Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Nguruvi,
Hapana sijakasirika ndugu yangu.

Wewe ni kipenzi changu.
Unanishughulisha sana.

Mie hupenda kuhangaishwa kifikra.
 
Platozoom,
Unataka kujadili ni mie habari ya ''chapati...''

Unajua nachokijadili, acha kunilisha hoja.Chapati si msingi wa nilichokiandika. Kama ingekuwa nimeandika ili
tujadili chapati pengine wewe ndiye ulikuwa wa kwanza. Usijikurupushe!
 
OO, Na hii sijui ndio reasoning gani jamani toka kwa Great thinker! hivi hujui kuwa unapomwambia Msichana Mwanamwali kuwa unataka kumposa halafu anyamaze bila kujibu hujui kuwa amekubali ombi lako? au wewe Mzee ungeendelea tu kumwambia hayo hayo?

Ndio mwanzo wa kumbaka mtoto wa watu kwa sababu unafikiri kasema "ndiyo"... mawazo ya kizazi gani sijui hichi... kama ukimya ni kukubali basi Mohammed Said - mwalimu wako - amekubali mengi sana katika mjadala huu.
 
tumeshakwambia na tunarudia hii lugha yako kama tuko kariakoo shimoni au Hariz action mart hapa si mahala pake.msomo unakuja na lugha ya "unajipunja" inatufanya to doubt credentials zako,tunaomba ufanye shule kama ilibidi uende sio umebahatisha

"Son...
Unajipunja...
Nami nakuacha hivyo ulivyo ya nini nikupe faida"
 
 
 
Last edited by a moderator:
P...
Umetaja chapati.

Na wewe ukahitimisha tunajadili chapati!! Nimeandika hivi:

 

Son...
Kwani hapo kwa kina Salim na Hamisi Hirizi si ndiyo kwetu.
Cha ajabu nini?
 
Huyu alikuwa mfadhili big time,na wala humsikii popote-huyu ufadhili wake sio kibaba cha mchele bali ni megabucks-wewe ushangai nimekuja na hiyo 33% na MS aja doubt

Son...
Unauliza mchango wa Mzee John Rupia?

Soma hapa chini michango yote:

TANU ILIPOUNGURUMA UMOJA WA MATAIFA, NEW YORK 1955
Huwezikuhadithia safari Nyerere Umoja wa Mataifabila ya kueleza mchango wa Idd Faizmafongo katika kufanikisha safari ile.

Kwa hakika na na katika mambo yakuhuzunisha sana kuwa wazalendo kama hawa leo hawatambuliwi wala juhudihazionekani kufanyika kuhifadhi historia zao.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba IddFaiz Mafongo alihudhuria mkutano wa kwanza kabisa wa uzinduzi wa TANU uliofanyikakatika Ukumbi wa Arnautoglu. Waliohudhiria mkutano huu hawatimii watu ishirini.

Haifahamiki kwa hakika hasa ni lini Idd Faiz alijiunga na TANU kwa sababu kadiyake ya kwanza ya uanachama ilipotea na akapewa kadi nyingine iliyokuwa nanamba 915 iliyotolewa tarehe 28 Agosti, 1954.

Watoto wake kwa kuthamini mchangowa baba yao katika kupigania uhuru wa Tangayika wamehifadhi nyaraka zake mojawapo ni hii kadi yake ya TANU.

Kwa kukisia tu kutokana na kadi ambayo IddFaiz mwenyewe aliitoa kwa kaka yake Idd Tosiri ambayo ilikuwa kadi namba 25 nayenye saini yake kama afisa aliyetoa kadi hiyo, inaweza kuchukuliwa kwa uhakikakuwa Idd Faiz alikuwa miongoni mwa wale watu wa mwanzo kabisa kuingia TANU.

IddFaiz na nduguye Idd Tosiri, muasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika,walikuwa Wakusu, moja ya makabila ya Kimanyema, kwa upande wa baba yao; na Wabwali kwa upande wa mama yao.

