Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Jinsi ninavyoona muelekeo wa mnakasha ni wazi ''fatigue''imetukumba.

Hata mimi sasa sipati maswali ya maana naona watu wanarudia humo kwa
mumo.

Si lazima tumalize kwa ''knockout.''
Tunaweza hata ikawa ''split decision.''

Hilo nalo si dogo.

Nimejitahidi kwa kiasi changu kueleza habari za wazee wangu na naamini
hata wale waliokuwa hawapendi historia hii kwa sababu moja au nyingine
wamesoma kitu.

Basi na tuishie hapa.
Au mnasemaje wanaukumbi?
 

Naona hoja zimekuiishia umeanza viroja.

Kwanza umesema kitabu cha Mohamed Said, ni cha uchochezi. umeshindwa kuthibitisha huo uchochozi mpaka sasa zaidi ya kusema tu neno uchochezi. Pili ukasema kitabu cha Mohamed Said ni ngano. Tatu umesema kitabu cha Mohamed Said ni sawa na kitabu cha aya za kishetani.

Mpaka hapo unazidi kujichanganya mwenyewe na umepoteza mwelekeo.

Namshukuru sana Mohamed kwa darsa ili. Mpaka sasa hivi huu munakasha umeishasomwa na watu zaidi ya elfu kumi.
 

Mohamed Said.

Endelea kutoa darsa kuna watu wengi sana wanasoma hii historia uliyoiandika.

Nachukuwa haya maneno kutoka kwenye kitabu chako.

"Uongo, kama vile nyasi juu ya maji huelea, Atafutae lulu hana budi kupiga mbizi"

Watu wanapiga mbizi kukusoma.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said kwa kweli unatoa darsa zuri sana,umeweka wazi mambo muhimu sana kwa taifa letu.Umeweka wazi ubaya na unafiki wa wale waliotaka waonekane ndio vinara wa harakati za uhuru wa tanganyika.Kwa hili ulilolifanya ni jambo kubwa sana athari yake itabaki milele.Mungu atakulipa kwa hili
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said kwa kweli unatoa darsa zuri sana,umeweka wazi mambo muhimu sana kwa taifa letu.Umeweka wazi ubaya na unafiki wa wale waliotaka waonekane ndio vinara wa harakati za uhuru wa tanganyika.Kwa hili ulilolifanya ni jambo kubwa sana athari yake itabaki milele.Mungu atakulipa kwa hili
 
Last edited by a moderator:

Mzee ni kweli; ila kama utakubaliana na haya yafuatayo kwa jinsi ambavyo tumefika naamini mnakasha utakuwa umefikia kikomo.

a. Ukubali kuwa hukuandika historia yote ya wapigania uhuru wa Tanganyika bali umeandika sehemu ya historia hiyo.

b. Katika kuandika historia hiyo ukubali kuwa hukutafuta vyanzo vyote credible vya taarifa ulizotumia na badala yake umetumia vyanzo vya upande mmoja tu na ni vile vyenye muono wako tu ndivyo umekubali.

c. Ukubali pia kwamba ili kufanya simulizi lako lionekane kuwa lina chembe ya historia imekulazimu kuweka kando majina ya wapigania uhuru wengine wote ambao ni Wakristu kwani kuwajumuisha miongoni mwa 'wazee wako' kutaharibu ile sura ya kuwa wapigania uhuru wengi wa mwanzo walikuwa ni Waislamu watupu kama unavyotaka watu waamini.

d. Ukubali pia kwamba katika kupinga kwako dhulma dhidi ya Waislamu au Uislamu au Tanganyika kuna kasoro kwani unaamini Nyerere alikuwa na dhulma dhidi ya Waislamu kwa sababu ni Mkristu lakini unaamini Waislamu sasa hivi hawadhulumiwi chini ya utawala wa Kikwete - Muislamu.

e. Ukubali pia kuwa hujajaribu hata kidogo kujenga mapatano kati ya Wakristu na Waislamu nchini na badala yake umekuwa ukichochea chuki kati ya watu wa pande hizi mbili kiasi kwamba unataka Waislamu wasiangalie adui yao kama mfumo wa kisiasa uliojengwa na CCM na wafikirie adui yao ni Kanisa na Wakristu.

Ukikubali mambo haya matano tulipofikia hapa huu mnakasha utakuwa umefikia mwisho.

