Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Swahiba wamgu Mohamed Said na wafuasi wako mtiifu,

Huku mkiendelea kutafakari jinsi tulivyoyanyambua maandishi ya kitabu hicho cha kichochezi cha Mohamed,

Hebu burudikeni na ngano hiii kutoka

"Vita dhidi ya Ugaidi"


DOLA YA AMERIKA YAWEZA KUANGUKA


Kuyumba kwa uchumi wa Marekani, vita ndefu ya Iraq isiyokwisha, kuendelea kuandamwa na jinamizi la ugaidi, ukosefu wa ajira, vita kali ya kiuchumi kati yake na China inayoonyesha dhahiri kuwa vijana wa Mao Tse-tung wanapata ushindi. Hayo yanakuwa nikiashirio thabiti cha kutabiri anguko la dola mufilisi. Taifa hilo lililo ishika dunia pabaya na dunia ikaacha kumsujudu Mungu na kuisujudi Marekani tena kwakutembelea magoti kabisa.

Amerika imeshindwa kusoma alama za nyakati, kwani kwanza, dunia ilianza kushuhudia kunako karne ya 15 uwezo wa kidunia ukishamiri mitaa ya Ulaya, Kitendo hicho kilizaa dunia tunayoifahamu hivi sasa ya sayansi na teknolojia, biashara, ubepari, na mapinduzi ya viwanda na kilimo. Hapo ndipo mataifa ya Magharibi yalipotawala mlengo wa siasa. Hayo yalitosha kabisa kuipa jeuri Ulaya.

Pili ni mwishoni mwa karne ya 19 ambapo bila kutarajia Ulaya ilizima kama mshumaa!, wale wababe na mashujaa wa kuiendesha dunia kama Adolf Hitler,(Ujerumani) Francisco Franco,(Hispania) Benito Mussolini (Italia) nk, Hawakufua dafu mbele ya alama za nyakati na kilichotokea ni uwezo wa kidunia kuhamia Amerika. Kutokana na viwanda, kilimo na masoko makubwa Amerika ikajiimarisha vya kutosha, mpaka ikaanzisha kupindisha nadharia na muundo wa vyombo vingi vya kimataifa kama Umoja wa Mataifa, Benki ya dunia, Kituo cha biashara cha kimataifa, Shirika la afya dunia nk na kuviundia mfumo hodhi kwa mwavuli wa sheria ya haki miliki. Mfumo huu na sheria hii ndivyo vilivyo izima Ulaya,

Karne ya 15 mfumo na sheria hii vingekuwepo Ulaya ingalikuwa bado inameno tena makali. Tafakari mfumo huo na sheria hiyo ingekuwepo enzi hizo, leo Mlima Kilimanjaro, Ziwa Victori, Ziwa Tanganyika na vivutio vingi vilivyopo barani Afrika ambavyo inanenwa kuwa viligunduliwa na wazungu kutoka Ulaya japo Wachaga,Wasukuma na Wahaa waliishi katika maeneo yaliyo bainishwa hapo, tusitumie rasilimali hizo bila kibali cha walio gundua.

Na karne ya 21 kinachotokea ni badiliko kuu la tatu kiulimwengu. Dunia inashuhudia mtikisiko mkubwa wa kiuwezo ambapo inabashiriwa kuwa baada ya miongo mitatu tu vitabu vya historia juu ya Marekani vitafunikwa na kufunuliwa vya ukanda mwingine ambapo njozi zinaelekeza Mashariki ya Mbali. Wamarekani wanaona dunia mpya inazaliwa, ila wasiwasi wao ni mfumo wa uzaliwaji unaopangiliwa na mataifa ya nje na watu wa nje kabisa.