Wote wawili walikuwa katika Batetera Union(Congo Association), chama kilichokuwa kikiwaunganisha Wamanyema wa Tanganyika.

Mzee bin Sudi alikuwa rais muasisi wa chama hicho na baada ya kifo chake Sheikh Hussein Juma alichaguliwa kushika nafasi hiyo.

Idd Faizi alikuwa mweka hazinawa Al Jamiatul Islamiyya na vilevile mweka hazina wa TANU.

Idd Faiz aliifanyiakampeni TANU kuanzia siku ilipoanzishwa, akifuatana na Nyerere katika safari zamwanzo kabisa za kukitangaza chama, akihutubia mikutano jukwaa moja naNyerere.

Ilikuwa ni Idd Faiz na kakayake Idd Tosiri ndiyo waliompeleka na kumtambulisha Nyerere kwa binamu yao Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo aliyekuwa khalifa wa Tarika ya Kadiria.

Ilikuwa ni baada ya utambulisho huu kwa Sheikh Ramia ndipo urafiki ukajengekakati ya Sheikh Ramia na Nyerere na TANU ikakubalika Bagamoyo.

Baraza la Wazee TANU chini ya uenyekti wa Sheikh Suleiman Takadir ilichukua mafanikioya safari ya Nyerere Umoja wa Mataifa kuwa jukumu lao binafsi.

Sehemu ya kwanzaya maandalizi ilitakiwa ifanyike kwa siri sana. Uongozi wa TANU ulikambidhi IddFaiz kazi ya kuandaa, kukusanya na kusimamia mfuko wa safari ya rais wa TANUkwenda Umoja wa Mataifa, New York.

Safari ilikuwa ifanyike mwezi wa Februari, 1955.
Wanahistoria wazalendo na hata yeye mwenyewe Nyerere alikuwa akitoa picha kamavile ile safari yeye aliipanga.

Ukweli ni kuwa fikra ya kwenda Umoja wa Mataifailikuwapo tola 1950 kabla hata Nyerere hajajulikana.

TANU ilihitaji takriban shilingi elfu kumi na mbili kumwezesha Nyerere kusafiri kwenda Umoja waMataifa, New York.

Kamati ya Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes iliyokuwa ikijishughulisha na mgogoro wa ardhi ya Wameru mwaka 1953 ilikuwa imekusanya kiasi cha fedha kutoka majimboni kilitumika katika safari ya Ally na Phombeah kwenda kwenye Pan African Congress mjini Lusaka. Kiasi cha fedha kilichobaki hakikutoshakumpeleka Rais wa TANU, Nyerere Amerika.

libidi fedha za ziada zitafutwekutoka kwa wananchi ili kumwezesha Nyerere kufanya safari hiyo.

John Rupia alichangia zaidi ya theluthi moja ya fedha zilizotakikana.

Wanachamawengine walichangia kwa uwezo wao wote lakini TANU katika siku zile ikiwa bado changa ilikuwa maskini, kiasi hicho kilikuwa bado kiko nje ya uwezo wake.

Ikitambua ule upungufu wa fedha za safari ya Nyerere, Idd Faiz aliombwa na uongozi wa Al Jamiatul Islamiyya kutoa fedhakatika mfuko wa Al Jamiatul Islamiyya na kuzitia katika hazina ya TANU kukiwezesha chama kumpeleka Nyerere Umoja wa Mataifa.

Hata pamoja na fedha zilekutoka Al Jamiatul Islamiyya hizo hazikuweza kukidhi haja.

Al JamiatulIslamiyya haikuwa na jingine isipokuwa kumuomba Idd Faiz asafiri kwenda Tanga kutafutamichango zaidi.

Mwalimu Kihere alikusanya fedha na ikawa anasubiriwa mtuakazichukue kuzipeleka makao makuu.

TANU ilipata habari kwamba yeyote ambaye atakwenda Tanga kuchukua fedha hizo kwa ajili ya safari ya Nyerere atakamatwa na makachero wa serikali.

