Hii ya TANU kaunda Abdu inafanana na ile ya CHADEMA kaunda Mtei! Angalau wewe sio mtu wa kufikiri kwa ufupi namna hiyo. Usimpende Abdu kwa kumdunisha Mwalimu. Unaujua vizuri uwezo mkubwa wa Mwalimu katika SIASA na UONGOZI. Mwalimu hakuwa mtu kusubiri Abdu aunde TANU. Kwamba Abdu hakuutaka URAIS wa chama alichokiunda yeye, halafu akawa mgombea, hilo tuwaachie wenye akili walitafakari.
Wild Card,
Inawezekana ni ujuvi.
Inawezekana pia ni kutojua historia ya Tanganyika.
Halikadhalika inawezekana na hasad na mengine mengi
kwako wewe kufananisha siasa za kikoloni na siasa hizi
za wakati huu tulionao.
Hakika mimi nakubaliana na wewe Nyerere si mtu wa
kusubiri Abdu Sykes aunde TANU Nyerere unavyoona
wewe ni mtu wa kuunda chama chake.
Tatizo liko hapa inawezekana kweli Nyerere alikuwa na
fikra ya kuunda TANU toka Butiama.
Na ikiwa utakuja ushahidi wa hilo labda alipata fikra hizi
kwa baba yake Chief Burito au kwa namna yoyote ile nani
atapinga?
Abdu mimi nasema kaunda TANU kwa sababu historia yake
yote kuanzia kwa baba yake ndiyo hiyo za siasa za mapambano
na ukoloni.
Huo mfano wa yeye na Chief Kidaha ni mmoja wa mifano hiyo.
Ukitaka mingene na iko mingi utarudi nyuma kwa baba yake na
yeye mweyewe katika maisha yake hadi TANU ikaaundwa 1954.
Ikiwa Nyerere aliunda TANU uwanja ndiyo huu uletwe ushahidi.
Isiwe Nyerere kuunda kwake TANU unafungamanishwa na historia
yake na Abdu Sykes na TAA pale New Street.
Lameck Bugohe mmoja wa waasisi wa TANU alipata kuandika makala
katika Raia Mwema akasema yeye alikuwa na fikra ya kuunda TANU
Mwanza katika miaka ya awali ya 1954.
Mimi niliandika makala ya kumuunga mkono.
Katika makala ile alilaumu wana historia kujikita kwa Nyerere bila ya
kufanya utafiti kwa wanasiasa wengine wa wakati ule yeye akiwa
mmojawapo.
Kuasisi TANU si milki ya Abdu Sykes peke yake yawezekana wako wengi
walikuwa na fikra kama zake.
Huu ni wakati muafaka kwa sisi kusikia habari za wazalendo hawa pamoja
na historia ya Nyerere katika juhudi zake za kuasisi TANU ama iwe Butiama,
Makerere au Tabora.