Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Ni wapi aliposema Rupia sio Mzee Wake?
Nyambala,
Kama umechukulia hiyo ni kutamba basi sii mwisho wa kutamba.
Nifahamishe kama kitabu cha kaka yangu Hammie Rajab, Shigongo nk. kama
vimepata review katika majarida ya kisomi.
Kitabu changu kina review mbili ndani ya Cambridge Journal of African History.
Moja ya John Iliffe na nyingine ya James Brenan.
Nadhani unawatambua mabingwa hawa wa historia ya Afrika.
Zipo nyingine...
Kutokana na kitabu hicho nimealikwa Chuo Kikuu cha Ohio na Chuo Kikuu Cha
Northwestern, Chicago ambako kote nimefanya mihadhara.
Au unataka nikuwekea hapa chini na vyuo vingine hapa Afrika ambavyo nimepata
kualikwa na kuzungumza?
Nilipata kuwa member wa Library of Congress zaidi ya miaka 25 iliyopita na katika
nchi nzima hatukuzidi watu watano.
Walimu walionisomesha hawakupata kupewa heshima hiyo.
Aliyekuwa akitoa hiyo alikuwa Mkurugenzi wa USIS.
Alipata kunisoma na ndiyo akanitunuku uanachama huo.
Bado unataka ''tambo'' zaidi au niishie hapa?
Soma hiyo hotuba ya maandishi ya rangi ya bluu, ukiiamini hiyo hutahitaji video tena.
Hiyo hotuba imekuwa bidhaa adimu? au Yericko bado yuko njiani kufuatilia TBC? hata na RITZ alishajitolea kulipia gharama ili Yericko akaichukue lakini kaishia mitini!
Hiyo hotuba ya maandishi kaileta JokaKuu na sisi tukakuambia kuna sehemu imechakachuliwa wewe mwenyewe ndiyo ukaja na ahadi kuwa utaenda TBC kuichukua uiweke humu leo miezi 4.
Ulisema inauzwa watu tukajitolea kuinunua tukakuambia sema kiasi gani kimya mpaka leo.
Mwenzako naye Son, alisema ndani ya masaa 24 hotuba itakuwa humu leo miezi 4.
Leo tena unakuja na habari zingine hutaki tena hotuba ya TBC.
Mzee Saidi mwalimu unayetusomesha hapa unaonaje tumalize kwanza ule mjadala wa sensa 1957/ 1967?
tunaomba ilm hapo Mohamed Said
Na ndiye huyo huyo anayesemwa alikuwa na uzoefu wa siasa kuliko ''debate'' za shule za Nyerere! please MoAngalia pia na ushuhuda huu hapa chini;
Kwamba huyo Abdul Sykes anayenukuliwa akimpa sifa Mwalimu Nyerere kwa kuleta mapinduzi ya fikra ndani ta TAA baada ya kuutwaa uongozi, ndiye huyo huyo Abdulwahid Sykes ambaye Mohamed Said anampa sifa zote za kuaasisi chama cha siasa, TANU, kilichopigania uhuru...makes one wonder!
Nyambala,
Elimu yangu mie si ya kufanya ubishi na watu.
Naeleza kitu kile ninachokijua na ikiwa atakuja mwingine na taarifa kinyume na ya
kwangu hapana ugomvi wala sitalazimisha kuwa taarifa yangu ndiyo yenyewe, la hasha.
Ubaya wa ubishi ni kuwa unapoteza muda.
Wewe uko hapo hapo lakini angali mie nishatoa darsa ngapi na kuhusu mangapi.
Mengi katika hayo wasikizaji hawakupata kuyasikia popote.
Leo watazamaji wamefika 130,000 and counting...
Basi nibaki na sensa, sensa, sensa, sensa...
Sahani ya santuri imekwama kwenye gramafoni.
Tija iko wapi?
Mohamed, kaa kitako na pata funda la maji. Mnyambala ana point muhimu sana.Nyambala,
Elimu yangu mie si ya kufanya ubishi na watu.
Naeleza kitu kile ninachokijua na ikiwa atakuja mwingine na taarifa kinyume na ya
kwangu hapana ugomvi wala sitalazimisha kuwa taarifa yangu ndiyo yenyewe, la hasha.
Ubaya wa ubishi ni kuwa unapoteza muda.
Wewe uko hapo hapo lakini angali mie nishatoa darsa ngapi na kuhusu mangapi.
Mengi katika hayo wasikizaji hawakupata kuyasikia popote.
Leo watazamaji wamefika 130,000 and counting...
Basi nibaki na sensa, sensa, sensa, sensa...
Sahani ya santuri imekwama kwenye gramafoni.
Tija iko wapi?
Ati mimi sijui hadhira ya JF...
Hivi wewe Nyambala kutia timu yako katika kiwanja hiki unaona ndiyo umefika?
Hapa si mdadi wako tu unaandika?
Uwanja huu si ''free for all?''
Hii si Hyde Park?
Wewe unajua timu yangu ishacheza viwanja gani duniani?
