Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mbona tuko pamoja? kama wewe unaona hatuelimishani ktk mijadala sawa tu! ila pointi yako ya mwisho nakubaliana nawe mia kwa mia kuwa tuheshimiane ktk kuamini! wewe heshimu Imani yangu kuwa Yesu Issa mwana wa Maryamu si Mungu wala mtoto wa mungu na mimi niheshimu Imani yako kuwa Yesu ni Mungu na ni Mtoto wake! kuna ubaya hapo?
Kadogoo

Mimi nilikuwa namaanisha mijadala ya kuhusu Dini. Ila mijadala kama hii mabishano yanatakiwa ili kupatikane mawazotaofauti na kuwe na changamoto.

Na ngoja nirekebishe kauli yangu,
''Inapokuja swala la dini ipi ndo the right dini, Mtume yupi ndo katumwa na Mungu, mimi siamini kama kuna cha kuelimishana, ila tunaweza kuheshimiana, kwa kuheshimu na kumvumilia anacho amini mwengine.''

Otherwise My friend Kadogoo, We are Brothers in Race,Nationality, and more over in Humanity.
 
Jasusi,

........ waandike kitapata soko sana Kanisani na kwenye vigango lakini siyo kwa Watanzania.......

Bahati nzuri kitabu chenu kitakuwa kimejaa wasomi watupu hakuna mmoja hata mwenye akili za madrasa, mnywa gahawa, washinda vibarazani, kina mwanameka.

Jasusi, jikusanyeni wote muandike hapo kweli humu jamvini hapatakalika lakini kwa Watanzania ndiyo itakuwa mtihani na kituko kusoma hizo ngano.

Nazism! It very unfortunate to have this perception in this Forum.
 
Hili la WML linaitaji majibu ya kina ili kuweka mambo sawa hapa,naomba lisipuuzwe
Ritz hauna hata majibu ya hili?!
Lingeulizwa la Mpakistani Malik, kurasa zima lingejaa porojo.
Lingeulizwa la Sheikh Amir wa nchi jirani, hata kurasa mbili zingejaa porojo.
Lakini hili la Mburundi Sheikh Rukara au la WML thubutu!
Tafadhali Ritz njoo uokoe jahazi...kuna hatari ya nzi kufia ndani ya kibuyu cha asali!
 
Last edited by a moderator:
Mnakasha bado unaendelea.. Nilipotea kwa kitambo, baada ya kupata conclusion kuwa NGANO za gerezani zilizonasibishwa kama za Tanganyika zimefifishwa.
 
Hili la WML linaitaji majibu ya kina ili kuweka mambo sawa hapa,naomba lisipuuzwe
Ritz hauna hata majibu ya hili?!

Rapherl,

Kama kuna mtu anajua chochote kuhusu Rukara ni vizuri alete humu jamvini tuvifahamu.

Kitu kikubwa kwetu kueleza dhulma walizofanyiwa Waislam, Mkapa alishawahi kusema dhulma zipi wanafanyiwa Waislam leteni ushahidi.

Waislam wakamletea ushahidi pale Diamond Jubilee akasomea risala kutoka umoja wa Waislam wote nchini. Alipopelekewa ushahidi huo badala ya kuchukuwa hatau, akarudi nyuma pasi kuchukuwa hatua zozote na kudai matatizo ya Waislam ni ya Kihistoria na hayatatuliki, jambo ambalo si sawa.

Kuna wengine humu jamvini wanasema Waislam hawajawahi kufanyiwa dhulma yeyote ni hisia tu hawa ndiyo wanajipanga kuandika kitabu chao.

Namalizia na maneno haya "Tunasema uongo haundoi shida bali uongo hukuza shida tu, pia shida itakuwa kubwa kwa sababu kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele athari ya jambo hilo linazidi kutanuka."
 
Mfumo Kristo Tanganyika umeanza toka wakati wa mkoloni Nyerere akaja kuundeleza.

Mkoloni wakati anakuja upande mmoja alikuwa mueneza dini ya Kikristo na upande mwingine akiwa na mkataba wa kimataifa wa kupewa eneo hili kulitawala kupitia mkataba wa Berlin.

Bahati mbaya sana tawala zote zimekuwa zikiwapuuza Waislam na madai yao badala ya kuyafanyia kazi.

Tumemsikia Mkapa naye kaja na habari mpya kuwa wakati wa utawala wake alikuwa anatawala kwa haki.

