Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Inasemekana mfadhili mkubwa wa TANU alikuwa Abdu Sykes alikuwa na "kabati" la hela nyumbani kwake!!

Ni nini kilitokea hela ya safari UN ikapungua mpaka atokee John Rupia kuokoa Jahazi?!
Rapheri,
Tufanye mjadala wa staha.

Unapokejeli "kabati la hela" unatoa raha ya historia ilivyokuwa.

Ukitaka tufanye mnakasha tukaelezana mambo yalivyokuwa
karibu sana.

La unaumizwa na taarifa hizi bora tuachane uendelee na wengine.
Safari ile iliwaelemea sana TANU.

Rashid Ali Meli alikuwa mweka fedha Dar es Salaam Municipal
Council.

Yeye alitoa fedha kwenye "safe" ya ofisini kumpa Idd Faiz hazikutosha.
Idd Faiz akatoa hela kutoka hazina ya Al Jamiatul Islamiyya hazikutosha.

Ndipo Idd Faiz akenda Tanga kwa Mwalimu Kihere kuchukua fedha nyingine.

Rapheri,
Leo unaweza ukakejeli kwa kuwa huyajui na waliyoyajua hawakutaka kuyasema.

"Mole" wa Waingereza Special Branch ndani ya TANU akapeleka taarifa za fedha
aloleta Rashid Ali Meli.

Asubuhi akaingiliwa na wakaguzi wanataka kukagua vitabu.
Pazuri hapa....

Rapheri,
Stahamili utajifunza mengi kwangu...

Ninachoomba kwako ni staha yangu.
Hukubaliani nami nipinge kwa heshima na adabu.

Huo ndiyo uungwana na ustaarabu wa mnakasha.
 

Mkuu Nguruvi,
Ndezi huyo!!,Ndezi huyo mkuu!aaaah!!!unanikumbusha Kerenge aisee!!
 

Asante Mkuu, niliposema ni afadhali nisome machapisho ya Mohammed Said kuliko kusoma Annur ndio maana akatahayari na kuniuliza; Mohammed Said ni nani na Annur ni nani.
Kumbe kuna ushirika usio rasmi.
 
Rapheri,
Tufanye mjadala wa staha.

Unapokejeli "kabati la hela" unatoa raha ya historia ilivyokuwa.

Ukitaka tufanye mnakasha tukaelezana mambo yalivyokuwa
karibu sana.

La unaumizwa na taarifa hizi bora tuachane uendelee na wengine.

Niwie radhi mkuu wangu ikiwa hujapendezwa na maneno yangu,

Tuendelee na mnakasha ila na wewe unawakweza sana hawa wazee wako(wetu)...
 
Asante Mkuu, niliposema ni afadhali nisome machapisho ya Mohammed Said kuliko kusoma Annur ndio maana akatahayari na kuniuliza; Mohammed Said ni nani na Annur ni nani.
Kumbe kuna ushirika usio rasmi.

Wimana,
Siwezi kutahayari kwa kunasibishwa na Annuur.

Wewe tu ndiyo hujui kama ninahusika na gazeti
hilo.
 
Niwie radhi mkuu wangu ikiwa hujapendezwa na maneno yangu,

Tuendelee na mnakasha ila na wewe unawakweza sana hawa wazee wako(wetu)...

Rapheri,
Hata Waamerika katika majumuisho yao walinambia hivyo.

Lakini ukweli ni kuwa hayo yote waliyafanya.
Nimeongeza vitu katika ile post.
 
Pitia bandiko la JokaKuu utakutana na neno Waislam.

Hivi wale watoto wanaokataa shule kule Makete, Ludewa, Magu, Nansio, Mwitongo, Nkasi, Kizi, Nyanguge, Njombe, Katoro, Ngudu, Tarime, wote ni Waislam.

