Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kama Mohammed Said angefuata 'historical method' ya kuandika matukio ya historia asingeweza kufikia mahitimisho aliyofikia na wala asingejenga hoja alizojenga. Yeye hakutaka kuandika historia kisayansi; yeye kaandika kama 'alivyojua' au alivyosimuliwa. Haijalishi kama chanzo cha habari kilikuwa biased or not au kama hakukuwa na ushahidi. Kwake ushahidi ni "wazee wangu'. Kwa vile wazee walimsimulia basi yeye kaamini kabisa na akatoka hapo akaenda kuwasimulia wengine.

Fikiria mtu anasimuliwa na mzee wake.

Mwanangu unajua wakati wa Vita ya Idi Amin mimi nilitafutwa na mtu wa Ikulu; akaniambia kuwa natakiwa kuripoti pale Lugalo Jeshini. Huyu bwana alikuwa anafahamika sana na miye nilikuwa na mfahamu, tumeishi mtaa mmoja. Basi miye nikatii agizo nikaenda kuripoti pale Lugalo. Pale nikamkuta Major Jenerali Tumainieli Kiwelu, Generali Musuguri, Brigedia Generali Mwita Kyaro pamoja na maafisa wengi tu wa jeshi.

Basi wakaniuliza juu ya utalamu wangu wa mambo ya simu, nikawaeleza na wakata niwape ushauri wa jinsi ya kuweza kuvuruga simu za Jeshi la Uganda. Wakaniapisha kuwa kile nilichoshiriki kufanya ni siri kuu (top secret). Mwanangu nakuambia ushindi wa Tanzania dhidi ya Uganda usingewezekana bila ya mchango wangu ule. Hii ilikuwa ni mwaka 1975 wakati vita ndio inaanza.

Basi na mtoto naye anaamini hilo simulizi; anakuwa mtu mzima na kufuatilia na kukuta ni kweli baba yake alishiriki vita ya Uganda na kutoka hapo anaanza kusimulia "mchango uliosahauliwa' wa baba yake. Sasa watu wote watakaosikia hilo simulizi watakuwa na uchaguzi mmoja tu kukubali au kukataa. Lakini wapo ambao watapenda kuhoji kidogo ukweli wa hiyo habari kwa kadiri inavyowezekana.

Mohammed Said amesimuliwa mengi sana na wazee wake na mengi ameyaona - ikumbukwe wakati wa harakati za Uhuru yeye hakuwa na umri wa kuweza kusema alikuwa sehemu ya harakati hizo; yote anayoyasimulia ni masimulizi kutoka kwa watu wengine au kujisomea kutoka maandishi ya watu mbalimbali - hasa kutoka kwa Iliffe. Ndio maana hapendi kujibu maswali mengi yanayohusiana na substance ya maandishi yake.

Dah Aisee,kweli kumbe kuna watu wameamua kabisa kupinga kwa kila namna waionayo wao inafaa..
Ina maana huyu rejea zote alizopewa hajaziona au??
What a shame..!
 
Kadogoo, wakati mwingine huwa unanishangaza kweli kweli...sijui kama ni ubishi tu wa kitoto ama ni ukosefu wa elimu tosha. Kweli hujui historia ya utumwa? Utumwa wa bahari ya Atlantic uliendeshwa na Wazungu lakini utumwa wa bahari ya Hindi uliendeshwa na Waarabu na ndio uliodumu kwa kipindi kirefu hata baada ya kupigwa marufuku...ilibidi nguvu za ziada zitumike kuwabana mamwinyi wa Kiarabu kuachana na biashara ya utumwa. Source, kama unataka zimejaa mtandaoni na wala si siri...kwa mfano bonyeza hapa;

Kadogoo, kuna mambo ya kuweza kuzua mjadala lakini kwa hili la utumwa nakuomba uanzishe mada ya peke yake uweze kupewa darasa. Ila hapa kwenye mada hii tutaendelea kukosoa maandiko potofu ambayo mhusika, Mohamed Said, kwa hila aliamua kuipotosha sehemu ya jamii akiwalenga wale wenye uelewa duni.

