Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Geeky,
Nafanya staha.

Hao Pan Africanists hivi sasa hawapo.
Ipo mada mnasaba na mimi ikiwa nitaalikwa.

Watu wa Kigoda wananijua.
Nafanya staha.

Nami nakusifia jambo moja tu si mwepesi wa jazba kama wenzako wengi humu na sina unafki imebidi nikusifie
that being said I dont really think you understand the severity of what you set out to do here you are touching to change the history of this beautiful country as we know it and that is a huge undertaking sir I hope you understand that. na jambo linalonitatiza : kwa ninavyojua (nimeangalia midahalo na majarida ya books reviews kama book review of London) writers are usually torelant to criticism, now since this book has been brought into criticism here I have reason to hope there is some constructive criticism here that will be thrown your way as well as compliments I just dont know/understand why u cant seem to conceed any. seeing that you are critically acclaimed among your scholars. ni hayo tu.
 
Nimemuuliza anisaidie kufafanua kauli ya jumbe, Mhh naona kimya!
 

Nguruvi,
Unanogesha mnakasha lakini tatizo ni kuwa unaingia kwa kutaka ushindi.

Mimi niko hapa kutaka kueleza ninayojua ili na wengine wayasikie hata kama
hatukubaliani.

Ndiyo maana hata lugha zetu mie na wewe hazishabihiani.
Sikukujibu kwa kuwa unanichosha unasoma kwa haraka.

Ile barua ambayo Nyerere hakupelekewa aloandika Ivor Bayldon
haikutoka UTP.

Ilikuwa mwaka 1953 hata TANU bado.

Hebu rejea kwanza nyuma usadikishe hilo kisha Insha Allah nitajibu
hayo mengine.
 

Bado hujanionyesha ni kwa kifungu kipi cha sheria Vatican ni state. Labda nikuulize kutoka kwenye maneno yako mwenyewe uliyoyatoa Wikipedia nifafanulie nini maana ya sentensi hii?

The Holy See, as a non-state sovereign entity and full subject of international law
 
Lile tulishalimaza nilikuwa naweka sawa tu kuhusu kauli yako kuwa nauliza tu.Hilo lisikutie wasi wasi.

Tuendelee na hili la mfumokristo, je, kwa ufupi sana nini definition halisi. Tumekuwa tunasikia tu mfumokristo kila mtu akija na lake, sasa wewe maalim mtoa darsa unaweza kutupa maana tu kwa uchache ili wakati mnakasha unaendelea basi tujue tunaongelea nini.
 

Jokakuu,

Kukujibu wewe na Nguruvi kwa pamoja naweza kusema hivi mashirikiano ya kibalozi ya Tanzania na Saudi Arabia, Cuba na Urusi ni ya kimataifa na yanaendana na makubaliano ya umoja wa mataifa kuwa nchi ziwe na ushirikiano.

Vatican ni taasisi na sio nchi na mashirikiano yake na Tanzania ni bilateral relationship kama iliyo Tanzania na PLO (Palestine Liberation). Sasa kikugumizi kinaanzia hapo iweje Tanzania iwe na ushirikiano na taasisi ya kidini ? Na je mashirikiano hayo ya kidiplomasia kwanini basi Tanzania nayo isishirikiane na OIC vile vile maana kama precedent Nyerere alikubali Vatican basi hakuna hoja ya msingi mpige kelele Tanzania isijiunge na OIC. Hamna hoja yenye mashiko kabisa. Na Bernard Membe alikuwa sahihi kusema hakuna ubaya kwani sio tatizo lolote.

Binafsi I do not see the problem Vatican kuwepo nchi ila I see the problem mnapoikataa OIC kwa kigezo ati Tanzania haina dini halafu mkaiacha Vatican. Huo ni udini na ubaguzi
 
Uongo wa hapo ni nini?

Je umesoma kitabu cha Mohamed Said kiitwacho maisha na nyakati za Abdul Sykes nilichokipinga katika uzi huu?
Uongo ni kuwa si kweli kwamba historia ya Mohammed Said imeanza 1954+ kama ulivyosema mwanzoni mwa mjadala huu.Nashangaa kwanini tumefika mbali kote huku kujadili uongo wako.
 
