichowezekana; unajaribu kukataa uwepo wa jua wakati linakumulika! Wewe umeshajiamulia kuwa Vatican City si nchi na hivyo ushahidi wote hata uwekwe mbele yako vipi utaukataa. Utatafuta 'wanasheria' wanaotetea msimamo wako wakati wapo wengi wanaoenda kinyuma na huo (na hivyo hutojitofautisha na M. Said).

Sasa sijui tukusaidia vipi kujua historia ya Vatican City - Papa alitawala Papal States kwa karibu miaka 1000! Ukumbuke kuwa Vatican kama makao makuu ya Papa imekuwepo kabla ya ujio wa Uislamu. Papa kama kiongozi wa kidini na kiserikali amefanya hivyo kama halifa wa Petro. Suala la dini na serikali kama sehemu moja ya mfumo wa utawala imekuwepo kwenye Ukristu kabla ya kuwepo kwenye Uislamu.

Leo hii ukisikia Waislamu wanasema kuwa dini na serikali havitofautishwi watu wanadhania ni dhana mpya au imekuja na Uislamu. Dhana hiyo imekuwepo kwenye Kanisa kwa muda mrefu. Hata hivyo, baada ya migongano ya kihistoria Kanisa Katoliki liliamua kujikita katika "ufalme wa Mbinguni" kuliko "Ufalme wa Duniani" na hivyo kujikita kwenye masuala ya kiroho na maisha ya duniani hapa bila kudai haki za kiutawala wa kidunia. Baada ya Italy kuunganishwa (Unifikication) kulikuwa na uadui uliodumu kwa karibu miaka sitini kati yake na Vatican City (chini ya Papa) kwa ardhi kubwa ya nchi za Papa yalichukuliwa na ufalme wa Italy hadi mkataba wa Lateran mwaka 1929. NImeshakudokeza hapo nyuma juu ya historia hiyo.

Vatican City basi haijawahi kuwa chini ya nchi ya Italy; imezungukwa na Italy kama Lesotho au Swaziland zilivyozungukwa na Afrika ya Kusini. Vatican City haijawahi kuwa chini ya Mfalme wa Italy bali hata Roma yenyewe (ambayo ni makao makuu ya Italia) imewahi kuwa chini ya Papa.

Sasa ukweli huu unaweza kuudhi, unaweza kuuchukia lakini ni ukweli wa historia. Siyo ukweli wangu mimi au kusema nasema hivyo kwa sababu nami ni Mkatoliki la hasha. NI ukweli wa historia kwa sababu huwezi kutumia historia kuupinga. Kama unaweza naomba ujibu maswali haya:

a. Vatican City ina uhusiano gani na Italy?
b. Mkuu wa Vatican City ni nani?
c. Holy See ina uhusiano gani na Vatican City na vyote viwili vinauhusiano gani na Papa?
d. Je, Vatican City inajitambuaje yenyewe (ni mkoa, kijiji, au sehemu ya Italy)?
e. Je Papal States zilikuwa ni nini?

Jaribu tu kutafuta majibu haya kwenye historia uone kama yatapingana na nilichosema mimi. Sasa, unaweza kuwa na hoja kuwa hutaki Nchi ya Papa iwwe na uhusiano na Tanzania kwa sababu ni nchi ya Kidini au ya Kikristu. Hii ni haki yako na unaweza kuanzisha mwamko wa kutaka Tanzania ivunje uhusiano nayo. Unaweza kujaribu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…