Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Ami,

Hilo bandiko ni mpini wa maana hakuna anayesubutu hata kuli-quote.
 

Duh, jamaa wamekuja na kali tena la easter sunday! nisawa na watoto 2 mmoja kamzaba kibao mwenzake mvumilivu na katokea Mzee mmoja nakumuona yule mzabaji analia huku anamsingizia mwenzake ati kamzaba kibao!

Waislamu miaka nenda miaka rudi wanachezewa rafu na mfumo Kristo lakini wenzetu wanadharau na kukanusha hakuna kitu kama hicho! leo wao ndio wanalia na kudai kuna Sytematic Persecution!

WIMANA,
Unaweza kutufafanulia huo mfumo ni vipi una dhulumu Viongozi na dini yao Kristo?
 

Kadogoo,

Unasubiri "Definition" kuwa na subra labda watakuja na vitu Hadhwarani.
 
Last edited by a moderator:
Ami,

Hilo bandiko ni mpini wa maana hakuna anayesubutu hata kuli-quote.
Si walitaka definition.Tayari imepatikana.Yako mengi tu ambayo huyakalia kimya halafu wakaja na hoja eti hawakujibiwa.
Yuko wapi Spike afyonze definition ya mfumokristo kwenye compyuter yake?.
 
Ami,
Ahsante ndugu yangu kwa kutuanikia mfumokristo.

Wangazija wana msemo maiti hafi ila kwa mzishi wake.

Tumesubiri hadi mzishi ulipowasili na sanda na vyote
vinavyomuhusu maiti.

Kazi kwake aliyekuwa anamkomalia Mohamed Said atoe
"definition."
 
Reactions: Ami
Sahih International
And do not mix the truth with falsehood or conceal the truth while you know [it]. wacha uongo Mwanakijiji usichanganye haki na batili baba
Huyu Mwanakijiji kuchanganya haki na batili ndiyo fani yake.Ritz ndiye anayemfahamu vizuri.

Nikamuuliza
Hii taarifa yako ni ya uongo mtupu na yenye kujichanganya.
Huyu papa aliyetawala papal states kwa 1000 years ni yupi.
Ukiweza kujibu hiyo jibu na hii
Ukristo na Uislamu ni ipi dini iliyotangulia mwenzake?.
Hakujibu kabisa lakini huko mbele atarudi na ngonjera zake na kumshutumu Mohammed kwamba anakwepa kujibu kadhaa na kadhaa....
 
Si walitaka definition.Tayari imepatikana.Yako mengi tu ambayo huyakalia kimya halafu wakaja na hoja eti hawakujibiwa.
Yuko wapi Spike afyonze definition ya mfumokristo kwenye compyuter yake?.

Ami,
Spike hasikiki.

Ghafla utamshtukia kaibuka.
Vup!
Huyu hapa nyuma yako.
 
Huyu Mwanakijiji kuchanganya haki na batili ndiyo fani yake.Ritz ndiye anayemfahamu vizuri.


Hakujibu kabisa lakini huko mbele atarudi na ngonjera zake na kumshutumu Mohammed kwamba anakwepa kujibu kadhaa na kadhaa....


Sikujibu kwa sababu sikuamini mtu mwenye chembe za Ubongo zinazofanya kazi vizuri hawezi kuuliza swali kama hilo. Kwani jibu lake liko dhahiri kwa mtu yeyote ambaye hana hofu ya kufikiri. Kwa vile hata hivyo umeuliza na licha ya kukuacha kwa muda ujifariji (nikitumaini utagundua fallacy ya swali lako) bado umeendelea nalo. Ili kutokukutafunia na kukumezea nitajibu swali lako kwa kutumia Socratic method...

Swali: Ukristo na Uislamu ni ipi dini iliyotangulia mwenzake?

Jibu: Ukijua nani alianza kufundisha kati ya Mohammed na Yesu utajua dini gani iliyotangulia mwenzake?*


NB*: Uislamu kama dini umekuja na kujulikana baada ya Mohammed kuanza mafundisho yake na ukakua na kueleweka zaidi baada ya kuenea kwake katika Bara Arabia na sehemu nyingine za dunia hadi leo hii; kabla yake hakukuwa na watu walioamini katika Uislamu kama tunavyouelewa sasa.
 
