Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Maswala ya Waislam yapi ambayo siyafahamu?

Unamjua vizuri Makamba Jr?

Si kama hayo ya WML!

Makamba si huyu mtoto wa Yusuph Makamba au wewe unamjua yupi aliyekuwa Magogoni?au ulitaka nimjuaje?
 
Si kama hayo ya WML!

Makamba si huyu mtoto wa Yusuph Makamba au wewe unamjua yupi aliyekuwa Magogoni?au ulitaka nimjuaje?

Madai na dhulma dhidi ya Uislam yapo wazi tatizo la sio WML.

Huyo huyo Makamba wewe si ndiyo umemtaja mwanzo tujuze ni dini gani?
 
Gombesugu,
Kumbe na wewe umo huvumi tu.

Umenipeleka mbali sana.

Shariff Attas mara ya mwisho kumuona ilikuwa Eid Fitr 1990 mimi na Kleist Abdulwahid Sykes
tulikwenda kufuturu nyumbani kwake asubuhi baada ya sala ya Eid.

Alitupa kisa kizuri sana kati yake na Nyerere pale Sokoni Kariakoo ofisini kwa Abdu Sykes.
Kisa ambacho kila mtu akikisikia atapata simanzi.

Nilifika kijiji cha Blantyre nje kidogo ya Glasgow, Scotland.
Hapa ndipo alipozaliwa David Livingstone na kijiji hiki chote kimefanywa kuwa makumbusho yake.

Nilifanya kipindi na BBC Swahili Service ''Barua Kutoka Glasgow'' kuhusu kijiji hiki na Mkuu wa BBC
Swahili Service siku zile Mzee Neville Helms alikipenda sana.

Hapa Dar es Salaam Mtaa wa Lumumba kuna kijana ana collection ya picha nyingi sana za watu
maarufu walioishi katika huu mwambao wa pwani.

Mimi nina hakika hakuna mtu Afrika Mashariki hii amekusanya picha kama hizo.
Nimeona hata picha ya Al Manzil na wanachama wake nk.

Sheikh Mohammed Said,

Asalaam Alaykum! Tafadhali nijaalia fursa kukuletea bayana yangu hii nyepesi. Niwie radhi maana awali nalisema ningepumzika lakini kuona yale malumbano ya yule "Bibi wa baibui", mambo ya chapati na lile kabati la senti Wallahi nimeshindwa kustahamili!ahaha!! Waswahili hunena; "kisebusebu na kiroho papo".

Naona kila ukiwaambia Jamaa hapo huijui hiyo habari ya huyo "Bibi wa baibui",unalazimishwa na kufanziwa inadi ya kuwa shurti utoe jibu. Ashakum si matusi; mathalan ukinena kuwa yule "Bibi wa baibui" alipata fadhila ile sababu alikuwa ni kimada wa Bwana Nyerere!? Si ndo yatakua yaleyale kwamba una chuki na Mwalimu,unamkashifu na kumfanyia tashtit. "Funika kombe mwanaharamu apite"! Mola takujaalia usije ukangia mtego wao kwa kujibu usolijua au uso hakika nalo.

Nimefurahika na ile safari yako. Napajua uzuri pale Blantyre Lanarkshire. Nastaajabu kuwa Serikali hapo Tanzania ati mpaka leo bado inamuenzi "mvumbuzi" "Dr" Livingstone na kumwachia aendelee kujinasibu na moja ya mitaa yetu maarufu hapo Mzizima!?
Kuna "tambara" chafu mno limemfumka (new evidences has emerged/ been extracted) pale Royal Geographical Society kuhusu unyama ,udhalim,umaluuni,uzandiki na vitimbi vingi mno alofanza huyo swahib yako "Dr" Livingstone!ahaha!!