Kabla ya kuondoka, Oscar Kambona, Katibu Mkuu wa TANU, na JohnRupia, Makamo wa Rais wa TANU, walikwenda kuonana na Idd Faiz nyumbani kwakeIlala kumuaga, kumtakia safari njema na kumpa maelezo kwa ufupi.

Safari ya kwenda Tanga haikuwa na tatizo lolote, lakini katika wakati wa kurudi basi ambalo Idd Faiz alikuwamo lilisimamishwa njiani Turiani na makachero.

Idd Faizalikamatwa, akavuliwa nguo na kupekuliwa, lakini hakukutwa na fedha.

Hili lilimshangaza na kumchanganya yule afisa aliyemkamata kwa sababu walikuwa na taarifa kwamba Idd Faiz alikuwa amechukua fedha kutoka kwa Mwalimu Kihere kuleTanga.

Idd Faiz aliwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa Dar es Salaam kwa usailizaidi wakati wote akiwa analindwa na askari wenye silaha. Wkati wote Idd Faizyeye alikataa akisema hajui chochote kuhusu fedha za TANU kutoka Tanga.

Ilibidi wamuachie huru kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wowote wa kumtia hatiani.

Wakati Idd Faiz yuko mikononi mwa polisi fedha za safari ya Nyerere tayari zilikuwa zmeifika makao makuuya TANU Dar es Salaam, salama salimini.

Idd Faiz hakuwa amezishika yeye zilefedha. Zile fedha alikuwa amepewa msichana mdogo aliyekuwa abiria ndani ya basi lile alimokuwa Idd Faiz.

Mnamo tarehe 17 Februari, 1955 Nyerere aliondoka kwenda New York kuhutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa.

Nyerere aliiweka wazi nia ya TANU kuwa alikuwaametumwa na wananchi wa Tanganyika kuwasilisha ujumbe ufuatao kuwa "Kuonakanuni ya uchaguzi ikianzishwa na Waafrika kujiwakilisha katika taasisi zote za umma... Hii tunaamini, ni kwa mujibu wa masharti ya Makubaliano ya Udhamini na Ibara ya 76 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa."

Mbele ya Umoja wa Mataifa, TANU haikuwa ikidhihirisha tamko lolote jipya, yale yote yaliyowasilishwa paleyalikuwa ni maoni ya kamati ndogo ya siasa ya TAA yaliyowakilishwa kwa Constitutional Development Committee ya Gavana Edward Twining mwaka wa 1950.

Mapendekezo ya TAA ambayo Gavana Twining aliyapuuza.
Badala yake aliendelea na mipango yakeya kuwa na wawakilishi wa rangi zote katika Baraza la Kutunga Sheria.

Wakoloni hawakukubali kushindwa kirahis serikali ilituma ujumbe wake Umoja wa Mataifa kuipinga TANU uliowakilishwa na I. C. Chopra, Mwasia; Sir Charles Phillips,Mzungu na Liwali Yustino Mponda, mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria kutoka Newala.

Inastaajabisha sana leo kusikia wanasiasa wakizikebehi juhudi za akina Abdulwahid Sykes kuwa ati walikuwa wakiendesha chama cha starehe.

Sawa TAA natujaalie kilikuwa chama cha starehe, nayo Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika nayo kilikuwa chama cha starehe?

Nyerere alirudi kutoka New York Jumamosi, tarehe 19 Machi, 1955 na alipokelewa uwanja wa ndege na halaiki ya watu.

Dossa Aziz anakumbuka kuwa aliruhusiwa pale uwanjawa ndege kuingiza gari yake hadi ndani ya uwanja chini ya ndege hadi chini yangazi ili kumrahisishia Nyerere kuingia ndani ya gari na kuepuka msongamano wa watu.

Dossa Aziz anasema kama isingekuwa kwa msaada huo Nyerere angesongwa sanana watu na ingekuwa kazi kubwa kumtoa pale.

Watu walikuwa kila mahali wakisukumana na kusongamana wakijaribu angalau kumtia Nyerere machoni.

