Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ami,
Serikali tumewaeleza tatizo la mfumokristo.

Sheikh Ilunga katembea nchi nzima kuwaeleza Waislam
kuhusu mfumokristo. Kipi kitushughulishe kwa Nguruvi?
Mfumokristo unaueleza kule wasikojua kwa bahati mbaya.

Ni utaratibu huo huo unaoutumia kuwatumbukiza watu katika maandamano wewe ukiwa salama salimini.
Wengine wapo segerea wala huna habari nao una laptop na kupika lingine.

Sisi tunawaweleza wasomaji kuwa hicho kinachoitwa mfumokristo ni dude ambalo hata waundaji hajui mbele ni wapi na nyuma ni wapi. Wamepata definition ya kusikitikitisha na kuumba umba kutoka kwa Serengeti boys!

Mohamed, kama unasubiri vijana wa Form II waje wakusaidie kutoa definition, ni hatari kwa umma kwasababu sijui wewe na Ilunga mnaeleza nini huko mwendako.

Mfumokristo mnaoueleza ni ule wa takwimu za Daily news! teh teh teh
Ndio ule Mohamed! please people deserve better!

Mohamed, Uislam ni ukweli na haki. Ni dini inayosisimama kwa misingi yake kwa kufuata mwongozo wa Mwenyezi mungu, hadithi na Sunna. Ukiondoka katika ukweli unakufur. Waeleze waumini kile kilicho kweli na bora.

Mohamed, kuna hoja viporo huko nyuma, tuendelee na mnakasha.
 
Wakati mwingine huwa nacheka sana kuna watu wanajidanganya na kujifariji kuwa kitabu cha Mohamed Said wao ndiyo wamekipinga baada ya miaka 15, ha haa haaa!!

Kwa kuwafahamisha tu baada ya miaka 15 tena kupitia huu uzi kitabu cha Mohamed Said kinazidi kununuliwa bahati mbaya mikoani kilikuwa hakipatikani saizi watu wanakitafuta.

Watu wanakisoma kitabu cha Mohamed Said wanakutana na vitu ambavyo hawajawahi kuvisoma popote pale katika historia ya Tanganyika.

Hata hawa wapingaji wa kitabu cha Mohamed Said hawaji na historia yeyote uhuru wa Tanganyika wanayoifahamu zaidi ya kupinga hapo ndiyo wasomaji wanapojionea wenyewe makundi mawili kuna la kwanza la Mohamed Said ambaye anakuja na historia halafu kundi la pili la wapingaji ambalo linakuja na meneno matupu.

Mohamed Said fanya mpango uongeze machapisho ya kitabu chako Watanzania wanakitafuta mashubaka yao yanaitaji kitabu chako.

Mohamed Said endelea kutoa darsa Watanzania wanakusoma Watanzania wa sasa siyo watu wakushikiwa akili tumshukuru sana Allah kwa kukupa fursa hii ya kuja JF kutoa darsa la historia ya Tanganyika katika harakati za uhuru.

Hawa wapingaji napenda waongezeke wanafichuwa mengi yaliokuwa yamejificha chini ya kapeti.
 

Ritz,
Hawa ndugu zetu mimi niliwaambia tokea mwanzo kuwa haya nisemayo
yametendeka kwetu na wazee wangu.

Historia ya uhuru wa Tanganyika haikuanza na Nyerere 1954.
Wao wanashikilia kuniuuliza nani rais muasisi?

Jibu ni dhahiri halina shida.

Lakini nawaambia kuna kisa mpaka TANU imekuja asisiwa mwaka 1954.

Historia hii nyie hamtaki kuijua?
Mbona ni historia nzuri na ya kusisimua?

Hata nilipokuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam nawauliza
walimu wangu.

Mshapata kumsikia mtu anaitwa Abdulwahid Sykes?
Mnajua tarikh yake?

Mnajua kama unataka kutoa sifa kwa mtu mmoja kuhusu TANU basi atakuwa
Abdu?

Butwaa kubwa na sura za mshangao!

Ritz,

Hivi nani anajua kuwa ule mkutano wa 1954 wa kuasisi TANU hela katoa Abdu, Ally,
Dossa na Rupia.

