Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kwani wewe hapa umefanya nini?

Nimetoa hoja za kuthibitisha kwamba ama Nyerere ni MNAFIKI au ni CHIZI. Sasa wewe chagua moja kati ya sifa anayostahili ama MNAFIKI au CHIZI. Kama una hoja ya kumnusuru kutoka kwenye sifa mojawapo kati ya hizo alizojijengea mwenyewe kutokana na hotuba yake kama ilivyowewekwa na muanzisha thread hii, basi mnusuru kwa hoja.
 
Wacha uongo wewe, kama hakukua na vita, akina Milambo ma Mkwawa walipanuaje milki zao za utawala? au unamaanisha nini unaposema hakukuwa na vita hapo zamani?
 
Peleka chuki zako binafsi kwa wapumbavu wenzako!
 
Wickama, mimi nimewekwa kwenye "shit list" ya Mohamed Said na sasa nadokezwa kuwa na gombesugu naye anatayarisha "shit list" yake, nitashangaa kama sitakuwamo humo. gombesugu anadai kuwa Mohamed Said ametufunza mengi hapa tulokua hatuyajui.
Gombesugu said:
Mfano nagundua hata Mag3, nae siku hizi anatumia neno Wazee Wetu!
Masikini gombesugu, hajui kwamba ni Mohamed Said ndiye kapata funzo humu...kwake historia sahihi ilikuwa ni ya "wazee wangu" mpaka pale tulipomuelimisha kuwa "wazee wetu" walishirikiana bila kubaguana kwa misingi yoyote ile.

Kwa aliyefuatilia kwa karibu huu mnakasha na mingine iliyopita ataweza kutambua mara moja hii chuki ya Mohamed Said kwa Mwalimu Nyerere ni matunda ya simulizi alizozipata kutoka kwa wazee wake. Kama ni kweli baadhi ya madai ya Mohamed Said yanatokana na simulizi kutoka kwa hao wazee wake, ni wazi kuwa walisononeka walipotambua mapema kwamba hawakufikia kiwango cha uwezo na sifa alizokuwa nazo Mwalimu.

Nachelea kusema kwamba kutokusikika kabisa kwa Abdulwahid Sykes baada ya kuundwa TANU hadi uhuru unapatikana, yawezekana ni kielelezo cha alivyoumizwa rohoni na mwamko wa Watanganyika nje ya Dar es Salaam, mimi namwita Mohamed Said muongo...sababu zangu ni hizi
Mohamed Said said:
Sihitaji kuthibitisha chochote kwa yeyote awaye yule. Nithibitishe nini ili iwe nini na kutaka nini?
Ukweli ukipiga hodi, uongo hutokomea!
Mohamed Said said:
TAA ilitokana na African Association chama kilichoanzishwa na Kleist Sykes 1929 yeye akiwa katibu na rais akiwa Mzee bin Sudi.
Uongo! Mwaka 1929 Raisi alikuwa Cecil Matola.
Mohamed Said said:
Kuwa baba yangu alikuwa akijua kuwa Abdu alikuwa akaifanya mipango ya kuunda TANU toka 1950 na akimdokeza mambo yalivyokuwa yanakwenda?
Uongo! Hiyo ilikuwa TANU ya kufikirika, TANU iliasisiwa 7/7/1954
Mohamed Said said:
Abdulwahid ndiye aliyempokoea Dar es Salaam ile ya miaka ya 1950 na akamjulisha kwa wenyeji wa mji. Wapenzi wa Nyerere hadi leo ukiwauliza Nyerere alisema nini kuhusu ukweli kuwa si yeye aliyeasisi TANU wamekuwa kimya.
Uongo! Mwalimu alishaikanyaga Dar miaka ya 1940 na kukutana na wenyeji wa mji kama Dossa Aziz.
Mohamed Said said:
Mwalimu Nyerere told Mshume Kiyate that he was going to Kariakoo Market to buy provisions but he did have a single sent in his pocket. Mshume Kiyate dipped his hand into his pocket and gave Mwalimu Nyerere two hundred shillings.
Uongo na upuuzi! Mtu atoke nyumbani kwake kununua kitoweo Kariakoo bila senti mfukoni!!
Mohamed Said said:
Ndiyo maana haikuwa ajabu kuwa Nyerere alipofika Dar es Salaam 1952 ilibidi na yeye aingie nyumba ile akatambulishwe kwa Abdulwahid Sykes Rais wa TAA. Ile nyumba ndiyo yalikuwa makazi ya Rais wa TAA. Ndiyo ilikuwa "Ikulu" yao kwa wakati ule.
Uongo! Kwa nini uchaguzi wa kumtafuta Rais wa TAA ufanyike miezi michache baadaye?
Mohamed Said said:
Inasemekana Mzee Mshume alipata kumpa Nyerere fedha nyingi sana kwa matumizi yake na ya familia yake ili asihangaike na atie nguvu zake zote katika kupigania uhuru.
Uongo na Upuuzi! Lakini kama inasemekana, aliyekusimulia alikudanganya!
Uongo na upuuzi. EAMWS ilikuwa ina wenyewe hadi ilipovamiwa na AMNUT!
Uongo, upuuzi na aibu! Huku ni kujikweza, yaani Mwalimu aliyepambana na viongozi wakuu wa dunia kwa nguvu za hoja afyate kwa Mohamed Said!
Mohamed Sykes said:
Abdulwahid Sykes akiwa jeshini wakati wa Vita Kuu ya Pili ndipo alipokuja na wazo la kuasisi TANU. Hii ilikuwa tarehe 25 December 1945 na fikra hii aliandika katika shajara yake (diary).
Uongo! Kwa nini alipotua Dar baada ya vita hakufanya kweli? Je alikuwa na wadhifa gani AA kabla ya mwaka 1948?
Uongo, thubutu! Mambo ya kujitungia tu.
Loo! Kumbe ndio maana wazee walisononeka! Linalogomba ni uongozi wa nchi!
Mohamed SaidMimi nimendika historia ya [B said:
wazee wangu[/B] watu niliokuwa nikiwajua toka utoto
wangu. Bila shaka huko kwenu nanyi mna wazee hebu andikeni habari zao tuzisome.
Alaa kumbe!