ETI,,"THERE WAS NO ABOLITIONIST MOVEMENTS WHICH DEVELOPED OUT OF ISLAM OR MUSLIM COUNTRIES"
Propaganda kama hizo katafute watoto wa chekechea uwalishe,uislam katika suala la watumwa tokea ufunuo unashuka ulishakemea mambo hayo,very clearly,tena kwa aya mbali mbali na ukihitaji hapa tunakuwekea,
hao kwa kuona dini fulani ilijihusisha moja kwa moja kwenye biashara hiyo basi wakataka katika kuelezea historia hiyo basi waijumuishe dini nyingine kwa kutumia mwamvuli wa waarabu washenz washenz ili ionekane kuwa dini fulani au zote zimehusika na zina case ya kujibu,
umefeli katika hilo kama walivofeli hao waliokumezesha historia hiyo..
 
THE BIG SHOW,

..sasa na hawa wazee wa gerezani mnaodai walikomboa Tanganyika na wenyewe mliwapitia mmoja mmoja na kuwahakiki na kuwathibitisha kwamba ni Waislamu??

..kuna mahali nimesoma kwamba kulikuwa kunafanyika mpaka matambiko ya kimila. tena kuna kisa cha tambiko moja ambapo walitaka kumvika Mwalimu Nyerere ngozi mbichi ya mbuzi. inasemekana Mwalimu alikataa kutokana na imani yake. kisa hicho nimekisoma ktk gazeti la raia mwema.

..pia kuna tambiko lilifanyika kwa Mzee Jumbe Tambaza. hili Mwalimu alilisimulia mwenyewe kwenye ile hotuba yake kuwaaga wazee wa Dsm.

..ndiyo maana wengine tunasema harakati zile zilisukumwa na suala la UZALENDO kuliko imani za kidini.

cc: Nguruvi3, Jasusi

Well,niseme mimi kama mimi nikubaliane na hoja yako,,
Nakuuliza swali,kama harakati hizo zilisukumwa na suala la uzalendo kuliko imani za kidini,iweje sasa wengine wafutwe na kupuuzwa huku wengine watukuzwe na hadi kufikiwa kupewa ubaba wa taifa??
Na kwanin wale waliopuuzwa wengiwao upo ushahid unaonesha kuwa walikuwa ni watu wa imani ya Mohammed na wale waliotukuzwa wameonekana sana ya kwamba walikuwa ni watu wa iman ya jesus of nazareti?
Kuna nini hapo?Mohammed lost and jesus won? or jihad failed and crusade won?
Nyie wenyewe mmeyasababisha,watu wakichambua yakiwa makavu makavu mnasema wachochez,sasa hiyo akili au matope??
 
ETI,,"THERE WAS NO ABOLITIONIST MOVEMENTS WHICH DEVELOPED OUT OF ISLAM OR MUSLIM COUNTRIES"
Propaganda kama hizo katafute watoto wa chekechea uwalishe,uislam katika suala la watumwa tokea ufunuo unashuka ulishakemea mambo hayo,very clearly,tena kwa aya mbali mbali na ukihitaji hapa tunakuwekea,
hao kwa kuona dini fulani ilijihusisha moja kwa moja kwenye biashara hiyo basi wakataka katika kuelezea historia hiyo basi waijumuishe dini nyingine kwa kutumia mwamvuli wa waarabu washenz washenz ili ionekane kuwa dini fulani au zote zimehusika na zina case ya kujibu,
umefeli katika hilo kama walivofeli hao waliokumezesha historia hiyo..

Utumwa ulikuwepo na waarab walioleta uislam ndio waliokua na utumwa mbaya zaidi kukataa hili ni kukataa historia .
Vp kuna ukweli kuhusu uislamu kuanza kwa kusilimisha watu kwa upanga yaani 'jihad' na kwamba utaisha kwa 'jihad' aka the sixth pillar of islam.

