Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

JokaKuu,

Unaweza kutupa takwimu Tanzania wanaokataa shule ni Waislam.

Hapa umetumia maneno ya Maghembe kama ushahidi lakini sisi tukitumia maneno ya Kitwana Kondo, Prof Njozi, Prof Kigoma Malima, mnasema ni hisia tu.

Hebu jiulize kwani iwe watoto wa Kiislam wa Pwani tu ndiyo hawataki shule wasiwe watoto wa Uturuki, India, Pakistani, Indonesia, Dubai, Iran, Saudi Arabia, Misri, Singapore, Qatar.

Ritz,

..Prof.Maghembe alikuwa waziri wa elimu, kwa hiyo hizo takwimu alizotoa zinatosheleza. unachoweza ku-argue kutokea hapo ni conclusions alizotoa.

..kwa mtizamo wangu Prof.Jumanne Maghembe ni kama vile ametoa majibu kwa madai ya Prof.Malima, Prof.Njozi, na Mzee Kitwana Kondo.

..Prof.Malima alidai tatizo fitina na kutokuwepo kwa utaratibu wa namba za mtihani. sasa Prof.Maghembe amekuja kubainisha kwamba tatizo ni UTORO wa wanafunzi.

..mimi sisemi kwamba Uislamu ni tatizo, ila nasema Waislamu ni waathirika wa mazingira ya kijamii/social na kiuchumi/economic yanayopelekea utoro wa wanafunzi ktk mikoa ya Pwani.

..inawezekana shule ni mbaya, inawezekana wazazi hawana uwezo ni masikini, au pengine hakuna mwamko, huenda kuna mila na tamaduni mbaya etc etc. ushauri wangu ni kwamba tuangalie kila kitu, na tusiweke udini mbele, bali tuongozwe na UMOJA wetu kama WATANZANIA.

cc: gombesugu, Nguruvi3, Kadogoo, Ami, Son of Alaska, THE BIG SHOW
 
Last edited by a moderator:
Mimi nimeongea na akina Suleiman Kitwara kule Kamunyonge,Musoma.
Vijana wake walikuwa marafiki.Mzee huyu alikuwa mtaratibu na mcha mungu sana.
Hebu angali picha za mwanzo au muulize Mohamed huyu ni nani.

Sisi tukiongea nao hatupigi pua tunapata maarifa na kukupasia wewe. Post iliyopita nilikupa kitu kuwa nitapitia kwa Mzee Erasto Mangenya(chifu)una mjua huyo. Halfu December nitapita kule kwa akina Akili Daniel.

Umeshawahi kumsikia Mzee Hemed Mkali, hao tukiongea nao. Familia ya Magogo Mputa kwangu ni nyumbani.
Sisi wengine hatuna sababu za kujifaragua na kupiga pua, haaata! hekima tu.
Ndio maana tukimpeleka kona mzee huwa hatoki ila kwa time out!
Kuonana na wazee wetu ni hidaya na namshukuru mwenyezi mungu. Hakika tuna mengi tukieleza mtashtuka

Nshapata ugali kwa ndezi aliyeungwa na ngogwe. Ritz mashallah unatoka mate.

Muheshimiwa Nguruvi3,
Nimefurahi saana kwa umahiri wako wa hao watu na mitaa/sehemu hizo! Nakukubali kwa u-Al Watan wako!ahaha!! Nahisi sasa unaanza kuwa pamoja na Sheikh Mohammed Said, na pia ni uzuri tumwache atupe darsa kwa utaratibu na huku sootetunamuuliza maswali ya kina na kwa ustaarabu. Kidogodogo ndo mwendo lakini tutafika.

Hivi ni nani alikua msomaji wa kwanza wa mashairi na tenzi kwenye Radio Kichwele!? Tafadhalini naomba tujuzane wenzangu?

Huku kwenye nchi za wenzetu/"mataifa ya magharibi" wana utaratibu mzuri na wanathamini na kuwaenzi saana "wazee wao" na watu walotoa michango kwenye Historia/ ya nchi zao. Hakuna mchango ati mdogo saana au wa kipuuzi katika harakati za kupatikana uhuru wa nchi au mapambano ya nchi! Nashangaa sisi tumepoteza tamaduni hizi tulorithi toka kwa mababu zetu!

Tafadhali jamaa na nyie kutoka mikoani,kipata fursa tusaidiane japo kiduchu kutaja baadhi ya majina yalosahaulika. Nachelelea baadae tusijemlaumu Sheikh Mohammed Said kuwa ati kapendelea mno Wazee wake na vinyozi wa Kipata na Mkunguni!? Nashauri tukishamaliza mnakasha huu,nasisi soote kwa pamoja tukusanye makabrasha yetu humu na kuandika rasmi "Marekebisho ya Historia ya Tanganyika kutoka JF".

Sheikh Mohammed,tafadhali kipata wasaa tena naomba udondoshe tena na kusherehesha kwa yale majina na mitaa ya enzi. Huwa nafarijika mno na najifunza mengi yalopita zama hizo kila ninapokusoma.
Naona ulianzia Gerezani na Kipata lakini naona sasa unateremkia Mwembe Togwa na Tuwe Tugawe. Nafikiri pale Swahili no.34 alikua akikaa Shariff Abdalla Al Attas kwa miaka mingi ,halafu akahamia Lumumba Street na mara ya mwisho kabla ya kufariki nafikiri alikua akikaa pale kona ya Sikukuu na Twiga opposite na Masjid Al Shadhily. Pale Msikitini ndio ilikua Al Qadiria kubwa ya kina Sheikh AbdulRahman Shamte,Sheikh Nurdin Hussein Al Shadhily na Sheikh Hashim Haji Abdallah. Kama wajua pia tupe nini asili ya mtaa wa Mwazarau pale Magomeni Mapipa kuitwa jina lile? Na nini asili ya Skuli/Shule ya Msingi Mzimuni magomeni kuitwa jina lile?
Nilicheka saana kile kisa cha yule jamaa wa kibondei Martin Kayamba/Kwiyamba kumbe alikua ni mzandiki na mamluki wa wakoloni tu!?