Watuwalikuwa wakiimba na kucheza mganda, ngoma ya Kizaramo, wakiimba "Baba KabwelaYuno."
Maana yake "Baba karudi kutoka UNO."

Jambo la kushangaza ni kwambahakuna mtu aliyewahi kuusikia wimbo huu kabla ya siku ile na hakuna ajuaye lini ulitungwa.

Ile gari ya Dossa Aziz aliyopanda Nyerere ilisukumwa kutoka uwanjawa ndege hadi nyumbani kwa Nyerere, Magomeni Majumba Sita, kiasi cha kama kilo mita ishirini.

Siku iliyofuata ilikuwa Jumapili.

TANU ilifanya mkutano wahadhara Mnazi Mmoja ambao ulihudhuriwa na umati ambao kamwe haukupata kuonekana Dar es Salaam.
Inakisiwazaidi ya watu 40,000 walikuja kutoka kila upande wa mji kumsikiliza Nyerere.

Hakuna mtu aliyekuwa na raha ya kuandika kuhusu mkutano ule na safari yakihistoria ya Nyerere kwenda Umoja wa Mataifa kuliko Mashado Plantan katika gazeti lake Zuhra.

Mtambo wa gazeti wa Mashado uliokuwa Mtaa wa Ndanda, Mission Quarters ulichapisha nakala za ziada za gazeti hilo na toleo lote liliuzika.

Mikutano ya TANU ya siku za mwanzo ilikuwa ikifanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja mbele ya Princess Hotel.

Kwenye jukwaa lililojengwa kwa miti walikuwa wakikaa wale viongozi wa mstari wa mbele ndani ya TANU - Nyerere rais wa TANU, Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, Bibi Titi Mohamed, John Rupia na Clement Mtamila.

Sahani ya santuri ilikuwa ikipigwa katikagramafoni kupitia kipaaza sauti kuvutia watu kuja mkutanoni.
Mwimbo uliokuwaukipigwa ulikuwa wa Frank Humplink.

Frank alikuwa kijana wa Kichagga kutoka Moshi.

Baba yake alikuwa Mzungu.Hamplink alikuwa mwimbaji na mpiga gitaa maarufu sana wakati ule akipiga muziki wake na dada zake wawili Maria na Regina Humplink.

Wimbo uliopendwa sana naTANU na ndiyo uliokuwa ukipigwa katika mikutano yake yote na uliosisimuawananchi ulikuwa na mashairi yafuatayo: ''
Ugandanayo iende, Tanganyik aikichangamka, Kenya na Nyasa zitaumana.'' Mwimbo huu ulikuwa na ujumbe wa kisiasa kwa Waafrika wa Tanganyika.

Ujumbe katika wimbo huo ulikuwa kuwa, Tanganyika itakapoamka, kutakuwa vilevile na mapambano nchini Uganda, Kenya na Nyasaland.

Wimbo huu ulikuwa ukivuma toka kwenye vipazasauti mfululizo kabla ya mkutano huku watu wakikusanyika viwanjani. Haikupitamuda mrefu serikali ya kikoloni ilipata maana halisi ya wimbo huo.

Mara moja mwimbo huo ukapigwa marufuku na serikali hauruhusiwi tena kupigwa Sauti ya Dares Salaam.

Serikali ya kikoloni iliamuru kwamba mashairi ya wimbo huo yalikuwa yakiwashawishiwatu kuasi.

Lakini kabla ya wimbo huo kupigwa marufuku ulipendwa sana naulikuwa ukiombwa na wasikilizaji na kupigwa katika Sauti ya Dar es Salaam.

Baada ya amri ya serikali kutoka kituo hicho kiliacha kabisa kupiga wimbohuo. Huenda huu ulikuwa wimbo wa kwanza kupigwa marufuku katika historia ya utangazaji Tanganyika. Kwa muda mrefu sana wimbo huu ulikuwa kama wimbo rasmi wa TANU.

Inaelekea uzalendo na shauku yauhuru ndiyo vitu vilivyomtia hamasa Humplink hata akatunga na kuuimba wimbo huo.

