Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Shukran Wild Card: Wajua Mimi ni maskini kwa vile wewe ni tajiri?; Wild Card, hivi kama sio mimi kukupokea na kukupa malazi nani angekujua hapa Arusha???????; Aisha nilikuoa ukiwa katika hali duni sana, sasa nimekulisha chakula changu na kukuvisha hadi umependeza kisha unaanza kunijibisha? wajua fadhila wewe?; Kwenye ibada; Wenzangu nawaaseni kuishi na watu kwa subira na haki na matendo mema. Kuweni wakarimu, hakika Mwenyezi hukipangia kila kiumbe riziki yake!!!!!! na saidieni yatima, wasafiri, wanyonge na watu kama hao. Fanyeni hayo yote kwa kumtanguliza Mungu na malipo yapo kwa huyo aliyekwezesha wewe. TUKO PAMOJA WILD CARD? BASI, JIONI NJEMA
 
Kama Abdul ndiye aliteunda TANU kwanini asiwe na kadi namba moja? Kwa heshima yake?

Swali hili linaulizwa na mtu mwenye weledi kweli?
Lina mantiki?kwahiyo kama Abdul alikua muasisi basi ni sharti angekuwa na kadi namba moja sio?
Lakini ulishajibiwa swali hilo,sema unajitoa ufaham kwa makusudi kabisa..
 
Hivi wewe mpumbavu kwanini usijitoe kwenye huu mnakasha na ukabaki msomaji wa hoja za wenzio? Hivi huu upumbavu unao uandika hapa unadhani nani anaufurahia zaidi ya huyo mzee wako mpuuzi na mchochezi MOHAMED!


Tumeusiwa katika uislam kutowajibu watu wapumbavu,kwan mpumbavu ukijibishana nae huwa hachagui ya kuongea,mwsho wa siku analeta athari kubwa hata kwa wasiohusika,
kujibu hoja yako kumesababisha mimi kumtukanisha mwalimu wangu Moh Said,
kosa hili sitalirudia tena,japo ww ndio umekuwa kinara wa kunifata fata kila napozungmza na wenzangu humu jamvini..
Nakurudisha kwenye daraja lako lile lile la kupuuzwa..
 

Ritz shukran. Usiipunje Dar Bwana. Dar ndio kila kitu Ritz. Taa za kuongoza magari za kwanza tanganyika (dar), Magorofa (dar), vilabu maarufu vya kandanda (dar), misikiti/makanisa makubwa makubwa (dar). Wanazuoni wanaouujua uislamu vizuri kuliko wengine WOTE tanganyika (dar), waumini wacha Mungu kupita wengine (dar), madereva werevu zaidi tanganyika-dar (yaani kuchomekea-akifika sekenke/lukumburu anaomba aendeshewe), siasa za kueleweka (dar), mapato ya serikali (dar), gesi (dar/kusini?), NECTA (dar), vijana "wanaoshinda" mashindano ya kuhifadhi kurani (dar?), vyuo vikuu (dar), wakina mama wenye maadili safi sana (dar). Usiipunje dar Ritz. Mwisho wa siku ni kuwa haya ni maisha. Tumekutana mji huo kwa mahitaji na mikasa tofauti. Ridhika na hiyo lakini usijejidanganya hata siku moja kuwa familia ya kawaida hapo dar ina maisha bora zaidi ya ile ya Arusha/Bukoba/Nyamongo/Namanga au Kahama mjini.
 



Moh Said tunakusoma sana,
Hatubanduki hapa 24/7,labda ubanduke wewe,
Tafadhwali Mwaga Darsa Huru ikhuan..
 

Mie sipo huko unapoelekea mimi nimejikita kwenye maneo ya Nyerere hapo juu.

Wapi nimekuambia Dar watu wana maisha mazuri kuzidi sehemu zingine?

Mnakasha huu unaelezea habari za AA, TAA, TANU, huwezi kuiweka Dar pembeni wakati ndiyo makao makuu ya harakati kama nimekukwanza kuitaja Dar niwe radhwi kaka.