Nikiamua kukaa chini na kutaja uongo woote wa Mohamed Said, hili jukwaa halitatosha!
cc. gombesugu.
 


Nimemsoma Mohammed Said kwa kina sana na kwa werevu wote unaohitajika. Naweza kusema pasi ya shaka kabisa kuwa maandishi yake ni ya kichochezi (provocative) na yenye lengo la kupandikiza jazba miongoni mwa jamii ya Kiislamu kwa kuwaaminisha kuwa wanaonewa na ndugu zao Wakristu. Lengo lake ni kupandikiza uadui dhidi ya Kanisa kwa kulipa nguvu lisilookuwa nalo.

Mimi na wewe hatujui kilichomo moyoni mwake; tunajua kile anachokisema hadharani tu. Maandishi yake yanathibitisha kuwa lengo lake si jema kwa Watanzania. Kumbuka ukimsoma vizuri ndugu kwake na jamaa zake wa Karibu na ambao maslahi yao ana yajali sana ni ya Waislamu. Kwake Waislamu ni walio bora kuliko wengine; dhulma dhidi yao ni mbaya zaidi kuliko kudhulumiwa wengine, mafanikio yao ni muhimu zaidi kuliko mafanikio ya Watanzania wengine. Kwamba anajali "Umma wa Waislamu" kuliko Umma wa Watanzania wote hili liko wazi na ndio kiini cha histohisia yote.

Jamii anayoijali yeye katika Tanzania si ya Watanzania wote bali ni ya Waislamu wa Tanzania. Maandishi yake hayamuoneshi hata kidogo kama mtu anayetaka haki usawa na utu wa Watanzania wote uzingatiwe.
 
Aya ya kwanza Mohamed anaonyesha kuwa uchache (under representation of muslims in the Parliament) unasababu.
Kwa mtu wa Ibadan Nigeria au average Tanzanian hili atalijua kama sehemu ya uonevu.
Mohamed anajaribu kuonyesha kuwa wabunge wanateuliwa na si kupigiwa kura.
Hii ni sehemu ya madai yake kuwa mfumo umetawala kila mahali.
Lakini basi Mohamed anapaswa ajiulize, je bajeti inayopitishwa bila kupingwa kwa majority ya CCM au mswada wa kuanzisha machakato wa katiba uliopita bila kupingwa nao pia ulihusu wingi wa watu wa imani fulani.

Mtu anaweza kudhani Mohamed ana upungufu wa maono, la hasha anajua anachokifanya na kundi alilolenga.
Kwa wale wanaouliza wapi uchochezi wa Mohamed, mambo ni kama haya.