Nimesikitika mno kuyasikia hayo japo sikushangaa. Aliwatendea mengi machafu wa -Afrika katika hizo safari zake za "uvumbuzi". Nina mawasilano pale na "jamaa" na tunafuatilia hili kwa makini,"mpaka kieleweke"!ahaha!! (niwie radhi maana humu JF nimejifunza mengi na hasa lugha mpya!)ahaha!!
Nalipatwa na "Duaa Al Mustaajaba" niliposikia at hata Mwai Kibaki nae kapewa jina la mtaa/barabara maarufu hapo Mzizima!? Hivi hiyo nchi ina wenyewe kweli!? Ama kwa hakika kuna mengi ndipo, Wazee wetu walinena; "kuwa uyaone"!

Nimefurahi habari za yule "jamaa wa Lumumba Street" mwenye picha kadhaa,Insha Allah nikijaaliwa kufika italazim "tukamwamkue". Nina group photograph ya BBC Swahili enzi zile ikinguruma kikweli,nina hakika itakuwa wengi wao unawafahamu. Mfano Zena Bakhressa na nafikiri Mzee Bin Dallas!?
Nakumbuka mno enzi za Madrasa maarufu kama:Kwa maalim Sakina, Shariff AbdilQadir Juneid,Al baadawy na Al madrasat Al Hassanain!

Ahsanta na nakutakia kila la heri kwa shughuli nzito ulonayo.

CC: Ritz,Ami,Boko Haramu,Mfumo,Kadogoo,Barubaru,The Big Show,Wickama,JokaKuu,Jasusi,Nguruvi3,Mag3
 
gombesugu,

Miaka mitatu ya nyuma tumemzika Sheikh Shariff Juneid. Msikiti wake Qibrateen mtaa wa Aggey.
 
Last edited by a moderator:
Geeky,

Salaam na nafurahi kufahamiana humu.

Hicho Kigoda cha Mwalimu,nasikia kuna wakati wanafunzi/waalikwa walimzoma pita kiasi Professor Ustaadh Malenga Dr. Abdilatif Abdalla,ati kisa ni kuwa alitoa mada yake kwa kutumia lugha ya Kiswahili!? Na mpaka ikalazim Professor Shariff AbdilRahman Babu aiiingile kati kuwatuliza. Hivi hiki kisa kilitokea kweli hapo "kigodani"!? Tafadhali nihadith japo kiduchu ndugu yangu.
Maana ya kukuuliza hivi ni kuhusu ule "mwaliko" ulotoa na kutaka kujua taratibu na usalama wa watu wenye majina kama yetu!? ahaha!!

But in a serious note,niliposikia kisa hicho nalisikitika mno. Laiti hao jamaa wangelijua mahaba na hishma kubwa alokua nayo Ustadh Latif kwa Bwana Nyerere tangia kipindi hicho basi wala wasingethubutu kufanza hayo!?
Abdilatif is one of the most distinguished Pan Afrikanists alive. Na kwa wale wajuvi wasotaka kujua kawaulizeni kina Professor Abdul Mutajuka,Dr. Zubeida Tumbo,Dr. Massamba,Professor Kezilahabi,Jenerali Twaha Khalfani Ulimwengu na Bwana Walter Bgoya. Maana wanamfahamu huyu mtu kwa umahiri na ustaarabu alonao.
Wale mlio nje mwaweza kumjua huyu mtu kwa Professor Ngungi wa Thiongo,Professor mwana Malenga Ali Mazrui,Dr. Yoweri Museveni,LSE-London School Of Economics na Leipzig University.

Kwa hiyo Bwana Geeky tutaufikisha mwaliko ulotoa kwa wanataaluma/ma-Professor lakini "pembuka" japo kidogo!(niwie radhi natuma "lugha ya JF"!)ahahaha!!

Ahsanta.

CC; Ritz,Ami,Sheikh Mohammed Said,Barubaru,Jasusi,Jokakuu,The Big Show,Kadogoo,Boko Haram,Mwanakijiji,Mfumo,Nguruvu3,Mag3,Wickama
 
gombesugu,

Miaka mitatu ya nyuma tumemzika Sheikh Shariff Juneid. Msikiti wake Qibrateen mtaa wa Aggey.