Nani anajua haya?

Nani anajua kuwa Abdu ndiye alichelewesha kuundwa kwa TANU ikafika 1954 baada ya
TAA Politica Subcommittee kuamua kuwa waunde TANU 1951?

Laiti Chief David Kidaha Makwaia angekubali kogombea nafasi ya urais wa TAA historia
ya Tanganyika ingekuwa nyingine.
 
Mohamedi Said,chali! Yaani unazidi kujivua nguo kwa majibu mepesi unayojibu hapa kutoka kwenye maswali magumu.

Huyo ndiyo Nguruvi3...aka GOOGLE ya JF kwa watu wabishi na waongo kama wewe mzee Said na wanafunzi wako hapa jamvini. Nguruvi3 aka GOOGLE na kampani yake wanapenda hoja na si viroja...na wanapenda jibu zuri kutoka kwenye swali gumu. Pole sana mzee Mohamed!
 

Nguruvi,
Buko na definition.

Definition si ushapewa na Ami?
Au huridhiki hadi itoke kwangu?

Angalia hatari ya kuzungumza usichokijua...
Hadith na Sunna...

Hiyo ni bahari nyingine kabisa.
 

BashaDido,
Ahsante nishapoa.
 

Hapa ndiyo tofauti yako na wao vitu kama hivi bahati mbaya hawana masikini.

Kitakachofuatia hapa kwenye kukujibu watayakata vipande vipande maandishi yako na kuandika majibu ya kupinga mwazo mwisho...ha haa haaa.

Ukiwauliza andikeni basi ukweli wenu tuusome wanakuwa wakali wanasema baada ya miaka 20 wao wanakuja kupinga.

Lakini la msingi ni kuwafahamisha wafuatiliaji wa huu mnakasha historia ya uhuru wao wapo kama njia tu ya kuwafikia Watanzania.
 
Kwa hizi historia zenu za kizushi ipo siku mtakuja na madai ya kuwa waarabu hawakuhusika na biashara ya watumwa na zanzibar haikuwa soko la watumwa kwa kutetea "Arabism" na Uislamu wenu.
 

Unajua Mzee MS aliposema wawili watatu ndiyo hawamwelewi nilibaki kucheka tu, hiyo
wawili watatu ujue ina maana kubwa sana...Imemvua nguo. Nguruvi ukiona mtu
anayejinasibu kwamba hapa anatoa darsa tena akirudia rudia ujue ni pigo kubwa amepata.

Alikuwa amezoea kulisha watu pumba huku anawachanganyia maziwa kidogoo. Hapa watu wanapata
mchanganyiko maalum. Kwa ambao walikuwa wanameza tu sasa wataelewa MS anposema 20% au
10% ya utafiti fulani huwa ana malengo yake kichwani.

Sasa wanajua hila zake katika uandishi. Watu wanajua Garang alipokuja UDSM alikuwa ni alumni
kama yeye alivyo alumni wa ST Joseph, na kwa kweli Kardinal Pengo akiita Alumni wa St Joseph
Mzee MS atapewa kiti cha mbele kama ambavyo Garang alipewa.

Sasa sote tunajua 10% ya Waislam UDSM (source Daily news?) ambao hawakumuuliza maswali Garang ni takwimu zisizokuwana mtetezi (iko siku ataita vijana wake walielezee kwa sababu yeye hana ujuzi nalo!).

Sasa Watu wanajua wazi Warioba alikuwa anajulikana vizuri tu wakati wa uteuzi wake kuwa Waziri mkuu.
Sasa watu wanajua Muasisi wa dhana ya Mfumo Kristo ameshindwa kutupa maana yake ila anajua "unavyo
fanya kazi! Yaani kwa maneno mengine anaijua vizuri mitaa ya Gerezani na Kipata lakini hajui iko mkoa gani!!

Sasa wengine tunamjua ni mtu mwenye misheni zake na hila. Ukiona ameandika kitu kwa makosa ujue ana hila
zake. Ukiona anasema magazeti ya Africa Events yalikusanywa na kuchomwa moto msikilize vizuri sana, halafu
muulize ya kweli hayo? (atajua kuna kitu unajua) halafu atakwambia yaliondolewa kwenye News stand!!
Soma vizuri "News stand"!!

