Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Dah ! Wickama na Wilcard leo mumenisoma kutoka huko mliko, nawashukuru sana. Kila mlichosema ndicho nilichotaka kusema.Heshima yako Mzee MS. On the contrary sina cha kuhofu. Nahofu nini? Mzee MS, nimefundishwa kuwa kusengenya ni kuelezea watu wengine habari ya mtu kiasi kwamba mwenyewe isingemfurahisha au tuseme ngemuudhi, hata kama unachosema ni kweli. Wewe ndio umezungukwa na maustadh wazito wazito wanajua mambo haya. Waulize. Unasengenya sheikh wangu. Zisikudanganye "likes". Mimi siogopi kukwambia. Na hata marehemu Abdul angekuwako asingefurahishwa na tabia yako. Nyerere alikuwa mgeni wake. Ilikutosha kuishia hapo. Yupi alihamia chumba gani ilitakiwa yeye Nyerere aseme kama aliona ina manufaa sio Sykes wala wewe. Sykes hakulisema kwa vile alilijua kidini ni dhambi sheikh. Hayo uliyoyakomalia ya Ally kuhamishwa ampishe ni masengenyo baba yangu. Kwenda sokoni hana senti ya kununua chochote ni masimango ustadh na hayana uhusiano na muslim struggle against the british. Na hata kama uliambiwa, nini maana ya hekima ya kuchuja mambo MS? Bora anayekwambia ukweli. Nilishaweka hapa aya husika inayokataza kusengenya lakini naona gari yako iko kwenye over-drive. Uliiruka. Wachana na ma-book ya kina Mandela, wewe umeshajivalia uislamu katika kusimulia mada zako, lazima usimulie mambo ndani ya stara ya kiislamu.
Leo huwezi kusikia mwandishi mwenye akili nzuri akiandika kuhusu Mandela alivyobeba mitondoo huko Robben. Hata usaliti wa Winnie kwa huyu mzee unaandikwa kwa staha yake.
Mohamed kaenda hadi kufikia kusema wapi Nyerere alipunzika. Hivi Mama yetu Maria au watoto wake wakisikia hili wanajisikiaje. Wickama umesema vizuri sana kuhusu usengnenyaji, sasa huyu ndiye mtu anayetaka haki na anayesema anasimama kwa ajili ya uislam ule ule asio u-practice.
Tulimwambia siku nyingi kuwa kuna mambo katika uandishi unayaangalia na impact yake. Wapi Nyerere alilala na kitoweo alipata wapi ingeweza kuandikwa kwa namna ya staha kama kweli ilitokea hivyo. Lakini katika kuhakikisha kuwa anamdhalilisha Nyerere katika kiasi anachoweza Mohamed amekwenda mbali kumzulia hata mengine ya uongo.
Mohamed, this is too low! Kwa wajinga na wasiojua dini au ustaarabu wa mwanadamu hizi ni habari njema. Kwa mwenye kutumia asilimia 10 ya ubongo wake hii ni dhalilili kubwa sana katika fani ya uandishi wako.