Sahih International
And do not mix the truth with falsehood or conceal the truth while you know [it]. wacha uongo Mwanakijiji usichanganye haki na batili baba

Nukuu hii ndugu yangu ingemfaa sana Mwalimu wenu humu; ni yeye aliyeandika historia akichanganya ukweli, uongo, porojo na hisia zake na kuziita "ukweli"! Ni kipi nilichokisema mimi ambacho si cha kweli? NONE.
 
Mkuu,

Mie PhD yangu nimeipatia huko ndio maana nikamshauri aende huko kama wewe ulisoma huko basi sawa tu lakini nachofahamu mie ndio nilichokipendekeza.
Mie sijasoma kokote zaidi ya Vigwaza S/M ambako hawatoi PhD kama yako. My thoughts ni kwamba Sabean Wahhabi Satanists are more relatable to Somalia & Saudi Arabia, thats why I was wondering/
 
"Definition" ya Mfumo Kristo ina mantiq

Katika Posti ya ndugu yetu Ami hapo juu (akinukuu mwingine) aanasema nnini maana ya Mfumo Kristo: Kwamba,

Mfumokristo ni hali ambayo Wakristo wa Tanzania wamehodhi madaraka ya ngazi zote muhimu katika serikali na katika vyombo vya maamuzi, na kuzitumia nafasi hizo kuwaendeleza Wakristo na Ukristo na kuwabagua Waislamu na dini yao.

Sasa kwa haraka haraka mtu anaweza kukubali hili. Na ninaomba kwa sekunde chache tukubaliane na tafsiri hiyo kabla sijaionesha kuwa haina ukweli na haitafsiri Mfumo Kristo ninavyouelewa mimi. Ukisoma maana hiyo Mfumo Kristu ni:

1. Hali - Ni "condition" au tuseme siyo kitu ambacho ni 'concrete'.

2. Wakristo wa Tanzania - ina maana Mfumo Kristu hauwahusu Wakristu wa sehemu nyingine duniani na inapozungumzia Wakristu wa Tanzania inazungumzia "Wakristu" wote.

3. Wamehodhi Madaraka - kwa maneno mengine "Monopoly of power". Kwamba hao watu wa kundi hilo hapo juu wamehodhi madaraka bila kutoa nafasi kwa watu wa dini nyingine.

4. Madaraka ya ngazi zote muhimu za serikali na maamuzi - Hii ni sifa muhimu sana ambayo tutakapoiangalia tutaona inavunja kabisa dhana ya uwepo wa "mfumo huu". Ikumbukwe 'operative word' hapa ni "zote". Nitarudia hili hapa chini kidogo.

5. Kutumia nafasi hizo kuendeleza Wakristu wenzao na Ukristo na kuwabagua Waislamu.

Sifa hizi tano kutokana na maana ya mfumo kama kina Ami wanaamini au wanataka tuamini zinafanya mfumo kuwepo na kutenda kazi. Lakini katika hayo matano ni hilo la nne ndilo HASA linafanya mfumo huu kuwepo kwani bila kushika madaraka yote muhimu hauwezi kuwa na nguvu.

Niwarudishe kidogo kwenye falsafa na hususan kwenye somo la Mantic (Logic). Mantik ni somo ambalo linamsaidia mtu kujenga hoja vizuri, kuepuka makosa ya hoja (fallacies) na wakati huo huo kuhakikisha anagundua makosa hayo kwa wengine. Ukisikia mtu anasema "hii haina mantiki" manake nikuwa kilichosemwa hakijakubaliana na fikra zake - hata kama anaweza asijue maneno yote ya logic.

Kosa la Kwanza la tafsiri ya "Mfumo Kristu" kama alivyoweka Ami iko kwenye kutokuelewa Mantiki na walioandika hilo wenyewe wanaweza kufikiri wamesema cha maana kumbe ndani yake imejaa makosa ya hoja. Nitoe mfano.

Mtu anakuja na kusema "Mimi ni Mtanzania" halafu anasema "Watanzania WOTE ni waongo" halafu akasema "Mimi sisemi uongo".

