Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Still beating around the bush! Unachotakiwa ni kukanusha kwanza halafu ueleze unachokijua. Mag3 alisema nyumba hiyo ilitolewa na David Cameron ambaye wewe umemwandika kama liberal governor.
Nguruvi3, swali lako lilikuja kujibiwa kama nitakavyomnukuu Son of Alaska, hapa chini;
Kuhusu kuanzishwa kwa chama cha siasa TANU, historia yake kwa ufupi ni hii;
Ni Mwalimu Nyerere, kama Raisi wa TAA aliyetoa uamuzi tarehe 10 Octoba 1953 kwamba sasa TAA basi, muda muafaka kwa chama cha siasa kuzaliwa umewadia! Hizo longolongo zingine kuhusu nani alikuwa kinyozi mtaa gani, nani alikuwa mchuuzi sokoni au nani alikuwa shoga yake nani, hayo tuwaachie wapiga porojo mabarazani.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Said shukran kwa darsa #2 . Nakikumbuka hiki kitabu na visa ulivyoviweka (nadhani ndicho cha Maisha ya Abdulwahid Sykes, sina uhakika sana) nilikisoma some years ago. Ila bwana wee, Yanga na Simba walishasoma Ahlil badri(sijui tarehe)kwa hiyo tusiyakuze kupita mapimo yake. Uzuri wa artiles zako ni kuwa, huyu mwandishi kachukua mtazamo wake wa Islamic-bias toka awali. Hana kosa na wala sio tatizo. Ndivyo alivyoamua. Kesho atakuja mwingine ataandika christian outlook. Lakini pia uzuri wa bwana huyu hajaandika kwenye kitabu chake kuwa Watanganyika wasiokuwa Waislamu waliikataa TAA, TANU, au waliikataa migomo kama ule wa TRAU, bandari, au waliisusia mikutano ya Bibi Titi au waliugomea uhuru. Hajasema vitu kama hivyo. Hawezi kulaumiwa. Wahindi pia wakitaka kuandika mchango wa dini yao kwenye uhuru wa Tanganyika mashallah, tutanunua vitabu. Nisichokubali ni kumhukumu mtu AWALI kwa imani yake ya dini. Ndio maana napinga nia yoyote ya kuonesha kuwa mtumishi (mwajiriwa wakati ule) aliyekuwa anatimiza masharti ya ajira yake eti hakuwa mzalendo. Hata leo twaona wafanyakazi wanapogoma kama UDSM, Muhimbili, Bugando etc. mabosi wao HAWAJIUNGI nao hata kama kiroho wapo nao. Kwa hiyo kama mwandishi anataka kujenga taswira eti Fredrick Mchauru alipowasihi TRAU warudi kazini alifanya hivyo kwa sababu hakuwa na machungu na sababu sio mwislamu (na sio kwamba alikuwa kiongozi wa taasisi husika) basi atakuwa amekosa uadilifu katika kuiandika historia. Mi nadhani hakuwa na maana hiyo.
 

Na Nyerere huyu huyu mnayemsema udini akamwachia urais Ali Hassan Mwinyi. Nyerere angeweza kuunda mazingara kama alivyofanya Kenyatta kwamba rais yeyote atakayefuata lazima akubalike kwa Wakikuyu. Hii haipo Tanzania. Leo Tanzania hatuna kundi lolote la kikabila linaloweza kusema kuwa rais tunayemtaka sisi ndiye lazima awe. Lakini Kenya wanalo. That is the difference.
 
Whaat? inaonekana huijui historia ya nchi yako!! tumetwangana sana....

Wenye hulka za kutwangana wanatoka maeneo anayotoka Mwalimu! angalia mara vita vya wakurya na watani wao!,
MM,
Tupe ushahidi kama unao kwamba Tanganyika tulitwangana sana ili tupate Ilm na darsa kama anavyofundisha mwenzako MS.
 
Makabila ya Wajaluo na Wakurya katika vijiji vya Kitenga na Nyanduga kata za Koria na Bumera.