Matukio yaliyotokea ndani ya miaka nane kati ya mwaka 2000-2008 yanatanabaisha kuporomoka kwa dola hiyo mfano: Jengo refu kuliko yote duniani lipo Taipei (Taiwan), Kiwanda cha kutengeneza ndege kubwa kiko Ulaya, Binadamu aliyeishi miaka mingi zaidi duniani alipatikana mwaka 2007 Kilimanjaro (Tanzania), Katika orodha ya matajiri zaidi duniani Marekani ilibakiwa na wawili kwa mujibu wa takwimu ya mwaka 2007, Kamari inachezwa zaidi Macao China kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2006,

Takwimu hizi zinaweza kuonekana kama za kipuuzi! Lakini, hicho ni kiashiria tosha, kwani miaka 15 nyuma Marekani ilikuwa kinara wa kila kitu duniani. Wakati dunia inaenda kwa kasi ya ajabu katika mageuzi mbalimbali wamarekani wamepigwa butwaa na kuacha Mashariki ya mbali wakienda sambamba na mageuzi hayo. Haiyumukiniki kama Marekani itakuwa akilini mwa mwanadamu baada ya miongo mitatu hivi, labda kwa bara la Afrika lisilojitambua kuwa nitajiri, lililopandikizwa mfumo musonge na sera mufilisi baada ya kukubali kufuata torati za mashirika mumiani ya kimataifa

Hayo ndiyo yaliyo iimarisha Marekani na kuwa taifa lenye nguvu duniani tangu karne ya 19 mpaka karne ya 21 ambapo dalili zinaonyesha safari ya kupokezana kijiti cha ubabe wa dunia inaenda sehemu nyingine. Baada ya uwezo wa kidunia kuonyesha dalili za kushamimiri na kuhamia kabisa pale Maashariki ya Mbali, kwa kufuata mtiririko wa alama za nyakati taswira ya dhahiri inaturudisha Afrika. Afrika panatabiriwa kuja kuwa mahali pa tamko kuu la kidunia katika nyanja zote baada ya miongo mitano.


Na Yericko Nyerere
 


Una uhakika alihutubia Bunge? au unarudia alichosema Mohammed Said? Kulikuwa na kikao gani cha Bunge kinaendelea Mei 15, 2003?
 
MZEE MWANAKIJIJI;

Haya umepata jibu lako kuhusu Balozi wako! ndio ulitaka kusema nini vile!

na wewe umeamini kweli Robert Royall alihutubia Bunge la Tanzania? Mzee Said anaweza kutunga chochote akakipa tarehe na mahali nawe utaamini tu...
 
Una uhakika alihutubia Bunge? au unarudia alichosema Mohammed Said? Kulikuwa na kikao gani cha Bunge kinaendelea Mei 15, 2003?

Mkuu wala wasikuumize kichwa,

Mimi nilikifuatilia semina ile kwa ukaribu kabisa, haikuwa kulihutubia bunge kama anavyodai Mohamed Said.

Ninachokumbuka nikuwa ubalozi wa USA uliamua kuendesha semina ile baada ya kuona dalili za kupingwa kwa mswaada wa sheria ya Ugaidi.

Sasa anaekaririshwa na Mohamed Said kuwa BALOZI wa USA alilihutubia bunge tumsamehe tu kwani hajui aaminicho.
 

Tatizo Mzee Said haina ile intellectual humility ya kusema kuwa "niwieni radhi nimechanganya madawa tu; ni kweli Balozi Royall hakuhutubia Wabunge bali alizungumza nao kwenye semina ya Lobbying ili kupitisha mswada wa sheria dhidi ya Ughaidi". Akisema hivyo basi tutaelewa tu kuwa alighafirika kidogo na tutamsamehe.
 
Wakijiji rejea katika yale yaliyotokea Bosnia.

Wakati Waserbia wakiwaua Waislamu Marekani alikuwa ametulia tu lakini mara tu pale kikundi kidogo cha Mujahidin kilichokuwa Afghanistan kilipoingia Bosnia na kutangaza Jihad na kupata Waislamu wengi Wabosnia wa kuwaunga mkono na kuanza kuwatandika Waserbia huku kila kijiji wanachokikomboa wanapandisha bendera ya Uislamu ili kuweka shariah ndipo Marekani kwa hofu ya Bosnia kutawaliwa Kiislamu alipoomba mandate ya UN kwenda "kuwasaidia" Waislamu dhidi ya Waserbia!