Miaka mingi baadae nikizungumza na Mzee Humplink nyumbani kwake Lushoto alisema kuwa hakusalimika, alikamatwa Moshi na kuwekwa ndani hadi alipotolewa kwa msaada wa Chifu Thomas Marealle aliyewaambia wakoloni kuwaFrank alikuwa kijana akipiga muziki tu wala hakuwa na lolote nje ya hilo.

Askari wa kikoloni wakaingia nyumba hadi nyumba wakiisaka ile santuri ya Frank na ilipopatikana ilivunjwa hapo hapo.

Katika mikutano ya TANU katika zile sikuza mwanzo, kabla Nyerere au Bibi Titi kuhutubia umma, Sheikh Suleiman Takadir alikuwa akisimama na kuomba dua kisha kumtambulisha Nyerere kwa wananchi.

Baadaya hapo atasimama Bibi Titi kuhutubia na mwisho atapanda Nyerere.

Bibi Titi alikuwa akijulikana kwa maneno yake makali wakati Nyerere alikuwa bingwa wa fikra tulivu na utoaji wa ujumbe mzito.

Sheikh Suleiman Takadir mwenyewe,vilevile alikuwa msemaji mzuri sana.

Ilikuwa kwa sababu hii na umri wake mkubwandiyo alipewa heshima na wazee wa mji ya kuzungumza kwanza kabla ya yoyote hajasema.

Katikati ya hotuba na mwanzo na mwisho wa mkutano vijana wa Bantu Group kama akina Hamis Bakas, Juma Mlevi, Rajab Sisson na wenzake walikuwa wakichangamshakwa vibweka vyao vya kila aina huku wakiungwa mkono na nyimbo za lelemama zaakina Bi. Hawa bint Maftah, Tatu bint Mzee, akina bint Chanzi.

Hawa Bantu Groupndiyo walikuwa wakitoa ulinzi kwa Nyerere wakiwa wamevaa majani na huku wameshika pinde, vishoka na silaha nyingine za kijadi. Bantu Groupwalichangamsha sana mikutano ya TANU.

Hotubaaliyotoa Nyerere siku ile pale Mnazi Mmoja kama taarifa yake ya safari ya Umojawa Mataifa ilikuwa ya kusisimua.

Hapa ndipo hasa ndiyo mwanzo wa historia mpyaya Tanganyika.

Kabla ya hapo Waafrika wa Tanganyika hawakupata kuonyesha shauku na matumaini katika mustakbali wao kwa kiwango kile.

Katika viwanja vya Mnazi Mmoja Nyerere aliwaeleza halaiki ya watu wenye furaha na waliokuwawakimsikiliza kwa makini kuwa miongoni mwa mataifa kumi na mbili yanayounda Baraza la Udhamini saba kati yao yalitoa idhini kuwa muda wa utawala wa ndani wa Tanganyika utakapowadia, Waafrika wa Tanganyika lazima wapewe nchi yao.

Katika hotuba yake Nyerere alitilia mkazo sera ya TANU kuhusu mahusiano mema baina ya Waafrika na watu wa mataifa mengine na aliwaonya wanachama wa TANU ambao walikuwa wameanza kuwabagua watu wa rangi tofauti kuwaambia kuwa hivyohaikuwa sawa. A

lisisitiza juu ya umoja miongoni mwa wananachi na hatimaye aliwadhihaki wasikilizaji kwa kuwauliza ikiwa wangesubiri kwa miaka ishirini na tano kuwa huru.

Halaiki hiyo ya watu kwa pamoja ilipiga kelele, "Hapana." Wananachi kwa pamoja walijibu kwa sauti kubwa wakisema walitaka uhuru kesho au kesho kutwa.

Nyerereambaye alikuwa akiogopa kuchukua uongozi wa TANU tangu 1953 alikuwa amefarajika sana na mshikamano huu ulioonyeshwa na wananchi.

Sasa ilikuwa dhahiri kwake kwamba rafiki yake Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na uongozi mzima wa TANU pamoja na lile Baraza la Wazee wa TANU lilikuwa limemsafishia njia kuongoza harakati kwa niaba yao.