Inna Lillahi Wa Inna Illahi Rajiuni. "Qul Nafs Dhaalikat Al Maut"

Ahsanta kwa kunijuza, nimepata simanzi mno. Wazee wetu wanazidi kututoka kula kukicha lakini ndo kilimwengu,baki Ya Rabih Ya Alllah!!
 
Katika madai ya baadhi ya waislam ni kuonewa.
Uonevu huo ulikuwa pamoja na kufukuzwa kwa masheikh, kuweka ndani na kunyanyaswa kutokana na imani yao.
Jingine ni kuvunjwa kwa taasisi za kwaendeleza kama EAMWS, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kujiunga na mashirika ya kimataifa.

Wakati hayo yakiendelea wenzao wakristo wameendelea kuwa na fursa.

Hawa World Muslim League (WML) nia yao ilikuwa ni kutoa misaada kwa waislam katika mambo kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na elimu na afya.

Kwa muda waliokuwa hapa nchini,ilikuwa taasisi ya watu wachache wakuchumia tumbo na mmojawapo ni huyu Rukara.
Mohamed anajua hilo ndio maana anakwepa kuliongea.

Hakuna hata VETA iliyoachwa na WML sasa leo tunaambiwa EAMWS ilitaka kujenga chuo kikuu wakadhaulumiwa!!
Madai kuwa wamasheikh wananyanyaswa si kweli kwasababu sheikh Rukara akiwa mrundi na raia wa kigeni alikuwa anafanya harakati za kisiasa ndani ya misikiti.

Sheikh huyo huyo alikuwa na passport ya kusafiria ya Tanzania.
Sasa leo tunaposikia eti kuna mfumokristo, ni jambo la ajabu sana.
Mfumo upi huo uliomuacha Rukara akaendesha siasa akiwa kiongozi wa dini tena nje ya nchi yake?
Hivi rais mwenye akili timamu atasita kumweka Rumande mtu kama huyu!

Mtu huyo anamiliki nyumba na viwanja kama Mtanzania mwingine kwa kutumia hati chafu ya utanzania aliyopewa na watu walioko madarakani ambao wengi ni wa mfumokristo! Angalieni confusion hapa!
Hivi hili dudu mfumokristo lipo kweli au ni njozi tu za ''nabii'' wa zama zetu.

Funzo moja ambalo waislam lazima walielewe na hili tunaeleza bila kusita, haya mashirika mnayoambiwa yamezuiwa hilo halipo. Kuna mashirika ya kimataifa ya taasisi za kiislam yanafanya kazi nchi.

Msizingatie aina hii ya ghilba na upuuzi.Msidanganywe kuwa mashirika hayo yapo kwa ajili yenu, WML wamekuja hadi wameondoka kuna waislam hajui hata uwepo wa shirika hilo. Ni ulaji tu.

Baada ya ulaji huo atatokea mtu na kusema eti kuna chuo cha ufundi kilikuwa kijengwe Kibaha serikali ikakataa.
Sasa waislam wenye mapenzi mema na maono wajiulize, kama walikuwa hawajui WML uwepo wake, pesa zilivyofadhili vita na kufungwa kwa shirika kutokana na ''uhalifu wa ndani '' nani akubali kuwa uhalifu huo ulikoma na WML na wala si wa ujenzi wa chuo Kibaha.

Ikifika hapa huwa nawaasa watu waangalie kiini cha tatizo kwanza.
Hizi tambo za mfumokristo ni kutaka kuwapoteza na kuwapumbaza watu.
Tatizo lipo ndani ya society kwa kuanzia.
Zinatafutwa sababu za kutuhumu mfumo bila sababu ili kujaza watu jazba. WML ni ya waislam na imehujumiwa na waislam wenyewe. Hili halisemwi ndio maana Mohamed anakimbia sana hii hoja. Kuna uchafu mwingi sana anaujua ukiwekwa wazi hoja zake zitabomoka zenyewe

Tunapata majibu kuwa kuna mfumo nje ya ule mfumokristo uliowezesha waaasi wa Burundi kupata passport, kuishi na kufanya kazi ndani ya misikiti na kuhujumu hata shirika la dini.