Sasa mtu mwingine anaweza kuamini hilo lakini mara moja mtu mwenye uelewa mdogo wa mantiki ataonesha "inconsistency" katika madai hayo. Ataonesha hivi:

Kama Wewe ni Mtanzania, na Watanzania wote ni waongo basi wewe huwezi kuwa unasema kweli. Kwa hiyo na huyo anayesema hivyo ama ni mwongo au si Mtanzania. Kama Watanzania WOTE ni waongo basi hakuna Mtanzania anayeweza kuwa anasema kweli.

Mtu akisema Viongozi "WOTE" wa ngazi za juu ni "Wakristu" basi ni lazima tuone kuwa ni Kweli viongozi wote ni "Wakristu". Ukifanikiwa kuonesha kuwa kiongozi mmoja tu ni Mpagani basi hoja kuwa "Viongozi WOTE" ni Wakristu inakufa pale pale.

Ami ametuletea bandiko ambalo tafsiri ya Mfumo Kristu inadai kuwa Wakristu wameshika "nafasi ZOTE MUHIMU". Sasa hii ni rahisi kuonesha; ukionesha Wakristu wameshika nafasi zote muhimu za serikali na "za Maamuzi" basi unathibitisha uwepo wa Mfumo Kristu at least kwa suala la idadi kabla hatujaangalia ile element ya mwisho (ya tano). Lakini ukifanikiwa kuonesha kuwa mojawapo ya nafasi muhimu zinashikiliwa na Muislamu au mtu asiye Mkristu basi hoja kuwa Wakristu wanashika nafasi zote muhimu inakufa. Ukiweza pia kuonesha kuwa zipo nafasi muhimu zinazoshikwa na Waislamu basi HOJA KUWA NAFASI ZOTE ZIMEHODHIWA NA WAKRISTU nayo inakufa.

Hapa inabidi nilete zile orodha alizozileta Ritz kwa fahari kubwa akiamini kuwa anasema kitu very profound:

Ametuwekea 'composition' ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:


Sasa, kitu cha kwanza kuangalia ni kuwa mawaziri wote na manaibu wao wameteuliwa na Rais Kikwete ambaye ni Muislamu. Nafasi kubwa kabisa nchini ya serikali na ya kimaamuzi nchini Tanzania inaongozwa na Muislamu. Ni Muislamu ndiye mtu mwenye nguzu zaidi ya maamuzi Tanzania. Hii ni KWELI (its a Fact). Kikwete akihutubia Bungeni miaka michache nyuma alitamba kuwa ana madaraka makubwa kiasikwamba akitaka Dr. Slaa akamatawe anaweza akakamatwa! HUYU NI MUISLAMU. Hakuna Mkristu yeyote anayempita au kumkaribia kwa madaraka.

Nafasi Muhimu:

Kina Ami wanasema nafasi "Muhimu" zimeshikiliwa na Wakristu hebu tuangalie:

Urais - Jakaya Mrisho Kikwete - Muislamu
Makamu wa Rais - Ghaibu Bilal - Muislamu
Waziri Mkuu - Mizengo PInda - ni Mkristu - aliyeteuliwa na Muislamu!
Waziri wa Mambo ya Nje - Bernard Membe - Mkristu - kateuliwa na Muislamu
Waziri wa Ulinzi - Vuai Nahodha - Muislamu
Waziri wa Viwanda na Biashara - Abdallah Kigoda - Muislamu
Waziri wa Maliasili na Utalii - Khamis Kagasheki - Muislamu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Shukuru Kawambwa - Muislamu (ikumbukwe wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kufeli waliingia kidato cha kwanza hadi cha nne chini ya uongozi wake- NECTA iko chini yake)
Waziri wa Maji - Jumanne Maghembe - Muislamu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii - Hussein Mwinyi - Muislamu
Waziri wa Nchi TAMISEMI - Hawa Ghasia - Muislamu

Sasa hizo ni nafasi "muhimu" za kutosha tu. Nafasi nyingine zote za Mawaziri Wakristu wote wameteuliwa na Rais Muislamu na yeye ndiye mwenye madaraka juu yao.

Je ni kweli "nafasi zote muhimu" zimehodhiwa na Wakristu? kina Ami na Ritz na vijana wengine humu wasiojua mantiki wanasema kwa haraka "ndio"!!

Mfumo Kristu - kwa maoni yao - ndio umewaweka Waislamu hawa kwenye madaraka makubwa hivyo!