Ni huyu huyu Mohamed alisema walipita wakinong'onezana waichague CCM.
Ni CCM hiyo ndiyo ina majority kuanzia zama hizo anaandika paper.
Sasa inakuwaje tena analalamika under-representation ya jambo lile alilounga mkono?

Aya ya pili anaongelea kuhusu waislam kwa ujumla. Mohamed hajui kuwa katika waislam wapo BAKWATA, Ismailia, Bohora, Shia na Sunni na kwamba hicho anachokiongelea ni kikundi chake na wala si waislam.
Jitihada zake ni kuonyesha ulimwengu uzito wa jambo hili kama tutakavyoona.

Aya ya tatu, inapaswa kumshangaa Mohamed. Yeye anasema Marekani ilishinikiza sheria ya ugaidi ili iweze kuweka nguvu za majeshi yake, nguvu ambayo hawakuwa nayo siku za nyuma.
Na kwamba siku sheria ilipopitishwa FBI kwa kushirikiana na Polisi walikuwa tayari kuwakamata waislam.

Mohamed anasahau kuwa Tanzania ilikuwa na tukio la Ugaidi wa ubalozi kabla ya hapo(twin mbombing).
FBI walikuja na kumkamata Mohamed Ghailan pale kwao.
Sikwamba FBI walianza kuwepo wakati huo, walikuwepo siku zote.

Mohamed hajiulizi mabalozi wa Marekani wanateuliwaje, mashirika yao ya misaaada yanafanya kazi vipi.
Kama angelijua hilo basi asingeandika alichoandika kwasababu FBI hawahitaji ruhusa kuingia popote! wanaingia wakitaka.
Mohamed, hii forum si ya kutupa tupa unachodhani!

Aya ya nne anasema wale waliokamatwa hawakuhusika na mambo ya kigaidi isipokuwa wapinzani wa CCM.
Wapinzani wa chama kile kile alichokipigia upatu kwa kunong'nezana nadhani kuanzia zama hizo.
Kama si hivyo lini uswahiba wa ''waislam akina Mohamed'' na CCM ulianza?

Kaendele kusema, miongoni mwa waliokamatwa ni wale wa mashirika ya misaada kama ya kusaidia kujenga shule, afya na yatima. Kwa mtu anyewakilisha paper alitakiwa aeleze nani na washirika gani.

Aeleze kwasababu akitokea mtu akasema World Muslim League ni mojawapo Mohamed atapingaje wakati yeye haijui?
Kwa kiwango cha paper hii ni tatizo kubwa sana la mzee wetu, kuandika vitu kwa ujumla bila kuwa na specific pengine kukwepa ukweli. Akataja shule ya Al Faruq ili kujaza jazba bila kutaja mashirika.

Aya inayofuata amedai balozi za Marekani zilitoa pesa kwa nchi za EA, na kudai kuwa balozi wa Marekani ilihutubia bunge! Kwa hili yawezekana anajua undani wa kile kilichoongelewa.
Tunachomuuliza Mohamed ni kuwa lini balozi huyo alihutubia bunge?

Tunauliza ili kuondoa dhana ya kuwa suala hilo la waislam wa Mohamed lilikuwa kubwa kiasi hicho.
Ni mazoe ya Mohamed kutaja watu au mahali katika kuongeza nguvu za hoja zake hata kama hakuna ukweli.

Mohamed alishawahi kusema kuwa katika baraza la Idd mwaka 1988 aliyehudhuria alikuwa makamu wa rais mzee Kawawa.
Hilo alilisema makusudi kuonyesha nguvu ya hoja yake. Ni kutokana na mwiba huo uliotuchoma ndio maana tunamuuliza Mohamed, balozi alihutubia lini Bunge! Swali hili ni muhimu kwasababu limebeba paper nzima.

Mohamed, lini balozi alihutubia Bunge?
 

Ni kweli wazee wa wakati ule hawakuwa wadini lakini Nyerere alikuwa mdini aliyekubuhu.

Ushahidi uliowekwa na muanzisha thread hii kwamba Askofu Maranta alikwenda kwa Sheikh Issa ili aone jinsi Kanisa linavyoweza kuingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kudai uhuru hapo mwaka 1948 na kushauriwa ajiunge kwenye vyama vilivyopo ni dhahiri kwamba Sheikh Issa alikuwa analikalibisha Kanisa kwenye African Association ambapo Masheikhs walishajitambulisha na hicho chama tangu kinaanzishwa mwaka 1929. Na inaonekana hapa kwamba mipango ya Kanisa Katoliki kuanza mikakati ya kumpandikiza Nyerere kwenye TAA ilianza kusukwa hapa kwani Kanisa halikuwa na sababu yeyote ya msingi ya kutaka kuonana na Masheikhs kujadiliana nao jinsi gani Kanisa litaingia kwenye harakati za kudai uhuru wakati Kanisa lilishafanya uamuzi kwamba hawawezi kujiunga na vyama ambavyo havina wasomi. Haiingii akili kwenda kumuona mtu ambaye tayari umeshamuhukumu kwamba hafai!!!!