Kama tutakubali kuwa kuna mfumo mwingine basi tukubali kwanza hakuna mfumo wowote na hivyo hili dudu mfumokristo ni sehemu ya kuficha uchafu unaofanywa na waislam wenyewe.

Mohamed hawezi kulezea kuhusu WML kwa kutambua ule ulikuwa mradi na ulifisadiwa na waislam wenye na hakukuwa na kikwazo cha WML kufanya kazi.

Nadhani hata wale wabishi tu watakubaliana nami kuwa kina Mohamed ni tatizo kabla ya mfumokristo.
Leo anaficha madhambi na udhalim wa WML huku akinyooshea kidole watu wasiohusika.
Huyu ndiye akueleze kitu kuhusu EAMWS au Chuo cha Kibaha ukiingize akilini, atakuwa amekudharau sana!

cc. Ritz, Wickama, Big show, Gombesugu, JokaKuu, Mag3, Jasusi, Mwnakijiji, Platoozom
 
JokaKuu,

Hebu jiulize kwani iwe watoto wa Kiislam wa Pwani tu ndiyo hawataki shule wasiwe watoto wa Uturuki, India, Pakistani, Indonesia, Dubai, Iran, Saudi Arabia, Misri, Singapore, Qatar.
Ritz,

..actually hatuna haja ya kwenda mbali kote huko.

..hapahapa Tanzania, kwanini Muislamu wa Machame anazingatia elimu wakati wa Mkuranga hathamini elimu?

CC: Kadogoo, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Pitia bandiko la JokaKuu utakutana na neno Waislam.

Hivi wale watoto wanaokataa shule kule Makete, Ludewa, Magu, Nansio, Mwitongo, Nkasi, Kizi, Nyanguge, Njombe, Katoro, Ngudu, Tarime, wote ni Waislam.
Ritz,

..hayo maeneo uliyoyataja naweza kusema ni predominantly ya Wakristo.

..lakini sidhani kama wanaweza kuzua fitina kwamba wamekwama kielimu kutokana na hujuma za Waziri wa elimu na katibu mkuu wa wizara ambao ni Waislamu.

cc: Kadogoo, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Ritz,

..actually hatuna haja ya kwenda mbali kote huko.

..hapahapa Tanzania, kwanini Muislamu wa Machame anazingatia elimu wakati wa Mkuranga hathamini elimu?

CC: Kadogoo, Nguruvi3

Na mie nakuuliza swali kama hilo kwa nini wanafunzi wa Kikristo Nyamurutunguru, Ngudu, Bariadi, Buchosa, Uzinza, Makete, Nyasho, Ngara, nawo hawasamini elimu tofauti Wakirsto wa Machame?
 
Last edited by a moderator:
Barubaru, mbona unapata taabu kuuelewa huu mnakasha unahusu nini, kinchogomba si Mohamed kuandika historia ya wazee wake, hapana, ni namna anavyowahadaa wananchi kwa madai ya kipuuzi yasiyo na ukweli wowote...hata hivyo naomba kwa niaba ya hao wengine usiowataja nikutake uzingatie mambo matatu muhimu;