Fanya staha lau kidogo hata kama jina langu ni Mohamed.
Ndio maana tulisema wapi ushahidi? Wewe ulimnukuu akisema, kuna wengine hawakusikia sasa prove kwao kuwa ndivyo ilivyokuwa. Kama ulisikia una proof tatizo ni nini?Kadogoo,
Suala halikuwa kutajwa Abdu katika hotuba ya muago wa Nyerere pale Ukumbi
wa Diamond.
Suala ni kuwa Nyerere alisema hakumbuki Abdu alikuwa na cheo gani katika TAA.
Kwangu mimi wala hili halinishughulishi.
Kadogoo rafiki yangu, ebu njoo uone matumizi ya neno hili "anaropoka" lilivyotumika na mzee wako Mohamed. Hivi mtu anayeropoka huitwa nani? Sisi kule kwetu mtu huyo huitwa mropokaji. Hivi mimi Gwalihenzi nikisema mzee wenu Mohamedi Said amekuwa akiropoka na kwahiyo ni MROPOKAJI nitakuwa nimemtukana?Geeky,
Huyo jamaa anaropoka hajui maingiliano ya watu wa Dar es Salaam.
Angelikuwa ananijua mimi vizuri hata asingesema hayo.
Wala sina haja ya kusema mengi katika hilo.
Yeye anamjua Rupia leo.
Wazee wetu wamekuwa na maingiliano ya miaka.
Ndio maana tulisema wapi ushahidi? Wewe ulimnukuu akisema, kuna wengine hawakusikia sasa prove kwao kuwa ndivyo ilivyokuwa. Kama ulisikia una proof tatizo ni nini?
Unataka video! ulipomnukuu Nyerere ulikuwa na mkanda wa video na kama hukuwa nao unahitaji wa nini.
Jokakuu kaweka hotuba! kanusha kuwa si kweli
Sio kweli,Wakati mwingine uwa nacheka sana watu wanatumia mabandiko ya John Iliffe kama ushahidi wakati John Illife miaka ya mwishoni ya 1960 akiwa idara ya historia ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, aliweza kukusanya habari nyingi sana na muhimu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wake mtoto wa Abdulwahid Sykes, Daisy Sykes.
Binti huyu alimfahamisha John Iliffe kuwa habari alizokuwa akiandika katika semina kuhusu historia ya Tanganyika alikuwa akizipata kwa baba yake.
John Illife alichota sana Ilm kutoka kwa mtoto wa Abdulwahid Sykes na kumshauri aandike historia ya maisha ya babu yake Kleist Sykes.
Leo hii Mohamed Said anatoa Ilm bure kabisa kupitia JF.
Lakini kuwa watu wanapinga na kusema hizo habari za Gerezani kwa wanywa gahawa washinda vibarazani lakini John Illiffe akija na habari za Wazee wa kariakoo hakuna tatizo. Msomeni John Iliffe kwenye kitabu chake "A Modern History of Tanganyika."
Ndicho wengi tunachokitaka akifanye hapa,Ndio maana tulisema wapi ushahidi? Wewe ulimnukuu akisema, kuna wengine hawakusikia sasa prove kwao kuwa ndivyo ilivyokuwa. Kama ulisikia una proof tatizo ni nini?
Unataka video! ulipomnukuu Nyerere ulikuwa na mkanda wa video na kama hukuwa nao unahitaji wa nini.
Jokakuu kaweka hotuba! kanusha kuwa si kweli
Hiyo hotuba ya maandishi siku ilipowekwa tu mimi nilisema kuna sehemu imechakachuliwa kilichoandikwa na tulichokisikia RTD ni vitu viwili tofauti.
Gwalihenzi;
Hapana, sisi sote ni Wa TZ! ila siwezi kubadilisha kauli ya Mwenye enzi Mungu kuwa, Sema: Enyi makafiri! mimi siabudu mnachokiabudu, Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu, Wala sitaabudu mnacho abudu, Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu, Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu. (Qur:113)
Tanzania katuumbia Bwana Mungu tuishi humu humu hata kama tunaimani tofauti! la muhimu ni kila mtu aheshimu dini ya mwenzake na muhimu zaidi ni kuvumiliana! mfano: Wewe unaamini kuwa Yesu ni Mungu na ukiimba na kutangaza kila mahali hivyo sina budi nivumilie lakini na wewe pia huna budi kuvumilia pale mimi ninapotangaza kuwa Yesu si Mungu! hayo ndio mafundisho ya dini yangu! Gwalihenzi unakubaliana na mimi?
Sio kweli,
John Iliffe katika utafiti wake na uandishi wa historia ya Tanganyika hakumtumia Daisy Syke kama rejea kuu bali alimtumia kama kiambata tu tena cha 0.001 ya taratibu za utafiti wa kihistoria.
Yasome mandishi ya Historia ya Tanganyika ya mwanazuoni huyu Mr J. Iliffe na kisha rejea kwenye vielelezo vyake utaona Daisy Sykes sio alama kuu ya maandishi yake.