Tujiulize mahali pengeine ambapo pamewahi kuwa na mifumo ya kibaguzi:

Utawala wa Makuburu wa Afrika ya Kusini ulitukuza rangi nyeupe kwa muda wa karibu miaka mia nne. Je, ulitengeneza weusi wangapi kwenye nafasi muhimu? NI vipi mfumo wa kibaguzi ulifanya kuwepo Rais Mweusi, mawaziri weusi wakautumikia? NI mweusi gani aliyekuwa na nafasi ya juu kabisa katika serikali ya utawala wa makaburu?

Hili ni kweli hata Marekani wakati wa mfumo wa ubaguzi wa rangi (segregation). Ni vipi mfumo ule uliwezesha kutoa nafasi kwa weusi kushika madaraka ya juu?

Kimsingi mfumo wa kibaguzi wa kundi hautoi nafasi kwa wanaobaguliwa kushika madaraka mazito. THIS HAS NEVER HAPPENED BEFORE ANYWHERE IN THE WORLD! Hakuna mahali duniani ambapo mfumo wa kibaguzi (sifa ya tano ya tafsiri ya Mfumo Kristu kama alivyotuwekea ndugu yetu Ami) umewapa madaraka ya juu wanaobaguliwa. Ila wanatuambia Tanzania hili linawezekana. Kwamba Mfumo Kristu katika Tanzania unatupatia viongozi wa Kiislamu!!

Hii tunaweza kusema ni oxymoronic!!

Naomba nitoe changamoto kwa wale wanaoamini kwamba upo mfumo wa kibaguzi dhidi ya Waislamu Tanzania uitwao "mfumo Kristu". NIONESHENI MAHALI POPOTE DUNIANI AMBAPO MFUMO WA KIBAGOZI (A DISCRIMINATORY SYSTEM) IMEWEZA KUTOA VIONGOZI WA WALE WANAOBAGULIWA NA KUWAPA NAFASI MBALIMBALI HADI ZA JUU KABISA WAKATI MFUMO HUO UNAFANYA KAZI!

Naomba mfano mmoja tu.

 


Tatizo kubwa la hadithi zako mzee Saidi pamoja na kukosa "mantiki" kama walivyosema wanajanvi wengine ni "inconsistencies" na hili ndiyo haswa linathibitisha kuwa una nia ovu na uko tayari kusema lolote na kwa ushahidi wowote no matter how sloppy and irrelevant ili kutimiza lengo lako. Waziri mkuu seven years earlier (Rashidi Kawawa) alikuwa amesoma mpaka darasa la ngapi? Je na yeye aliwekwa na Christian lobby? Na hili la Nyerere kumshauri Sokoine ajiuzulu uwaziri mkuu on medical grounds unaweza kulithibitisha?????
 


Tatizo kubwa la hadithi zako mzee Saidi pamoja na kukosa "mantiki" kama walivyosema wanajanMi wengine ni "inconsistencies" na hili ndiyo haswa linathibitisha kuwa una nia ovu na uko tayari kusema lolote na kwa ushahidi wowote no matter how sloppy and irrelevant ili kutimiza lengo lako.

Waziri mkuu aliyetangulia (Rashidi Kawawa) alikuwa amesoma mpaka darasa la ngapi? Je na yeye aliwekwa na Christian lobby? Na hili la Nyerere kumshauri Sokoine ajiuzulu uwaziri mkuu on medical grounds unaweza kulithibitisha?????
 
Mzee Saidi hebu kula darsa kuhusu Sokoine hapa chini, maana hizi ngano zako inabidi ziwe zinawekwa sawa asubuhi asubuhi!!! Faida kwa vijana wako.






 
Mzee Saidi hebu kula darsa kuhusu Sokoine hapa chini, maana hizi ngano zako inabidi ziwe zinawekwa sawa asubuhi asubuhi!!! Faida kwa vijana wako.




Nyambala,
Ungejiepusha na maneno kama ''ngano'' nk ningefurahi wacha wengine watumie hayo
mimi sijui vipi lakini nakuhisi nawe nikafanya majadiliano ya maana na wewe.

Sitoweza kufanya hivyo na mtu ambae ananikebehi.

Nakushukuru kwa bandiko hilo lakini ukweli ni kuwa hizo si habari mpya kwangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…