Lakini Padri Walsh na Wamishionari katika shule yaMtakatifu Francis, Pugu, walitazama harakati hizi kwa mtazamo mwingine kabisa.

Wamishionari hawakuweza tena kumvumilia Nyerere kuwa mmoja wa walimu katika shule yao.

Hatima ile ile iliyowasibu wazalendo wengine kabla yake sasa ilimkabili Nyerere. Aliambiwa ama abakie mtumishi mtiifu wa kanisa au ajiuzulu; Kanisa halikuweza kukaa kimya na kumuangalia Nyerere akiwatumikia mabwana wawili.

Nyerere alilipeleka tatizo hili kwa Clement Mtamila, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya TANU. Mtamila aliitisha mkutano wa kamati kuu nyumbani kwake mtaa wa Kipata na TANU ilijadili tatizo hilo.

Tarehe 23 Machi, 1955 Nyerere alijiuzulu ualimu.
 
Nguruvi,
Sheikh Rukara wala si mtu wa Dar es Salaam.Alikuja Tanzania kama mfanyakazi wa World Muslim League.
Kwahiyo baada ya mkataba wake kwisha alirudi Burundi. Kuna mahali anaunganishwa unganishwa sana na harakati za waasi. Anyway sijui. Sasa ilikuwaje huyu alikuwa anaratibu shughuli za ndani za misikiti kupanga mikakati akiwa mfanyakazi tu wa washirika la ''Kimataifa''.

Na hawa world muslim league waliwezaje kuingia na kufanya shughuli hapa nchini maana kwa maandiko yako Tanzania ikiwa chini ya mfumo hairuhusu kujiunga na mashirika ya kiislam.

Hawa World Muslim league walikuwa wanafanya shughuli gani kiasi kwamba mfumokrkristo ambao hauruhusu Tanzania kuwa na mahusiano na mashirika ya dini ya kiislam ukawasahau.
Na vipi huyu mfanyakazi wa kigeni aliweza kumiliki Nyumba na kujihusisha na shughuli za harakati za waislam nchini.

Mohamed, hili tuliweke sawa lisije likaleta utata kwa vizazi vijavyo kama la EAMWS.

cc Mwanakijiji, Mag3, JokaKuu, Jasusi, Ritz, Platoozom, Wickama, Raphaerl,Big show
 

Nguruvi,
Swali lako umelielekeza sipo.

Hayo ni ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
 
Dr. Slaa alikwishatoa ufafanuzi juu ya MOU. Na nadhani uzi huo umo humu ndani ya mnakasha huu. Hakuna fedha za walipa kodi zilizochotwa ila naona wewe ni mmoja wa wale wanaoamini kuwa uwongo ukirudiwa mara kwa mara watu wataamini kuwa ni ukweli.

JASUSI:
Wewe huwa unaamini na kukubali anayosema Dr. Slaa?
 
Nguruvi,
Swali lako umelielekeza sipo.

Hayo ni ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Wewe ndie uliyeutangazia ulimwengu kuwa Tanzania niyamfumo kristu,

Sasa tukihoji kuwa mtu huyo wa kigeni alifikaje nchini kufanya kazi za uislamu? Wewe unatuambia tukahiji wizara????????? Inaingia akilini mkuu?
 
Hapa ndipo nashindwa kabisa kuelewa lengo la Mohamed Said ni nini anapotoa madai ya uongo kama haya baada ya kujifungia chumbani na kutunga upuuzi kama huu na kuuita ukweli na kuna watu wanaamini hizi ngano. Ni kweli Julius Nyerere alikuwa Mwalimu katika shule ya St. Francis Pugu, shule iliyomilikiwa na Kanisa Katoliki lakini hakuwa mwajiriwa wa Kanisa, alikuwa mwajiriwa wa serikali na alilipwa na serikali (He was a civil servant) Ni serikali ndiyo haikufurahishwa na yeye kujiingiza katika siasa na katu si Kanisa...Kanisa liliendelea kushirikiana naye na kumpa msaada ilipolazimu katika harakati zake za kisiasa hata baada ya kujiuzulu Ualimu. Ni uongo, ni ulaghai na ni udanganyifu usiovumilika kwa mtu anayedai kafanya utafiti kuhubiri upuuzi huu.