Kama kuna Mwanajamvi mwingine yeyote nae tafadhali pia atujuze habari za hawa wafuatao/sehemu hizo,na habari zao japo kiduchu za michango yao yoyote walojitolea kwenye harakati za kumng'oa mkoloni na hatimae kufanikisha uhuru:

Bint Sungura wa kona ya Congo na Rufiji,Mwinchande Kidato,Mtumwa Mkenge. Wale wa Korogwe vipi Mzee Mtanmbo wa Gonera nae? Na mtokao Chongoleani na Mikindani mpo? Buyuni Kuu,Ununio,Mkwaja na Saadani mpo!? Sheikh Mwinyikombo Bin Hassan wa Kisiju. Malenga Sheikh Mathias Mnyampala wa Dodoma. Rajab MwinyiKhamis Kiguu cha mbuzi. Chief Bategwa Rusimbi na Sheikh Khalfan Kiumbe wa Kigoma. Vipi wana wa Tongoni na Gombero mpo!? Sheikh Shame wa Mbuyu kutoka Kwale. Bwana Jasusi tafadhali nawe kipata wasaa tudokeze habari za Chief Burito wa Butiama/Mwisenge na Mzee Makongoro wa Musoma mjini. Mwanza kwa kina Sheikh Mohammed Magongo na Idd Mtingwa!? Ramadahani Lofa na Miraj "Mzuri" Al Jahazmy wa Mlingotini. Ramadhani Mwinyipingu wa Jiwe la adabu. MwinyiKhamis wa Dodo,Maalim Mohammed Mwita,Sheikh Khamis Bin Akida Said Al Shirazy,Bwana Al Ruweihy wa Tungi,MwinyiBakari Mwinyimboni Al Amir,MwinyiShomari Mohammed Kimbau wa Mafia,Bwana Keis Bin Ali,Bwana Maalim Bin Salim Al Awadh,Bwana Abdallah Bin Jumaa Luga,Bwana Shaaban Al Madheheby,Sheikh Abdallah Kau wa Kibada. Maalim Pera Ridhwan wa Gombe kutoka Mnyanjani. Bila ya kumsahau Maalim/Sheikh Jumaa Bin Umar wa Bagamoyo.
Hivi hapo Tanzania zipo Archives za Serikali kuangalia kwa kina vitu kama hivi,au ndio vyoote vinapatikana kwenye maktaba za wazungu huku Europe na Amerika!?

Sheikh Mohammed Said,hivi ni kweli kuna kisa cha "Sheikh mmoja" alofanza mijadala na majibizano makali mno kwenye Dar Es Salaam City Legislative Council na kumshinda Al noor Kassum ili kutetea na kuhakikisha city plan ya wakati huo inaidhinisha na kujenga Mororgoro Road hapo ilipo leo Uswahilini!? Niliwahi pia kusikia ati Sheikh huyo huyo ndiye alotetea na kumshawishi mfadhili kukubali hiyo Anatouglo Hall iwepo/ijengwe pale Uswahilini ilipo leo!?
Nakumbuka kuna wakati Sheikh Mohammed pia uliwahi kutaja "mandava" wa enzi zenu!aahaha!! Niruhusu na mimi nijaribu kutaja japo wachache kutoka mikoa mbalimbali ya Tanganyika; Juma Kabati,Dongo la Maka,Sauti ya Chuma,Kunyamale,Hamis Subah, na Salum Machapati!ahahaha!!!
Nahisi ukiwatafuta nduguzo Mpuya Rupia na Abdallah Awadh sonara nao watakukumbusha wale walosahaulika wengine wa Tungi,Kibada,Mjimwema,Jiwe la adabu,Mbwa Maji,Vijibweni na Tuangoma.

Tumalizie na kina Mrisho Mkukuninga mpiga zumari ya Msanja na Rashid Kishingo mpiga Beni bati!aahaha!!

Nasikia pia kulikua na Al Watan,Al manzil na Egyptian Club. Hivi ndio vilikua vyama vya starehe na mapumziko lakini sio TA wala TAA.

Ahsantani.

CC: Ritz,JokaKuu,Kadogoo,Mfumo,Boko Haram,Ami,The Big Show,Jasusi,Sheikh Mohammed Said.

Kadogoo

Kipi tutaelimishana kwenye Imani?

Mimi namuamini na naamini Yesu ni Mtu Kweli na Mungu Kweli. Sijui kitu gani utaniambia au kwakutumia nini utanishawishi i believe the contrary.

Na wewe Unamuamini Mtume Mohammed (S.A.W).

sidhani kama tutaelimishana katika hilo, Ila naamini tunaweza kuheshimiana katika kuamini. Mimi naheshimu unachoamini na ninaomba kwa Mungu (naamini pia ni Mungu mmoja) atupime kwa matendo yetu pia si Imani peke yake.

Mbona tuko pamoja? kama wewe unaona hatuelimishani ktk mijadala sawa tu! ila pointi yako ya mwisho nakubaliana nawe mia kwa mia kuwa tuheshimiane ktk kuamini! wewe heshimu Imani yangu kuwa Yesu Issa mwana wa Maryamu si Mungu wala mtoto wa mungu na mimi niheshimu Imani yako kuwa Yesu ni Mungu na ni Mtoto wake! kuna ubaya hapo?
 
JokaKuu,

Unaweza kutupa takwimu Tanzania wanaokataa shule ni Waislam.

Hapa umetumia maneno ya Maghembe kama ushahidi lakini sisi tukitumia maneno ya Kitwana Kondo, Prof Njozi, Prof Kigoma Malima, mnasema ni hisia tu.

Hebu jiulize kwani iwe watoto wa Kiislam wa Pwani tu ndiyo hawataki shule wasiwe watoto wa Uturuki, India, Pakistani, Indonesia, Dubai, Iran, Saudi Arabia, Misri, Singapore, Qatar.

RITZ:
Jiwe ulilompigia JOKAKUU kichwani ni zito! sidhani kama ataweza kunyanyua kichwa juu!
 
Kadogo,
Mbona mgumu wa kuelewa? Umeambiwa Nyerere hupuuza mambo ya kipuuzi na ambayo hayana tija kwake.
Na alimjibu kambona kulingana na hadhi na umri wa kambona.
Hakuona haja kuhangaika na hadisi za Ms, ndo maana alimpuza tu, na ujuwe Mwl, aliwapuuza wengi sana si Ms, peke yake.