Dont take my word for it :

Jihad-(English-pronunciation:-/dʒɪˈhɑːd/;-Arabic:جهاد‎-ǧihād-[dʒiˈhæːd]), an-Islamic term, is a religious duty of-Muslims. In-Arabic, the wordjihād-translates as a noun meaning "struggle".Jihad-appears 41 times in the-Quran-and frequently in the idiomatic expression "striving in the way of God-(al-jihad fi sabil-Allah)".[1][2][3]-A person engaged in jihad is called a-mujahid; the plural is-mujahideen. Jihad is an important religious duty for Muslims. A minority among theSunni scholars-sometimes refer to this duty as the sixth-pillar of Islam
Source -wikipedia

Here its interesting to note that the terror organization under Osama that fought the USSR to its fall was 'Mujahideen'

What I am trying to stress is that religion is used over and over again by western and middle eastern european countries to devide and conquer. Kushabikia waarabu au wazungu hadi kufikia point ya kukataa hawakufanya utumwa ni ignorance ni bora ukubali ukweli ili usiurudie.
 
ETI,,"THERE WAS NO ABOLITIONIST MOVEMENTS WHICH DEVELOPED OUT OF ISLAM OR MUSLIM COUNTRIES" Propaganda kama hizo katafute watoto wa chekechea uwalishe...
THE BIG SHOW, hebu anzisha mada husika tukupe darasa...ukiweza kufungua hiyo thread swali langu la kwanza kwako litakuwa unitajie abolitionist movements katika nchi za Kiarabu zilizoupiga vita utumwa na ziliongozwa na nani, utaje hata jina moja tu...

...ila kwa sasa acha kututoa kwenye mada kuhusu Uchochezi wa mohamedi Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar kwa madai kuwa kama si kwa juhudi za mamluki wa Kizulu, Kimanyema na Kinubi waliotumikia jeshi la Wajerumani, Tanganyika haikuwa na watu wa kuweza kuendesha harakati za kudai uhuru.
 
Vp kuhusu uislamu kuanza kwa kusilimisha watu kwa upanga yaani 'jihad' na kwamba utaisha kwa jihad aka the sixth pillar of islam

hakuna kitu kama hicho,
uislam unasema hakuna kulazimishana katika dini,kila mtu katika dola ya kiislam yuko huru kuamin kile anachokiamin..
islam is peaceful to somebody who is peaceful to it,
islam is torelant to somebody who is torelant to it,
and vice versa is true..
 
RITZ,
we ni kiboko yaani jamaa wanauliza na wewe unajibu tena kwa uhakika! hivi anaishi wapi huyu asiejua kuna vita vya kikabila huko anakotoka Baba yao wa taifa? Mwalimu alisahau charity begins at home?
With all due respect, hivi vita vya ukoo baina ya Wakurya vimeanza upya 16 years ago baada ya Mwalimu kutoka mamlakani. Enzi za Mwalimu akiwa likizo pale Butiama akisikia kuna chokochoko Tarime alikuwa anapeleka FFU na viongozi wote wa koo wanawekwa ndani. Baada ya muda hali ilitulia kwa sababu Wakurya waliona huyu mura hana mchezo. Haya mapigano ya juzi yameanza miaka ya karibuni kwa sababu wameshabaini kuwa serikali ya sasa ni dhaifu.
 
THE BIG SHOW, hebu anzisha mada husika tukupe darasa...ukiweza kufungua hiyo thread swali langu la kwanza kwako litakuwa unitajie abolitionist movements katika nchi za Kiarabu zilizoupiga vita utumwa na ziliongozwa na nani, utaje hata jina moja tu...

...ila kwa sasa acha kututoa kwenye mada kuhusu Uchochezi wa mohamedi Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar kwa madai kuwa kama si kwa juhudi za mamluki wa Kizulu, Kimanyema na Kinubi waliotumikia jeshi la Wajerumani, Tanganyika haikuwa na watu wa kuweza kuendesha harakati za kudai uhuru.