Kuna mengi yamenifanya nimjue huyu mtu. Na kwa kweli huu uzi umemwacha uchi. Na dalili zake ni hizi....
"Mimi ndiyo nayetoa darsa hapa" kuna watu 10K+ wanaonisoma mimi sio nyie"...Hah ha ha .
 

Nguruvi,
Ikiwa unastareheshwa na kubaki hapo hapo umegota sawa.

Ila mimi nishakwambia silazimishwi jambo.
Kawaida yangu kwenda mbele.

Pokea zawadi hii kutoka kwangu ushushe joto.
Kazi na dawa:

Ukivuka Livingstone ndiyo unafika sasa katika nyumba ya Bi Mluguru bint Mussa mama yake Abdulwahid Sykes.

Kuna kisa kimoja, kilitokea hapa wakati wa kudai uhuru, viko vingi lakini kwa ajili ya muda ntaeleza hiki kimoja.

Hii nyumba mkasa huu ulipotokea ndiyo ilikuwa ''retrreat'' ya Nyerere na Abdu wakiwa na jambo zito la kufanyiwa uamuzi katika chama.

Nyumba hii ipo hadi leo ingawa imebadilishwa kidogo na kuchukua sura nyingine.

Nikifumba macho namuona Bi. Mluguru anapanga chupa zake za togwa barazani na mimi na rafiki yangu Ebby Sykes tunanyemelea kupewa chupa moja kubwa ya mapenzi maana huyu ni mke wetu lazima tumuonjee togwa lake.

Ah! Wakati umekwenda wapi?

Siku moja Nyerere alikuwa pale Kirk Street pamoja na Abdulwahid Sykes na Mama Maria na mama yake Nyerere Bi Mugaya pia alikuwapo.

Ghafla Nyerere alipindukwa na tumbo baada ya kula chakula cha mchana na akawa katika maumivi makali sana.

Hali ilipozidi kuwa mbaya, Mama Maria akamwita pembeni Bi Mwamvua maarufu akijulikana kama Mama Daisy, mke wa Abdulwahid na kumwambia kuwa mama yake Nyerere Bi Mugaya ana wasiwasi kuwa mwanae anakufa kapewa sumu.

Mama Maria hofu ilikuwa imempata na akawa na wahka mkubwa.

Mama Mugaya akamnong'oneza Bi Mluguru kuwa ana wasiwasi kuwa aliyempa sumu mwanae si mtu wa mbali.
Nyerere hakuwa amelishwa sumu.

Habari hii ilienea mji mzima na ikaleta hofu kubwa kwa wana TANU.
Lakini ukweli ni kuwa Nyerere alikuwa amepindukwa tu natumbo.

Ukitoka nyumba ya Bi Mluguru sasa kabla hujakatiza Sikukuu Street mkono wa kulikuwa na kinyozi aliyekuwa maarufu akiwanyoa watu wote wa Gerezani na kwengineko akijulikana kwa jina moja tu la Muingereza.

Muingereza alikuwa akinyoa chini ya mti wa Mkwaju na umuhimu wa mahali pale ilikuwa ni barza wakikutana watu kwa mazungumzo hasa nyakati za alasiri.

Hapa katika miaka ya 1950 mazungumzo yalikuwa siasa tu.

Leo Gavana Twining kasema hili, leo Nyerere kajibu vile, B Titi kawashambulia wakoloni, Mtemvu kafanya hiki na habari zote zilikuwa zikifika pale na kuwekwa uwanjani kwa mjadala.

Wakati gumzo likiendelea sauti ya mkasi wa Muingereza ulikuwa ikisikika ikila nywele katika kichwa kat, kat, kat...na yeye mwenyewe Muingereza alikuwa mtu wa vichekesho sana hakuwa nyuma katika kutupa neno hapana pale kama vile, "Sikiiza bwana huyu Twining Nyerere keshamtafutia mbeleko yake, atabebwa tu hana ujanja."

Hapo pembeni anaweza kuwa amekaa Abdulwahid,Dossa na jamaa wengine tena wamekalia gogo (maana kwa Mwingereza kulikuwahakuna viti) lakini wote wakiunganishwa na mapenzi yao kwa TANU.