RITZ,
we ni kiboko yaani jamaa wanauliza na wewe unajibu tena kwa uhakika! hivi anaishi wapi huyu asiejua kuna vita vya kikabila huko anakotoka Baba yao wa taifa? Mwalimu alisahau charity begins at home?
 
Na kile kitabu alichoandika Mbotela wa Mombasa, "Uhuru wa Watumwa" kilikuwa riwaya tu. Hakuna mtumwa aliyepelekwa Arabuni wachilia mbali wale waliohasiwa ili wasihujumu "harems' za ma'ustaadh.

Jasusi,

Njoo na data na facts za kutosha kuhusu watumwa waliohasiwa.

Halafu sijui umeipata wapi kuwa nusu ya Wasaudia Arabia ni Watumwa.

Nashangaa sana mwandishi wa habari kama wewe unaokota habari mitaani bila utafiti wa kutosha.

Soma historia ya Saudia Arabia hilo ni taifa kongwe tofauti na Marekani.
 

Kwahiyo Nyerere alipoingia madarakani ndipo vita hivyo vikasimama? na kikao cha kusuluhisha makabila yaliyokuwa yakipigana kilifanyika wapi? ni Nyerere ndie aliesimamia au alimtuma Kambona na Kawawa kwaniaba yake wakasuluhishe? hembu tupe darsa la vita vya makabila ya Tanganyika somo jipya hili! huko kwetu Kibosho mpaka leo kuna kuibiana kuku na vifaranga kati ya Wakibosho na Wamachame na kati ya wa Kirua na wa Kishmundu na panatokea kukatana mapanga mpaka mauaji lakini sijasikia hata siku moja vikiitwa ni vita vya makabila ya Tanganyika au ugaidi!
 
RITZ,
we ni kiboko yaani jamaa wanauliza na wewe unajibu tena kwa uhakika! hivi anaishi wapi huyu asiejua kuna vita vya kikabila huko anakotoka Baba yao wa taifa? Mwalimu alisahau charity begins at home?

Kadogoo,

Hawa jamaa wanachekesha kwao Musoma kashindwa kuwatuliza ndiyo kuna tabia za kukatana mapanga, mikuki, mishale.
 
Last edited by a moderator:

Siku hizi kuna utumwa mamboleo! mfano: Serikali au chama cha siasa kuomba mikopo na misaada toka nchi tajiri na kukubali masharti yao!
 

Kadogoo,

Wewe mbaya...
 
Last edited by a moderator:



Huku ndiko kuazimia kisitokee tena?
 

Kama Mohammed Said angefuata 'historical method' ya kuandika matukio ya historia asingeweza kufikia mahitimisho aliyofikia na wala asingejenga hoja alizojenga. Yeye hakutaka kuandika historia kisayansi; yeye kaandika kama 'alivyojua' au alivyosimuliwa. Haijalishi kama chanzo cha habari kilikuwa biased or not au kama hakukuwa na ushahidi. Kwake ushahidi ni "wazee wangu'. Kwa vile wazee walimsimulia basi yeye kaamini kabisa na akatoka hapo akaenda kuwasimulia wengine.

Fikiria mtu anasimuliwa na mzee wake.

Mwanangu unajua wakati wa Vita ya Idi Amin mimi nilitafutwa na mtu wa Ikulu; akaniambia kuwa natakiwa kuripoti pale Lugalo Jeshini. Huyu bwana alikuwa anafahamika sana na miye nilikuwa na mfahamu, tumeishi mtaa mmoja. Basi miye nikatii agizo nikaenda kuripoti pale Lugalo. Pale nikamkuta Major Jenerali Tumainieli Kiwelu, Generali Musuguri, Brigedia Generali Mwita Kyaro pamoja na maafisa wengi tu wa jeshi.

Basi wakaniuliza juu ya utalamu wangu wa mambo ya simu, nikawaeleza na wakata niwape ushauri wa jinsi ya kuweza kuvuruga simu za Jeshi la Uganda. Wakaniapisha kuwa kile nilichoshiriki kufanya ni siri kuu (top secret). Mwanangu nakuambia ushindi wa Tanzania dhidi ya Uganda usingewezekana bila ya mchango wangu ule. Hii ilikuwa ni mwaka 1975 wakati vita ndio inaanza.


