THE BIG SHOW
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 16,950
- 13,527
Kama Mohammed Said angefuata 'historical method' ya kuandika matukio ya historia asingeweza kufikia mahitimisho aliyofikia na wala asingejenga hoja alizojenga. Yeye hakutaka kuandika historia kisayansi; yeye kaandika kama 'alivyojua' au alivyosimuliwa. Haijalishi kama chanzo cha habari kilikuwa biased or not au kama hakukuwa na ushahidi. Kwake ushahidi ni "wazee wangu'. Kwa vile wazee walimsimulia basi yeye kaamini kabisa na akatoka hapo akaenda kuwasimulia wengine.
Fikiria mtu anasimuliwa na mzee wake.
Mwanangu unajua wakati wa Vita ya Idi Amin mimi nilitafutwa na mtu wa Ikulu; akaniambia kuwa natakiwa kuripoti pale Lugalo Jeshini. Huyu bwana alikuwa anafahamika sana na miye nilikuwa na mfahamu, tumeishi mtaa mmoja. Basi miye nikatii agizo nikaenda kuripoti pale Lugalo. Pale nikamkuta Major Jenerali Tumainieli Kiwelu, Generali Musuguri, Brigedia Generali Mwita Kyaro pamoja na maafisa wengi tu wa jeshi.
Basi wakaniuliza juu ya utalamu wangu wa mambo ya simu, nikawaeleza na wakata niwape ushauri wa jinsi ya kuweza kuvuruga simu za Jeshi la Uganda. Wakaniapisha kuwa kile nilichoshiriki kufanya ni siri kuu (top secret). Mwanangu nakuambia ushindi wa Tanzania dhidi ya Uganda usingewezekana bila ya mchango wangu ule. Hii ilikuwa ni mwaka 1975 wakati vita ndio inaanza.
Basi na mtoto naye anaamini hilo simulizi; anakuwa mtu mzima na kufuatilia na kukuta ni kweli baba yake alishiriki vita ya Uganda na kutoka hapo anaanza kusimulia "mchango uliosahauliwa' wa baba yake. Sasa watu wote watakaosikia hilo simulizi watakuwa na uchaguzi mmoja tu kukubali au kukataa. Lakini wapo ambao watapenda kuhoji kidogo ukweli wa hiyo habari kwa kadiri inavyowezekana.
Mohammed Said amesimuliwa mengi sana na wazee wake na mengi ameyaona - ikumbukwe wakati wa harakati za Uhuru yeye hakuwa na umri wa kuweza kusema alikuwa sehemu ya harakati hizo; yote anayoyasimulia ni masimulizi kutoka kwa watu wengine au kujisomea kutoka maandishi ya watu mbalimbali - hasa kutoka kwa Iliffe. Ndio maana hapendi kujibu maswali mengi yanayohusiana na substance ya maandishi yake.
Dah Aisee,kweli kumbe kuna watu wameamua kabisa kupinga kwa kila namna waionayo wao inafaa..
Ina maana huyu rejea zote alizopewa hajaziona au??
What a shame..!