Pamoja na mauaji ya Mwembechai, na Pemba kwake ni haki.
 
Usidharau usichokijua. Hivi kweli leo Mag3 na Nguruvi waunganishe nguvu zao waandikie kitabu patakalika kweli hapa jamvini?

Kama kweli una yakini kabisa kuwa wanaweza sasaKWANINI WASIWATENDEE HAKI WATANZANIA VIZAZI VYA SASA NA VIJAVYO KUWEZA KUJUA HISTORIA SAHIHI YA NCHI YENU. Mimi nashauri tena kama wanaweza waanze hiyo kazi na kama kuna gharama basi waziweke hapa barazani na mimi naahidi kuwa mchangiaji mkubwa ili kufanukisha kitabu hicho ambacho najua kitakuwa na manufaa kwa wengi kama hichi cha Al Akhiy Mohamed Said
 
Lingeulizwa la Mpakistani Malik, kurasa zima lingejaa porojo.
Lingeulizwa la Sheikh Amir wa nchi jirani, hata kurasa mbili zingejaa porojo.
Lakini hili la Mburundi Sheikh Rukara au la WML thubutu!
Tafadhali Ritz njoo uokoe jahazi...kuna hatari ya nzi kufia ndani ya kibuyu cha asali!

Mag3,

Jenga heshima Sheikh Hassan bin Amir alikuwa kadhi wa kwanza wa Tanganyika na mwalimu kafundisha Masheikh wengi na ni mtu ambaye anayehishimika katika jamii ya Kiislam ya Tanzania, ingawa wewe unaweza kumkejeli unavyotaka.
 
Last edited by a moderator:
Mfumo Kristo Tanganyika umeanza toka wakati wa mkoloni Nyerere akaja kuundeleza.

Mkoloni wakati anakuja upande mmoja alikuwa mueneza dini ya Kikristo na upande mwingine akiwa na mkataba wa kimataifa wa kupewa eneo hili kulitawala kupitia mkataba wa Berlin....
Point of correction Ritz, ilikuwa Mkataba wa UNO kuiweka Tanganyika chini ya udhamini wake, Mwingireza alipewa na umoja wa Mataifa wakati huo baada ya Ujerumani kushindwa kwenye WW1 (1924-1918). Na ndio maana Uhuru wa Tanganyika ulidaiwa UNO, Mwingereza alitawala kama Mdhamini kuiandaa Tanganyika kwa uhuru.
 
Rapherl,

Kama kuna mtu anajua chochote kuhusu Rukara ni vizuri alete humu jamvini tuvifahamu.

Kitu kikubwa kwetu kueleza dhulma walizofanyiwa Waislam, Mkapa alishawahi kusema dhulma zipi wanafanyiwa Waislam leteni ushahidi.

Waislam wakamletea ushahidi pale Diamond Jubilee akasomea risala kutoka umoja wa Waislam wote nchini. Alipopelekewa ushahidi huo badala ya kuchukuwa hatau, akarudi nyuma pasi kuchukuwa hatua zozote na kudai matatizo ya Waislam ni ya Kihistoria na hayatatuliki, jambo ambalo si sawa.

Kuna wengine humu jamvini wanasema Waislam hawajawahi kufanyiwa dhulma yeyote ni hisia tu hawa ndiyo wanajipanga kuandika kitabu chao.

Namalizia na maneno haya "Tunasema uongo haundoi shida bali uongo hukuza shida tu, pia shida itakuwa kubwa kwa sababu kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele athari ya jambo hilo linazidi kutanuka."

Mkuu Ritz,
Sasa kama masuala ya Waislamu wenyewe wewe huyajui vipi sisi tutayajuaje?!

Haya matatizo mnayosema mnayo mbona mlikuwa mnamlalamikia Nyerere alivyoingia Mwinyi ni ya Serikali...alivyoingia Mkapa ni ya Mkapa...sasa yupo Kikwete vipi yamegeuka tena ni ya Serikali?! na kuna ndugu yetu mmoja anasema Kikwete anaandikiwa Hotuba na Watu wa Mfumo kukandamiza Waislam na Uislam vipi kipindi yupo Makamba Jr pale Magogoni alikuwa mtu wa Mfumo?
 
Point of correction Ritz, ilikuwa Mkataba wa UNO kuiweka Tanganyika chini ya udhamini wake, Mwingireza alipewa na umoja wa Mataifa wakati huo baada ya Ujerumani kushindwa kwenye WW2. Na ndio maana Uhuru wa Tanganyika ulidaiwa UNO, Mwingereza alitawala kama Mdhamini kuiandaa Tanganyika kwa uhuru.