Jee, alimpuuza chaguo lake Mzee Mkapa baada ya kuuza mashirika yote ya umma likiwemo NBC? au alifurahia kazi nzuri aliyofanya Rais wake?
 
Yaani wewe hujui nani ni kiongozi anayekufaa mpaka upate muongozo kutoka kwa viongozi wako wa Dini?!

Hii ndo aina ya wanafunzi wa Mzee Mohamed,
Kwa style hii mtalalamika sana mfumo Kristo...

Umenishangaza sana Mtanzania mwenzangu

Viongozi wa Kiislamu wakitoa muongozo wa nani anafaa kutuongoza ni wachochezi! Maaskofu wakitoa ilani na hata kufunga ili roho mtakatifu awaonyeshe kiongozi stahili wao ni watakatifu!
Duh! ama kweli Waislamu wana damu ya kunguni!
 
Inasemekana mfadhili mkubwa wa TANU alikuwa Abdu Sykes alikuwa na "kabati" la hela nyumbani kwake!!

Ni nini kilitokea hela ya safari UN ikapungua mpaka atokee John Rupia kuokoa Jahazi?!

From a reliable source nimeambiwa,bila John Rupia,safari ya Nyerere UNO,ilishaota majani-i have in my posession breakdown nzima ya huo mchango-haifai kuwekwa hapa-cause heads will roll. Nyerere kutokuandika kitabu amefanya jema-ingebidi aandike uongo kuwahifadi watu
 
Nimekusoma vizuri kwa hiyo tatizo siyo serikali ya CCM kwenye elimu tatizo ni Waislam wenyewe.

Ritz, Mimi nina imani tofauti kidogo. Hadi sasa nafanya sana kazi wilaya ya Lushoto hapa Tanga. Ni wilaya ambayo kwa mujibu wa Thesis ya Pfeiffer (1990) ni asilimia 75% waislamu (kwa sasa nadhani Lushoto ina wakazi sio chini ya 470,000). Lakini mwamko wa elimu Lushoto ni mzuri. Hata tabia ya wazazi kufuatilitia watoto kimasomo sio mbaya. Lushoto familia nyingi hazina utani inapokuja kwenye elimu na hata biashara. Tembelea kariokoo shimoni. Kimaendeleo mabwana hawa wapo mbele. Tanga hii pia zipo wilaya desturi na mwamko ni tofauti kabisa. Sio kwa waislamu au wakiristo. Hapa huenda mchango mkuu ni desturi za jamii husika. Haya nimeyakuta pia Machame, Ugweno, Kamachumu na Babati. Duniani, siifahamu dini inayo-design watu kuwa wavivu, au kuwarudishia maendeleo nyuma. Maendeleo-physical, hayana uhusiano na dini (wajapan, wahindi, wachina largelly sio wakiristo au waislamu). Ni dhana watu wanayounda ili wawatukane au kuwadhulumu baadhi. Hata kwa waislamu, angalia kuwa the most advanced muslim nations ni za Asia (Malaysia, Indonesia na akina Turkey nk)sio za hapa Middle East pamoja na resources walizonazo.
 
Ritz,

..Prof.Maghembe alikuwa waziri wa elimu, kwa hiyo hizo takwimu alizotoa zinatosheleza. unachoweza ku-argue kutokea hapo ni conclusions alizotoa.

..kwa mtizamo wangu Prof.Jumanne Maghembe ni kama vile ametoa majibu kwa madai ya Prof.Malima, Prof.Njozi, na Mzee Kitwana Kondo.

..Prof.Malima alidai tatizo fitina na kutokuwepo kwa utaratibu wa namba za mtihani. sasa Prof.Maghembe amekuja kubainisha kwamba tatizo ni UTORO wa wanafunzi.

..mimi sisemi kwamba Uislamu ni tatizo, ila nasema Waislamu ni waathirika wa mazingira ya kijamii/social na kiuchumi/economic yanayopelekea utoro wa wanafunzi ktk mikoa ya Pwani.

..inawezekana shule ni mbaya, inawezekana wazazi hawana uwezo ni masikini, au pengine hakuna mwamko, huenda kuna mila na tamaduni mbaya etc etc. ushauri wangu ni kwamba tuangalie kila kitu, na tusiweke udini mbele, bali tuongozwe na UMOJA wetu kama WATANZANIA.

cc: gombesugu, Nguruvi3, Kadogoo, Ami, Son of Alaska, THE BIG SHOW

Hii conclusion yako ya inawezekana, labda, huenda au pengine haileti maana wala tija kwa tatizo hilo la elimu! Umoja wa Kitanzania mmeufanya kuwa ni wimbo huku mkijifanya mnaipenda sana Tanzania kuliko Wengine!
Kama mnatambua tatizo la elimu kwa wanafunzi wanaoishi maeneo yenye Waislamu wengi tangu tupate uhuru kwanini mnapata kigugumizi Waislamu wakiitaka SErikali iunde tume huru kuchunguza tatizo hili?

Mbona Serikali imeunda tume haraka sana baada ya wanafunzi kufeli vibaya mwaka jana? Serikali ya Nyerere iliunda tume kuchunguza tatizo la kabila la Wabarbeig na kupata ufumbuzi! Serikali ya Mkapa iliunda tume kuchunguza kifo cha mbwa wa Mjerumani! Kwanini likija suala la Waislamu wimbo wa umoja na mshikamano huwa ni silaha ya kwanza inayotumiwa na Serikali na washirika wake kama wewe Jokakuu, MM na wengine!

Rais mstaafu Mkapa alikiri kuguswa na mgogoro uliokuwepo Zanzibar tangu mwaka 1995 na kudai huwa hapati usingizi tokana na tatizo hilo! ktk miaka yote 10 ya utawala wake watu wamepoteza maisha, mayatima kuongezeka, na hata kuzikana ilikuwa ni adimu! kwanini Ktk awamu ya kwanza tu ya Rais Kikwete ghafla Zanzibar kuna fanyika uchaguzi huru na salama na kuundwa Serikali ya umoja wa kitaifa! why?
 
Mbona tuko pamoja? kama wewe unaona hatuelimishani ktk mijadala sawa tu! ila pointi yako ya mwisho nakubaliana nawe mia kwa mia kuwa tuheshimiane ktk kuamini! wewe heshimu Imani yangu kuwa Yesu Issa mwana wa Maryamu si Mungu wala mtoto wa mungu na mimi niheshimu Imani yako kuwa Yesu ni Mungu na ni Mtoto wake! kuna ubaya hapo?