  1. Hicho kitabu, tofauti na ngano za Mohamed Said, kitachambua michango ya Watanganyika wote bila kutanguliza makabila yao, dini zao, eneo wala rangi zao...hakutakuwepo na cha sisi na wao.
  2. Hicho kitabu kitaongelea michango ya Watanganyika zaidi ya milioni nane kutoka kila kona ya nchi na hakitajikita katika watu wa Dar es Salaam tu ambao walikuwa hawafiki laki moja na nusu.
  3. Hicho kitabu kikiandikwa kwa staili hii hii alotumia Mohamed Said, nakuhakikishia kitapata upinzani kama huu huu unaoushudia hapa hata kama mwandishi atadai na yeye kafanya utafiti wa miaka 50.
gombesugu, maadamu umeamua na wewe kuingia kwenye mkumbo huo huo wa kuwatazama waliokuwa Watanganyika katika misingi ya wao na sisi katika harakati za uhuru, naomba nikukumbushe jambo moja muhimu...huko unakoita mikoani ndiko walipoishi zaidi ya asilimia 98% ya wananchi milioni nane. Kwa idadi ya wakazi wa Dar es Salaam wakati huo, unaweza kuwataja hadi vichanga, hutaweza kufikia idadi ya wakazi wa kadistrict kamoja tu ka Mwanza. Heri mfungue thread mahsusi mtajiane majina yote yale tangia Arab Street, Kichwele, Ring Street, Main Avenue hadi mtaa wa Unter Den Akazien.

Kwetu wengine tutabaki tukitanguliza Utaifa (Utanganyika) kwanza na kuwatukuza wazee wetu bila kuangalia tofauti zao kama za wenye mji na watu wa kuja au watu wa pwani na watu wa bara.

Baada ya hayo machache naomba turudi tupate maelezo kutoka kwa mwalimu mtoa darsa Mohamed Said, je ilikuwaje katika unaoitwa MfumoKristo shirika la World Muslim League (WML) likaweza kuruhusiwa kufungua ofisi nchini hadi expatriate wake Mburundi akapewa Uraia na pasi ya Tanzania!

Bwana Mag3,

Salaam.
Naomba kuchukua tena fursa hii kuwaeleza na kuwathibitishia Wanajamvi wenzangu, kuwa pamoja na dhana nyingi nilizopewa tangia siku ya mwanzo kuingia humu, lakini hasha! Mimi si mdini/"mfia dini",wala sipendi kabisa kujali watu kwa urangi wao,u-Taifa wao,mtabaka au mila na dasturi. Insha Allah Bwana Mag3 siku moja nitapembuka vizuri na utajisikia vibayakwa kunizulia haya yoote. Ama kwa hakika I feel marginalised and terribly alienated! Maana kila kukicha hamwishi kunipa shutuma za Udini,je ushahidi uwapi au dhana tu!? Au labda lugha nnayotumia inaleta khitilafu humu jamvini!? Kwa hilo italazim nisamehewe na nipewe japo muda kiduchu wa kujirekebisha. Mimi ndo kwanza mgeni humu na najifunza hizi dialects na terminologies za hapa JF.

I always believed in human fabric and above all I am a dreamer of Global villlage! Kwahiyo ndugu yangu ukiniona nakosea tafadhali saana naomba unirekebishe na nakuhakikishia takuomba radhi. I'm so proud to let you know that in My family tree we have people from almost all over the world with different backgrounds,cultures,customs and set of values. Infact, I find your comments quite laughable. Kwahiyo tafadhali saana usifikiri mimi ni mtu wa matabaka ya"wao na sisi". La hasha na shaka ondosha asilan! Tuacheni jokes za kitoto tuendelee na mnakasha,maana napenda pale unapouliza maswali yako ya nguvu.

Labda kama ile post yangu ya jana na majina ya wale Wazee wetu ndo imekukera basi pia nisamehe na sitarudia dasturi ile. Lakini mbona Bwana Nguruvi3 alipoweka hukumwambia kitu!? Mie nilikua namfatisha yeye,na kama uliisoma kwa makini utaona ujumbe mzito ndani yake,na pia nilijitahidi kutaja maeneo mengi mno ya Tanganyika na dini zoote kubwa watu walikuwemo mle!? Probably,you are just too sensitive on some issues and take things out of context quite easily!? If that's the case, then you may need to think again if you are at the right place/forum.

