Wanajamvi huyu
Mohamed Said ni mtu wa kuogopa kama ukimwi. Huko nyuma aliwakana Cecil Matola, Dr Vedasto Kyaruzi na Mwalimu Nyerere kama Maraisi waasisi wa AA mwaka 1929, TAA mwaka 1950 na TANU mwaka 1954 huku akiwamwagia sifa makatibu wao Kleist Sykes na baadaye mwanaye Abdulwahid Sykes. Sasa shuhudieni hapa anavyomweka kando Balozi Christopher Tumbo katika harakati za Tanganyika Railway African Union (TRAU) na kummwagia sifa babu yake Salum Abdala kama Mwenyekiti muasisi na aliyeongoza mgomo wa Wafanyakazi wa Reli mwaka 1960. Namnukuu;
Sasa yatubidi tujiulize, hii simulizi ni ya kweli au imetiwa chumvi. Wanajamvi hebu linganisheni hii na ripoti ya mgomo wa TRAU mwaka 1959/1960, mwaka moja kabla ya uhuru. Je "
star" wa huu mgomo alikuwa nani? Hapa chini nanukuu kutoka kwa wakoloni wenyewe;
Wanajamvi, yako mengi ningeweza kuyaandika hapa lakini nawaomba mjiulize tu kwamba katika vyama vya wafanyakazi popote duniani, nani ni mtendaji mkuu? Juzi juzi hapa tumemshuhudia Nicholas Mgaya akiandamwa na serikali kuhusu mgomo wa wafanyakazi (ingawa mpaka sasa wameweza kumnyamazisha) lakini wangapi wanamjua mwenyekiti wake?
Mohamed Said kama kawaida anamtukuza babu yake na kumpa sifa zoote huku akimweka kando aliyekuwa Katibu na Mtendaji Mkuu wa TRAU, kulikoni?
Je viongozi wakuu wa vyama vya wafanyakazi walioitikisa dunia na kuleta mapinduzi kama Lech Walesa wa solidarity Poland, nani alimjua aliyekuwa mwenyekiti wake? Kwa vyama vya wafanyakazi katibu wake ndiye mtendaji mkuu au hata hili huyu mzushi mkubwa
Mohamed Said anayedai amezunguka dunia nzima halijui? Jamani tukubaliane huyu mchochezi ama kwa makusudi au kwa hila, lengo la kumwaga ngano zake ni kuleta machafuko ya kidini nchini na amini usiamini, hata Waislaam wengi hawamuungi mkono.