Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Balozi wa Marekani hajawahi kuhutubia Bunge la Jamhuri yaMuungano; niko tayari kusahihishwa. Lini Balozi Royall alihutubia Bunge laTanzania? ili tupitie hansard.
Nguruvi3 and sweke34 like this
Like zenu za bure Angalia mwereka aliopigwa Mwanakijiji hapa
..................
Balozi Royall alihutubia Bunge la Tanzania tarehe 15 May 2003 na madayake
ilikuwa ''Blood Money and Financing Terrorism.''.............
Huo mwereka aliopata Mwanakijji unafanana na ule wa Nguruvi.
Angalia Mwereka kwa Nguruvi.
Yuko wapi Invisible aone mzee mwenzake anavyowabwaga vijana wake
 
Mundungus Fletcher;

Mbona Marekani isivamie Venezuela nchi ya Kikristo yenye utajiri wa mafuta! nchi hiyo ni adui mkubwa na Marekani lakini subutu!

Kwa taarifa Mzee wa kijijini, nchi ulizotaja ni washirika wakubwa wa Marekani! anaevamiwa hakubali kuburuzwa!
Sasa kama hawa ni washirika wa Marekani inakuwaje wewe unasema Wamarekani wanavamia na kuvamia nchi za kiislamu kwasababu ya Uislamu wao?? haileti Mantiki, unajichanganya mwenyewe....

Kama wao wanauchukia uislamu inakuwaje wanakuwa na washirika wa kiislamu...????
 

Ritz,

Naangalia hapa kwa utuvu,na sisi tunatumia ustaarabu tulorithi toka kwa Wazee wetu. Tukiona jamaa wameadhirika tunawapa nafasi ya kupumua na kujipanga upya. Lakini wao wana dasturi mbaya hawatoi nafasi kabisa,lakini haina neno tushiwajua!ahaha!!

Leo niwie radhi maana sina hata chembe ya kuchangia humu,nacheka tangia jana usiku niliposoma bayana ya Mag3!ahahaha!! Yaani kashindwa kabisa kujizuia ghadhabu zake kwa Sheikh Mohammed Said,kwa hiyo badala ya kujibu hoja yeye kamuwekea maneno ya kumsuta na kumsuduku!ahaha!! Wallahi,nimecheka pita kiasi. Mag3 nampenda saana. Na itanilazim nimuombee Sheikh Mohammed Said amfute kwenye ile "Shit List"!ahahaha!!

Halafu kairejesha upya ile habari ya kitoweo na madikodiko ya Mshume Kiyate!ahaha!! Yaani najaribu kufikiri kwa undani jinsi hishma aliyonayo Mag3 kwa Nyerere,halafu ghafula kaibuka mtoto wa Kariakoo anamwambia ati huyo Nyerere wako alikua hana hata senti ya kununua kitoweo!?ahahaha!! Wallahi,nahisi wiki hii nitaumwa kwa kucheka!!ahah!

Insha Allah tuendelee na mnakasha.

Cc: The Big Show
 

Mag3,

Nafurahi saana kukusikia ndugu yangu. Naona ulikua kimya kitambo nikaanza kupatwa na fadhaa, na hasa kuna wakati pia nilisoma khutba/maakilio yako ikionyesha kama vile ulikua ukitoa wasia na kutuaga!?

Mag3,nakuhakikishia mimi sina mamlaka hapa jamvini ya kuwa na ile "Shit List",lakini kama akitokea mtu kunikera basi nitamuomba fursa Sheikh Mohammed Said amuweke kwenye ile yake.

Nafanza mpango kumuomba Sheikh Mohammed Said,akuondoe kwenye ile list Insha Allah.

Nimependa saana huo msuto hapo juu ulomfanyia Sheikh Mohammed Said,lakini nahisi kama ulikua katika muhma na kizaazaa kisicho mfano. Kwa ufupi nimecheka usiku kucha nilipoona hiyo milumbano baina yenu!ahaha!! Nastaajabu kwanini umeirejesha ile habari ya kitoweo cha Nyerere!?

