nafikiri kama utatumia busara kidogo na kutazama ni lini namba zilianza kutumika katika mitihani ya Tanzania na kuachana na kuandika majina na kutazama wakti huo nani alikuwa waziri wa Ilmu utaligundua hilo. Kwani Hata wizara ya ilmu ya Tanzania watakusaidia hilo wala haliitaji mjadala. Ila kwa mimi nakwambia ilikuwa kipindi Prof malima akiwa waziri wa Ilmu. Fanya uchunguzi utaligundua hilo.
Suala la Warioba naye yupo hai unaweza ukamuuliza tu kwani miongoni mwa aliosoma nao darasa moja Chuo kikuu (marhum Brigadia mang'enya ) mimi niliwahi kumuuliza kuhusu huyo hakuwa na jipya zaidi ya ukabila tu ulimbeba kama ilivyokuwa kwa akina Nyirabu na wengine kutoka mkoa huo enzi za JKN.
Ritz, Mohamed Said, Kadogoo, gombesugu, Barubaru, THE BIG SHOW,
Niambieni kama mmewahi kusikia Rais/Mwenyekiti wa TANU tangu inaanza hadi kufutika kwake mbali na Mwalimu.
Ritz, Mohamed Said, Kadogoo, gombesugu, Barubaru, THE BIG SHOW,
Niambieni kama mmewahi kusikia Rais/Mwenyekiti wa TANU tangu inaanza hadi kufutika kwake mbali na Mwalimu.
Ritz
Unanchekesha (Courtesy of Faizafoxy)!
Yaani hujawahi kusikia kabisa? Wewe upo tu na Chadema, Nyerere na Mfumo kristo basi...
Soma hizi links hapa:
Iraqi Kurdish cleric says female circumcision recommended by Islam
Indonesia's Top Muslim Clerics Back Female Circumcision, Call It A "Human Right"... | Weasel Zippers
FEMALE GENITAL MUTILATION FEMALE (CIRCUMCISION) IN AFRICA, MIDDLE EAST AND FAR EAST
EGYPT: Hosni Mubarak banned Female Genital Mutilation, but now the Muslim Brotherhood is trying to make it mandatory | BARE NAKED ISLAM
https://groups.google.com/forum/#!topic/uk.politics.misc/mO4qCRu57gU
INDONESIA - ISLAM Indonesian Ulema in favour of female circumcision: a "human right" - Asia News
Female genital mutilation "is part of the Sunna of the Prophet"
Female Circumcision in Kurdistan | Arab Reporters for Investigative Journalism (ARIJ)
Mengine unaweza ukatafuta mwenyewe. Just have an open mind. Don't enter into a state of denial. Seek Ye the truth and the truth shall set ye free!
Nitakuwa nimejijibu nikikujibu hili. Nijibu tu ulivyolielewa swali langu.WildCard,
Kabla mimi sijakujibu labda nikuulize kwanza unauliza au unataka kujua au unapinga hakuna mtu yeyote ambaye alikuwa na vyeo ivyo TANU tofauti na Nyerere.
Kilicho wafanya wamarekani wavamie Iraq ni hicho cha mafuta na wewe mwenyewe umejijibu. hawaku wavamia kwasababu ni waislamu, au wanataka kuupinga uislamu, ingekuwa hivyo wangevamia indonesia basi au Bangladesh.marekani waliivamia iraqi kwa kudai saddam alikuwa na silaha za maangamizi! matokeo yake wamepeleka makampuni yao ya mafuta ili wanufaike na mafuta ya iraqi! baada ya kumnyonga saddam wamegawa silaha kwa makundi ya kidini leo wairaqi wanachinjana wenyewe kwa wenyewe!
Libya walianza revort wenyewe ndani ya nchi, Gadaffi was killed by Fellow Libyani, tena kama kuku.baada ya hapo wameivamia libya kwa kusaidia uasi ili wanufaike na mafuta yao na baada ya gaddafi kuuwawa leo libya haina usalama kwa sababu ya uvamizi wa nchi za kikristo!
Wickama,
..kama lijitu lina zali zake na Wamarekani na linatafutwa basi tusikubali kulipa hifadhi.
..zaidi, hawa jamaa wakianza kumtafuta mtu basi uwezekano mkubwa kuna kitu amekifanya, or he is about kukifanya.