Well
Inasemwa Pwani kwa sababu Pwani inakaliwa kwa sehemu kubwa na Jamii ya Waislam. Na tazama kwa makini,
mwamko wa Elimu upo chini sana karibia maeneo yote, nenda Kisarawe, Mkuranga, Rufiji (huko hata walimu hawana
raha kuishi), Kilwa, Lindi, Tanga n.k n.k. Kiwango cha watoto wanaoacha shule ni kikubwa sana kulinganisha na Mikoa
inayokaliwa na Wakristo wengi.

Huko unapopasema ni kweli kuna Wanafunzi wanaacha shule njiani, lakini lazima uweke katika Mizania ili uujue ukweli.
Kwa mfano huwezi kulinganisha Tarime na Rufiji au Mkuranga kwa mwamko wa Kielimu. Ni jambo la kawida kwa Mzee
wa Kikurya kuuza ng'ombe wake ili mtoto aende shule.

Au nenda Tarime sekondari, Nkende, Magoto uone idadi ya wanaomaliza kidato cha nne na cha Tano kama inalingana na ya hizo Wilaya. Lakini pia ni rahisi kuwakuta Walimu wazawa katika Wilaya hiyo, Madaktari, Wahandisi n.k. Sina hakika kama kuna Wazaramo, Wadengereko, Wakwere ama Wamatumbi wangapi wewnye Taaluma hizo kwenye maeneo yao waliyozaliwa!

Fanya ulinganisho huu kwa angalau Mikoa michache, mathalani Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Mara, Kagera (kwa mtazamo wa haraka ni mikoa inayokaliwa na Wakristo wengi), na Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara, Kigoma (Mikoa inayokaliwa na Wais
lam wengi). Kwa ufupi kuna Mikoa ambayo ina Mazingira rafiki ya Kielimu kwa maana ya watu wake.

Drop out ya Wanafuzni Pwani ni kubwa sana. Na hata ule mwamko wa Wazazi kwa Elimu ya Watoto wao upo chini mno.
Sasa kama hilo linasababishwa na Tamaduni zao nk lazima litaakisi kwenye Jamii ya Kiislam kwa ujumla wake kwa sababu
wana Dini yao na ni wengi.

Wilaya ya Rufiji ikiandikisha watoto zaidi ya 90% na baadaye wakamaliza shule ya Msingi 30% nafikri unajua impact yake
baadaye.
 

Yaani wewe hujui nani ni kiongozi anayekufaa mpaka upate muongozo kutoka kwa viongozi wako wa Dini?!

Hii ndo aina ya wanafunzi wa Mzee Mohamed,
Kwa style hii mtalalamika sana mfumo Kristo...

Umenishangaza sana Mtanzania mwenzangu
 
JASUSI:
Wewe huwa unaamini na kukubali anayosema Dr. Slaa?

Yeye ndiye aliyekuwa Katibu Mkuu wa TEC wakati huo mkataba ukiandaliwa hadi kusainiwa. Sasa tuambie tumwamini nani? Hao kina Sheikh Ponda? Maana Serikali kwa upande wake ipo kimya kama kawaida yake, pale linapokuja suala la dini hadi pale vurugu zinapotokea ndipo inaingia, wakati madhira yameshatukia.
 
Wimana,

Hapo ndugu yangu umenipoteza Mteke ni chakula gani nipe darsa kaka.

Mteke ni dagaa fresh wa Ziwa Tanganyika (bila shaka Sheikh Said anajua sana) ukipikwa kwa mafuta ya mawese na kukauka vizuri ni kitoweo mujarab kwa ugali wa muhogo.
 
Ni mie nikuulize wewe unaamini Tanzania nzima watoto wa Pwani ndiyo hawataki kusoma kutokana na Uislam wao.