Baadae ilipokuja Congress kama chama cha upinzani wanachama wa Congress hawakukosa pale na barza sasa ikiwa imestawi hasa.

Hii ilikuwa barza ya baba yangu.

Mijadala kati ya TANU na Congress wenyewe wakiisifia wakiita ''Mwamba Usiovunjika'' kwa kawaida ilikuwa mikali hata kushinda ya Sunderland na Yanga.

Mazungumzo yatabadilika siku Sunderland wako uwanjani Ilala Stadium wakicheza na Yanga.

Hapo tena siasa inawekwa pembeni mazungumzo yanahamia kwenye mpira na washabiki wa timu zote walikuwa wanabaraza wa Kinyozi Muingereza.

Wakati ule Yanga walikuwa na mchezaji wao maarufu bingwa wa kupiga kona Hamisi Mtoto tena yeye mwenyewe alikuwa mkazi wa Gerezani, Mtaa wa Somali Street kona na Sikukuu.

Sunderland wakijuvunia Harold Mgone walompachika jina "Wamisalaba," Mashaka Abdallah maarufu kwa jina la "Mashaka Prince," Salum Kheri Kilanga, Salum Ali maarufu kwa jina la "Jini" na wengineo, (kisa cha Salum Ali kuitwa jini ni kuwa alikuwa akitumia mguu mmoja tu katika uchezaji wake. Salum Ali alicheza mpira hadi katika miaka ya 1960 katikati) huyu Kilanga alikuwa Yanga kisha akahamia Sunderland.

Wakati huo huo Mambo Mzinga aliyekuwa Yanga nae akatoka akaenda Sunderland.

Mambo Mzinga alikuwa mwalimu wa madras iliyoanzishwa na baba yake Sheikh Mzinga.

Watoto wengi wa Dar es Salaam pamoja na baba yangu wamesoma chuo hiki ambacho kipo hadi leo Mtaa wa Mafia kona na Chura.

Yanga walikuwa na wachezaji wengine wakali kama Stumai Mzee, Juma Mbimbi, Hamisi Fotini, Badr Malande, Mwenda Mushi na wengineo.

Baadhi ya wachezaji hawa ndiyo walichukua kombe la Gossage mwaka 1949.

Nguruvi,
Kuzaliwa mjini dawa.

Hawa watu nimewaona katika udogo wangu na khabari zao ndiyo kama hivi sasa nakupa na wewe na wasikizaji mpate kustarehe.

Hivi ndivyo ilivyokua historia hii na ndiyo ikashangaza Nyerere kutoa medali Abdu hakumpa.
Historia ya TANU imeandikwa Abdu hayumo.

Ukipenda niweke visa vya uhuru ninavyo vingi sana.

Insha Allah nitakuwekea movie hapa uburudike at zero cost.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa.

Hayo maneno ya mwisho nimemuibia Walter Conkrite.
 
Mwanakijij na Nguruvi bila kujibu hoja kwa kukiri au kukanusha hakuna haja ya kuturudisha nyuma.Tuna shughuli nyingi za kufanya.
Definition ya mfumo kristo mumeiona ?.njooni na uzi mrefu kujibu hilo kwanza.
BHANG!....
 
Nguruvi,
Buko na definition.

Definition si ushapewa na Ami?
Au huridhiki hadi itoke kwangu?

Angalia hatari ya kuzungumza usichokijua...
Hadith na Sunna...

Hiyo ni bahari nyingine kabisa.

Ha ha haa mzee MS nilishakwambia huyu Nguruvi ni sawa na kasuku kila analosikia anazungumza bila kufanyia utafiti eti hadith na sunna dah hapa ndio kaonyesha ni kiasigani ni mtu dhaifu hii ni fani nyingine wala usirudie kuzungumzia mfano nakupa kupitia avator yako Girrafe na Twiga upo hapo bwana mdogo
 

Plato...
Nimekusoma.

Una hayo tu?
Vipi mikutano ya siri ya kuasisi TANU pale Stanley na Kirk Street?

Je una lolote la kusema?
 
Nguruvi,
Buko na definition.

Definition si ushapewa na Ami?
Au huridhiki hadi itoke kwangu?

