Mzee ni kweli; ila kama utakubaliana na haya yafuatayo kwa jinsi ambavyo tumefika naamini mnakasha utakuwa umefikia kikomo.
a. Ukubali kuwa hukuandika historia yote ya wapigania uhuru wa Tanganyika bali umeandika sehemu ya historia hiyo.(AMEANDIKA HISTORIA YA WALE AMBAO WALIFUTWA KWA MAKUSUDI ILI KUFICHA MCHANGO WAO KATIKA UKOMBOZI WA NCHI HII,TUNASHUKURU TULIOKAWA HATUFAHAM SASA TUMETOKA GIZANI,UKIWEMO WEWE..!
b. Katika kuandika historia hiyo ukubali kuwa hukutafuta vyanzo vyote credible vya taarifa ulizotumia na badala yake umetumia vyanzo vya upande mmoja tu na ni vile vyenye muono wako tu ndivyo umekubali.(VYANZO VILIVOTUMIKA NI CREDIBLE NA VYENYE KUJITOSHELEZA,,KAMA WAMEKUBALI TAASISI KUBWA ZENYE WELEDI MKUBWA ULIMWENGUNI WA KUHOJI MANTIKI KAMA OXFORD,CAMBRIDGE NA HAVARD SEMBUSE WEWE??
c. Ukubali pia kwamba ili kufanya simulizi lako lionekane kuwa lina chembe ya historia imekulazimu kuweka kando majina ya wapigania uhuru wengine wote ambao ni Wakristu kwani kuwajumuisha miongoni mwa 'wazee wako' kutaharibu ile sura ya kuwa wapigania uhuru wengi wa mwanzo walikuwa ni Waislamu watupu kama unavyotaka watu waamini.(..:nono:
:nono:SI KWELI,WAPO WAKRISTU ALIOWATAJA,NA USIJARIBU KUPOTOSHA NDUGU,ILA KAANDIKA KWA KIAS KIKUBWA KUHUSU WAZEE WAKE AMBAO MOJA KWA MOJA ANAWAFAHAM NA ANA TAARIFA ZAO ZA KUTOSHA KAMA WALIVOKAWA NAZO KINA JULIUS KIPINDI HIKO LAKINI KWA MAKUSUDI YAO KABISA WAKAAMUA KUWAFUTA KATIKA HISTORIA HIYO,TUMPONGEZE NDUGU MOH'SAID KWA HILO)
d. Ukubali pia kwamba katika kupinga kwako dhulma dhidi ya Waislamu au Uislamu au Tanganyika kuna kasoro kwani unaamini Nyerere alikuwa na dhulma dhidi ya Waislamu kwa sababu ni Mkristu lakini unaamini Waislamu sasa hivi hawadhulumiwi chini ya utawala wa Kikwete - Muislamu.(KIPIMO CHA NYERERE CHA DHULMA YAKE NI KUDHARAU JUHUDI WALIZOZIFANYA WAASISI WA WA KUPIGANIA UHURU HUO KABLA YEYE HAJAKARIBISHWA MJINI NA KUJIVISHA KWA MABAVU JUHUDI HIZO ILI LEO APATE KUITWA MTAKATIFU,ILA TUNASIKITIKA HILO LIMEFELI KWA KIZAZI HIKI NA VIZAZI VYOTE VINAVOKUJA)
e. Ukubali pia kuwa hujajaribu hata kidogo kujenga mapatano kati ya Wakristu na Waislamu nchini na badala yake umekuwa ukichochea chuki kati ya watu wa pande hizi mbili kiasi kwamba unataka Waislamu wasiangalie adui yao kama mfumo wa kisiasa uliojengwa na CCM na wafikirie adui yao ni Kanisa na Wakristu. (KAMA KUELEZEA HISTORIA YA WAZEE WAKE KIUNAGA UBAGA NI KUCHOCHEA CHUKI DHIDI YA WAKRISTO NI UZANDIKI WA MANENO,UTUELEZE CHUKI HIYO IMECHOCHEWA KWA NAMNA GANI?KAMA ANGEKUWA MCHOCHEZI KWANI USIENDE KUMFUNGULIA MASHTAKA KORTINI AU KWANIN SASA NI MIAKA 15 KITABU HIKI KINASOMWA SERIKALI ISIMCHUKULIE HATUA NA HALI INAMFAHAM?UTAJA ONA HOJA ZAKO HAZINA MASHIKO NA UNAPATA UKAKASI KUUMEZA UKWELI HUU,JITAHID KUUVUMILIA TUH NA UUMEZE KIUTU UZIMA NDUGU?
Ukikubali mambo haya matano tulipofikia hapa huu mnakasha utakuwa umefikia mwisho.
Shukrani.(MJADALA HAUWEZ KUFIKA MWSHO HADI MKIRI KWA DHATI YA MIOYO YENU NA MJE MSHUKURU KWA DARSA MARIDHAWA KAMA HILI.
AHSANTE KWAKO MZEE MOH' SAID,UKWELI UNAZID KUDHIHIRI.