Nathamini saana michango na maarifa yenu makubwa humu. Na pia nafahamu kuwa mimi ni mgeni natakiwa niwe na staha kwa wenyeji na wakubwa zangu mlonitangulia hapa jamvini.

Ahsanta. Naomba tufurahi na tupendane soote kwa pamoja! Mimi binafsi tangu kujiunga humu,yaani nacheka mpaka jamaa hapa ofisini wanashangaa yamenisibu yapi. Ama kweli JF kuna vituko,najuta nilikua wapi siku zoote nikakosa raha na buraha za humu!?ahahaha!!!

CC:Ritz,Ami,Boko Haram,Kadogoo,Sheikh Mohammed Said,JokaKuu,Jasusi,Nguruvi3,The Big Show,Mfumo,Wimbi la Mbele
 
Ritz,

..hayo maeneo uliyoyataja naweza kusema ni predominantly ya Wakristo.

..lakini sidhani kama wanaweza kuzua fitina kwamba wamekwama kielimu kutokana na hujuma za Waziri wa elimu na katibu mkuu wa wizara ambao ni Waislamu.

cc: Kadogoo, Nguruvi3

Kwa hiyo unataka kuniambia hayo maeneo niliyotaja ni predominant ya Wakirsto serikali hawahusiki?
 
Last edited by a moderator:
Zama vizuri katika historia ya Tanganyika kuanzia Mjerumani kisha rudi tujadiliane upya. Hunajua chochote kuhusu mkutano wa Berlin kuweka mipaka ya nchi na kuzigawa.

Ritz, Mkutano wa Berlin uliitishwa na Wajerumani ili kukubaliana namna ya kugawana Makoloni kwa amani bila Wakoloni kupigana wao kwa wao. Matokeo ndio Tanganyika, Rwanda na Burundi wakapewa Wajerumani.
Vita ya WW1 Mjerumani aliposhindwa, Tanganyika ikakabidhiwa kwa Waingereza, Rwanda na Burundi zikamegwa kutoka Deutshe Ost Africa (Tanganyika) wakapewa Wabelgiji. Waingereza waliombwa na UNO kuitawala Tanganyika na kuiandaa kwa Uhuru, ndio maana uhuru wa Tanganyika ulidaiwa UNO!
Ritz, wewe unakubali darsa la mtu mmoja tu humu ndani-Mzee Said, wengine hatujui kitu!
 
Ritz, Mimi nina imani tofauti kidogo. Hadi sasa nafanya sana kazi wilaya ya Lushoto hapa Tanga. Ni wilaya ambayo kwa mujibu wa Thesis ya Pfeiffer (1990) ni asilimia 75% waislamu (kwa sasa nadhani Lushoto ina wakazi sio chini ya 470,000). Lakini mwamko wa elimu Lushoto ni mzuri. Hata tabia ya wazazi kufuatilitia watoto kimasomo sio mbaya. Lushoto familia nyingi hazina utani inapokuja kwenye elimu na hata biashara. Tembelea kariokoo shimoni. Kimaendeleo mabwana hawa wapo mbele. Tanga hii pia zipo wilaya desturi na mwamko ni tofauti kabisa. Sio kwa waislamu au wakiristo. Hapa huenda mchango mkuu ni desturi za jamii husika. Haya nimeyakuta pia Machame, Ugweno, Kamachumu na Babati. Duniani, siifahamu dini inayo-design watu kuwa wavivu, au kuwarudishia maendeleo nyuma. Maendeleo-physical, hayana uhusiano na dini (wajapan, wahindi, wachina largelly sio wakiristo au waislamu). Ni dhana watu wanayounda ili wawatukane au kuwadhulumu baadhi. Hata kwa waislamu, angalia kuwa the most advanced muslim nations ni za Asia (Malaysia, Indonesia na akina Turkey nk)sio za hapa Middle East pamoja na resources walizonazo.

Wickama,

Salaam. Nashukuru kufahamiana humu.
Just few lines to show my love and respect to you. I'm quite pleased to read what you said. I wish most of us in here have that kind of attitude,progressive and quality way of thinking. Bravo!