Angalia hatari ya kuzungumza usichokijua...
Hadith na Sunna...

Hiyo ni bahari nyingine kabisa.

Hadith na Sunna tujifunze kwake ha haa haaa!! Sijui kama anajua ni mtu gani ambaye anatakiwa kufikisha hadith.
 
Ha ha haaaa....naona watu wamechanganyikiwa kwa nondo na sasa wanajifariji kwa vioja uchwara.
 


Well,mimi huwa naziita Nguruvi3's histohisia..

hakuna Farki inayojengwa kwa kusemwa kwa uhalisia wa upande fulani,tatizo kubwa sio criticisms zako,tatizo hutaki tuh kuelewa na kuikubali historia hii..
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi ukicheka,ukilia hakuna atakayekuamini kuwa definition hii ya mfumokristo uliyoomba ni ya kuumba umba.
Unaitukana nafsi yako bure kwa kukanusha wataalamu wengi walioitayarisha.
Wimbo wa Taifa – unaomba mungu aibariki nchi

2. Dua ya Bungeni – ina muomba mungu

3. Kuapishwa kwa wanaochukua nafasi za uongozi.
Japo wanaoapa huapa kwa dini zao, aneapishasi kiongozi wa dini husika bali wa serikali au wabunge.
 

Kama wameshakula yamini kutoamin basi hata ueleze nini hawawez tuh kuamini,

Kikubwa ukweli unazungumzwa na wenye akili zao timamu wenye kupima na kudadavua mambo wanajua Moh Said,

Labda wao wameona njia ya kujitafutia umaarufu ni kum-challange na kumkejeli Moh Said,sio mbaya sana..

Wamejaribu,Tumeona,,ila sasa wameshindwa moja kwa moja kutetea hoja zao kuhusu uchochezi wako na farki unayoijenga..

Sisi tunastareheka na hoja zao za kiabunuasi..
 
Nguruvi ukicheka,ukilia hakuna atakayekuamini kuwa definition hii ya mfumokristo uliyoomba ni ya kuumba umba.
Unaitukana nafsi yako bure kwa kukanusha wataalamu wengi walioitayarisha.


Ami ndugu yangu,,

Muwie radhwi bure huyo Mzee Mwanakijiji,

Sisi tunamwita mzee mfia dini,mara nyingi utamuona anakuja na speed kali sana ya kuufanyia clarification uislam ili kututoa nje ya mada,mbaya zaid hakuna anachokifaham kuhus uislam wetu labda kwa kukariri anakofanya,,

Tulishampa rai mda mrefu Mwanakijiji achutame aficha tupu zake kwani si busara kwa mtu wa heshima kama yeye kwa jins alivojitanabaisha hapa jamvini kushadadia mambo asiyokuwa na ilm nayo,hataki,..!!


Anataka kujifanya yeye ni TABII TABIINA,Wapi na wapi??

Anazid kujidhalilisha tuh zomba alishamvua nguo huyo mda mrefu tuh..
Mohamed Said ni kiboko yao,Allah kamjalia kheri kuelezea mambo yaliyokafichikana,na sisi tunathamini uhalisia huu,sio kwa kuwa ni muislam mwenzetu au kwa kuwa anaelezea upande wa pili ambao unaakisi waislm na uislam la hasha,
Ila kwa kuwa anaueleza uhalisia ulivyo kwa maslahi ya taifa na tanzania ilivokawa hapo zamani,ilivyo sasa na jins itavyokuwa,ni jukumu letu sisi sote kupima na kuangalia wapi tulikosea na kuukubali ukweli na kuijenga nchi yetu,kuupinga hakutasaidia hata kidogo..
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Ami
Ha ha haaaa....naona watu wamechanganyikiwa kwa nondo na sasa wanajifariji kwa vioja uchwara.

BashaDido,
Si utani.

Hali ya mambo yamebadilika sana.

Mie sijifariji kwa lolote kwani sina
sababu hiyo.

Historia ya wazee wangu inasomeshwa
kwingi katika vyuo duniani.

Kitabu kimepewa catalogue "Islam, Politcs."
Ikiwa wewe huikubali hiyo ndiyo hali ya dunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…