Marekani alipoingia Bosnia kitu alichofanya ni kuwapiga mabomu Waserbia na Mujahidin kwa pamoja mpaka akafanikiwa kuifanya Bosnia kuwa ni nchi ya kisekula badala ya muelekeo waliokuwa wakielekea wa Kishariah...huyo ndiye Mmarekani kiuhalisia wake!

Cha kusikitisha zaidi ni kuwa Dunia iliaminishwa kuwa Marekani alikwenda kuwasaidia Waislamu wa Bosnia!
 
Hapo umemwaga kivi ili upate kukimbia.Ikiwa hujui kivi gombesugu atakuwekea wazi.
Ufupi wa mambo ni kuwa Royall alizungumza na wabunge wa JMT na madhumuni yake ilikuwa kushinikiza sheria ya ugaidi ipite ambayo inaendelea kuwatesa waislamu.
Hapa mnasema balozi hakuhutubia bunge bali alizungumza na wabunge.Kule Nyerere alikaribishwa tu kwenye TANU lakini mnataka sote tuamini kuwa yeye ndiye muasisi.
Nyinyi mkoje?.Kwanini hampendi kuukubali ukweli.
 

Na thats your story? haya bana sasa tutafanyaje...
 

Ami,

Kuna msemo:" Smoking the same tobacco using different pipes."

Asikushughulishe.
 

... koh koh koh.... ukweli haubadiliki kuwa uongo kwa sababu huupendi. Ndugu yangu na wewe hujui tofauti ya "kuhutubia Bunge" na kuzungumza na Wabunge na implication ya yote mawili?
 
Dah,nakusikitikia sana,unahoji kitu ambacho jibu unalo mwenyewe...!
Tokea lini mfano wa nchi kama Iran n like,wakawa na urafiki na waamerika...

Hivyo, kwa vila haina uhusiano na Marekani Iran ni nchi ya Kiislamu zaidi kuliko Saudia, Oman, Misri, n.k ? Kwani Marekani imeharamishwa kwa Waislamu?
 
Najua mkiishiwa hoja mankimbilia kutukana matusi. Mimi sina alergy ya kutukanwa. Ndio maana naitwa Zali la Mentali.
Tukiwaita wajinga na akili zenu hazina akili sijui kwanini huwa mnakasirika na kutoa mapovu ati mmetukanwa. Sasa hebu soma huu ujinga wako hapa uone kama husitahili kuitwa mpumbavu! Sasa hapo wewe hujatukana? au wewe ndio mwenye haki miliki ya kutoa lugha za kifedhuri na wengine wakikanusha mitusi yako hiyo waonekane wabaya? Na ulivyokosa akili ati unaamini hiyo mitusi yako dhidi ya Nyerere ni hoja ! shame on you and your embicile old man!
 

Gombesugu,
Ahsante.

Insha Allah.
 
Hivyo, kwa vila haina uhusiano na Marekani Iran ni nchi ya Kiislamu zaidi kuliko Saudia, Oman, Misri, n.k ? Kwani Marekani imeharamishwa kwa Waislamu?


Mwanakijiji you are smarter than that,ndio kusema hujui hulka ya marekani na vipaombele vyake?
Wapo hata wananchi ambao ni raia wa marekani ambao ni muslims na non muslims wanaiochukia wazi wazi sera ya mambo ya nje ya marekani na kasumba ya kuupiga vita uislam..
Saudi marekani ana interest..
Oman,like wise..
Na kilichotokea Iraq na misri na hata kinachotokea syria marekani ana mkono wake moja kwa moja,tena anafadhili mabilion ya pesa kumwaga damu pale...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…