Respecteds Kadogoo, Fletcher and others; Here is a request; please restrain yourselves to your own religions and religious convictions, this has all indications that it will soon get nasty if you dont check yourselves and infect others; and we just dont want it. Lets focus on our topic regardless of our spiritual orientation. Else, you can just peruse the thread, read, and safely log off.
 
Nimekusoma vizuri kwa hiyo tatizo siyo serikali ya CCM kwenye elimu tatizo ni Waislam wenyewe

Mchango wa Serikali ya CCM katika kushuka kwa kiwango cha Elimu liko pale pale nafikiri hakuna haja hata ya kubishana
juu ya hilo. Mathalani miuondombinu ya Elimu kwa maeneo mengi nchini haipo vizuri, Nyumba za Walimu, Madarasa,
Vitabu na zana za kujifunzia na kufundishia ni haba sana. Ukichanganya hilo na mwamko wa Elimu wa Watu wa eneo husika unauwa kabisa Elimu.

Kwa hili la mwamko siwezi kusema ni Uislam ndiyo umesababisaha hayo, ila la Msingi ni kukubali kuwa kuna Tatizo kubwa
kwenye hayo maeneo na hilo liko wazi. Ukishakubali tatizo inakuwa rahisi sasa kutafuta njia na namna ya kuondoka hapo
ulipo.

1. Mathalani ni kwa kiasi gani Wakaazi wenyewe wa Pwani wanahimiza watoto wao kusoma (unatafuta suluhisho).
2. Ni kwa nini Walimu wanakimbia kufundisha kwenye hayo maeneo,? (Unatafuta jawabu na suluhisho)
3. Walimu wanapata ushirikiano wa kutosha toka kwa wakazi wa maeneo husika?
4. Mtazamo wa Wazazi kuhusu elimu ya watoto wao uko vipi?

Mchango wa wazawa wa eneo husika katika masuala ya Elimu kwenye ufanisi au uharibifu ni mkubwa sana hata kama
Serikali italeta Walimu, Vitabu nk. Ni vyema pia kujifunza kwa wengine: Kwa mfano nimeishi Kenya, kule maeneo ya Waluo
ukimtembelea Mzee fulani na akawa ana mtoto yupo Sekondari au Chuo hata kama hujamuuliza atakwambia tu kuonyesha
kujivunia Kijana wake anayepata Elimu. Kwao ni fahari sana na kitu cha muhimu sana kusoma.

Hata Kilimanjaro au Kagera au hata Mbeya kupata Elimu ni kitu cha kujivunia sana. Lakini Mikoa ya Pwani hali iko hivyo?
au wanaridhika na hapo walipo? Kama wanafunzi wanaweza kubaka Walimu au kupiga Walimu na Wananchi wakachukulia
sawa tu unategemea nini?

Hizo hoja juu ndiyo Taasisi kama ya WARSHA ya akina MS walitakiwa wayafanyie kazi si "Utafiti" wa kutafuta mchawi
huku ukiwa na jibu mfukoni. Na ndiyo maana uliporomoka kama nyumba ya barafu.
 
Muheshimiwa Nguruvi3,
Nimefurahi saana kwa umahiri wako wa hao watu na mitaa/sehemu hizo! Nakukubali kwa u-Al Watan wako!ahaha!! Nahisi sasa unaanza kuwa pamoja na Sheikh Mohammed Said, na pia ni uzuri tumwache atupe darsa kwa utaratibu na huku sootetunamuuliza maswali ya kina na kwa ustaarabu. Kidogodogo ndo mwendo lakini tutafika.

Hivi ni nani alikua msomaji wa kwanza wa mashairi na tenzi kwenye Radio Kichwele!? Tafadhalini naomba tujuzane wenzangu?

Huku kwenye nchi za wenzetu/"mataifa ya magharibi" wana utaratibu mzuri na wanathamini na kuwaenzi saana "wazee wao" na watu walotoa michango kwenye Historia/ ya nchi zao. Hakuna mchango ati mdogo saana au wa kipuuzi katika harakati za kupatikana uhuru wa nchi au mapambano ya nchi! Nashangaa sisi tumepoteza tamaduni hizi tulorithi toka kwa mababu zetu!

Tafadhali jamaa na nyie kutoka mikoani,kipata fursa tusaidiane japo kiduchu kutaja baadhi ya majina yalosahaulika. Nachelelea baadae tusijemlaumu Sheikh Mohammed Said kuwa ati kapendelea mno Wazee wake na vinyozi wa Kipata na Mkunguni!? Nashauri tukishamaliza mnakasha huu,nasisi soote kwa pamoja tukusanye makabrasha yetu humu na kuandika rasmi "Marekebisho ya Historia ya Tanganyika kutoka JF".

Sheikh Mohammed,tafadhali kipata wasaa tena naomba udondoshe tena na kusherehesha kwa yale majina na mitaa ya enzi. Huwa nafarijika mno na najifunza mengi yalopita zama hizo kila ninapokusoma.
Naona ulianzia Gerezani na Kipata lakini naona sasa unateremkia Mwembe Togwa na Tuwe Tugawe. Nafikiri pale Swahili no.34 alikua akikaa Shariff Abdalla Al Attas kwa miaka mingi ,halafu akahamia Lumumba Street na mara ya mwisho kabla ya kufariki nafikiri alikua akikaa pale kona ya Sikukuu na Twiga opposite na Masjid Al Shadhily. Pale Msikitini ndio ilikua Al Qadiria kubwa ya kina Sheikh AbdulRahman Shamte,Sheikh Nurdin Hussein Al Shadhily na Sheikh Hashim Haji Abdallah. Kama wajua pia tupe nini asili ya mtaa wa Mwazarau pale Magomeni Mapipa kuitwa jina lile? Na nini asili ya Skuli/Shule ya Msingi Mzimuni magomeni kuitwa jina lile?
Nilicheka saana kile kisa cha yule jamaa wa kibondei Martin Kayamba/Kwiyamba kumbe alikua ni mzandiki na mamluki wa wakoloni tu!?