Nyeree alificha makucha yake ya udini uliokubuhu wakati wa zoezi zima la yeye kuingia kwenye kwenye Siasa kupitia TAA. Makucha yake alianza kuyaanika mara baada ya kufanikiwa kujipenyeza ndani ya TAA na hatimaye kupata Urais wa nchi. Ndipo hapo Nyerere aligeuka kuwa zaidi ya Mdini. Alikuwa Mmadhehebu wa hatari sana. Alianza kuweka mikakati ya kuwapendelea Wakatoliki dhidi ya dini zingine na madhehebu mengine ya Wakristo. Akaanza mikakati ya kuuuwa Uislam.

Kitabu cha Jan P. Van Bergen kilimnukuu Nyerere akisema maslahi ya kanisa lake (Roman) yanakuja kwanza na hatokwenda kinyume na kanisa lake.

Alipokufa Pope Yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima!
Kabla ya kifo chake Pope Yohana wa 23 alimletea Mheshimiwa Nyerere barua ya pongezi kwa kuupanua Ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na Pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa kwenye gazeti la Tanganyika Standard.

Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele:
"KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC".
Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.

Mwaka 1970 Nyerere aliwaalika Ikulu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Tanzania Episcopal Conference Fr. Robert Rweyemamu na muwakilishi wa Papa Tanzania Mgr. Giovano Cerrano na Nyerere aliwaambia wageni wake alikuwa anafanya kila liwezekanalo katika mamlaka yake kuuimarisha Ukatoliki Tanzania. Aliwaomba pia waende kuwafahamisha ma bishops kwamba ameanzisha idara ya elimu ya siasa kwenye TANU na kwamba amemteua Mkristo Reverend kuwa mkuu wa idara hiyo sio kwa sababu ya uwezo wake katika siasa bali kwa sababu ya imani yake thabiti kwenye Ukristo. Jukumu lake ni kuongoza na kudhibiti muelekeo wa kisiasa wa chama. Aliwafahamisha vilevile kwamba katika Kamati Kuu ya Chama (NEC) wajumbe wawili ni Reverends. Alisema anaamini hiyo ndio njia nzuri ya kuhakikisha kwamba chama kinapata “watu” wazuri!!!!!! (van Bergen, 1981:333-336).

Si ajabu kutokana na agano lake hilo hapo juu kwamba Sivalon (1992:49) anaripoti kwamba katika mwaka huo huo aliotoa ahadi Wakatoliki walikuwa asilimia 70 ya asilimia 75 ya Wakristo wote waliochaguliwa kuwa wabunge. Kati ya wabunge 108 waliochaguliwa 5 walikuwa wanaamini kwenye dini zetu za asili, 23 walikuwa wanaamini kwenye Uislam, 24 walikuwa wanaamini katika madhehebu mengine ya Kikristo yasiyokuwa Katoliki na 56 walikuwa wanaamini katika Ukatoliki. Hivyo utaona Wakatoliki walikuwa zaidi ya nusu ya wabunge wote!!!!!!!!

Nyerere ndio mtu aliyetumika na Kanisa katika mikakati yao ya kuumaliza Uislam (Crusade). Hii inadhihirishwa na mpango wake wa kufanya mapinduzi Zanzibar kwa kumtumia mtu katili na mdini mwenzake Okello ili kuusambaratisha Uislamu ambapo zaidi ya watu 20,000 waliuawa kikatili na watu wasiopungua 200 walichomwa moto kwenye tanuri wakiwa hai!!!!!
 

Alnuur al taqiyya!
 
hii ndio inatoa picha halisi ni jinsi gani uongozi kwa maslahi ya umma ulivyo na changamoto kubwa. Kile kitendo cha mtu kuwa na upeo wa kutokuangalia dini, kabila, eneo bali binadamu si wote tunaweza kuufikia. Asante kwa ufafanuzi
 


Ha ha ha..!,
Kuna 'sisi' na 'wao',tena waanzilishi wa hali hii ni wao..
VIPOPOOO LEO UMESAHAU??
 