Tulizana kunywa maji fundo tatu munkari ushuke kisha rudi kwenye mnakasha.

Karibu gahawa nipo barazani huku nacheza dhumna.
 
Wewe sio muislam ila ni muganga njaa tu unayeishi kwa kujinasibisha na uislam! ungekuwa muislam usingekaa kutwa nzima hapa ukiwatukana watu wanaotofautiana fikra na Mohamed Saidi! Umemshambulia kwa mitusi Mzee Mwanakijiji kwa sababu ya kuandika Riwaya ambayo hata hujaisoma! ukamshambulia Yeriko Nyerere mpaka kumuita hana adabu ati kwanini ameandika kitabu! na hilo zee lako likaja na majivuno yasiyo na maana ati Yericko hawezi kuandika kitabu! ebo nyie mijitu mkoje? mnawezaje kujiita waislam safi wakati tabia zenu ni mbovu kuliko hata hao mnaowaita makafiri? Kwa muda mrefu sana nilikuwa nje ya mji kikazi nikawa natumia simu kuingia hapa jamvini, wewe na wapumbavu wenzako mkaandika humu mkiniulizia niko wapi na mkokoteni wangu! cha ajabu hilo umelisahau unakuja na ujinga wako uliokomaa ati nakufuata futa! Nitakufuatia nini wewe ambaye huna hata chembe ya maarifa zaidi ya kushangilia ujinga wa huyo Mohamed wenu? Kaa kando mjinga wewe huna unalolijua zaidi ya ushabiki wa kidini ambayo unaitumia kujinasibu nayo wakati huna hata chembe ya maadili yake!
 
Wanajamvi tunaomba majibu yenu kupitia huu mnakasha.

Chadema wanasema Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuna udini mkubwa.

Ni kweli tunaomba michango yenu.
 
Nguruvi,
Waamerika wana kitu wanaita "shit list."Humo wanatiwa watu ambao si waungwana
Mohamed, kama nipo katika ''shit list'' yako wala hilo halina tabu. Lisikupe wasi wasi, wewe endelea kuoga na vijana wako mtoni.

Sioni orodha yako ninayo fit.
Ile ya kukaa katika baraza au mkeka na kukubali kuwa Tanzania ni mwanachama wa commonwealth kwasababu ya mfumokristo! please

Tuendeelee na manakasha, ila sirudi nyuma wakati napiga katika mfupa.
Sihitaji kuwa muungwana kwa kukubali kuwa Warioba alianza siasa kutoka machungani,wala uungwana eti nisiseme Mohamed na Rukara ni maswahiba kama alivyo Mohamed na Ilunga. Unajua hilo

Hii ndio list yako unayofikiri kuniweka? Ilunga,Ponda, Rukara, Farid. Please usinitukane Mohamed.
 
Narudia tena kuuliza Chadema wanasema Chuo Kikuu cha Dodoma kina udini wa kutisha ni kweli kama kuna yeyote ambaye anafahamu jambo hili ni vizuri atujuze.

Kuna wajuvi humu wanakataa Tanzania hakuna mfumo kirsto vipi kuhusu UDOM kiongozi wa Chadema Mkirsto anasema kuna udini.

Hili mnakasha wetu wa uchochezi uende mbele zaidi tupeni michango yenu.
 
Moh Said tunakusoma sana,
Hatubanduki hapa 24/7,labda ubanduke wewe,
Tafadhwali Mwaga Darsa Huru ikhuan..

The Big Show,
Ahsante ndugu yangu.

Hii ni hidaya kutoka kwake Allah.
Tuna wajibu wa kuisomeesha bure.

Katika Uislam elimu haiuzwi.

Ndipo nilipomwambia ''publisher'' siwezi kuacha
kuandika JF.

Mchapaji anafikiria faida ya kitabu atakachotoa kapata
wasiwasi maana namwaga mchele wote hadharani.