Sawa,turudi kwenye mada kuu Mkuu,ila nyie ndie mnaeanzisha na kututoa nje ya mada,sisi tunakuja huko huko mnakotaka nyinyi twende ile jino kwa jino..
Kwangu mimi jibu kuhus mwanaharakati wa kiarabu wa kwanza kuupiga vita utumwa katika nchi za kiarabu ni mtume wa ALLAH S.W NAE NI MUHAMMADY(peace be upon him)..
Yeye alikua anahubiri wazi wazi watu kuwaachia huru watumwa na kwamba kufanya hivyo ni kukiuka maamrisho ya muumba,kwan Allah s.w katuumba wanadam katika rangi na mataifa mbali mbali na lugha mbali mbali ili tujuanea na tutambuane,na sio kunyanyasana na kudharauliana,na akasema mtu bora machoni mwa Allah s.w ni yule mwenye matendo mema zaid kwake yeye..
 
Jasusi,

Njoo na data na facts za kutosha kuhusu watumwa waliohasiwa.

Halafu sijui umeipata wapi kuwa nusu ya Wasaudia Arabia ni Watumwa.

Nashangaa sana mwandishi wa habari kama wewe unaokota habari mitaani bila utafiti wa kutosha.

Soma historia ya Saudia Arabia hilo ni taifa kongwe tofauti na Marekani.
Ritz,
Hujanielewa. Of course nusu ya Saudi Arabia si waafrika(watumwa) kwa sababu hawa hawakupewa haki yao ya kuzaana.
Wale ma ustaadh waliokuwa na harems hawakutaka makafiri wawashughulikie bibi zao. Ndio maana idadi ya weusi Saudi Arabia ni ya kuhesabika. Lakini Mungu alivyo mwema, hawakuweza kufuta kabisa historia ya kukamata watumwa kwani mpaka leo kuna mwana mfalme, aliyekuwa balozi hapa Marekani ni mweusi kama Maalim Seif.
 
Kwahiyo Nyerere alipoingia madarakani ndipo vita hivyo vikasimama? na kikao cha kusuluhisha makabila yaliyokuwa yakipigana kilifanyika wapi? ni Nyerere ndie aliesimamia au alimtuma Kambona na Kawawa kwaniaba yake wakasuluhishe? hembu tupe darsa la vita vya makabila ya Tanganyika somo jipya hili! huko kwetu Kibosho mpaka leo kuna kuibiana kuku na vifaranga kati ya Wakibosho na Wamachame na kati ya wa Kirua na wa Kishmundu na panatokea kukatana mapanga mpaka mauaji lakini sijasikia hata siku moja vikiitwa ni vita vya makabila ya Tanganyika au ugaidi!
Hapana. Chokochoko za kikabila zilisimamishwa na mwamko wa TANU. TANU ilitufanya sote tujione kuwa ndugu moja. Hayo ya kuibiana kuku na vifaranga ni kawaida kabisa popote pale kunapopatikana makundi ya mafukara.
 
Mzee Mohammed Said, huku niliko ilinipa shida sana kukumbuka kile kitabu ambacho niliona "ume-quote passages" nani kakiandika kwa vile nilikinunua Tanga mjini duka fulani (Mwongozo Shop)sikumbuki lini yawezekana 2008. Nimesafiri, sipo Tanga kwa sasa, zile passages zimenipa ushawishi sana wa kukagua kwenye internet na nimeamka ku-google; Sykes na wewe. Okay, now at least i can confirm ni wewe ulikiandika. Well, nilikisoma zamani (kama 4 years ago). Simulizi zako kwa maana ya mtiririko wa mawazo yako na kuunganisha matukio niliuona ni mzuri, na ni kitabu chepesi mtu kukielewa. Mimi wajibu wangu kama mwanataaluma (tofauti na fani yako) ni kukupongeza kwa jitihada zako. Baada ya kuyasema hayo, utaona kuwa tupo wengi tunaoangalia matukio hayo hayo tofauti na wewe. Na hiyo ndio ubinadamu. Ni muhimu sana ikajulikana kuwa utengano wa mtazamo wangu hauna lengo la kushusha thamani wala heshima ya kazi yako mbele ya jamii wala wasomaji wengine. Sasa tuendelee na mada na darsa lako. Iam all ears!!!!
 
Utumwa ulikuwepo na waarab walioleta uislam ndio waliokua na utumwa mbaya zaidi kukataa hili ni kukataa historia .
Vp kuna ukweli kuhusu uislamu kuanza kwa kusilimisha watu kwa upanga yaani 'jihad' na kwamba utaisha kwa 'jihad' aka the sixth pillar of islam.