Shukrani.
 
mbona wapo wakristo aliowataja katika harakati za uhuru katika kitabu chake.Ila ameweka wazi kwamba amewaelezea zaidi wazee wake ambao kwa makusudi yule mzanaki kaamua kuficha ili historia imtambue yeye ndo aliyeongoza harakati za kudai uhuru Mohamed Said Kaweka wazi mambo mengi lakini ajabu mnataka aandike mnavyotaka nyinyi.Busara kaeni chini nanyi muandike kitabu chenu,povu mbona linawatoka.Unataka akubali,nyinyi mbona hamkubali
 
Last edited by a moderator:

Haya uliyosema kama unayaona ni mapungufu basi ni wakati wa wewe kuandika historia iliyokamilika kuliko kupinga tu.
 
mbona mengi yameshaelezwa ndani ya uzi huu.Kujaribu kuficha juu ya wapigania uhuru wengine na kujiweka yeye kama kiongozi na mwasisi wa TANU.Kushirikiana na kanisa kuwakandamiza waislamu nk yote haya na mengine yamewafanya mtoke povu wakristo
Na ndiyo maana akaulizwa, Mwinyi na Kikwete nao vipi? Mbona inapokuja kwa rais muislam basi hatajwi yeye bali serikali?
Angekuwa ni rais Mkristu wakati huu akina Ponda na wenzake wanasota jela si mngesema kama wakati ule wa Nyerere eti aliwakamata mashehe na kuwaweka ndani!?
Mohamed Said akiulizwa hayo anakwepa na kusema anazungumzia historia ya TANU tu...lakini tukitega mgongo anakwenda mbele zaidi na kuzungumzia dhulma alizowafanyia Nyerere waislam kwa kushirikiana na Kanisa. Yote kuanzia kutowaenzi wapigania uhuru wa kiislam. Kuanzishwa BAKWATA. Kukandamiza waislam kielemu kupitia wizara ya elimu nk.
Hebu angalia hapa.
Baada kumfuatilia kidogo kuhusu hilo hapo juu, anatupa jibu hili...
By Mohamed Said



Haitawezekana kwa sasa.

Katika kikao kilichofanyika Dar es Salaam cha wadau wa
elimu Waislam hawakuruhusiwa hata na karatasi moja kutokanayo
nje ya ukumbi.
Tunae rais muislam na waziri wa elimu muislam. Wote hawa wanashirikiana na Kanisa kuwakandamiza waislam kielimu kama mlivyosema Nyerere alishirikiana na Kanisa kuwakandamiza waislam kielimu?
 
Hongera Mohammed Said kwa elimu unayotupatia wengi tunafunguka macho baada ya upogo wa muda mrefu katika vitabu vyetu vya historia mashuleni. May Almighty increase unto u more power to deliver this knowledge.
 
Usimlaumu nadhani hajui uzito wa vyuo hivyo. Unajua hata nilipowaambia kuwa kitabu changu
kimefanyiwa review na maprofesa wawili wa historia na review hizo zimo katika Cambridge Journal
of African History walibeza.

Hapo ndipo nikajua kuwa kati ya mawili hawa ni wachache wa elimu au wana husda inawala.

Mimi walimu wangu mpaka leo na wengine washastaafu heshima hii hawakujaaliwa.

Twende nao hivi hivi taratibu na tujitahidi kuwaeleza kuwa hivyo ni vyuo vikubwa duniani si
vya kubezwa.
 
Ahsante hilo ni shairi la John Dryden.

Linasomeka hivi:

Errors, like straws, upon the surface flow;
He who would search for pearls must dive below.

Kwa hakika katika historia hii uongo ukawa umezagaa
kote sasa kutafuta ukweli ikabidi nipige mbizi nende chini
ya bahari.

Huu ukweli umewashtua watu wengi sana.
Imekuwa tabu sana kukubali kuwa hiyo historia iliyokuwa ikisomeshwa
Miaka nenda miaka rudi haikuwa historia ya kweli.

Mambo mengi yalikuwa yamekwepwa tena kwa makusudi kabisa.
Vipi uandike historia ya TANU usimtaje Abdu Sykes?
 


out of the point,,
sasa unataka kikwete alipe kisasi??
Hoja hujibiwa kwa hoja,usitafute visingizio ndugu.
 
Hilo swali la Mwinyi ni nje ya maudhui lakini nimeeleza kuwa nilialikwa
Kenyatta University mwaka 2006 na nilieleza mengi kuhusu utawala wa
Mwinyi na uhusiano wake na Waislam.