Zama vizuri katika historia ya Tanganyika kuanzia Mjerumani kisha rudi tujadiliane upya. Hunajua chochote kuhusu mkutano wa Berlin kuweka mipaka ya nchi na kuzigawa.
 
Mkuu Ritz,
Sasa kama masuala ya Waislamu wenyewe wewe huyajui vipi sisi tutayajuaje?!

Haya matatizo mnayosema mnayo mbona mlikuwa mnamlalamikia Nyerere alivyoingia Mwinyi ni ya Serikali...alivyoingia Mkapa ni ya Mkapa...sasa yupo Kikwete vipi yamegeuka tena ni ya Serikali?! na kuna ndugu yetu mmoja anasema Kikwete anaandikiwa Hotuba na Watu wa Mfumo kukandamiza Waislam na Uislam vipi kipindi yupo Makamba Jr pale Magogoni alikuwa mtu wa Mfumo?

Maswala ya Waislam yapi ambayo siyafahamu?

Unamjua vizuri Makamba Jr?
 
394640_10151045596984605_542804218_n.jpg
 
Kama kweli una yakini kabisa kuwa wanaweza sasaKWANINI WASIWATENDEE HAKI WATANZANIA VIZAZI VYA SASA NA VIJAVYO KUWEZA KUJUA HISTORIA SAHIHI YA NCHI YENU. Mimi nashauri tena kama wanaweza waanze hiyo kazi na kama kuna gharama basi waziweke hapa barazani na mimi naahidi kuwa mchangiaji mkubwa ili kufanukisha kitabu hicho ambacho najua kitakuwa na manufaa kwa wengi kama hichi cha Al Akhiy Mohamed Said

Mwenyezi Mungu akujaze kila kheri na nia yako nzuri. This is one of the best statements ever made in this thread. I will also avail own resources for this noble goal.
 
GimbeSugu

Nijambo jema lakini mafaa zaidi ni kujua nini walifanya katika harakati za uhuru na mchango wao.

Muheshimiwa Yericko Nyerere,

Nashukuru kwa ujumbe lonitumia,ama kwa hakika nafurahika kila kinitupia maswali japo umenibadili jina kiduchu!!ahaha!!
Nafikiri hiyo sasa ndio shughuli ya wanaHistoria mahiri kama Sheikh Mohammed Said, Professor Mushi na wengineo kufuatilia na kufanza kazi zao kwa utuo. La muhimu Serikali iwajali na kuwapa misaada ya hali na mali kufanikisha shughuli zao bila ya kuzongwa na ma-Politicians au watu wa Kanisa na Misikiti. Nasi tulobaki tujaribu kuwakubali na kuwapa moral support kwa manufaa ya taifa letu.

Japo kwa uchechefu wangu, najua kwa yakini wengi kati ya hao Wazee wetu tunaowakumbuka na hata wale tulowasahau;walikua na taaluma mbalimbali,walifanza mengi mno pita kiasi na walijitoa muhanga mkubwa kwa nchi yao bila ya kujali matabaki au tafauti zao.

Ukiondoa wale "Mandava",wengi ya hao Wazee wetu walikua ni; Merchants,Thinkers,Seafarers,Civil Servants,Artists,Pianists,Poets,others from Noble/Aristocracy families,Land owners,Traders,Activists,Scholars,Etymologists,Musicians,Teachers,Akidas,Liwalis,Town Criers Lexicologists and many other. Ndo maana mimi siku zoote niko so proud na hao Wazee wetu na sisikilizi kabisa ile "Historia za wazungu/wakoloni",ati walipokuja walikuta Wazee wetu woote wanaishi juu ya miti na wala hawajui kusoma wala kuandika!? Inanikumbusha yalowakuta ma-Irish kutoka kwa Oliver Cromwell!!

Napata wasiwasi pale ninapoona jitihada za Sheikh Mohammed,tena kwa kuanza kuandika kuwataja waTanganyika kiduchu tu na inaleta tafrani je huko twendako tutafika kweli!?

Ahsanta.

CC: Ami,Barubaru,Mwanakijiji,Sheikh Mohammed Said,Ritz,JokaKuu,Jasusi,Mfumo,Kadogoo,Boko Haram,The Big Show,Wimbi la Mbele,Nguruvi3,Mag3
 
Back
Top Bottom