Dont take my word for it :

Jihad-(English-pronunciation:-/dʒɪˈhɑːd/;-Arabic:جهاد‎-ǧihād-[dʒiˈhæːd]), an-Islamic term, is a religious duty of-Muslims. In-Arabic, the wordjihād-translates as a noun meaning "struggle".Jihad-appears 41 times in the-Quran-and frequently in the idiomatic expression "striving in the way of God-(al-jihad fi sabil-Allah)".[1][2][3]-A person engaged in jihad is called a-mujahid; the plural is-mujahideen. Jihad is an important religious duty for Muslims. A minority among theSunni scholars-sometimes refer to this duty as the sixth-pillar of Islam
Source -wikipedia

Uislam si waarabu,nishakujibu swali lako,labda kama hujanielewa..
Na maana ya jihadi ni zaid ya hiyo uliyoichukua kwenye hiyo english - arabic translation dictionary,
Jihad ni kujitoa katika kuipigania nafsi yako katika kuisimamisha dini ya Allah kiroho na kimwili..
Na jihadi ya dhati huanza kwa mtu kupigania nafsi yake kuitoa kwenye maovu na kuiingiza kwenye mema na nuru ya mola,kisha familia yake wake zake na watoto wake,pamoja na ndugu na jamaa zke,ksha jamii nzima in ayomzunguka,
Pia kama kuna watu wamekuja kuitokomeza dini ya Allah kwa kutumia njia za vita na unyanyasaji n,k.unapopinga na kushindana nao kwa njia hzo hizo pia unahesabika umepigana jihadi na kwamba ukifa hapo malipo yako unahebiwa heri na siyo shari..
Turudi kweye hoja kuu.,mtuoneshe wapi kwenye uchochez wa Moh Said..
 
Sawa,turudi kwenye mada kuu Mkuu,ila nyie ndie mnaeanzisha na kututoa nje ya mada,sisi tunakuja huko huko mnakotaka nyinyi twende ile jino kwa jino..
Kwangu mimi jibu kuhus mwanaharakati wa kiarabu wa kwanza kuupiga vita utumwa katika nchi za kiarabu ni mtume wa ALLAH S.W NAE NI MUHAMMADY(peace be upon him)..
Yeye alikua anahubiri wazi wazi watu kuwaachia huru watumwa na kwamba kufanya hivyo ni kukiuka maamrisho ya muumba,kwan Allah s.w katuumba wanadam katika rangi na mataifa mbali mbali na lugha mbali mbali ili tujuanea na tutambuane,na sio kunyanyasana na kudharauliana,na akasema mtu bora machoni mwa Allah s.w ni yule mwenye matendo mema zaid kwake yeye..
THE BIG SHOW, hongera sana...kumbe ukinuia unaweza! Kwa mara ya kwanza nimesoma posti yako bila usumbufu, zile font unazotumia, Duh! Nakuomba uendelee hivyo hivyo, internet inazo etiquette zake. Si vibaya mara moja moja uki highlight neno ama sentensi lakini...lakini post nzima? :nono: Pamoja na hayo, FYI. aliyeanza kututoa kwenye mada ni moja katika wanafunzi wanafunzi watiifu wa Mohamed Said ukifanya utafiti mdogo, utamfahamu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kigezo hicho utaona kuwa Mwalimu wenu Mohammed Said anatakiwa awe kihiyo na kanjanja nambari moja kwani maandishi yake yamejaa "inawezekana", "inasemekana" na "huenda"...!!
Mwanakijiji hawa vijana wa Mo hawawelewi kwanini mtu anatumia uwezekano.

Nilichokuwa naongelea ni statistics na nilikuwa naonyesha probability inayoweza kutokana na statistic kwa jinsi zinavyotafsiriwa. Hapa ni upungufu wa kuelewa wa vijana wa mzee.

Unakumbuka hapo nyuma nilisema huyu anayefundisha kutengeneza sehemu za ngano kwakweli si mtaalam.
Kukiwa na kitu kinaitwa study kinachohusu vitu kama takwimu, lazima uangalie assumption, probability n.k.