Hatuwezi kusema tunaamini hivyo ila pia tunashangazwa na stats. Kuanzia kiwango cha ufaulu hadi mwitikio wa wanafunzi na walimu kuenda huko. Nimeisha wahi toa nukuu ya Shukuru kawambwa akishangazwa kwamba kati ya walimu 26, 500 + ni walimu wakufunzi watano tu (5) walichagua kwenda kilwa na mikoa ya kusini kama mtwara na lindi hali ni hiyo hivyo na hata wakipelekwa alisema uzoefu unaoneshwa kuwa wanakataa kushuka ktk gari la almashauri wakiangua kilio kama wamechanganyikiwa (clouds imeishawahi rusha moja ya matukio hayo) baadhi ya sababu ni kuogopa kupigwa na wanafunzi hali kadhalika na wazazi in fact mwaka jana kumekuwa na tukio la wanafunzi kutishia kubaka walimu huko rufiji kama ilivyoripotiwa na nipashe in an exposé :

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...walimu-wao-shule-kufungwa-ni-huko-rufiji.html

Nako bagamoyo Mwaka jana wanafunzi nane walimbaka mwalimu kwa zamu.
Nao walimu kutishiwa kulogwa na kushughulikiwa na wazazi ni moja kati ya challenge nyingi wanazokutana nazo walimu huko so jiulize sehemu kama hizi elimu inachukuliwa kwa umakini unaohitajika?

Mambo hayo yote yanatisha na ni challenge zetu kama watanzania and you know what? haina haja kuyashangilia au kuyakataa. Tatizo lipo na suluhisho naona ni kuwapelekea incentives au kuwaelimisha wakazi wa huko kwa kuanzia kuwatumia prominent figures wa huko kama lowassa anavyofanya akiwa lwaiganan wa wamasai -I think its a stroke of genius! Watu kama membe, raisi wetu na mh mkapa kwa kuanzia wakifanya juhudi kama hii pia na Moh akaacha kuwalisha 'historia mpya' akazingatia mitaala iliyopo. Mambo hayo yote yangekua muujiza huko.
 
Mohammed Said says this in one of his posts (quoting from his book):


it sounds reasonable doesn't it? but, if we were to apply the same standard towards his own writings as far as Nyerere is concerned are we satisfied that he exercised the same level of intellectual courtesy that he demands of others? Doesn't he commit what he accuses of others? When he condemns the so called Kivukoni historians for failing to reach out to sources closest to Abdulwahid Sykes in their "official history of TANU" doesn't he as well condemn himself for doing exactly the same when fails from doing the same when writing about Nyerere as his chief protagonist in relation to Abdulwahid Sykes?

If I were to call those who believe such flawed narrative as '------' will I be accused of insulting them or just giving them the rightful title? How can one believe a history written without adhering to historical method while the same author accuses others of doing exactly what he himself actually does?

IF they are not ------ -an argument can be made to show why they are - what name can we call those who believe in these modern fables disguised as historical narratives?
 
Ritz,
Ahsanta nyingi zimwendee Sheikh Mohammed,ama hakika hii shughuli ni ndefu mno na ni nzito yataka kutuama kwa yakini ili kufahamu na kuzingatia. Nami sitaki kuwa kati ya wale wanaotaka kujipunja!ahaha!!
 

Aisee wewe ndugu yetu unatatizo kubwa sana...
 
Mzee Saidi umeeleza kuhusu namna fedha zilivyopatikana kuwezesha Nyerere kwenda UNO ile ya 1955 na 1957. Historia inasema between 1955 and 1957 Nyerere alifika UNO mara tatu. Kwa faida ya jukwaa je unaweza kutueleza ni nani alifadhili hiyo safari ya tatu??
 
Ritz,
Ahsanta nyingi zimwendee Sheikh Mohammed,ama hakika hii shughuli ni ndefu mno na ni nzito yataka kutuama kwa yakini ili kufahamu na kuzingatia. Nami sitaki kuwa kati ya wale wanaotaka kujipunja!ahaha!!

Gombesugu,
Marehemu Malima alikuwa na msemo akisema, ''Mtu akikutukana ulevini na wewe mtukane hapo hapo
la ukimsubiri akiwa mzima atasema alikuwa kalewa.''

Nimerushiwa kijembe ati nikiandika tena nisisahau kisa cha yule bibi wa baibui.

