Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

View attachment 88720
Kwa wale waliokuwa wanazungumzia census ya 1967 nawawekea hapa summary yake

Jasusi,
Nilichukua likizo ya siku saba.

Lakini kwa hili nimeona nirudi kazini lau kwa siku moja.
Hebu ona na hii hapa chini kutoka ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes...''

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]About two-thirds of East African Muslims reside in Tanzania[1] which is the most populous of the East African countries, i.e. Kenya, Uganda and Tanzania.

This includes Zanzibar-a predominantly Muslim country with a 99% Muslim population and once the centre of Islamic
learning in East and Central Africa.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 752, bgcolor: transparent"]According to the 1957 population census, Muslims outnumbered Christians at a ratio of three to two.
This, at that time, meant that Tanzania was a leading Muslim nation South of the Sahara.

But in the first post-independence census of 1967 the total figures for Tanzania Mainland were 32% Christian, 30% Muslim and 37% local belief.

These figures show Pagans as a leading majority in Tanzania.

The 1967 census has not been able to show the reasons for the sudden decrease of Muslim population nor the growth of animists amidst believers in the span of the last ten years.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 752, bgcolor: transparent"]
This was the last population census showing religious distribution.

It is widely believed that the figures for the 1967 census were doctored for political reasons to show that Muslims were trailing behind Christians in numerical strength.

There is evidence that the government in 1970, having realised that Muslims were a majority in Tanzania, directed the Statistical Department to destroy all the 1967 census results.
[2]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 752, bgcolor: transparent"]Unfortunately power sharing in the political system in Tanzania is very much skewed against Muslims, although it is known that the stability of any nation depends on proper balancing of these factors.

Different sources provide different Muslim-Christian religious distribution figures.

These conflicting figures are as a result of sensitivity of the issue.

Among African countries with sizable population of Muslims and Christians, like Tanzania and Nigeria,[3] the inquiry as to which faith commands a leading majority, is a source of potential conflict and controversy.

Tanzania is of no exception. D.B. Barret
[4] gives figures which shows Muslims as a minority in Tanzania.

The Muslim population is purported to be 26%, Christian 45%, local belief 28%. Tanzania National Demographic Survey figures for 1973 put Muslims in Tanzania slightly above Christians at 40%, Christians 38.9% and local belief 21.1%. But according to Africa South of The Sahara,
[5] Muslims in Tanzania are a leading majority at 60%. This figure has remained constant in all its publications since 1982.

Since research by Tanzanian Muslims on Islam is scant or almost non-existent, the issue of Muslim population has yet to be tackled from an Islamic point of view.
[6]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 752, bgcolor: transparent"]Distribution of authority and power sharing is a factor which should not have been a cause of conflict in independent African countries.

Ironically this has become a point of controversy only under indigenous governments.

It is a sensitive issue because ethnicity, religious identity and clanship is an important factor in independent African states.

Power distribution and numerical strength has also to be reflected in the sharing of political power along those lines.

During colonial rule, distribution of power under ethnicity and religious bias in Africa by colonising powers were not perceived as so serious a breach of trust by subjects as to warrant civil upheavals.

Fortunately tribalism is not pronounced in Tanzania, but religion has been a factor of discrimination since colonial days.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[1]August H. Nimtz Jr, Islam and Politics in East Africa, University of Miannapolis,1980,p.11.
[2] See Family Mirror, Second Issue, November,1994, p. 6.
[3] Ali A. Mazrui, ‘African Islam and Competititive Religion: Between Revivalism and Expansion', in Third World Quarterly Vol.
10. No.
2 April, 1988, pp. 499-518.
[4]D.B.Barret, Frontier Situations for Evangelisation in Africa ,Nairobi,1976.
[5]Africa South of The Sahara, Europa Publication, London, No. 20, 1991, p. 1027.
[6]The only conclusive Muslim research is by Dar es SalaamUniversity Muslim Trustee (DUMT), see 'The Position of Muslims and
Islam in Tanzania,' in Al Haq International (Karachi)September/October 1992.
 