Mimi siandiki kupata fedha naandika jina la Allah liwe juu.
 

Ami, hivi michango na hoja za namna hii nazo utazingizia kuwa sababu ni Nyerere, Ukatoliki na Mfumo Kristo kweli?

Nasikitika sana kusema kuwa Sheikh Said amekosa watu wenye uwezo wa kumuunga mkono kwa hoja na badala yake wanarusha vijembe tu na mipasho!

Pamoja na vurugu zote na mara nyingine kwenda nje ya hoja, ni Ritz pekee na Gombesugu ndio wanajitahidi kuja na kujenga hoja za kumuunga mkono Sheikh Said. Wewe Ami na The Big Show naona ni wanogeshaji tu wa kijiwe.
 
Mzee mo,

Kuna msemo usemao kizuri.....!
Kibaya chajitembeza.
Wewe na umaalufu wako na uislam wako kwanini usijitolee umuuze lipumba achukue ichi hii?
Ni miaka mingapi anahangaika?
Mzee wangu kukiuza kitu lazima kiwe kinauzika.
 


Nguruvi3,
umepanic sana,kuoga na watoto mtoni ndio kipimo cha kauli zako zilizochuja kimantiki..
Mission yako imefeli,ushahid dhidi ya uchochez wa Moh Said haujaonekana hadi saiz.mmebaki kubwabwaja tuh..
Victory Won..!
 
Swali hili linaulizwa na mtu mwenye weledi kweli?
Lina mantiki?kwahiyo kama Abdul alikua muasisi basi ni sharti angekuwa na kadi namba moja sio?
Lakini ulishajibiwa swali hilo,sema unajitoa ufaham kwa makusudi kabisa..

The Big Show,
Ungemwambia tu kuwa kadi ya kwanza alipewa Nyerere kwa ajili ya heshima
ya yeye kuwa ndiye rais wa TANU.

Kadi zilizofuatia za akina Dome Budohi, Bi Titi, Idd Faiz Mafongo na ndugu yake
Idd Tosiri, Boi Selemani, Dossa Aziz, Marsha Bilal, Schneider Abdillah Plantan na
ndugu yake Ramadhani Mashado Plantan, Mshume Kiyate, Shariff Attas, Tatu biti
Mzee ndiyo hao tena waliokuwapo mstari wa mbele nk. nk.
 
Mzee mo,

Kuna msemo usemao kizuri.....!
Kibaya chajitembeza.
Wewe na umaalufu wako na uislam wako kwanini usijitolee umuuze lipumba achukue ichi hii?
Ni miaka mingapi anahangaika?
Mzee wangu kukiuza kitu lazima kiwe kinauzika.

Mgashi,
Hii naona ufungue uzi mpya hapa itakuwa hatufaidi.

Wasemaje mkuu?
Hivi mie maarufu?
 
Nikweli kabisa unamtetea Alah kwa kuchoma makanisa inelekea una nguvu kuliko yeye
 

Nani wa kukuulizia wewe kwa lipi lamaana uliloliweka hapa brother uwe na adabu wala hakuna mtu alikuwa anataka kujua ulikuwa wapi hayo mambo ya kikazi ni kwa faida yako na familia yako ,ohh mzee MS mpumbavu,mchochezi,mjinga baba humuwezi mzee MS umegonga ukuta:frusty: hakuna mtu anayefurahia unayoyafanya kwenye huu mnakasha :nono::nono: nakueleza kwa mara nyingine unapopiga kichwa ukuta sikitikia kichwa chako usisikitikie ukuta!!!!!!!!!!
 

Mohamed Said,

Naona unaweka mambo Mubashar hadhwarani haya yote tungeyajua wapi hiyo orodha ya wanachama wenye kadi haipo kwenye kitabu cha Kivukoni kuna wanachama 19 tu.

Tupe darsa nani alipewa jukumu la kuchapa kadi za TANU na nani alikuwa anauza hizo kadi.
 