Mohamed Said;6015002]Abdu aliyekujapewa medali na taifa hili miaka
50 baada ya uhuru.Nyerere alitoa medali 3979 jina la Abdu halikuwapo.Kasahaulika.
Allah una miujiza.
Mohamed, kadri unavyoongea ndivyo unavyowatoa mashaka wale waliokuwa nayo.
Nyerere alitoa nishani hizo kwa akina nani katika kundi la wazee wako na kumsahau Abdul?
Je, Mwinyi aliyemfuata Nyerere alitoa ngapi na kwa akina nani na kwavipi alimsahau Sweet abdul.

Endapo hutakuwa na jibu basi nitakuomba urudi nyuma post# 10828 umpongeze yule muungwana aliyesema kuhusu jaribio dhaifu.
 

Mdondoaji; soma mada yangu kuhusu OIC niliyoandika mwaka 2007; mimi sina tatizo na Tanzania kuwa na Ushirikiano wa kibalozi na OIC as a matter of fact labda nilikuwa mtu wa kwanza kutaka hilo lifanyike kwa kanuni hiyo hiyo ya kuwa tuna ushirikiano na Holy See. Tatizo ni kuwa kwenye kauli yako umechanganya mambo; "kujiunga" kuwa mwanachama wa OIC siyo sawasawa na kuwa na uhusiano wa kibalozi. Nakuhakikishia hutakutana na mtu yeyote anayeelewa mambo ambayo anaweza kupinga Tanzania isiwe na uhusiano wa kibalozi na OIC; none. At least not among those I know.

Hili la kuwa na uhusianow a kibalozi lilikuwa ni jambo rahisi sana na lilipaswa kufanywa tangu zamani. Tatizo ni kuwa wapo wanaotaka Tanzania iwe mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu. Tanzania siyo Mwanachama wa Holy See au wa Vatican City State! Sasa kwanini unalinganisha maembe na samaki? Kama unataka Tanzania iwe na uhusiano wa kibalozi na OIC jiunge kwenye treni wengine tulishaitisha hilo miaka mingi imepita sasa!

Karibu upande huu; lakini siyo kujiunga kwani kama Tanzania haijajiunga na Vatican au Holy See kwanini ijiunge na OIC? Unataka Tanzania iwe na uhusiano wa kIbalozi na OIC kama ilivyo kwa taasisi nyingine za kimataifa au unataka Tanzania iwe mwanachama wa Nchi za Kiislamu? Well, angalau umesema unataka uhusiano wa kibalozi (a position that I had taken many years back) lakini wengine hawataki uhusiano wa Kibalozi; wanataka Tanzania iwe nchi ya Kiislamu kwa kujiunga na OIC (kuna masharti ya uanachama mwanachama anatakiwa kuyakubali na baadhi ya masharti ya OIC ni ya kidini).

Tukubaliane tutilie mkazo Tanzania iwe na uhusiano wa kibalozi na OIC kama ilivyo na Holy See (I just noticed the two words rhymes)!?

Unasemaje ndugu yangu? Maana ninachoona unachotaka hasa ni equity kuwa kama Tanzania ina uhusiano wa kibalozi na Vatican kwanini isiwe na uhusiano wa kibalozi na OIC. Hili halina shida; lakini humo humo umechanganya na kujiunga; hiyo siyo equity.
 
Ahsante kwa kujibu pamoja ingawa swali langu halikuwa limelenga huko.

Ni msaada wa mawazo kwasababu ninatatizika sehemu.
 
Mzee ms,Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani.Tatizo lako kubwa ni mdini sana, laiti usingekuwa mdini una mengi ya kujifunza kutoka kwako.Kingine kama we ndo unaetoa hili darsa, basi usikwepe maswali.ili sie tusojua tupate ilim. Jibu kila kitu kwasababu upo hapa kueleza yale yaliyofichwa.
 
Kwa mfumo huu mjadala huu hautafika mwisho na hatimae itakuwa ni sehemu ya kupoteza muda badala ya kupata elimu.
Mtu aliyeshindwa kujibu hoja anasubiri vumbi litulie halafu aibuke kujitangazia tena ushindi.Au mtu aliyeshindwa kujibu hoja hata akikumbushwa mara ngapi anakaa kimya halafu anadhani watu wote wamesahau anarudi tena kuleta hoja ile ile.
Wewe Nguruvi ni hodari zaidi wa kukimbia hoja zinapokuwa hot kuliko Mohammed.Ukirudi bila kujibu unadhani unazungumza na watu wapya kabisa.
Wasomaji wapya na wa zamani SOMENI HAPA halafu mje na uamuzi wenu.
 