Mzee Saidi unajua kuna baadhi ya hoja zako zinafifika kutokana na muda na wakati tu, mfano katika moja ya vitabu vyako ulikuwa unasisitiza kuhusu idadi ya wabunge kidini. Hii ilikuwa ni kipindi cha chama kimoja. Ukadai eti majina ya waislamu yalikuwa yanakatwa na kamati kuu.... Leo tuna vyama vingi hiyo hoja haina mashiko tena maana kuna freedom ya kuhama kule unakopenda kama tulivyoshuhudia kwa akina Slaa, Shibuda, akina madevu etc. Hili kwa sasa haliteeki huwezi kusema leo eti watu hachaguliwi ubunge kwa sababu ya dini zao. By the way wabunge si wanachaguliwa na majority voting, sasa inakuwaje majority (60%) kama ulivyodai hapo juu wanashindwa kuchagua viongozi wanaowataka??? I can smell ur excuse, Christian lobby hahaaaa ahahaha!!!!!! Kama in 2010 Mbeya mjini, Mwanza, Arusha walisimamia kuhakikisha chaguo lao haliibiwi kura za ubunge ni wapi the majority walifanya hivi bado the so called lobby ikawashinda? Nachokushauri mzee wangu ni ku-move on!!!!! hizi hila na ujanja ujanja wa kujenga hoja bila ushahidi timilivu hazitasaidia vijana wetu kamwe. Zaidi zaidi watazidi kuachwa nyuma in this globalized world, hapa nazungumzia vijana wote wa kitanzania.
 
Nje ya Qurani hakuna ushahidi wowote kuwa Yesu au mtu mwingine yeyote kabla ya ujio wa Uislamu alijitambua, alijua au alikuwa Muislamu.
OK inabidi utupatie tafsiri ya Uislamu kwanza kama unavyofahamu wewe.
Mzee Mwanakijiji said:
Yesu alizaliwa Myahudi na alikufa na kukufuka kama Myahudi. Ukristu haikuwa dini ya Yesu; Yesu kwa dini alikuwa ni Myahudi
Hakuna Muislamu atakaye kukatalia kuwa Yesu alikuwa ni Myahudi wa kabila.
Je, wewe una maanisha Yesu alikuwa Myahudi wa kabila, wa dini au vyote kwa pamoja?
Mzee Mwanakijiji said:
Ukristu unaitwa hivyo baada ya watu kuanza kuamini ujumbe wa Yesu Kristu na kuufuata na hivyo kutofautisha na watu wengine walijitambulisha kama "Wa-Kristu" kwa maana ya kuwa wafuasi na waamini wa mafundisho ya Kristu.
Ni sehemu gani katika Biblia Yesu anajiita Krist?
 

Mkuu haya masuala mmeshauriwa kuyapeleka kwenye jukwaa la dini. Mkaanzishe uzi kule wanaopenda watakuja tu!!!!!!!
 

Nenda Chadema kaangalie wabunge wa viti maalum kama ukukuta Wakirsto watupu.
 
Mkuu haya masuala mmeshauriwa kuyapeleka kwenye jukwaa la dini. Mkaanzishe uzi kule wanaopenda watakuja tu!!!!!!!

Nyie watu wa ajabu sana Mwanakijiji akisema masuala ya dini mpo kimya watu wakimjibu eti mnawashauri waende jukwaa la dini...ha haa haaa haaaa!!
 

Unameza mazima mazima sababu aliyekuletea ni dini mmojo huwezi kumpinga hata kama anakudanganya.
 
Nyie watu wa ajabu sana Mwanakijiji akisema masuala ya dini mpo kimya watu wakimjibu eti mnawashauri waende jukwaa la dini...ha haa haaa haaaa!!



Nadhani na Mwanakijiji alishalisema hili huko nyuma, happy now?????

 
Geeky,
Umeshangilia goli kabla mpira haujagusa wavu.

Nimeweka kitu kuhusu sensa.
Kipitie Insha Allah.

Mohamed Said,

Ndiyo maana FIFA wameweka kifaa mbira ukivuka mstari unaonyesha goli sasa huyu ndugu yetu anataka goli kwa nguvu hata mpira haujagusa mstari.
 
Mzee Saidi unaonaje na wewe ukiweka mnyumbulisho wa iyo sensa ya 1957 kama alivoweka jasusi? Au inatubidi tuamini tu kwa sababu imesemwa na wewe?

Ujalazimishwa kuamini wewe amini ya Jasusi tatizo lipo wapi.
 
Wanajamvi, baada ya kulitolea ufafanuzi suala la jedwali la Mohamed linalohusu sensa 1967 siku za nyuma tuliamua twende mbele na mnakasha.

Kwa bahati mbaya au nzuri vijana wa Mohamed kwa kutoelewa wamekuwa wakilisema sana bila kujua wanamvua mavazi.
Niliamua kutowajibu kwasababu tuna lugha tofauti na viwango tofuati vya ufahamu.

Kinachonifanya nirudi kuelezea jedwali kinatokana na ukweli kuwa pamoja na kumuonyesha Mohamed tatizo na kosa la takwimu zake, ima haelewi au anaelewa na anafanya makusudi kuwachagiza vijana warushe matusi.