Nilichowambia ni kuwa probability ya distribution population kuongezeka au kupungua ni vitu kadha wa kadha.
Kwamba hivyo ni vitu vya kuangalia, na kwasababu Mohamed na kundi lake hawakuangalia basi matokeo ndiyo hayo ya kuwa na takwimu kama namba na wala siyo stats kwa kiwango cha mtu kusema utafiti na stats zinasema abcd.

Endapo ningesema ''kuna uwezekano'' warioba alikuwa waziri wa sheri wakati anateuliwa kuwa waziri mkuu, au ningesema Warioba alikuwa mwanasheria hapo ni kweli kuwa neno inawezekana ni kiashirio cha kutokuwa na uhakika.
Lakini nilisema Wakati anateuliwa alikuwa waziri, na kabla ya hapo mwanasheria mkuu na pia alikuwa Mbunge facts ambazo Mohamed hakujaribu hata kuuliza. Anajua Nyerere hakumchukua Warioba kutoka machungani.

Mohamed anaposema inasemekana Nyerere alifanya abcd, inasemekana Wakristo walifanya abcd au inasemekana TANU iliundwa hapo ni kuwa hana ushahidi kwasababu haongelei probability.

Nadhani umesema vizuri, kama mimi nikisema inawezekana takwimu zingekuwa abcd hilo linaonekana kama kutokuwa na uhakika basi wanapaswa kumwambia Mohamed nusu ya kitabu chake hakuwa na uhakika kwasababu ametumia ''inasemekana'' mara nyingi sana
Tumeonyesha inasemekana za kutosha tu.

Wasi wasi wangu ni kuwa akina Mohamed wanazeeka sasa vijana wanaotarajiwa kuchukua mikoba kama ndio hao basi tutarudi kule kule kwa kundi la watu wenye fikra za kuonewa kujifungia mahali na kutafuta namba halafu kuja nazo hadharani kama utafiti. Kinachofuata ni aibu na soni!

Vijana wa Mohamed na yeye waliomba tafsiri ya sensa nikaweka, hakuna aliyehoji hata mmoja akiwemo mwalimu wao.
Nimeweka jedwali nikaligeuza upside down, hakuna hata mmoja aliyesimama kulitetea. Maana yake wanakubali lakini wafanyeje?
Nashangaa wanasema ''hakuna uhakika'' wakati hakuna, narudi hakuna hata mmoja aliyenukuu mstari na kuuelezea tofauti.
 
Hello Mr. Kadogoo, Aslaam aleykum, Sheikh wangu napata shida kidogo na wewe kushindwa kumuona huyo pharaoh aliyezamishwa huko Cairo. Shida yangu ni kuwa serikali ya Misri inategemea sana pesa za watalii wanaoenda kwenye yale Ma-pyramid pale Giza na sehemu zingine. Sasa kuzuia watu kama nyie kutembelea alipolazwa pharaoh wa Musa kwa misingi eti wanaoenda wanamfananisha huyu pharaoh na Sadat, si mtihani Ustadh? Au huyo "guide" wenu alikuwa amechoka siku hiyo? Sababu za serikali kuzuia watu wasiende kwa wingi alipolazwa Pharaoh wa Musa utazikuta: Rational Islam? - Letters to a Muslim: Ramses II and/or Merneptah and the Islamic miracle of the preserved Pharaoh. Kifupi ni kuwa watalii kujazana kwenye chumba alipo huyu Pharaoh kuligundulika kusababisha maambukizi ya fungus kwenye huyu Mummy na kuleta hofu ya yeye kuoza kwa kuzingatia hali ya joto la Cairo. Awali alishawahi kutibiwa matatizo haya. Ndio maana serikali inapunguza wanaoruhusiwa kufika chumba alicholazwa. Kama "guide alikwambia hadithi ya Sadat, Ustadh kadai hela zako.
 