Huyu saidi anayeamini katika mfumo kristo ana tofauti gani na ponda na ilunga na yule shehe wa uamsho? Hawa watu wana chuki tu na ukristo na si jingine. Tofauti ya hao niliowataja ni kuwa huyu said ni msomi (bila shaka) anayeuandama ukristo kwa hasira ya kalamu. Watu kama hawa si wema na si wa kuwaendekeza. Hii mada inaendelea kumpa huyu mtu fursa ya kueneza itikadi zake na za waliomtuma. I am done here.
 
Nimemuuliza anisaidie kufafanua kauli ya jumbe, Mhh naona kimya!
Tatizo jengine la Nguruvi na wenzake,ni kulazimisha jibu hata Mohammed akisema jambo fulani halimhusu au hana ujuzi nalo kuliko wengine.

..Haya mambo ya udini-udini ukiyaendekeza mara nyingine unaishia kuwa kituko, na mfano wa kituko ni kauli unayodai imetolewa na Raisi Mstaafu Aboud Jumbe kuwa Tz ina dini kwasababu ina mahusiano na Vatican.!
Inakuwaje unamlazimisha Mohammed akupe majibu yanayomhusu zaidi Jumbe na Ilunga?.
Hata kama atakuwa na majibu kulingana na uzoefu wake lakini hakuna mantiki kulazimika kujibu kuhusu watu wengine ambao wako hai na wewe una uwezo wa kuwafikia na kuwauliza kupata undani halafu ukaja nao hapa jamvini na sisi tukafaidika.
 
Hao wote uliowataja ni wasomi. Kwa hiyo unataka huu uzi ufungwe mbona amueleweki wengine wanataka uendelee.
 
Sheikh Said nimepata taarifa sasa hivi wewe Dr???(Kwa maana nyengine umeingia kwenye chama chetu cha wenye PhD?) Kama ni kweli basi hongera sana welcome to the club Dr na nisamehe kwa kutokujua wewe ni Dr. Kuanzia sasa kwenye mnakasha huu nitakuwa ninakuita Dr Mohamed Said.
 

RITZ,
Mi nawasiwasi na MM huenda ndie aliekuwa Bosi wa Kiwanda cha uchapishaji! kumbuka Mohamed Said ilibidi akachapishe vitabu vyake Nairobi na London! ndio maana unaona MM anavyohangaika na propaganda za kizamani! mara anatafsiri Qurani, anachambua kauli na fatwa za Ilunga, makala za Waislamu na CCM, malalamiko yake kwa Pengo utafikiri nchi haina Serikali! mara utamuona anaisifia Bakwata! mara yuko JF akijaribu kumchafua MS na kumuita mchochezi, mzizi wa fitina na matusi kibao!

Sasa amekuja na mpya kabisa! anasema yeye hana tatizo na Tanzania kujiunga na OIC! hii ni karata yake ya mwisho anaitupa ili apate kuungwa mkono na Waislamu! hajui kuwa Kanisa lake ambalo yeye ni mtiifu kwalo halikubali TZ kujiunga na OIC? anataka kutengwa na Kanisa lake? amesahau wenzake huko kusini walivuliwa dini kisa waliipigia kura CCM mwaka 2010?
 


Mdondoaji,
Umenikweza bure.

Mie sijafikia makamu hayo yenu ingawa natamani.
Lakini jua limeshakuchwa Maghrib sasa kwangu mimi.
 

Raia Fulani,

Tofauti kati yangu na masheikh uliowataja ni kubwa sana.
Hao mimi ni viongozi wangu na ni alim yaani wajuzi.

Mimi ni maamuma yaani wananiongoza.
Mimi sijatumwa na yoyote ni akili zangu ndizo zinitumazo.

Kuendekeza sijui nani anamwendekeza nani kwa kuwa kuna
mengi wazee wangu walibaki kimya hadi wanakufa.

Katika hali kama hii aliyekuwa anaendekezwa ni nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…