Katika kufanya hivyo ameonekana kuwashukuru sana wale vijana ambao hakika nukuu zao na ufahamu wao ni wa kiwango cha mtaani kama nitakavyonukuu mbeleni.

Kwahiyo kupitia Mohamed Said ambaye tunaweza kuongea lugha moja anapoacha ''kuoga mtoni na watoto na kuwashangilia'' kwa hisani narudi tena mjadala wanyuma na niwieni radhi.

Focus ya mjadala iwe katika jedwali lifuatalo:
Kwanza tuangalie historia ya sensa. Tanzania imewahi kufanya sensa mwaka 1967,1978,1988,2002,2012 kama takwimu ni sahihi.

Pili, matokeo aliyochukua Mohamed ni ya mwaka 1978,1979,1980. Endapo angetaka kupata uhalisia wa idadi na asilimia kwa kuangalia waislam ilibidi atumie sensa ya mwaka 1978. Kwasababu asizoeleza alitumia sensa ya mwaka 1967.

Kwa utafiti na takwimu hapa ametumia values mbili ambazo hazipo katika muda mmoja.
Idadi ya watu huenda ikibadilika na kigezo kizuri cha kufahamu hilo ni kutumia the most recent data kama alizotumia mwaka 1978,79,80 kupata idadi ya wanafunzi.(nitafafanunua kuhusu variation ya population huko mbele).

Kwa yeye kurudi nyuma na kuacha sensa ya mwaka 1978 tayari alikuwa biased na utafiti unakuwa na ''fraud''.Haukufuata kanuni.

Kwa maneno mengine hii ni sawa na kutumia takwimu za mwaka 1980 kujua watanzania wangapi wameathirika na malaria au ukimwi mwaka 2000.

Katika mstari alioanza na NB Mohamed ameonyesha wazi kuwa total selected ilikuwa ni jumla ya waislam na Wakristo.
Hapo ameondoa watu wa imani nyingine kama wahindi, wapagani na wasioamini.
Kwa maelezo yake makundi hayo hayakuwa na wanafunzi waliochaguliwa!

Data za Mohamed amezichukua idara ya elimu ya jiji la Dar es Salaam. Inafahamika kuwa Dar es Salaam ni metropolitan na kwahivyo kuna mchanganyiko wa makabila, rangi na imani tofauti.

Haiwezekani wanafunzi waliochaguliwa wawe wakristo na waislam tu. Hii maana yake ni kuwa hiyo percentage si kweli kwasababu yeye ametumia wakristo na waislam kama 100%.

Tulimululiza Mohamed(Warsha) ni kigezo gani kilitumika kujua huyu ni mwislam na yule ni mkristo. Hakuwa na jibu.
Katika nchi kama Tanzania Juma, Zawadi, Bahati, Upendo, Mariam, Yusuf, wanaweza kuwa upande wowote ule.

Lakini pia wapo akina Mariam au Miriam, Juma au Jumanne ambao kwa mapenzi yao wamerithi majina ya bibi au babu. Sasa hiyo 100% ya waislam vs wakristo ina uhakiki gani(verification).Na kwamba ni kweli mtu akiitwa Jumanne au Khamisi, tatu au pili ni mwislam na hawezi kuwa mkristo au kinyume chake.

Hatukuishia hapo tukamuuliza je Kasuku Ngunangwa, Chausiku Musika, Mkele Mhina wao walitambuiliwaje kwa imani zao.

Tukiangalia sampling, Mohamed amechagua Dar es Salaam. Kwa kuzingatia hili ni jiji watu wanaingia na kutoka.
NI vipi aliwezaje kupata uhakika kuwa hao ndio wakazi wa Dar es Salaam.
Kwanini asifanye sampling ya mikoa miwili au mitatu zaidi ili kuweza kupata data zinazoakisi hali ya nchi nzima.

Kwa mtafiti serious sampling ingeweza kufanywa Dar es Salaam, Tabora, Bukoba , Tanga na Songea kwa kuzingatia kuwa yeye alikuwa anakusanya data tu kutoka katika idara za elimu na wala si kufanya utafiti wa mitihani kwa uhalisia.

Na mwisho wa jedwali amesema sensa ingeakisi idadi ya wanafunzi kwa kuwa na waislam wengi waliochaguliwa kwa vile sensa hiyo inaonyesha idadi ya waislam katika jiji ni kubwa kuliko wakristo.

Hapa ni mwendelezo wa kosa lile lile la 100% Muslims Vs Christians.