Uislam si waarabu,nishakujibu swali lako,labda kama hujanielewa..
Na maana ya jihadi ni zaid ya hiyo uliyoichukua kwenye hiyo english - arabic translation dictionary,
Jihad ni kujitoa katika kuipigania nafsi yako katika kuisimamisha dini ya Allah kiroho na kimwili..
Na jihadi ya dhati huanza kwa mtu kupigania nafsi yake kuitoa kwenye maovu na kuiingiza kwenye mema na nuru ya mola,kisha familia yake wake zake na watoto wake,pamoja na ndugu na jamaa zke,ksha jamii nzima in ayomzunguka,
Pia kama kuna watu wamekuja kuitokomeza dini ya Allah kwa kutumia njia za vita na unyanyasaji n,k.unapopinga na kushindana nao kwa njia hzo hizo pia unahesabika umepigana jihadi na kwamba ukifa hapo malipo yako unahebiwa heri na siyo shari..
Turudi kweye hoja kuu.,mtuoneshe wapi kwenye uchochez wa Moh Said..

Haya bana, kwa kasi uliyonayo wakirudi leo hawa jamaa wanaweza kukuchukua tena ktk ships zao, only this time minyororo itakua ni dini. Ndio maana naona watu hapa wanashabikia kwenda arabuni kama mbinguni.

Tukirudi katika mada kuu ninashauri Moh aviweke vitabu stika ya "HALAL" au aviandike "histohisia za wazee walodhulumiwa" ili sie wengine wenye tabia ya kusoma mambo critically tusokubali lishwa vya walolishwa tunaposoma vitabu hivi tusipate shida. Maadam kanihakikishia kwamba ni historia iliyosahaulika ya wazewe mie I have less interest in that... haidhuru. ila nikuulize kama kitu unakielezea kwa mara ya kwanza kuna haja gani ya kusistiza kusahaulika kwake au am I missing something here. Au kuna kitu kinatafutwa hapo.

Again kusema tujikite ktk masimulizi hayo hainisaidii kila mtu ana wazazi wake. Yeriko hajaandika details za 'wazee wake' (japo ingeleta maana zaidi) na kwa sababu wazi : no good can come out of that for us all. Tunaposoma historia ya wazee wa fulani tukaishangilia then what tunajenga minara au? barabara zenyewe zimeanza kuitwa Mwaikibaki.

Pia kama bonus nikueleze both katika historia na vilevile kazi nyingi tu za literature kunakuwa na star anayebeba sifa katika mapambano mfano : wayahudi wao wanamuona king David kama ndiye symbol ya taifa lao na shujaa wao ndio maana bendera yao ina 'nyota ya daudi' Africa ya kusini 'madiba' ana stand out kwanza wengi hatuijui vizuri historia ya South Africa suffice it is to say Madiba sums it up for many of us. China kuna dynasties nyingi zilikuwepo kabla ya Mao ila Mao anatosha kwa wengi. Ninachojaribu kisema hapa ni kwamba mwanadamu kwa kawaida anatafuta symbolism na heroes katika kila jambo hata katika commercial branding kuna dhana ya flagship na hata historia inauza zaidi kukiwa na hero anaye stand out. Hii haimaanishi details hazipo na Moh anacheza na hii kitu kijanja sana aidha kwa kujua au kutojua kwamba : si kila kitu kitapata front row in history kwa sababu wazi. Kama hawa wazee hawakuwa wajanja kujua historia huwa inanoga na heroes wakamwachia Mwalimu ashine au walijua hilo ila hawakua na namna kutokana na influence aliyonayo hiyo ni shauri lao.
 
Kisa cha kuvunjika EAMWS ni kirefu sana kwa hapa sitokitendea haki
Lakini kwenye kitabu changu nimekieleza chote pamoja na wahusika
wakuu nimewataja kwa majina yao.

Kuwa kwa nini huko kwengine nako chama kikafa sababu sijui.
Ila sababu ya hapa kupigwa marufuku ni kuwa EAMWS ilikuwa
inataka kujenga chuo kikuu.

Hii ikatia hofu Kanisa Katoliki na Nyerere ikabidi afanye kila juhudi
EAMWS ipigwe marufuku.

Source ya hiyo info. ya sensa ni Islam and Politics cha August Nimitz
unaweza kupata thesis yake Maktaba ya Chuo Kikuu.