Nguruvi,
Ndugu yangu punguza ghadhabu, jitulize na andika kwa utulivu na kwa adabu.

Vinginevyo utageuka kuwa Lancelot Gobbo.
Si unamkumbuka huyu mtu katika ''Merchant of Venice'' ya William Shakespeare?

Nilieleza habari zake hapa JF.

Umesema mengi lakini nitakujibu moja.
Hili la Balozi Robert Royall.

Balozi Royall alihutubia Bunge la Tanzania tarehe 15 May 2003 na mada yake
ilikuwa ''Blood Money and Financing Terrorism.''

Nitakuongeza kitu.

Hiyo paper yangu iliyozua swali lako ndiyo lilikuwa jibu la hotuba ya Robert Royall
na ndiyo sababu ya kukumatwa uwanja wa ndege Dar es Salaam mwaka 2007
nilipokuwa narejea kutoka Tehran.

Nakutakia siku njema na utulivu wa fikra.
 
BY Nguruvi3""Aya ya pili anaongelea kuhusu waislam kwa ujumla. Mohamed hajui kuwa katika waislam wapo BAKWATA, Ismailia, Bohora, Shia na Sunni na kwamba hicho anachokiongelea ni kikundi chake na wala si waislam.
Jitihada zake ni kuonyesha ulimwengu uzito wa jambo hili kama tutakavyoona. ""

Usichanganye mambo na kuweka histohisia zako nguruvi3,bakwata ni chombo chenu kilichowekwa na nyerere kusimamia maslahi yenu na si maslahi ya waislam..
hilo lipo wazi na tunalitamka kwa kifua mbele kabisa,tatizo lako unajikanyaga kanyaga,unapiga hatua tano mbele kisha unarud hatua 25 nyuma,jitulize,hebu tulizana..
 
Last edited by a moderator:


Swadaka Mohamed Said,
Nadhani sasa atakuwa kaelewa kama tulivyoelewa wenzake pia,lakini tuendelee..
Kama jazwba zitakuwa zimempungua atarudi kwa hali yake ya kawaida Nguruvi3 jamaa yetu huyu tunamjua Ritz hebu mletee leso afute chozi na glass ya juice ya muwa baridii apozee koo...
 
Last edited by a moderator:

Mwanakijiji.

Nimeisoma sana Historia ya tanganyika na hakukuwa na vita vikubwa ambavyo vilihitaji mtu au watu watumike kuleta amani kama ilivyokuwa kwa Kenya na Uganda ambavyo kulikuwa na tabaka za makabila. Tanganyika hakukuwa kabisa na tabaka hizo za ukabila kiasi cha kuifanya nchi kukosa amani.

Labda nidadavulie Ni amani gani aliyoileta Nyerere ambayo ilikuwa haipo kabla ya uhuru wenu? Na amani hiyo ilikuwa inavurugwa na nani? Nasubiri darsa lako hapa.


CC.. Nguruvi3, Ritz, Mohamed Said,
 

Swadakta maneno yako.

Mimi mpaka leo najiuliza nchi yenu au Serikali yyenu ya JMTz haifungamani na dini yoyote ila viongozi wana dini zao binafsi.

Swali langu kwanini JMTz inakumbatia Bakwata na kuilazimisha kuwawakilisha waislam wa Tanganyika? Ukitaka kuona hilo angalieni anapoapishwa Rais wenu wa JMTz, utaona viongozi wa dini wanaalikwa na kutoa neno. Utaona wakristo wanawakilishwa na Umoja wa makanisa, TEC ambaye ni mwakilishi wa wakatoliki, Bakwata mwakilishi wa waislam wa Serikalini na hindu.

Je wenzangu amjaligundua hilo? Juilizeni Why?

 
Mimi naamini kwa wale wachache waliowahi kufanyakazi na Nyerere kuna mengi sana utagundua katika uongozi wake.

Kwanza hakupenda kabisa kufanyakazi na wasomi hususan waliokuwa wanajiamini. 95% ya wasomi alioweza kufanyakazi nao walikuwa ni waoga na ndio Mzee kwa kila asemalo JKN kwani waliamini wazi kuwa ZIDUMU FIKRA ZA JKN.

Hakuheshimu professionals na alitumia siasa na kujuana katika kupata viongozi wake na wengi walikuwa wanafunzi wake.

Na hilo ndio Tanzania mnalokumbana nalo mpaka sasa kwani kila pahala siasa tupu hakuna kuchapa kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…