Hata hivyo asichoelewa Mohamed ni ukweli kuwa idadi si kitu kinachokwenda sambamba na ubora.
(Quatity is not necessarily direct proportioanl to Quality).

Inaweza kuwa hivyo endapo
1. Wanafunzi walioandikishwa darasa la 1 walimaliza la 7
2. Wanafunzi hao walipata elimu bora kwa kulinganisha na minority
3. Wanafunzi hao waliingia katika chumba cha mitihani.

Hivyo hoja ya kwamba idadi ya waislam ilikuwa kubwa na hivyo kupaswa kuakisi waliochaguliwa ni mufilisi na haina mashiko. Ni hoja iliyojengwa kwa fikra za mtaani zaidi ya weledi na elimu.

Na mwisho, Mohamed hakueleza kwanini alitumia takwimu za mwaka 1978-1981. Upo uwezekano takwimu hizo zilichukuliwa mahususi kabisa ili kukidhi haja ya matakwa ya ''tafiti'' ambayo hadi hapa tunaona ni namba na wala si tafiti au takwimu.

Inaendelea sehemu ya Pili.
 
Sehemu ya Pili...
Mohamed, vijana wako ambao umeandika na kuwashukuru na hivyo kunyanyua pua zao kuhusu hili nao pia wanapaswa kujibiwa kupitia mwalimu wao.

Nadhani una uwezo mzuri wa kuwasiliana nao kwa lugha mnazowasiliana hasa tukizingatia kuwa hapa tunaongelea hoja na si matusi.
Naomba uwafikishie salamu hizi:

Wakati nikiandika nilifafanunua moja ya hoja za vijana wako kama ifuatavyo:
 
Karibu tena Mo, tulikwambia hata kama ukiondoka mnakasha upo tu na utaendelea. Si umeona uanarudi kutoka likizo as an emergency.

Hizi kutoka kitabu chako ni official stats!
Tusubiri na vitabu vimeagizwa. Hili naliona linaelekea mahali la! naogopa maana linaelekea kuongeza matundu kabisa.
 
Tumalizie viporo vyako.Inaonekana umechanganyikiwa.
Katika fani ya ualimu wa madrasa mwanafunzi anaposhindwa kujibu kwanza huwa tunamchapa,akishindwa zaidi hatuendelei kumchapa huwa tunakariri naye.Hata shule za msingi walimu wetu walituwekea mapengo kujaza ili tushindwe moja kwa moja kupata jawabu.
Kwa upande wako Nguruvi nataka usishindwe moja kwa moja kutoa jawabu ya mfumo kristo.Nakuwekea mapengo ujaze ili jawabu zako zikusafishe na kashfa ya definitiion ya mfumokristo.Najua wewe si mtu wa kuchomoka chomoka.Ukimaliza kipengele 1 tutaendelea na 2 mpaka mwisho wa Lile jawabu langu.
Mfumokristo ni hali ambayo Wakristo wa Tanzania wamehodhi madaraka ya ngazi zote muhimu katika serikali na katika vyombo vya maamuzi, na kuzitumia nafasi hizo kuwaendeleza Wakristo na Ukristo na kuwabagua Waislamu na dini yao.

Hapa jaza tu Kweli si kweli.....................................................

Kuendeleza mfumo wa kibaguzi katika elimu kama ulivyoachwa na wakoloni.

Jawabu yako
......................................................................
....................................................................


ii. Kuzipa shule za wamisheni msaada wa kifedha kutoka kodi za wananchi huku wakizibagua zile za Waislamu (Tazama Roland: 1970: 205,na Cameroon and Dodd 1970:50) .

Jawabu yako
..........................................
..........................................


i. Kuweka mpango mkakati wa kuwabagua na kuwahujumu Waislamu na Uislamu wao. Tazama Roland 1970:205, Kurtz 1972:29. Cameroon and Dodd 1970:114..


Jawabu yako.

.....................................................

...................................................







Jawabu yako.Refusha kidogo majibu..
...................................................................................................................................................................

..................................................................................................................................................................


 
Ami,

Mimi nakusoma taratibu huku nakunywa gahawa naona umeomba Baadhwi ya mapengo yajazwe.

Takuwa mchoyo wa Fadhwila nisipokusoma. Jamaa anasema Waislam wamepungua waliritadi kazi kweli kweli.

Ami, naendelea kukusoma na miwani ya 3D.
 
Last edited by a moderator:

Ami,
Nakuvisha kilemba na nakuwekea kashda begani kwako.

Kilemba hiki na kashda hii nakutunuku kwa niaba ya marehemu
Sheikh Hassan bin Amir.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…