Nakupenda saana ndugu yangu na tuendelee na mnakasha.
 

Mundugs Fletcher;

Mfumo wa Serikali ya TZ kama wanaipenda Uislamu kwanini wawe na ushirikiano na Bakwata taasisi dhaifu isiyo na ushawishi wowote juu ya Waislamu? Marekani iko ktk vita na Uislamu na kama Serikali yoyote ya Kiislamu itakataa kushirikiana nayo ktk vita hiyo, basi wataondolewa madarakani kama yaliyowakuta Taliban na wengine! na hapa yanayowakuta akina Shehe Ponda na wenzake kila mtu anajua!
 
Mohamed ukisoma nilichoandika hakuna ghadhabu hata sentensi moja.
Nimeuliza kama balozi amehutubia bunge na lini.

Mohamed, umeweka tarahe nadhani watu watapitia hansard za bunge kujua na kujiridhisha kwa hilo.
Kuna kuhutubia bunge na kuhutubia semina ya wabunge,hivi ni vitu viwili tofauti!

Halafu usiwe na wasi wasi na mimi, nipo katika 'shit list yake '' wala sihitaji nafasi nyingine zaidi.
Angalia tu maneno yako!
 

Sheikh Mohammed Said,

Salaam.

Kuna wakati tulikwenda pale Kisiwandui Unguja na Salim Ahmed. Akapanda jukwaani David Wakati, kwa kuwa yeye ni mtoto wa Mkunazini ili kumkaribisha Salim ahmed azungumze. Basi maskini Salim Ahmed,kwa ustaarabu wake akaanza kutaja nasaba yake na akasema yakuwa yeye pia ana damu na asili ya Kimanyema. Basi wale Virongwe wa fikra wakaanza kusonya na kumzoma kichinichini,maana zile chuki na fitna za yule Mnyasa zishawakolea.

Kwa hiyo hapa jamvini,pia pana jamaa zetu wanaanza kutuhoji makabila,labda hawajui sisi tuna michanganyiko mahsusi na ndo maana tukaitwa Waswahili. Na ni aghalab kumkuta Mswahili ati anabagua kwa makabila

Pana mengi hapa tunaulizwa,na tuna majibu yao yaso mipaka lakini aha! Yanini? Haya tulonayo kitahanani chake ndo hivi tuonavyo.

Tafadhali,nakualika Ramadhan uwepo hapa kwangu Insha Allah. Nakukaribisha mno Al Akhiy uje kupumzika japo kiduchu,na kwa sasa hali ya hewa kama ujuavyo ni njema.

Ahsanta.
 
:A S shade:
 
Swadakta kwa analysis yako. Sasa jiulize kama wakristo wana TEC iweje waislam wasiwe na chombo chao? Kwani kuna tatizo gani kwa wakristo kuwa na TEC? Kwamba, tatizo la waislam kuwa disorganized kwanini liwe la wakristo.
Barubaru hii habari ya kujilinganisha ni mbaya sana. Fikiria kama BAKWATA ni ya serikali kwanini ina wafuasi?

Na je nje ya Bakwata, hawa akina haki za waislam, mali za waislam, Istiqama, Mohamed Saidi, Baraza kuu, muslim foundation nao wanamwakilisha nani? kwanini wasiwe kitu kimoja hadi usote kidole TEC.

Lazima watu wafikiri umbali mrefu zaidi. Ushabiki ndio umekufikisha mahali ukaamini kuwa ''classmate'' wako Warioba aliokotwa akiwa machungani na kuwa PM? Ustadh, tulizana Mohamed kesha sema kitabu chake si mashaf.
 
Naomba wanajamvi tuwekane sawa kidogo juu ya madai ya Balozi wa USA kuhutubia bunge kama anavyodai Mohamed Said,

Naomba niwafahamishe ama niwakumbushe kuwa kikao kile cha 15 May 2003 haikuwa kulihutubia BUNGE bali ilikuwa semina elekezi ya kikao cha baadhi tu ya wabunge tena kilifanyika nje ya ukumbi stahiki wa bunge la jamuhuri.