Basi, bwana Ritz,Naona bado unazunguka kwenye kichuguu kama nguchiro tupe ushahidi wa hao viongozi na majina yao hizi links sijawaona viongozi wakuu wa dini kutoka Misri wakiruhusu ukeketeji, usichanganye mila za watu na Uislam.
gombesugu,
..hawa wazee wako wa Tanga wao walishiriki harakati za uhuru??
..je, Mohamed Said amewataja katika kitabu chake?
..Mohamed hakupaswa kurekebisha "historia ya Kivukoni" kwa kuandika "historia ya Kariakoo/Gerezani" halafu adai ndiyo historia ya Tanganyika.
Ngongo,
Naona vibaya kuja na maneno ambayo kwa wengine yanachoma.
Kwa ajili hii nitasema kitu kimoja tu.
Kama ni kutaka kusema kuwa Nyerere alisimama kwa miguu yake
mwenyewe alipofika Dar es Salaam na hakuwa muhitaji hii si kweli.
Hayo ya umaarufu kabla ya kutoka UNO Machi 1955 wala sitatia neno.
Ila jiulize kipi kilichofanya Tanzania ya leo impe Abdu na Ally Sykes medali
baada ya miaka 50 ya uhuru?
Kipi kikubwa walichofanya?
Wazee wetu kawataja japo ni kiduchu mno,la sivyo ingemlazim ajaze kurasa. Na mimi sitathubutu kulalama ati kwanini hujamtaja babu yangu fulani?ahaha!! Itakua ni kinyume na maadili nilolelewa nayo na pia nilojifunza masomoni.
Ahsanta.
Barubaru,
Katika ibra za Allah ni mambo kama haya ya Abdu Sykes na Nyerere na urafiki wao.
TANU chama alichokiasisi Abdu kikaja kuwa mbele kumkana muasisi wake.
Leo zaidi ya miaka 60 tuko hapa tunabishana na wakati mwingine kutukanana.
Mundungus Fletcher;
Usiume ume neno na kuwa na kigugumizi juu ya vita vya Wamarekani dhidi ya Uislamu. Hembu jiulize, kwanini hawaivamii Korea ya Kaskazini au Zimbabwe? unafikiri nchi hizi zingekuwa za Kiislamu zingebaki hivi mpaka leo bila ya kuvamiwa?
Unaposema "Wazee wetu" ni lazima uwe muwazi sana. Mohammed Said anapozungumzia 'wazee wangu' anamaanisha wazee wake wa Kiislamu. Hamaanishi Wazee waliochangia katika harakati za Uhuru bila kuangalia dini zao. Na anapozungumzia "wazee wangu" hamaanishi wazee wote wa Dar na mchango wao la hasha; anazungumzia wale wazee wa Kariakoo tena wale Waislamu tu. Nyerere kwenye hotuba yake hapo juu aliposema "wazee wetu" alikuwa more inclusive than Mohammed Said.
Sijui wewe unapozungumzia "Wazee wetu" unafuata mfano wa Nyerere (kwamba wote wazee wetu - wa Kiislamu na Kikristu nawenye imani za jadi) au uko kwenye mstari wa Mohammed Said kuwa wazee "wenu" ni wale wazee wa Kiislamu tu katika jamii uliyokulia?
Naam! lakini siyo hivyo tu; ni kuiandika histohisia hiyo ya Kivukoni akitumia dini kuelezea matukio ambayo hayakuwa ya kidini huku akikebeki dini za wale wasio Waislamu na kudunisha mchango wao. Mashujaa wake katika hili simulizi lake jipya ni Waislamu watupu.
gombesugu,
..asante, asante.
..tukishajuana kwa majina na familia zetu basi hata kuambizana ukweli kwa staili ya JF kutakwisha.
..unajua kule mtaani kuna watu wakitaka kukupa ukweli wako lazima kwanza waenda kilabuni kunywa bia mbili tatu. wanasema kuondoa nishai.
..sasa sisi hapa Jamii Forums hatulazimiki kufanya hivyo, majina ya bandia ndiyo kazi yake. Yanasaidi kuondoa nishai.
..halafu ukishataja familia yako, watatokea vichwa maji in the heat of the debate wakakushambulia na kuhusisha wasiohusika.
..mimi nakusihi uendelee kutumia jina lako la gombesugu.