Nitajaribu Insha Allah kuangalia kitabu nikupe na ukurasa ninacho katika
''archives'' yangu.
Mohamed, umesema mara nyingi sana kuwa maandiko yako yapo katika utafiti kwa maana yametafitiwa. Unajua wazi kuwa EAMWS ilianzia Mombasa na ilianzishwa na Wapakistan.

Unafahamu habari zake zote.Kama unadai kuwa hujui kwanini ilikufa Uganda na Kenya basi utafiti wako haukuwa sahihi au kamili.Huwezi kuandika utafiti wa kifo bila kuzaliwa kukua na kuenea kwa EAMWS!!! kwamba ni dude lilianguka kutoka angani!!

Nadhani hapa kuwa mkweli kwa Namren, unajua sababu zitaondoa maana halisi iliyokusudiwa katika kisa kizima vinginevyo ungemueleza alichohitaji.

Ama kuhusu kifo cha EAMWS kama njama za kuzuia kujenga chuo kikuu naona unaturudisha nyuma ambako tulikubaliana kabisa kuwa mabaki ya AMNUT ndiyo yalijificha katika kivuli cha EAMWS.

Kama ni fihi na husuda mbona taasisi za Agakhan aiyekuwa mlezi hazikuondoka na zinajenga chuo kikuu?
Hofu imewaondoka lini?

Kuhusu Sena ya mwaka 1957 kwanza nikupongeze kwasababu kwa mara ya kwanza unakubali kuwa historia yako si masimulizi ni pamoja na nukuu za kazi za wengine jambo ambalo ni kawaida katika uandishi na utafiti.
Nadhani somo zuri ulilojifunza ni lile la kujivika kazi usizo na ushahidi nazo ukashadidia kuwa huo ndio ukweli.
Na pengine ni mwanzo mzuri wa kuitambua Tanganyika na si Mtedeni kama Tanganyika.

Sasa nenda mbali na kuacha kukata vipande vya kitabu chako ukasema huo ni ukweli, kwasababu kuna ukweli kwingine.
Kazi ya kujua ukweli aachiwe msomaji bila kumtisha kiimani, usafiri wa nje, majina ya vyuo n.k.

Hata hivyo bado swali linabaki kuwa ni kweli Tanganyika ilifanya sensa mwaka 1957 ni taasisi gani ilipewa jukumu hilo hata kama tulikuwa chini ya Mwingereza. Kuanzia hapo tutaendelea.
 
Nguruvi,
Sipo hapa kwa ajili ya ubishi.
 
Hello Mr. Kadogoo, Aslaam aleykum, Sheikh wangu napata shida kidogo na wewe kushindwa kumuona huyo pharaoh aliyezamishwa huko Cairo. Shida yangu ni kuwa serikali ya Misri inategemea sana pesa za watalii wanaoenda kwenye yale Ma-pyramid pale Giza na sehemu zingine. Sasa kuzuia watu kama nyie kutembelea alipolazwa pharaoh wa Musa kwa misingi eti wanaoenda wanamfananisha huyu pharaoh na Sadat, si mtihani Ustadh? Au huyo "guide" wenu alikuwa amechoka siku hiyo? Sababu za serikali kuzuia watu wasiende kwa wingi alipolazwa Pharaoh wa Musa utazikuta: Rational Islam? - Letters to a Muslim: Ramses II and/or Merneptah and the Islamic miracle of the preserved Pharaoh. Kifupi ni kuwa watalii kujazana kwenye chumba alipo huyu Pharaoh kuligundulika kusababisha maambukizi ya fungus kwenye huyu Mummy na kuleta hofu ya yeye kuoza kwa kuzingatia hali ya joto la Cairo. Awali alishawahi kutibiwa matatizo haya. Ndio maana serikali inapunguza wanaoruhusiwa kufika chumba alicholazwa. Kama "guide alikwambia hadithi ya Sadat, Ustadh kadai hela zako.

Wickama,
Hayo niliyoeleza hayakuwa kutoka kwa guide.

Kwa hakika kulikuwa na vyumba vingine vyenye vitu ambayo navyo
vilikuwa vimefungwa.
 
Back
Top Bottom