Sikutaka kuchelewesha nami nikajibu kuwa endapo nitaandika tena nitaandika
mkasa wa Abdu Sykes na ''intelligence surveillance'' alowekewa baada ya uhuru.

Akanivamia mtu na kusema kuwa yeye Abdu nani asiwekewe watu wa kumchunguza.
Hii ndiyo hatari ya kutojua historia ya nchi yetu.

Sasa katika majibu ya kijuba kama haya ndipo wanapopunjika watu hawa.

Laiti angeniuliza kwa utaratibu vipi ilikuwa mzalendo kama huyu si yeye tu bali baba yake
na wadogo zake wote walikuwa katika harakati akaja kuwa ''target'' akaja kuwa ''suspect''
angelipata mengi.

Lakini kuna uoga nadhani unawakumba ninapofunguka (kutumia lugha ya JF) hofu inawajia
wanaogopa kusikia mengi ambayo huenda yakawatia simanzi.

Hawa ndugu zetu hawajui lakini katika wanarakati wa TANU hakuna ambae hakula fadhila
za Abdu kuanzia Chief Marealle, Fundikira, Dunstan Omari nk. na si kwa kuwa Abdu alikuwa
na fedha nyingi sana.

La hasha alikuwa mtu karimu na muungwana kweli.
Hapa panatosha.

Unajua Abdu hadi anaingia kaburini hakupata kusema kuwa yeye ndiye aliyeasisi TANU au kusema
kuwa African Association aliasisi baba yake nk. nk.

Mwaka 1988 niliandika ''memoriam'' ya Abdu Sykes katika Africa Events miaka 20 baada ya kifo chake.

Daily News na Uhuru walipata shida sana kutoa kumbukumbu fupi waliyopelekewa kwa kusema ati iweje
historia ya nchi hii inafunganishwa na Abdulwahid Sykes?

Yeye ni nani?
Ni kweli alikuwa rafiki wa Nyerere?
Inabidi tuulize kwanza ukweli huu kabla hatujachapisha.

Na nafasi gazetini ilikuwa ya kununua.

Ahmed Rashad Ali siku alipokutana na mimi baada ya kuisoma na ilikuwa katika sala ya Eid Msikiti wa
Kitumbini, Mzee Rashad ambae alikuwa rafiki yake kipenzi alinikumbatia na machozi yakimtoka.

Mzee Rashad alinambia, ''Mohamed usitukumbushe habari za Abdu wewe hujapatapo kuona mtu kama
Abdu...''

Hatuwatukuzi hawa wazee kwa kuwakweza.
Hawa watu walikuwapo na wamefanya makubwa.

Abdu hakuingia katika harakati achume fedha.
Sana sana yeye ndiye aliyekuwa akitoa fedha kuipa TANU.

Insha Allah iko siku nitaeleza maziko ya Abdu yalikuwaje.
Yalivunja rekodi katika maziko ya Dar es Salaam.

Ule umma haukuja mazikoni kwa umaarufu wake au fedha zake.
Walikuja pale kwa ubinadamu wake na utu alokuwanao.

Ndiyo maana rafiki zake wakampa jina ''The Sweet Abdu.''

Gombesugu,
Dua yangu kwa Allah siku zote imekuwa asinihitimishe hadi nimeeleza yote niyajuayo kuhusu historia
ya uhuru wa Tanganyika na yale yalojiri baada.
 

Nimekusoma vizuri kwa hiyo tatizo siyo serikali ya CCM kwenye elimu tatizo ni Waislam wenyewe.
 

Tuachane na kabati la hela Mkuu wangu,

Sasa huyu bwana Rashid Ali Meli na Idd Faiz hizi hela kwenye hizi ofisi zao walikuwa wameiba au vipi kwasababu tunaona Wakaguzi walivamia ofisi ya Rashid Ali Meli hapo Dar es salaam Municipal Council?!Tafadhali naomba nipatie hicho kisa cha yaliyotokea baada ya hao wakaguzi kuvamia ofisi hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…