Ikiwa wanaukumbi watapenda nitaiweka hiyo paper humu. Ila kwa mimi
kuingiza hilo la Mwinyi hapa ni kutambaza majadiliano na hili katika usomi
halifai.

Kuna kitu kinaitwa ''demarcation''yaani mipaka katika somo.
Sitaki kujivunjia heshima yangu kwa kuacha kufata taratibu na sheria za mijadala.

Mimi sikwepi wala sikimbii swali.
kama swali silijui jibu lake ninasema sijui.
 
Mwanakijiji, Unatakiwa uerevuke kidogo na kupunguza ushabiki. Awali ya yote hakuna mtu binafsi anayeweza kuandika historia nzima ya nchi bali kila mtu anaandika baadhwi tu ya sehemu , sasa ni jukumu la Serikali kuzikusanya historia hizo na kurtoa historia ya nchi. Lakin pia naamini wazi hujakisoma kitabu cha Mohamed Said kwani ndanimwe ametaja mpaka wakristo na amewaeleza kwa vizuri tu kama walitenda vizuri na vile vile amebainisha hata baadhwi ya waislam kwa mabaya yao. nakushauri kisome Kisome kitabu cha Mohamed said KWA NIA YA KUELEWA basi mola atakusaidia utaelewa lakin kama utakisoma KWA NIA YA KUPINGA basi hasilan hautakielewa. Pole sana
 
Huku ni kuishiwa na kufilisika kwa hoja. Nilibainisha toka awali kuwa nina mashaka makubwa sana kitaaluma na huyu Y Nyerere kwani nilimwambia kuwa Tafiti yoyote inajibiwa kwa tafiti na sio vinginevyo. sasa hapa amejidhihirisha kuwa ni mtupu wa ilmu. Kwani sikutaraji kwa msomi yoyote kukifananisha kitabu cha S. Rushdie cha Satani verses na kitabu cha M Said. Kwani hicho satanic verses ni fiction na cha Mohamed Said ni cha Kitaaluma. Huwezi hata siku moja kuchanganya chumvi na sukari kisha ukajisifu. Pole sana
 
Mzee Mohamed,
Unajua kinachohubiriwa sasa kwenye misikiti na mihadhara ya Kiislam sio wazee wako kusahaulika. Agenda imepanuka zaidi na kuwa chuki ya ajabu kwa Mwalimu na ule mfumo wako wa kufikirika maarufu kama "MfumoKristu". Tanzania itabaki salama?
 
 
Unajua tatizo lako ni kuwa una shida katika uelewa wa mambo haya.

Itakubidi upige goti kwa walimu usomeshwe na hili si gumu wewe
bado mtoto.

Hakuna kitabu kilichokamilika duniani.
Lakini vipo vitabu vilivyoandikwa kwa kupotoshwa.

Hivyo vya kupotoshwa tuviache kwa sababu huwa vinajizika wenyewe.

Tuje katika vitabu vilivyoandikwa na wasomi makini.

Tuje kwa Iliffe 'Á Modern History of Tanganyika' London, Cambridge
University, 1977.

Illife ni msomi mkubwa sana mimi siwezi kuruhusiwa hata kubeba
viatu vyake.

Kitabu chake ni kizuri sana kuhusu historia ya Tanganyika.
Kaandika kile alichotafiti na kuna mambo mengine mle hamna.

Abdu Sykes kamtaja katika kitabu chake lakini hakumtaja Sheikh
Hassan bin Amir.

Mimi si kuwa nimmemtaja Sheikh Hassan bin Amir peke yake nimeeleza
jinsi wanafunzi wake walivyofanikiwa kuipa TANU wanachama na kwengine
viongozi wa awali nk. nk.

Tuje kwenye kitabu changu na hili nimelisema mara kadhaa wala si swali wewe
kulileta tena kwangu.

Nimesema na nyinyi andikeni mchango wa wazee wenu katika kupigania uhuru wa
Tanganyika.

Badala ya kushughulishwa na hili mmekazania kunishambulia mimi.
Mimi nimekuelezeni kuwa hiyo haitasaidia kwa kuwa kitabu changu kimekubalika
na kinasomeshwa vyuo vikuu vyote vyenye idara ya African Studies.

Hayo mengine sina haja ya kuyazungumzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…