Kwakuwafahamisha tu nikuwa balozi wa USA alikwenda dodoma kuwafunda wabunge wapitishe sheria ya UGAIDI, na alifanikiwa.
 
Duh gombesugu wanchekesha kweli kweli unafaa kuziba pengo la Issa Matona
.

 
:A S shade:

Ami,

Nahisi pale umeona kuwa Nguruvi3,anataka kutumia technicalities almurad awe hajakosea!

Ahsanta Al Akhiy kwa kugundua hicho kitu na ku-highlight kwa haraka!ahaha!!
 

Halafu ktk semina hiyo ya wabunge Balozi alikaa kama mwenyekiti, mtoa mada au msikizaji mualikwa?
 
Duh gombesugu wanchekesha kweli kweli unafaa kuziba pengo la Mohammed Issa Matona
.

Nafurahi kukuchekesha,lakini taratibu usicheke mno ukawa kama Kilwa Jazz! Wimbo wao wa mwisho ulikuwa ni chekacheka,kutamalaki na Band nayo pia ikavunjika!
 
Kadogoo kwanza unatakiwa ukubali ilikuwa ni semina elekezi na si mkutano ua kikao cha bunge ndiyo tuendelee.Masuala ya nani alikuwa mwenyekiti sijui msikilizaji yatakuwa na maana ikiwa utakubaliana na Yericko Nyerere

Halafu ktk semina hiyo ya wabunge Balozi alikaa kama mwenyekiti, mtoa mada au msikizaji mualikwa?
 
Last edited by a moderator:
Ami,

Nahisi pale umeona kuwa Nguruvi3,anataka kutumia technicalities almurad awe hajakosea!

Ahsanta Al Akhiy kwa kugundua hicho kitu na ku-highlight kwa haraka!ahaha!!
Gombesugu, nadhani umemsoma Ngongo na Yericko hapo juu.

Lazima watu wawe katika kiwango cha GT. Semina ya bunge si bunge.
Utaratibu wa kuhutubia bunge unajulikana na anayehutubia hualikwa na Bunge kwa mwaliko Maalum.

Mohamed, hajui taratibu za bunge na wala hajui tofuati ya semina ya bunge na Bunge la JMT.
Kama semina ndiyo bunge lenyewe basi nina orodha ya watu wengi sana waliofanya hivyo.
Kuanzishwa kwa mifuko ya jamii akina Dau nao walihutubia bunge.

Msimemeze tu kila kitu kutoka kwa ''nabii''
 
Ami,

Nahisi pale umeona kuwa Nguruvi3,anataka kutumia technicalities almurad awe hajakosea!

Ahsanta Al Akhiy kwa kugundua hicho kitu na ku-highlight kwa haraka!ahaha!!

Si umeona hapa.Yerico naye amethibitisha lilelile!
 
GWALIHENZI;

Kwa hiyo Nyerere ndie alikuja kupatanisha makabila yaliyokuwa yakipigana sio? au ulimaanisha nini?
Swala halikuwa Nyerere kupatanisha, swala lilikuwa kukanusha uwongo wenu na mwarabu wenu Barubaru kuwa hakujawahi kuwepo vita vya makabila! upo hapo ustaadh kadogoo!
 
Halafu ktk semina hiyo ya wabunge Balozi alikaa kama mwenyekiti, mtoa mada au msikizaji mualikwa?

Soma kwakutulia hicho nilichoandika ndugu yangu, jitahidi kumaliza maandishi yote, usisome juu juu tu
 

Mzee Said tafadhali; Royall hakulihutubia Bunge; alizungumza na wabunge kama mtoa mada katika mojawapo ya semina zao za kawaida ambazo watu wengi hualikwa kutoa mada. Kwamba alizungumza Bungeni wakati wa kikao cha Bunge mbele ya Bunge zima hii si kweli. Unless hujui tofauti ya "Kulihutubia Bunge" na "Kuzungumza na Wabunge"..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…