Last edited by a moderator:


Wanabarza,
Yapo makosa kidogo katika simulizi za TANU zinazochapwa hivi sasa.
Mathalan Mzee Bogohe anasema kuwa Mhasibu Mkuu wa kwanza wa TANU alikuwa Julius Mwasanyangi.

Ukweli ni kuwa mweka hazina wa kwanza wa TANU alikuwa Iddi Faizi Mafongo aliyekuwa mhasibu vilevile wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Iddi FaiziMafongo ndiye aliyekuwa na jukumu la kukusanya fedha za safari ya Nyerere kwenda Umoja wa Mataifa mwezi Machi 1955.

Katika nafasi yake ya kuwa mweka hazina wa vyama hivyo viwili Iddi Faizi alitoa fedha katika hazina ya za AlJamiatul Islamiyya na kuzitia katika mfuko wa TANU ili kufanikisha safari ile.

Iddi Faizi ana historia nzuri sana na ni jukumu lao sasa wanahistoria kuzitafuta habari zake. Iddi Faizi, Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere ndiowaliotembea Jimbo la Mashariki mwaka 1958 kuwahamasisha wana -TANU wasisusekuingia katika Uchaguzi wa Kura Tatu.

Iwe itakavyokuwa nyaraka za historia zinaonyesha kuwa alotoa jina la TANU alikuwa marehemu Abdulwahid Sykes na jina hilo alilitoa Kalieni Camp India mkesha wa Christmas mwaka 1945 akiwa askari wa 6 Batallion, Burma Infantry katika King's African Rifles (KAR) wakati wa Vita Kuu ya Pili.

Kalieni Camp ndipo askari waKAR walipokuwa wamekusanywa wakisubiri kurudishwa makwao baada ya kumalizikavita. Ukienda katika shajara yake ya mwaka huo taarifa hizi utazikuta.

Juu haya hilo haliondoi ukweli kuwa huenda na Mzee Bogohe na yeye vilevile alikuwa na wazo la kuanzisha chama cha siasa hata kama si kile cha TANU.

Ala kuli hali muhimu ni kwa wanahistoria kuwatafuta wazee hawa na kupokea hazina ambayo si muda mrefu itatoweka.

Wangapi leo wanajua kuwa ni Hamza Mwapachu na Abdulwahid Sykes ndiyo waliomsukuma Nyerere katika ulingo wa siasa?

Au wangapi wanajua historia ya madaktari watano – Dr. Vedasto Kyaruzi, Joseph Mutahangarwa, Dr Wlibard Mwanjisi, Dr Michael Lugazia na Dr Luciano Tsere na mchango wao katika kusukuma mbele harakati za TAA kati ya 1948 – 1950?

Kwa kumaliza napenda kumuuliza msomaji wangu kuwa je, haishangazi kuwa historia ya kutukuka kama hii ya wazalendo na mashujaa wetu leo imetupwa na haipewi thamani?

Kama inashangaza je, haiwi vyema tukajiuliza kwa nini imekuwa hivi?

Ni nini viongozi wetu wanachokiogopa katika kuwaenzi mashujaa wa uhuru wa Tanganyika?
Je ndiyo tuchukulie kuwa Tanzania ni nchi isiyokuwa na mashujaa wake?

Wasomaji hamkubaliani nami kuwa kuna haja kubwa sana ya kuandika upya historia ya uhuru wa Tanganyika na kuwaenzi wale wote waliotoa mchango katika vita vya uhuru?

Kwa kumaliza makala haya namshukuru Mzee Lameck Bogohe kwa kufunua kinywa na kutueleza yale anayoyajua katika kuanzishwa kwa TANU na kuonyesha kidole kwa yale ambayo ameyaona yanapotosha historia hiyo.

Nitafurahi sana Insha Allah kama watajitokeza wengine na kuandika wanayoyajua kuhusu mashujaa wetu wa uhuru ambazo habari zao hazijulikani na wengi. Je hapana hajaya kuiuliza CCM hivi hadi lini wataiacha historia yao inapotoshwa na kupotea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…