Mag3;6109922]
Barubaru, mbona unapata taabu kuuelewa huu mnakasha unahusu nini, kinchogomba si Mohamed kuandika historia ya wazee wake, hapana, ni namna anavyowahadaa wananchi kwa madai ya kipuuzi yasiyo na ukweli wowote...
Mag3, kwahakika wengi sana wamesema na wamerudia kuwa Mohamed akaiamua kutaja majina ya wajukuu, vilembwe na vining'inia toka miaka waarabu wanaingia Mzizima, wala hakuna atakaye nyanyua mdomo.
Tatizo linakuja pale ambapo, kwanza atatumia majina hayo kama Tanganyika, pili atayatumia kupandia ngazi kwa kudhalilisha michango ya wengine na muhimu kupotosha kama si kuficha ukweli au kudanganya.
Sijui Baru baru angependa kila mmoja aandike kitabu kuhusu maana na makusudio ya commonwealth.
Hivi kweli inahitaji kitabu hiyo. Lazima aelewe kuwa kama ameandika kitu, basi maandishi hayo yapo kwa credit, discredit, criticized and a the subject to critical thinking and analysis.
Hizi habari za kila mtu kuandika kitabu ni dalili za kukwepa hoja muhimu sana.
Kila mmoja ameonyesha mchango wake ingawa kwa bahati mbaya sana Mohamed hapendi kueleza ukweli.
Hivi sasa kuna hoja ya WML na Sheikh Rukara ambayo ameikabidhi kwa wizara ya mambo ya ndani.
Hoja hii ni muhimu sana kwasababu inafafana na madai yake kuwa sheikh Amir alifukuzwa kwa fihi, husda na inda na hakuwa na kosa.
Kwa kiongozi makini kama Nyerere Rukara aliyekuwa mfanyakazi wa WML asingeruhusiwa kufanya harakati za kidini.
Na watu hawaelewi kuwa huyu bwana ameoa na anamiliki vitu visivyoruhusiswa kwa mtu mwenye work permit.
Na wala hakuwa na work permit, alijulikana kama Mtanzania akiwa na hati zote hadi pale alipoteuliwa kuwa seneta.
Alijihusisha sana na makundi ya kisiasa wakati wa machafuko na ndiyo maana amerudishwa kula keki ya taifa Burundi.
Hapa ndipo tunasema Sheikh Amir kama alivyo Maliki na Rukara hawakuishi nchini kwa kufuata misingi na taratibu za kisheri.Taratibu zilizowawezesha wao kuishi na kufanya uharamia ni zile zile anazolalamikia Mohamed chini ya mfumokristo.
Lakini pia kuhusu WML hapa kuna funzo linalokataa kabisa maandishi na dhana nzima ya Mohamed kuandika kuhusu wazee wake.
Kilichomkuta sheikh Amir ni sawa na kile cha Maliki na Rukara.
Tunafaham kuwa Rukar alipata kibali cha kuishi na kufanya atakayo katika mfumo kristo
Tumeona WML wakiingia na kufungasha virago kwa hiyari yao.
Sasa wapi unatoka ushahidi kuwa wakrito wanapewa upendeleo na taasisi zao kusajiliwa tofauti na waisla.
Mo kaandika kuwa wakristo wanaruhusiwa kuwa na uhusiano na world church council, world vision na Vatican.
Waislam wamekataliwa. Sasa WML au Africa Muslim agency ni ya watu wa aina gani?
Hili nalo linahitaji kitabu kweli!
Kila tunapojaribu kuweka rekodi clear tunaambiwa tunapinga.
Tunaambiwa tuandike vitabu.
Mag3, Gombesugu baada ya kujificha ficha katika kivuli cha dini hakika ametoka kiukweli.
Sidhani kama kuna atakayepinga majina ya wazee wake. Lakini basi wazee wake si Tanganyika