Kama kuna Mwanajamvi mwingine yeyote nae tafadhali pia atujuze habari za hawa wafuatao/sehemu hizo,na habari zao japo kiduchu za michango yao yoyote walojitolea kwenye harakati za kumng'oa mkoloni na hatimae kufanikisha uhuru:

Bint Sungura wa kona ya Congo na Rufiji,Mwinchande wa Kidato,Mtumwa Mkenge. Wale wa Korogwe vipi Mzee Mtanmbo wa Gonera nae. Na watokao Chongoleani,Tongoni,Mnyanjani,Buyuni Kuu,Ununio na Saadani mpo!? Mwinyikombo Hassan wa Muhoro/Rufiji,Malenga Sheikh Mathias Mnyampala, wa Dodoma,Rajab MwinyiKhamis Kiguu cha mbuzi,Chief Bategwa Rusimbi na Sheikh Khalfan Kiumbe wa Kigoma. Vipi wana wa Tongoni na Gombero mpo!? Sheikh Shame wa Mbuyu kutoka Kwale. Bwana Jasusi tafadhali nawe kipata wasaa tudokeze habari za Chief Burito wa Butiama/Mwisenge au pale mwanza Mzee Makongoro,Sheikh Mohammed Magongo na Idd Mtingwa!? Ramadahani Lofa wa Mlingotini na Miraj "Mzuri" Al Jahazmy wa Mlingotini. Ramadhani Mwinyipingu wa Jiwe la adabu. Bila ya kumsahau Maalim/Sheikh Jumaa Bin Umar wa Bagamoyo.
Hivi hapo Tanzania zipo Archives za Serikali kuangalia kwa kina vitu kama hivi,au ndio vyoote vinapatikana kwenye maktaba za wzungu huku Europe na Amerika!?

Sheikh Mohammed Said,hivi ni kweli kuna kisa cha "Sheikh mmoja" alofanza mijadala na majibizano makali mno kwenye Dar Es Salaam CityLegislative Council na kumshinda Alnoor Kassum ili kutetea na kuhakikisha city plan ya wakati huo inaidhinisha na kujenga Mororgoro Road hapo ilipo leo Uswahilini!? Niliwahi pia kusikia ati Sheikh huyo huyo ndiye alotetea na kumshawishi mfadhili kukubali hiyo Anatouglo Hall iwepo/ijengwe pale Uswahilini ilipo leo!?
Nakumbuka kuna wakati Sheikh Mohammed pia uliwahi kutaja "mandava" wa enzi zenu!aahaha!! Niruhusu na mimi nijaribu kutaja japo wachache kutoka mikoa mbalimbali ya Tanganyika; Juma Kabati,Dongo la Maka,Sauti ya Chuma, na Salum Machapati!ahahaha!!!
Nahisi ukimtafuta nduguyo Mpuya Rupia nae atakukumbusha wale walosahaulika wengine wa Tungi,Kibada,Mjimwema,Jiwe la adabu na Tuangoma.

Tumalizie na kina Mrisho Mkukuninga mpiga zumari ya Msanja na Rashid Kishingo mpiga Beni bati!aahaha!!

Nasikia pia kulikua na Al Watan,Al manzil na Egyption Club. Hivi ndio vilikua vyama vya starehe na mapumziko lakini sio TA wala TAA.

Ahsantani.

CC: Ritz,JokaKuu,Kadogoo,Mfumo,Boko Haram,Ami,The Big Show,Jasusi,Sheikh Mohammed Said.

Gombesugu:

Kwa kweli Mohamed said katuamsha! mi nilikuwa mkali wa somo la Siasa na historia ya Nyerere kupigania uhuru nilikuwa naienzi sana na hakuna mtu niliekuwa nikimheshimu na kumenzi kama yeye! Lakini baada ya kuja kusoma historia tofauti na ile niliyofundishwa Shuleni, nimesikitika sana!

Wakati wa somo la historia tulijazwa uongo kuwa Vasco Da Gama alikuja Afrika Mashariki na hasa Tanganyika kutafuta viungo na njia ya kumpeleka India! kumbe huyu bwana alikuwa jasusi aliekuja kupeleleza utawala wa Kiislamu uliokuwa na makao yake makuu Kilwa Kisiwani!

Mohamed Said nakuomba ukipata nafasi kidoogo tujuze na historia ya utawala wa Kiislamu huko Kilwa Kisiwani nasikia walikuwa na hata sarafu zao wenyewe na uchokozi wa Wareno dhidi yao! bila kusahau migomo na habari za Marhum Profesa Kigoma Ali Malima.
 
From a reliable source nimeambiwa,bila John Rupia,safari ya Nyerere UNO,ilishaota majani-i have in my posession breakdown nzima ya huo mchango-haifai kuwekwa hapa-cause heads will roll. Nyerere kutokuandika kitabu amefanya jema-ingebidi aandike uongo kuwahifadi watu

Son...

Itakuwa vyema kama utaweka hiyo michango.

Hapa tuko katika kuiweka wazi historia ya uhuru na itapendeza kama wale
walochangia watajulikana huenda ipo siku wataenziwa.

TAA hadi TANU kuna wafadhili wa kudumu ambao wanajulikana na wapo wale
ambao walijitahidi kutoka kila ilipobidi.

Ni vyema hawa wote wakatambulika.

Ama hilo la Nyerere kutoandika kitabu halina uhusiano na azma yake ati anawahifadhi
baadhi ya watu.

Hii si kweli wala haingii katika mantiki.
Nimeona umeweka ''kabati la fedha'' tena isomwe.

Ngoja nikufahamishe.

Abdu Sykes alikuwa na kituo cha kuuza mafuta (filling station) pale Ilala Kitchwele Street
mkabala na ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Kituo hiki kipo hadi leo hii mahali palepale.

Sasa kinapofungwa kituo mauzo ya siku yalikuwa yanapelekwa nyumbani kwake Stanley
Street na hapo ndipo hizo fedha zinatiwa katika hilo kabati la Bi. Mwamvua.

Sasa inapotakikana fedha ofisi ya TANU ndipo hilo kabati hufunguliwa.
 
Muheshimiwa Nguruvi3,
Nimefurahi saana kwa umahiri wako wa hao watu na mitaa/sehemu hizo! Nakukubali kwa u-Al Watan wako!ahaha!! Nahisi sasa unaanza kuwa pamoja na Sheikh Mohammed Said, na pia ni uzuri tumwache atupe darsa kwa utaratibu na huku sootetunamuuliza maswali ya kina na kwa ustaarabu. Kidogodogo ndo mwendo lakini tutafika.