Basi na mtoto naye anaamini hilo simulizi; anakuwa mtu mzima na kufuatilia na kukuta ni kweli baba yake alishiriki vita ya Uganda na kutoka hapo anaanza kusimulia "mchango uliosahauliwa' wa baba yake. Sasa watu wote watakaosikia hilo simulizi watakuwa na uchaguzi mmoja tu kukubali au kukataa. Lakini wapo ambao watapenda kuhoji kidogo ukweli wa hiyo habari kwa kadiri inavyowezekana.

Mohammed Said amesimuliwa mengi sana na wazee wake na mengi ameyaona - ikumbukwe wakati wa harakati za Uhuru yeye hakuwa na umri wa kuweza kusema alikuwa sehemu ya harakati hizo; yote anayoyasimulia ni masimulizi kutoka kwa watu wengine au kujisomea kutoka maandishi ya watu mbalimbali - hasa kutoka kwa Iliffe. Ndio maana hapendi kujibu maswali mengi yanayohusiana na substance ya maandishi yake.
 

Mbona kila tunapokaribia na weekend tunaanza kutapika matusi?
 
Hakuna mahali nimesema utumwa ulifanywa na Waislamu.
Dunia ya sasa imetawaliwa sana na propaganda hata hivyo bahati mbaya ni kuwa sote tumekuwa wajanja wa kung'amua kinachoendelea.Kila siku Kikwete akilazimishwa kimazingira kujibu hoja za udini na kutoa kauli mbovu kwa waislamu wenzake walio wengi wataamini kuwa kuna udini na hatua zitakazochukuliwa hata kama ni za dhulma kwa waislamu watakaohoji ni wachache tu.Hapo maaskofu itakuwa wamepatia kupambana na uislamu uliowashindwa kupitia mijadala ya majukwaani.
Hivyo hivyo ikiandikwa kuwa waarabu ndio waliofanya biashara ya utumwa huku ikioneshwa kuwa waarabu ndio waislamu zaidi na walioleta uislamu Afrika basi moja kwa moja itakuwa umewatisha wanafunzi na kuwafanya wauchukie uislamu.

Nilichosema ni kuwa utumwa wa Afrika mashariki ulifanywa na Waarabu..
Hiki unachoonekana kuwa na uhakika nacho jee una mfano wowote kuthibitisha?.
 

Kwa kigezo hicho utaona kuwa Mwalimu wenu Mohammed Said anatakiwa awe kihiyo na kanjanja nambari moja kwani maandishi yake yamejaa "inawezekana", "inasemekana" na "huenda"...!!
 

Wickama,
Nakusoma na naona unavyijitahidi kutembea katikati.

Hilo unaweza ukafanikiwa kwengine lakini si katika historia
hii ya uhuru wa Tanganyika.

Jaribu kuandika historia ya uhuru wa Kenya bila ya Mau Mau.
 
Wakulaumiwa hapa ni huyo mzee wenu Mohamed Said aliyechochea chuki na uhasama wa kidini hapa nchini na haya ndio matunda yake. Cha ajabu nyie wafuasi wake mnajifanya hamnazo kutwa kuchwa mpo hapa kumpa masifa kem kem! Shame on you all!

Mkuu,
huu si wakati wa kunyoosheana vidole! kabla mambo hayajaharibika kuna ulazima wa kukaa chini na kujadili matatizo yote kwa uwazi na ukweli! na kama pande zote zitakaa kwa nia njema basi huenda pakawa na muafaka! nakuhakikishia kuwa Waislamu TZ hawatakuwa watu wa kwanza kuleta machafuko!
 

Kadogoo,
Jasusi aliniuliza wapi Sivalon kaandika kusema kuwa Kanisa Katoliki limesema Uislam ni adui wake?

Mimi sitosema kitu.
Naachia hapa.
 

Kenyatta alikuwa Mkikuyu lakini Arap Moi hakuwa Mkikuyu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…