Kwanza ni serikali iliyowapiga marufuku watumishi wake kujihusisha na mambo ya siasa na pili, uamuzi wa kujiuzulu ulikuwa ni wa kwake na hakupata shinikizo lolote kutoka kwa Kanisa. Mohamed Said hupenda kuhusisha Kanisa na maamuzi ya serikali na leo yeye ndiye mpiga debe mkuu wa harakati eti za kupambana na mfumoKristo... masikini hajui kwamba hata huo Ukristo sio Ukatoliki pekee! Mwalimu angeweza kabisa kuamua kuendelea kufundisha akiwa mwajiriwa wa Kanisa kama angependa ila kulingana na maneno yake mwenyewe, hangepata muda wa kutosha kuwapa huduma ya elimu wanafunzi wake jinsi angependa. Hata baada ya kujiuzulu aliporudi kijijini Butiama aliombwa na padre wa Katoliki afundishe lugha ya Kizanaki kwa malipo...
 
Last edited by a moderator:
Ndio mwanzo wa kumbaka mtoto wa watu kwa sababu unafikiri kasema "ndiyo"... mawazo ya kizazi gani sijui hichi... kama ukimya ni kukubali basi Mohammed Said - mwalimu wako - amekubali mengi sana katika mjadala huu.

Mzee Mwanakijiji:

Naona unataka twende mbali zaidi: hivi mila yenu ndiyo inawafundisha hivyo? kumposa msichana na kubaka wapi na wapi? au Mwanakijiji hujui maana ya neno posa? Mtu mzima na heshima zako unaenda kumposa Mwanamwali, kaona haya kwa kunyamaza huku anaangalia chini wewe unamrukia na mkubaka? hii mila ya wapi tena jamani? hujui kuposa ni hatua ya mwanzo kabisa kufikia jiko?
Msichana kama alinyamaza unatakiwa kwenda kwa baba ake na kupeleka posa kwani mwanamwali alishakubali pale mwanzo ulipomtaka kumuoa! sasa wewe na hii habari ya kubaka umeitoa wapi?

Halafu kwa taarifa yako ukiona mtu hataki kukujibu basi fahamu kuwa aidha hataki majibizano na wewe, au katahayari na kufadhaika au kakiri na kukubali kimya kimya ila hana ubavu wa kukujibu!
Sasa kwa upande wa Mwalimu hayo mawili ya mwisho yanamhusu kwasababu aliyotaja Mohamed Said ni makubwa,
yalimdhalilisha na kumsononesha! Kwa hulka yake Mwalimu asingeweza kunyamaza ndio maana mwaka 1992 Kambona alipomtaja ktk uwanja wa Jangwani kuhodhi utajiri mkubwa yeye na Amir Jamal na Rashidi bila kuchelewa alimjibu na kukiri kuwa kama ni yeye anakubali ya Kambona kwasababu si ajabu yeye kuhodhi utajiri kwani alipata medali na zawadi tele!

Akiwajibu waandishi wa habari huku akicheka Mwalimu alimsikitikia sana Kawawa kusingiziwa na Kambona kwani kwa anavyomjua Rashidi hana utajiri wa aina hiyo!
Sasa kama alimjibu Kambona kwa kumtaja hadharani tena siku moja tu! kwanini asijibu hoja za Mohamed Saidi za tangu mwaka 1998 mpaka Profesa haroub Othman aende kumhoji? na zaidi kwanini chama chake alichoasisi CCM mpaka leo kimeshindwa kujibu hoja hizo ila tunaona na kusikia mitandaoni mashabiki na wakereketwa wa Chadema ndio wako mstari wa mbele kukipinga kitabu cha Mohamed Saidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…