Hivi ni nani alikua msomaji wa kwanza wa mashairi na tenzi kwenye Radio Kichwele!? Tafadhalini naomba tujuzane wenzangu?

Huku kwenye nchi za wenzetu/"mataifa ya magharibi" wana utaratibu mzuri na wanathamini na kuwaenzi saana "wazee wao" na watu walotoa michango kwenye Historia/ ya nchi zao. Hakuna mchango ati mdogo saana au wa kipuuzi katika harakati za kupatikana uhuru wa nchi au mapambano ya nchi! Nashangaa sisi tumepoteza tamaduni hizi tulorithi toka kwa mababu zetu!

Tafadhali jamaa na nyie kutoka mikoani,kipata fursa tusaidiane japo kiduchu kutaja baadhi ya majina yalosahaulika. Nachelelea baadae tusijemlaumu Sheikh Mohammed Said kuwa ati kapendelea mno Wazee wake na vinyozi wa Kipata na Mkunguni!? Nashauri tukishamaliza mnakasha huu,nasisi soote kwa pamoja tukusanye makabrasha yetu humu na kuandika rasmi "Marekebisho ya Historia ya Tanganyika kutoka JF".

Sheikh Mohammed,tafadhali kipata wasaa tena naomba udondoshe tena na kusherehesha kwa yale majina na mitaa ya enzi. Huwa nafarijika mno na najifunza mengi yalopita zama hizo kila ninapokusoma.
Naona ulianzia Gerezani na Kipata lakini naona sasa unateremkia Mwembe Togwa na Tuwe Tugawe. Nafikiri pale Swahili no.34 alikua akikaa Shariff Abdalla Al Attas kwa miaka mingi ,halafu akahamia Lumumba Street na mara ya mwisho kabla ya kufariki nafikiri alikua akikaa pale kona ya Sikukuu na Twiga opposite na Masjid Al Shadhily. Pale Msikitini ndio ilikua Al Qadiria kubwa ya kina Sheikh AbdulRahman Shamte,Sheikh Nurdin Hussein Al Shadhily na Sheikh Hashim Haji Abdallah. Kama wajua pia tupe nini asili ya mtaa wa Mwazarau pale Magomeni Mapipa kuitwa jina lile? Na nini asili ya Skuli/Shule ya Msingi Mzimuni magomeni kuitwa jina lile?
Nilicheka saana kile kisa cha yule jamaa wa kibondei Martin Kayamba/Kwiyamba kumbe alikua ni mzandiki na mamluki wa wakoloni tu!?

Kama kuna Mwanajamvi mwingine yeyote nae tafadhali pia atujuze habari za hawa wafuatao/sehemu hizo,na habari zao japo kiduchu za michango yao yoyote walojitolea kwenye harakati za kumng'oa mkoloni na hatimae kufanikisha uhuru:

Bint Sungura wa kona ya Congo na Rufiji,Mwinchande wa Kidato,Mtumwa Mkenge. Wale wa Korogwe vipi Mzee Mtanmbo wa Gonera nae. Na watokao Chongoleani,Tongoni,Mnyanjani,Buyuni Kuu,Ununio na Saadani mpo!? Mwinyikombo Hassan wa Muhoro/Rufiji,Malenga Sheikh Mathias Mnyampala, wa Dodoma,Rajab MwinyiKhamis Kiguu cha mbuzi,Chief Bategwa Rusimbi na Sheikh Khalfan Kiumbe wa Kigoma. Vipi wana wa Tongoni na Gombero mpo!? Sheikh Shame wa Mbuyu kutoka Kwale. Bwana Jasusi tafadhali nawe kipata wasaa tudokeze habari za Chief Burito wa Butiama/Mwisenge au pale mwanza Mzee Makongoro,Sheikh Mohammed Magongo na Idd Mtingwa!? Ramadahani Lofa wa Mlingotini na Miraj "Mzuri" Al Jahazmy wa Mlingotini. Ramadhani Mwinyipingu wa Jiwe la adabu. Bila ya kumsahau Maalim/Sheikh Jumaa Bin Umar wa Bagamoyo.
Hivi hapo Tanzania zipo Archives za Serikali kuangalia kwa kina vitu kama hivi,au ndio vyoote vinapatikana kwenye maktaba za wzungu huku Europe na Amerika!?

Sheikh Mohammed Said,hivi ni kweli kuna kisa cha "Sheikh mmoja" alofanza mijadala na majibizano makali mno kwenye Dar Es Salaam CityLegislative Council na kumshinda Alnoor Kassum ili kutetea na kuhakikisha city plan ya wakati huo inaidhinisha na kujenga Mororgoro Road hapo ilipo leo Uswahilini!? Niliwahi pia kusikia ati Sheikh huyo huyo ndiye alotetea na kumshawishi mfadhili kukubali hiyo Anatouglo Hall iwepo/ijengwe pale Uswahilini ilipo leo!?
Nakumbuka kuna wakati Sheikh Mohammed pia uliwahi kutaja "mandava" wa enzi zenu!aahaha!! Niruhusu na mimi nijaribu kutaja japo wachache kutoka mikoa mbalimbali ya Tanganyika; Juma Kabati,Dongo la Maka,Sauti ya Chuma, na Salum Machapati!ahahaha!!!
Nahisi ukimtafuta nduguyo Mpuya Rupia nae atakukumbusha wale walosahaulika wengine wa Tungi,Kibada,Mjimwema,Jiwe la adabu na Tuangoma.

Tumalizie na kina Mrisho Mkukuninga mpiga zumari ya Msanja na Rashid Kishingo mpiga Beni bati!aahaha!!

Nasikia pia kulikua na Al Watan,Al manzil na Egyption Club. Hivi ndio vilikua vyama vya starehe na mapumziko lakini sio TA wala TAA.

Ahsantani.

CC: Ritz,JokaKuu,Kadogoo,Mfumo,Boko Haram,Ami,The Big Show,Jasusi,Sheikh Mohammed Said.

Gombesugu,
Kumbe na wewe umo huvumi tu.

Umenipeleka mbali sana.

Shariff Attas mara ya mwisho kumuona ilikuwa Eid Fitr 1990 mimi na Kleist Abdulwahid Sykes
tulikwenda kufuturu nyumbani kwake asubuhi baada ya sala ya Eid.

Alitupa kisa kizuri sana kati yake na Nyerere pale Sokoni Kariakoo ofisini kwa Abdu Sykes.
Kisa ambacho kila mtu akikisikia atapata simanzi.

Nilifika kijiji cha Blantyre nje kidogo ya Glasgow, Scotland.
Hapa ndipo alipozaliwa David Livingstone na kijiji hiki chote kimefanywa kuwa makumbusho yake.

Nilifanya kipindi na BBC Swahili Service ''Barua Kutoka Glasgow'' kuhusu kijiji hiki na Mkuu wa BBC
Swahili Service siku zile Mzee Neville Helms alikipenda sana.

Hapa Dar es Salaam Mtaa wa Lumumba kuna kijana ana collection ya picha nyingi sana za watu
maarufu walioishi katika huu mwambao wa pwani.

Mimi nina hakika hakuna mtu Afrika Mashariki hii amekusanya picha kama hizo.
Nimeona hata picha ya Al Manzil na wanachama wake nk.
 
Gombesugu, Kumbe na wewe umo huvumi tu. Umenipeleka mbali sana. Shariff Attas mara ya mwisho kumuona ilikuwa Eid Fitr 1990 mimi na Kleist Abdulwahid Sykes tulikwenda kufuturu nyumbani kwake asubuhi baada ya sala ya Eid. Alitupa kisa kizuri sana kati yake na Nyerere pale Sokoni Kariakoo ofisini kwa Abdu Sykes. Kisa ambacho kila mtu akikisikia atapata simanzi. Nilifika kijiji cha Blantyre nje kidogo ya Glasgow, Scotland. Hapa ndipo alipozaliwa David Livingstone na kijiji hiki chote kimefanywa kuwa makumbusho yake. Nilifanya kipindi na BBC Swahili Service ''Barua Kutoka Glasgow'' kuhusu kijiji hiki na Mkuu wa BBC Swahili Service siku zile Mzee Neville Helms alikipenda sana. Hapa Dar es Salaam Mtaa wa Lumumba kuna kijana ana collection ya picha nyingi sana za watu maarufu walioishi katika huu mwambao wa pwani. Mimi nina hakika hakuna mtu Afrika Mashariki hii amekusanya picha kama hizo. Nimeona hata picha ya Al Manzil na wanachama wake nk.
Tunakusoma sana Moh Said.. Tupe Darsa,mambo adim sana hayo..
 
Muheshimiwa Nguruvi3,
Nimefurahi saana kwa umahiri wako wa hao watu na mitaa/sehemu hizo! Nakukubali kwa u-Al Watan wako!ahaha!! Nahisi sasa unaanza kuwa pamoja na Sheikh Mohammed Said, na pia ni uzuri tumwache atupe darsa kwa utaratibu na huku sootetunamuuliza maswali ya kina na kwa ustaarabu. Kidogodogo ndo mwendo lakini tutafika.

Hivi ni nani alikua msomaji wa kwanza wa mashairi na tenzi kwenye Radio Kichwele!? Tafadhalini naomba tujuzane wenzangu?

Huku kwenye nchi za wenzetu/"mataifa ya magharibi" wana utaratibu mzuri na wanathamini na kuwaenzi saana "wazee wao" na watu walotoa michango kwenye Historia/ ya nchi zao. Hakuna mchango ati mdogo saana au wa kipuuzi katika harakati za kupatikana uhuru wa nchi au mapambano ya nchi! Nashangaa sisi tumepoteza tamaduni hizi tulorithi toka kwa mababu zetu!

Tafadhali jamaa na nyie kutoka mikoani,kipata fursa tusaidiane japo kiduchu kutaja baadhi ya majina yalosahaulika. Nachelelea baadae tusijemlaumu Sheikh Mohammed Said kuwa ati kapendelea mno Wazee wake na vinyozi wa Kipata na Mkunguni!? Nashauri tukishamaliza mnakasha huu,nasisi soote kwa pamoja tukusanye makabrasha yetu humu na kuandika rasmi "Marekebisho ya Historia ya Tanganyika kutoka JF".

Sheikh Mohammed,tafadhali kipata wasaa tena naomba udondoshe tena na kusherehesha kwa yale majina na mitaa ya enzi. Huwa nafarijika mno na najifunza mengi yalopita zama hizo kila ninapokusoma.
Naona ulianzia Gerezani na Kipata lakini naona sasa unateremkia Mwembe Togwa na Tuwe Tugawe. Nafikiri pale Swahili no.34 alikua akikaa Shariff Abdalla Al Attas kwa miaka mingi ,halafu akahamia Lumumba Street na mara ya mwisho kabla ya kufariki nafikiri alikua akikaa pale kona ya Sikukuu na Twiga opposite na Masjid Al Shadhily. Pale Msikitini ndio ilikua Al Qadiria kubwa ya kina Sheikh AbdulRahman Shamte,Sheikh Nurdin Hussein Al Shadhily na Sheikh Hashim Haji Abdallah. Kama wajua pia tupe nini asili ya mtaa wa Mwazarau pale Magomeni Mapipa kuitwa jina lile? Na nini asili ya Skuli/Shule ya Msingi Mzimuni magomeni kuitwa jina lile?
Nilicheka saana kile kisa cha yule jamaa wa kibondei Martin Kayamba/Kwiyamba kumbe alikua ni mzandiki na mamluki wa wakoloni tu!?

Kama kuna Mwanajamvi mwingine yeyote nae tafadhali pia atujuze habari za hawa wafuatao/sehemu hizo,na habari zao japo kiduchu za michango yao yoyote walojitolea kwenye harakati za kumng'oa mkoloni na hatimae kufanikisha uhuru:

Bint Sungura wa kona ya Congo na Rufiji,Mwinchande wa Kidato,Mtumwa Mkenge. Wale wa Korogwe vipi Mzee Mtanmbo wa Gonera nae. Na watokao Chongoleani,Tongoni,Mnyanjani,Buyuni Kuu,Ununio na Saadani mpo!? Mwinyikombo Hassan wa Muhoro/Rufiji,Malenga Sheikh Mathias Mnyampala, wa Dodoma,Rajab MwinyiKhamis Kiguu cha mbuzi,Chief Bategwa Rusimbi na Sheikh Khalfan Kiumbe wa Kigoma. Vipi wana wa Tongoni na Gombero mpo!? Sheikh Shame wa Mbuyu kutoka Kwale. Bwana Jasusi tafadhali nawe kipata wasaa tudokeze habari za Chief Burito wa Butiama/Mwisenge au pale mwanza Mzee Makongoro,Sheikh Mohammed Magongo na Idd Mtingwa!? Ramadahani Lofa wa Mlingotini na Miraj "Mzuri" Al Jahazmy wa Mlingotini. Ramadhani Mwinyipingu wa Jiwe la adabu. Bila ya kumsahau Maalim/Sheikh Jumaa Bin Umar wa Bagamoyo.
Hivi hapo Tanzania zipo Archives za Serikali kuangalia kwa kina vitu kama hivi,au ndio vyoote vinapatikana kwenye maktaba za wzungu huku Europe na Amerika!?

Sheikh Mohammed Said,hivi ni kweli kuna kisa cha "Sheikh mmoja" alofanza mijadala na majibizano makali mno kwenye Dar Es Salaam CityLegislative Council na kumshinda Alnoor Kassum ili kutetea na kuhakikisha city plan ya wakati huo inaidhinisha na kujenga Mororgoro Road hapo ilipo leo Uswahilini!? Niliwahi pia kusikia ati Sheikh huyo huyo ndiye alotetea na kumshawishi mfadhili kukubali hiyo Anatouglo Hall iwepo/ijengwe pale Uswahilini ilipo leo!?
Nakumbuka kuna wakati Sheikh Mohammed pia uliwahi kutaja "mandava" wa enzi zenu!aahaha!! Niruhusu na mimi nijaribu kutaja japo wachache kutoka mikoa mbalimbali ya Tanganyika; Juma Kabati,Dongo la Maka,Sauti ya Chuma, na Salum Machapati!ahahaha!!!
Nahisi ukimtafuta nduguyo Mpuya Rupia nae atakukumbusha wale walosahaulika wengine wa Tungi,Kibada,Mjimwema,Jiwe la adabu na Tuangoma.

Tumalizie na kina Mrisho Mkukuninga mpiga zumari ya Msanja na Rashid Kishingo mpiga Beni bati!aahaha!!

Nasikia pia kulikua na Al Watan,Al manzil na Egyption Club. Hivi ndio vilikua vyama vya starehe na mapumziko lakini sio TA wala TAA.

Ahsantani.

CC: Ritz,JokaKuu,Kadogoo,Mfumo,Boko Haram,Ami,The Big Show,Jasusi,Sheikh Mohammed Said.

gombesugu,

The Great Thinker, hiyo mipini yako ni "Mubashar" umetutajia wazee wetu umewaka Hadhwarani umenikumbusha mbali kuna wazee wengi umewataja nimewaona takuwa mchoyo wa Fadhwila nisipo kupongeza.

Umetaja Baadhwi ya mitaa yetu sisi wanywa Gahawa wa Stanley Street, Mbaruku Street, New Street, Manyema Street, Chura Street, Udoe Street, Mkunguni Street, Raha Street, Narung'ombe Street, Congo Street, Mchikichi Street, Livingstone Street, Msimbazi Street, Uhuru Street, Kipata Street, Lindi Street, Somali Street, Kariakoo Street, Tandamti Street, Pemba Street, Muhonda Street, Nyamwezi Street, Swahili Street....nimechoka kutaja maeneo ya wanywa gahawa.

Kuna mzee mmoja anaitwa Idd Mtingwa, marehemu nadhani ni baba ya Rukia Mtingwa wa Voda huyu mzee alikuwa rafiki kipenzi wa marehemu mzee alikuwa afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.

Mwenyezi Mungu hawape rehema hawa wazee wazalendo waliotangulia mbele ya haki.
 
Last edited by a moderator:
Thank you MM. Ameonyeshwa na amekubali.

Hapa ndipo tunasema hakuna utafiti na wala haihitaji mtu kuwa mtafiti au kufanya utafiti kujua kuwa hakukuwa na utafiti. Makala zake mwenyewe zimemuumbua.
Tumemuonyesha kuwa Dosa Aziz alikuwa anamjua kabla ya 1952! Kwa kutumia maandiko yake mwenyewe.

Dosa alikuwa inner circle wa TAA na HQ na wala hakuwahi kukanyaga Makerere.
Anaposema eti wenzake wa Makerere automatic ameshamuondoa Dosa katika inner circle.

Katika jitihada za kumdhalilisha Nyerere na kumkweza Abdul Sykes, Mohamed anajikuta anadhalilisha sana wazee wetu.
Keshamdhalilisha Dosa kuwa hakumjua Nyerere na hakuwa Makererian.
Keshamdhalilisha sana K.Sykes kwa kushindwa kutetea Ufisadi wa Nyumba kama ulivyobainishwa na Mag3
Kamdhalilisha Hamza Aziz kwa kumpa ushujaa leo tunajua alikuwa mhalifu na aliokolewa na Nyerere
n.k n.k

Kwa wale wanaodhani huwa tunachambua mistari ya Mohamed moja baada ya mwingine ili kumkomoa huu aliousema ni ushahidi kuwa Mohamed hana ground to stand. Leo amekiri, narudia baada ya kukana miaka nenda Ulaya na Marekani leo ndani ya free for all JF amekiri kuwa Nyerere alijulikana TAA. Case dismissed.

Nguruvi3, mwanakijiji na wengine.

Mtakuwa hamjawatendea haki waTanzania wenzenu kama mtaishia hapa hapa kubishana na kupongezana bila kukusanya haya mawazo yenu na kuyaweka katika kitabu ambacho kinaweza tumiwa na vizazi vingi vingi kupingana na Al Akhiy MS ambaye ametujuza mengi.

Nawanaswihi tumieni busara nanyi kuandika kitabu chenu na tutakuwa tayari kabisa kuwapa support kwa hali na mali ili vizazi vya sasa na vijavyo viweze pata historia sahihi ya uhuru wa Tanganyika.

watendeeni haki watanzania.
 
Ni ushauri mzuri, tumeusikia na tutaufanyia kazi mkuu
 
Back
Top Bottom