Have gud day Sir.
 
gombesugu,

Tafsiri ya kuwa mdini kwa hawa ndugu zetu ni hali ya mtu kuwa Muislam na kujiweka wazi.

Umeishajiuliza kwa nini Wakirsto hawaitwi wadini kwenye huu uzi kwa ni wadini ni Ritz, gombesugu, Boko haram, Kadogoo, Mohamed Said, zomba, THE BIG SHOW,

Lakini wale wanaowaita wazee wetu wana akili za madrasa, wapuuzi, wanywa gahawa, wavivu, washinda vibarazani, hawa wanaitwa wazalendo.
 
Last edited by a moderator:
Mfumo Kristo Tanganyika umeanza toka wakati wa mkoloni Nyerere akaja kuundeleza.

Mkoloni wakati anakuja upande mmoja alikuwa mueneza dini ya Kikristo na upande mwingine akiwa na mkataba wa kimataifa wa kupewa eneo hili kulitawala kupitia mkataba wa Berlin.

Bahati mbaya sana tawala zote zimekuwa zikiwapuuza Waislam na madai yao badala ya kuyafanyia kazi.

Tumemsikia Mkapa naye kaja na habari mpya kuwa wakati wa utawala wake alikuwa anatawala kwa haki.

Pamoja na mauaji ya Mwembechai, na Pemba kwake ni haki.

Ongeza na wale waliofukiwa wakiwa hai machimbo ya Geita! na Imamu kupigwa risasi ya moto baada ya kuswalisha sala ya Ijumaa Unguja! huo ndio utawala wa haki na kichekesho kuna chama kimoja cha kisiasa kinatamka hadharani kuwa Utawala wa Mkapa unaafadhali kuliko huu wa JK! hivi kweli wakati wa mkapa wangeweza kufanya haya bungeni? Vurugu Bungeni Februari 4, 2013 - YouTube
 
Ritz, Mkutano wa Berlin uliitishwa na Wajerumani ili kukubaliana namna ya kugawana Makoloni kwa amani bila Wakoloni kupigana wao kwa wao. Matokeo ndio Tanganyika, Rwanda na Burundi wakapewa Wajerumani.
Vita ya WW2 Mjerumani aliposhindwa, Tanganyika ikakabidhiwa kwa Waingereza, Rwanda na Burundi zikamegwa kutoka Deutshe Ost Africa (Tanganyika) wakapewa Wabelgiji. Waingereza waliombwa na UNO kuitawala Tanganyika na kuiandaa kwa Uhuru, ndio maana uhuru wa Tanganyika ulidaiwa UNO!
Ritz, wewe unakubali darsa la mtu mmoja tu humu ndani-Mzee Said, wengine hatujui kitu!

Hapana siyo kweli kuwa nakubali darsa la Mohamed Said peke yake, kama utakumbuka majibu ya Mkapa dhidi ya Waislam alisema matatizo ya Waislam yametokana na Ukoloni ni magumu kutatulika.
 
gombesugu,

Tafsiri ya kuwa mdini kwa hawa ndugu zetu ni hali ya mtu kuwa Muislam na kujiweka wazi.

Umeishajiuliza kwa nini Wakirsto hawaitwi wadini kwenye huu uzi kwa ni wadini ni Ritz, gombesugu, Boko haram, Kadogoo, Mohamed Said, zomba, THE BIG SHOW,

Lakini wale wanaowaita wazee wetu wana akili za madrasa, wapuuzi, wanywa gahawa, wavivu, washinda vibarazani, hawa wanaitwa wazalendo.

Ritz, mdini sio ku-practice dini yako au kuonyesha conviction ya imani mbele ya wengine. Mdini ni pale unapotoa au kunyima haki aina yoyote kwa mwingine kwa kigezo kwamba imani yake ya dini ni tofauti au inafanana na yako.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom