Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Heshima yako Mzee MS. On the contrary sina cha kuhofu. Nahofu nini? Mzee MS, nimefundishwa kuwa kusengenya ni kuelezea watu wengine habari ya mtu kiasi kwamba mwenyewe isingemfurahisha au tuseme ngemuudhi, hata kama unachosema ni kweli. Wewe ndio umezungukwa na maustadh wazito wazito wanajua mambo haya. Waulize. Unasengenya sheikh wangu. Zisikudanganye "likes". Mimi siogopi kukwambia. Na hata marehemu Abdul angekuwako asingefurahishwa na tabia yako. Nyerere alikuwa mgeni wake. Ilikutosha kuishia hapo. Yupi alihamia chumba gani ilitakiwa yeye Nyerere aseme kama aliona ina manufaa sio Sykes wala wewe. Sykes hakulisema kwa vile alilijua kidini ni dhambi sheikh. Hayo uliyoyakomalia ya Ally kuhamishwa ampishe ni masengenyo baba yangu. Kwenda sokoni hana senti ya kununua chochote ni masimango ustadh na hayana uhusiano na muslim struggle against the british. Na hata kama uliambiwa, nini maana ya hekima ya kuchuja mambo MS? Bora anayekwambia ukweli. Nilishaweka hapa aya husika inayokataza kusengenya lakini naona gari yako iko kwenye over-drive. Uliiruka. Wachana na ma-book ya kina Mandela, wewe umeshajivalia uislamu katika kusimulia mada zako, lazima usimulie mambo ndani ya stara ya kiislamu.
Dah ! Wickama na Wilcard leo mumenisoma kutoka huko mliko, nawashukuru sana. Kila mlichosema ndicho nilichotaka kusema.

Leo huwezi kusikia mwandishi mwenye akili nzuri akiandika kuhusu Mandela alivyobeba mitondoo huko Robben. Hata usaliti wa Winnie kwa huyu mzee unaandikwa kwa staha yake.

Mohamed kaenda hadi kufikia kusema wapi Nyerere alipunzika. Hivi Mama yetu Maria au watoto wake wakisikia hili wanajisikiaje. Wickama umesema vizuri sana kuhusu usengnenyaji, sasa huyu ndiye mtu anayetaka haki na anayesema anasimama kwa ajili ya uislam ule ule asio u-practice.

Tulimwambia siku nyingi kuwa kuna mambo katika uandishi unayaangalia na impact yake. Wapi Nyerere alilala na kitoweo alipata wapi ingeweza kuandikwa kwa namna ya staha kama kweli ilitokea hivyo. Lakini katika kuhakikisha kuwa anamdhalilisha Nyerere katika kiasi anachoweza Mohamed amekwenda mbali kumzulia hata mengine ya uongo.

Mohamed, this is too low! Kwa wajinga na wasiojua dini au ustaarabu wa mwanadamu hizi ni habari njema. Kwa mwenye kutumia asilimia 10 ya ubongo wake hii ni dhalilili kubwa sana katika fani ya uandishi wako.
 
Si jambo la ajabu Uingereza kumtukuza Nyerere kwani walikuwa wanamtumia kufanya crusade katika Africa. Mapinduzi ya Zanzibar yana mkono wao, Nyerere kuendelea kuwa Rais wa nchi hii kwa mabavu kuna mkono wao. Udicteta wa Nyerere kwa kiasi kikubwa sana umerutubishwa na mataifa ya magharibi na hasa Kanisa Katoliki.

Kati ya vibaraka wakubwa wa mataifa ya Magharibi waliotumika kuuwa maendeleo ya Wa Africa baada ya kupata Uhuru Nyerere ndie baba lao. Nchi hii itaendelea kusuasua kimaendeleo mpaka masalia ya utawala na mfumo aliouacha Nyerere utokomee kabisa.

Duuh,
Kama mitazamo ya watu ndiyo hii hamna haja ya watu tulio na akili timamu kujibizana hapa.
 
Dhambi ya kusema uongo ni kama ule wa mlevi wa pingu na kama unao mashabiki, kama hao hapo juu, kwa muda utaishi, utastawi na kunenepa, lakini mwisho wake, lahaula...hiyo harufu!

gombesugu, kama hata kwa jambo obvious kama hili ambalo linahitaji tu kuangalia hansard ya bunge Mohamed Said anathubutu kusema uongo, hebu fikiria yale yote anayodai kusimuliwa barazani mtaa wa Kipata! Cha kuhuzunisha wapo wanaomeza tu bila hata kutafuna...tarehe 15 May 2003 hapakuwepo na kikao cha bunge! Endeleeni kunywa pingu ila hakikisheni suruali zenu zimetiwa pingu watu wasije wakawakimbia!

Mag3,

Wallahi,sisi soote tumepata simanzi kuona umetuhusisha na laana za kilevi. Makwetu hayo ni mambo ya kijaaluta yaso mipaka. Tafadhali itakulazim ututake radhi ndugu yangu,hasa kwa Sheikh Mohammed Said. Sisi pia tunampa hishma kubwa mno kuliko ile wewe umpayo Nyerere.

Ni kama vile jamaa zako walivyompa challenge Sheikh Mohammed Said kuhusu "Mmanyema Mkristo",na mimi binafsi nakupa challenge ndugu yangu Mag3;yakuwa sijapata kuona Muislam mlevi ijapokuwa sijawahi kufika Tarime kuona vitimbi vya huko.

Mbona zile LIKE zako na jamaa zako Mwanakijiji na Nguruvi3 hazikushughulishi? Huoni nawe pia unatumia ukabila na udini. Ama kwa hakika umenihuzunisha ndugu yangu. Hata zile nguvu za kukuombea utolewe kwenye ile "Shit List" ya Sheikh Mohammed Said zimenisha.

Lakini haina neno bado nakupenda na kukuheshimu sana ndugu yangu.

Cc;Ritz,Barubaru,Kadogoo,Boko Haram,The Big Show,Ami
 
Swadaka Mohamed Said,
Nadhani sasa atakuwa kaelewa kama tulivyoelewa wenzake pia,lakini tuendelee..
Kama jazwba zitakuwa zimempungua atarudi kwa hali yake ya kawaida Nguruvi3 jamaa yetu huyu tunamjua Ritz hebu mletee leso afute chozi na glass ya juice ya muwa baridii apozee koo...
Pole sana ndugu ya Nguruvi3 kwa kupata mshutuko tumshukuru Allah akufanyie wepesi usije kupata maradwi mengine kama kiarusi na sukari haya yote yanaletwa na mshutuko.Nakushauri siku ingine ukipata mshutuko basi kunywa vijiko vitatu vya asali mbichi.Balozi Royall alihutubia bunge la Tanzania tarehe 15 May 2003.
Wakati nakunywa juisi ya muwa bariidi kama nilivyo aswa nikasikia sauti ya ngurumo hii hapa
Dhambi ya kusema uongo ni kama ule wa mlevi wa pingu na kama unao mashabiki, kama hao hapo juu, kwa muda utaishi, utastawi na kunenepa, lakini mwisho wake, lahaula...hiyo harufu!
gombesugu, kama hata kwa jambo obvious kama hili ambalo linahitaji tu kuangalia hansard ya bunge Mohamed Said anathubutu kusema uongo, hebu fikiria yale yote anayodai kusimuliwa barazani mtaa wa Kipata! Cha kuhuzunisha wapo wanaomeza tu bila hata kutafuna...tarehe 15 May 2003 hapakuwepo na kikao cha bunge!
Nikahisi nahitaji vijiko vitatu vya asali (ushauri wa Ritz) kwasababu mtafiti hakufanya utafiti lakini anabaki kuwa mtafiti kama anavyothibitisha hapa
Wanajamvi,Hebu tusaidiane:Tujaalie ilikuwa semina ya wabunge na Balozi Robert Royall hakuhutubia Bunge.Tatizo liko wapi?Taarifa nilizokuwa nazo zinasema na hapa nanukuu ''Addressing Members of
Parliament in Dodoma on the subject of ''Blood Money and Financing
Terrorism...''
Mie kama ingelikuwa ni semina ningelisema alihutubia semina ya Wabunge lakini
nyaraka nilizopitia wakati naandika ile paper zimesema kama nilivoonyesha hapo
juu katika bold.
Nikimalizia kijiko cha tatu ndipo nikasikia kishindo hiki
Taarifa ulizokuwa nazo hazisemi 'addressing the Tanzanian Parliament". You are a master of the English language and I bet you know pretty well the difference between "addressing" and "address to". Hilo la kwanza laweza kutafsiriwa "alizungumza" au "kuzungumza" lakini la pili linachukuliwa kama 'hotuba' yaani a formal speech to an entity (Bunge, Baraza nk).

Kile unachokiita "chanzo" chako si kingine bali ni ripoti ya mwandishi wa habari Alfred Msangya ambaye aliandika hivi kama sehemu ya taarifa yake (UNAWEZA KUSOMA TAARIFA YOTE HAPA)
Addressing Members of Parliament in Dodoma on the subject of «Blood Money and Financing Terrorism», the US ambassador to Tanzania, Robert Royall said: «We are proud to be your partners in this effort and I am deeply grateful that you have given me this opportunity to advance some of my thoughts on the topic of financial crimes, and especially in the matter of money-laundering».

Sasa hicho alichosema Alfred siyo sawa na ulichowaambia watu wa Ibadan - ukipotosha kwa makusudi (kwa sababu nina uhakika unaijua vizuri lugha ya Kiingereza) kuwa:

Ignoring the feeling of Muslims the then United States Ambassador to Tanzania Robert Royall addressed the Tanzanian Parliament expressing his government's satisfaction in Tanzania'ssupport in its war against terrorists and pledged USD 100m in aid to East African governments to help combat terrorism.

Sasa Mzee Said wewe ndiye uliweka hiyo tafsiri kuwa Royall alihutubia Bunge; hakukuwa na kikao cha Bunge na hivyo madai yako kuwa (he) addressed the Tanzanian Parliament are unfounded, and they are absolutely resulting from your own fabrication - a tendency that you are fond of.

Lakini kinachonisumbua mimi zaidi ni kuwa katika kuandika historia hauko tayari kuangalia vyanzo vyako na kufanya independend review of facts; cross checking etc. Kusema kuwa Balozi wa Marekani alihutubia Bunge la Tanzania kulikuwa na lengo moja tu: kuonesha jinsi serikali ya Tanzania ilivyoinama mbele ya Wamarekani na Wamarekani wakafanya wanachotaka! Mpaka Tanzania inatoa nafasi kwa Balozi kuhutubia Bunge nina uhakika wasikilizaji wako kule Ibadan walishangazwa sana na kuishangaa Tanzania kumpa nafasi balozi kufanya hivyo. Ungesema ukweli kuwa kalikuwa ni ka semina kalikokuwa na wabunge wasiozidi sitini au hata kama wabunge wote lakini ni semina tu ya kawaida impact ya madai yako isingekuwa kubwa kihivyo na wewe kujikutuza kwa kuimbua Tanzania mbele ya jamii ya kimataifa.

Wanaokuita mchochezi wamekupa heshima tu; lakini kwa kweli wewe ni mchonganishi. Unawachonganisha Waislamu na Wakristu wa Tanzania tena ule uchonganishi mbaya sana. Tulipokuwa wadogo shuleni kulikuwa na watu wanaitwa wachonganishi. Kazi yao ilikuwa ni kuchukua maneno hapa na kuyapeleka kule na kuyachukua ya kule na kuyapeleka hapa na katika kufanya hivyo kubadilisha ukweli wake, kutia chumvi na hata kuondoa maneno mengine ilimradi watu wagombane. Watu wakipata hasira na kutaka kugombana wale wachonganishi ndio wanakuwa wa kwanza kushika mchanga mkononi na kuwaimbia "Puta"! zipigwe.

Lakini marafiki wakiamua kukaa pamoja na kuulizana wanayodaiwa kusema wakagundua mara moja kuwa yule mtu wa tatu ndiye aliyekuwa akiwafarakanisha basi marafiki hupatana na kumtenga au kumsuta yuule mchonganishi. Mohammed Said wewe si mwanahistoria; hupiiganii haki za Waislamu, hutetei maslahi ya Watanzania wote; wewe ni mchonganishi. Unawachonganisha ndugu zako kwa misingi ya dini. Unatengeneza historia na kuiremba na kuipeleka kwa Waislamu ikiwa inawachochea wachukie Wakristu; unakuja huku kwingine na kutuambia mazuri ya Waislamu na dhulma ambayo Wakristu wamewafanyia ndugu zao. Umekaa unasubiri.... makanisa yanachomwa... unasubiri... mauaji yanatokea... unasubiri... Watu wanaanza kunyimana vyumba vya kupanga kwa sababu ya dini... unasubiri... leo wapo baadhi ya Waislamu wakisikia jina la Nyerere linatajwa wanasema "amelaaniwa"..... unasubiri.... unasubiri uone uchonganishi wako utazaa nini.

Mzee Said, katika hili kubali umeelewa vibaya na utasahihisha huko mbeleni. Vinginevyo unatupa wengine kazi kubwa sana ya kusahihisha your historical errors and logical inconsistencies...

Sikumbuki kama ni ile ngurumo au kishindo vilivyonichanganya, ninakumbuka kusikia kwa mbali kama sauti za umati zikigutia liar! liar! liar!Mo stop this, please! case dismissed.
 
Thanks Mzee Mwanakijiji: Ni kweli MS ni mchonganishi. Sipati picha hapo Ibadan walivyotuona Watanzania baada ya
kuambiwa Balozi amepewa nafasi ya kuhutubia Bunge letu. MS hajali, anachonganisha Waislam na Wakristo, ameandika uongo mwingi na mifano iko chungu nzima, anawagawa hata Waislam wenyewe kwa madaraja (Manyema, Zulu fist class),
anawasimanga hata Marehemu na zaidi hata ile heshima kidogo ya Nchi iliyobaki anai-damage huko nje ili tu a-achive his
mission. Sijui hili baadaye atasema "typo error".

Hata huo Uislam anaodai kuutetea inaweza kuwa geresha. Ni chuki tu.
Hapa chini Wickama amemwelezea kwenye "angle' nyingine.

By Wickama Heshima yako Mzee MS. On the contrary sina cha kuhofu. Nahofu nini? Mzee MS, nimefundishwa kuwa kusengenya ni kuelezea watu wengine habari ya mtu kiasi kwamba mwenyewe isingemfurahisha au tuseme ngemuudhi, hata kama unachosema ni kweli. Wewe ndio umezungukwa na maustadh wazito wazito wanajua mambo haya. Waulize. Unasengenya sheikh wangu. Zisikudanganye "likes".

Mimi siogopi kukwambia. Na hata marehemu Abdul angekuwako asingefurahishwa na tabia yako. Nyerere alikuwa mgeni wake. Ilikutosha kuishia hapo. Yupi alihamia chumba gani ilitakiwa yeye Nyerere aseme kama aliona ina manufaa sio Sykes wala wewe. Sykes hakulisema kwa vile alilijua kidini ni dhambi sheikh. Hayo uliyoyakomalia ya Ally kuhamishwa ampishe ni masengenyo baba yangu.

Kwenda sokoni hana senti ya kununua chochote ni masimango ustadh na hayana uhusiano na muslim struggle against the british. Na hata kama uliambiwa, nini maana ya hekima ya kuchuja mambo MS? Bora anayekwambia ukweli. Nilishaweka hapa aya husika inayokataza kusengenya lakini naona gari yako iko kwenye over-drive. Uliiruka. Wachana na ma-book ya kina Mandela, wewe umeshajivalia uislamu katika kusimulia mada zako, lazima usimulie mambo ndani ya stara ya kiislamu
 
Unnecessary pomps from someone who thinks that because he was born in Dar or Tanga or Zanzibar then he is a better and more knowlegeable muslim than those muslims from Kigoma, Kondoa and Tabora. Pathetic "mipasho" style!

Ndio yale yale 'madharau' ya kibaguzi.
Wtu w Bara waliwadharau sana watu wa Pwani kwa kuwaita 'Waswahili' na watu wa Pwani vivyo hivyo kuwaita watu wa Bara: Wabara au Wakuja!

Ubaguzi huu kwa kawaida huendelea kiwango kwa kiwango, Walipobaki watu wa Tanga wenyewe, walidharauriana na wale wa Pwani wakawadharau Wasambaa hata kuja na msemo 'Msambaa mmoja havunji soko'! Huendelea vivyo hata wanapobaki wa dini moja pekee, mfano ni UK ambapo katika 'Ukristo' wao wakaanza kubaguana kati ya Waanglikana na Wakatoliki hadi kusababisha via vya kidini.
 
MM,
Tutafanyaje? wewe huwezi kufanya au kubadilisha chochote! "THE NEW WORLD ORDER" aliyoitangaza Rais wa zamani Ronald Reagan ndiyo hiyo inayowatafuna Waislamu kila mahali kuanzia Guantanamo, Afganistani, Ulaya Mashariki, Mashariki ya kati hadi Afrika!
Wewe kama MM unachotakiwa kufanya ama uungane na Waislamu kusimamisha haki duniani au uwe na Adui wa Uislamu na Waislamu! Either you are with us or you are with the terrorists - YouTube

Kadogoo,

Salaam. Nilipenda saana ile minyambulisho ya masuala ya elimu mlofanya hapa na JokaKuu. Ilikua ni kwa bashasha na ustaarabu mzuri baina yenu. Nafikiri ile pia ni fundisho kwa wengine wenye kupenda kutuumiza vichwa kwa fedhuli zisizo maarifa.

Kwa ufupi nakutumia bayana yangu hii adimu kwako kukufahamisha kuwa si lazim kila swali uwajibu hawa jamaa,mengine waachie wenyewe tu. Najua kuna wakati wanatumia Psychological warfare ili kukuchosha,nawe inakua unaharibu bure effort na energy yako. Niwie radhi najua unayafahamu haya lakini ni uzuri pia kukumbushana.

Nimeona hivi mchana kutwa ulipokua unalumbana nao kuhusu masuala ya udhalimu wa Amerika. Jinsi baadhi yao walivyokua wakikujibu nahisi labda hata hawafahamu kiundani ile inner workings of American Military Complex and Geo-Political Orientation.

Ahsanta na Mola takupia fadhila zako Insha Allah.
 
Nafikiri kuna haja ya kuwapa wasomaji wapya mtiririko wa kwa nini mimi Mag3 ni moja kati ya watu waliowekwa kwenye "shit list" ya Mohamed Said kwa kumuita kwa jina lake halisi...muongo na mchochezi. Nanukuu madai ya Mohamed Said kwenye posti namba 914;
Mtu anayeweza kutoa madai ya uongo kama hayo tumwiteje? Mwalimu Nyerere tayari alikuwa kiongozi wa AA mwaka 1945 akiwa Tabora na mwaka huo huo alifika Dar es Salaam na kukutana na viongozi na wanachama wa AA mojawapo akiwa Dossa Aziz. Sasa, kama Mwalimu Nyerere na Abdul hawakukutana ni wazi kumbe Abdul Sykes hakuwa kati ya vinara wa AA mjini Dar es Salaam...swali la kujiuliza ni je, Abdul alikuwa nani ndani ya AA kabla ya kuvamia ofisi za TAA mwaka 1948 kwa ngumi na mateke? Katika msingi huo huo dai la Mwalimu Nyerere kuingizwa katika siasa na Abdu Sykes, linatokea na kuanzia wapi?


Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi; hapa akili na ujuzi wa Abdul eti unapambanishwa na uhodari katika ubishi wa Nyerere! Nini lengo la Mohamed Said hapa? Kwamba Nyerere pamoja na usomi wake wote hadi kuwa Mtanganyika wa kwanza kuwa na masters ya uchumi kutoka Edinburgh hakuwa lolote mbele ya Abdul mstaafu wa vita vya pili vya dunia?

Mohamed Said haishii hapa; kwa mbali nakumbuka alivyowahi kumponda, Dr. Vedasto Kyaruzi, msomi wa kwanza kuchaguliwa kuiongoza TAA mwaka 1950 Abdul akiwa katibu wake, nanukuu;

Madai yale yale ya dharau katika harakati za kuwainua wazee wake wa Gerezani...eti who was Kyaruzi!... Dr. Vedasto Kyaruzi, Raisi wa kwanza wa TAA wa kuchaguliwa ambaye aliwapa hofu wakoloni hadi akapewa kifungo cha uhamisho mbali na Dar es Salaam. Katika misingi hiyo hiyo Mohamed Said aliwahi pia kubeza mchango wa Raisi wa kwanza muasisi wa AA mwaka 1929, Cecil Matola, na katika njama za kumpa sifa zote baba yake Abdul, Klest Sykes...swali la kujiuliza ni hivi jitihada zote hizi za nini? Anaendelea na nanukuu;

Haya sasa, hapa katibu wa TRAU, msomi Balozi Christopher Kasanga Tumbo hata hatajwi; anatajwa tu baba, Rais muasisi wa Tanganyika Railway African Union, Salum Abdallah! Bahati mbaya katibu hakuwa Manyema wala Mzulu na hakuzaliwa Dar es Salaam. Tatizo linakuja kutokea wakati akina Mag3 wanapokosoa maandiko kwa kuhoji ukweli wa baadhi ya madai, jibu ni hili, nanukuu;

The audacity of it all..."andikeni na nyie" Mtoa mada, Yericko Nyerere, akajaribu kutoa ushauri, nanukuu;

Jibu alilopewa ni hili nanukuu;

???...Hapo ndipo tulipo, Mohamed Said hajaona upungufu wowote katika kitabu chake ingawa mnakasha anadai umemsaidia sana tena sana...kwamba sasa anaelewa kwa nini hata Nyerere hakupenda historia ya wazee wake ijulikane! Na mimi nasema kuwa, kama unayodai ni historia ya wazee wako ndio unayoiita historia ya TANU, basi kumbe hiyo TANU aliyoianzisha Abdul ni tofauti na TANU iliyozaliwa 7/7/1954 na kupigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana mwaka 9/12/1961.

  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes aliwahi kuchaguliwa kuiongoza TANU tangu kuasisiwa kwake hadi uhuru unapatikana.
  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes, aliwahi kusimama jukwaani akiinadi TANU tangu kuasisiwa kwake hadi uhuru unapopatikana.
  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes aliwahi kuwa kiongozi wa juu wa TANU katika ngazi ya taifa, Jimbo, Wilaya hadi Kata.

Mag3, this is a good and helful summary to those who have embarked in this dialogue/ debate few weeks ago.
Your arguments and comments are highly appreciated. Thanks.
 
Mag3, hebu ongeza katika ile orodha yako maarufu ya ''uongo wa Mohamed''. Yaani kila bandiko analonukuu lina chumvi, hamira, magadi soda ili mradi ngano iumuke.

Mo mpotoshaji mzuri sana, vijana wake walitoka mbio wakijua wamempata Nguruvi3. Kila siku huwa tunasema mtu akiuliza swali si kuwa hajui, ana sababu na ufahamu mzuri, hamezi tu kama makinda ya ndege tunduni.

Semina ya bunge ni kuwa sensitive wabunge na jambo fulani kabla ya mjadala. Yaani ni kukutana na wabunge kwa pamoja na hilo si Bunge! Kama ni bunge basi Dau naye keshahutubia Bunge kama alivyofanya A.Mpaunda na wengine wengi sana.

Sasa huwa sijui kama Mohamed ana ufahamu wa mambo haya kweli au anafanya makusudi kupotosha tu.
Halafu hana hata chembe ya aibu wakati anawaingiza ''kingi'' wasomi ! hapepesi macho! Mohamed alivyojaaliwa.
Ndani ya JF anatupa kila taka, hana wasi wasi na kumbu kumbu hizi zinazobaki hapa.
Kitu cha ajabu ana uwezo na anawapata hata watu wenye weledi bila wasi wasi. Wengi tu wanaunga mnyororo.

Mohamed, umeongopa hakuna kitu kama balozi kuhutubia bunge!

Gombe,Big,Baru, Mheshimiwa Ritz, kaeni chini pata funda tatu za maji, nyanyueni nyuso mumuombe mola msaada.
Poleni kwa kujeruhiwa tena. Sio suala la fuata nyuki ule asali, kuna nzi wanafanana na nyuki

Nguruvi3,

Nimejisikia unyonge sana kusoma hayo majambo yako hapo juu,lakini haina neno shughuli na iendelee.

Tafadhali itakulazim unitake radhi kwa kunikatisha jina langu,unajua fika yakuwa mimi ni Gombesugu wala si Gombe.

Mimi kwetu ni vibaya mno mtu kunikatishia jina. Nafikiri wewe pia ulidai hapa jamvini kuwa Sheikh Mohammed Said akutake radhi kwa kukwambia; "hilo neno usirudie tena". Ukadai ya kuwa kwenu Makorora ni matusi makubwa mtu kukwambia vile!?

Ahsanta.
 
Wakati nakunywa juisi ya muwa bariidi kama nilivyo aswa nikasikia sauti ya ngurumo hii hapaNikahisi nahitaji vijiko vitatu vya asali (ushauri wa Ritz) kwasababu mtafiti hakufanya utafiti lakini anabaki kuwa mtafiti kama anavyothibitisha hapaNikimalizia kijiko cha tatu ndipo nikasikia kishindo hiki

Sikumbuki kama ni ile ngurumo au kishindo vilivyonichanganya, ninakumbuka kusikia kwa mbali kama sauti za umati zikigutia liar! liar! liar!Mo stop this, please! case dismissed.

Nguruvi3,

Ndugu yangu tafadhali usipoteze bure maguvu yako kushangilia,mbona hii shughuli bado ni pevu mno. "Ndo kwanza mpopo unaalika maua"

Kwa hiyo tufanye sabra na utuvu,bado mambo ni mengi mno. Nakwambia hivi sababu mimi nakustahi sitaki uje adhirika mbele ya umma halaiki. Nafikiri umenifahamu.

Na pia utafanza vyema ukiwafahamisha jamaa zako wapunguze kidogo tashtit,la si hivyo mtasababisha ile orodha ya Sheikh Mohammed Said iongezeke bila sababu.

Tuendelee na mnakasha.
 
Gwalihenzi;

Najua wewe umeelewa maelezo ya Lisu kupitia nguvu za ufunuo! mimi mswahili mla kashata na gahwa uwezo huo wa kumuelewa Lisu ntaupata wapi? sisi tunateswa na hisi tu!
Kadogoo, wacha kejali, nguvu za ufunuo ndio zipi hizo?
 
Nguruvi3,

Ndugu yangu tafadhali usipoteze bure maguvu yako kushangilia,mbona hii shughuli bado ni pevu mno. "Ndo kwanza mpopo unaalika maua"

Kwa hiyo tufanye sabra na utuvu,bado mambo ni mengi mno. Nakwambia hivi sababu mimi nakustahi sitaki uje adhirika mbele ya umma halaiki. Nafikiri umenifahamu.

Na pia utafanza vyema ukiwafahamisha jamaa zako wapunguze kidogo tashtit,la si hivyo mtasababisha ile orodha ya Sheikh Mohammed Said iongezeke bila sababu.

Tuendelee na mnakasha.

Gombesugu,
Mnakasha umenoga.

Ugomvi ni kuwa Balozi wa Marekani hakuzungumza na Bunge bali
na wabunge wachache.

Sina ugomvi na hilo.
Ninachoshangaa ni kwa nini hili limewahamakisha kiasi kile.

Wanaona aibu kuwa Balozi wa Marekani kufika pale Dodoma au kitu
gani?

Sasa tatizo ni kuwa yale mengine niliyowaambia Waamerika wao
hawana haja ya kuyasikia wala kuyazungumza ila hili la halikuwa
Bunge bali wabunge wachache kama vile ingebadili msimamo wao.
 
Kuna tofauti kati ya kumtukana mtu na kumuelezea alivyo halisi. Mimi nimechambua hotuba yake na nikatoa hoja kuhalalisha kwamba ama alikuwa MNAFIKI au CHIZI. Hayo siyo matusi kwa sababu ndiyo taswira halisi inayochomoka kwenye hotuba yake. Sasa wewe kuniita Mpumbavu bila kufanya uchambuzi wowote wa hoja yangu ili upate uhalali wa kuniita mpumbavu baada ya kuchambua hoja yangu unakuwa huna uhalali wa kufanya hivyo. Unatumia vigezo gani kuniita mpumbavu wakati wewe umeshindwa kujibu hoja yangu?

Najua watu kama nyie mmekulia kwenye familia ambazo wazazi wenu kutukanana nyumbani ni kama sala hivyo sishangai kuamua kumtukana mtu ambaye huna ubavu wa kujadiliana naye. Hayo ni matatizo ya akili ya kawaida sana kwenye jamii hivyo sishangai.

Sasa narudia. Kutokana na hoja yangu niliyoijenga, Nyerere atakuwa ama MNAFIKI au CHIZI. NUKTA.
Safi sana kijana uliyezaliwa katika familia ya waislam safi wenye kumcha Allah! ukafundishwa kujenga kitu unachokiita hoja kwa kusoma hotuba kwa chuki zako na kufikia kutukana matusi matamu ya kiislamu ati mtu mwenye umri wa kumpita hata babu yako tena marhemu ati ni MNAFIKI au CHIZI. Mzee Mohamed angekuwa na chembe ya busara angekukemea mara moja kwamba huo si uislam!
 
Kwani kushika nyadhifa ndio hoja unamjua mtu anayeitwa ABDU JUMBE chunguza mambo yaliyo mkuta ndio utajua baba yako wa taifa alichokifanya kasome kitabu kinachoitwa THE PARTNERSHIP.
Boko, kubishana na wewe ni kupoteza muda, mzee muovu Mohamed Said kesha iua kabisa akili yako. Nadhani anapousoma ujinga wako huu atakuwa anashangilia kwa ushindi alio upata.
 
Gombesugu, nadhani umemsoma Ngongo na Yericko hapo juu.

Lazima watu wawe katika kiwango cha GT. Semina ya bunge si bunge.
Utaratibu wa kuhutubia bunge unajulikana na anayehutubia hualikwa na Bunge kwa mwaliko Maalum.

Mohamed, hajui taratibu za bunge na wala hajui tofuati ya semina ya bunge na Bunge la JMT.
Kama semina ndiyo bunge lenyewe basi nina orodha ya watu wengi sana waliofanya hivyo.
Kuanzishwa kwa mifuko ya jamii akina Dau nao walihutubia bunge.

Msimemeze tu kila kitu kutoka kwa ''nabii''
Mkuu, siumeona walivyopongezana! kwao wao huo ulikuwa ushindi mnono kama ule wa timu ya ujerumani (B.Munich) kuwachapa bao nne Barcelona jana!Ama kweli hasidi Mohamed Said kailamba ilivyo akili ya jamaa hawa!
 
Mag3, this is a good and helful summary to those who have embarked in this dialogue/ debate few weeks ago.
Your arguments and comments are highly appreciated. Thanks.

Wimana,

Ikiwa unapenda turudi nyuma katika kitabu changu na yote nilisema hapa
basi tuanze taratibu nami nakuwekea hii hapa na nitaweka bold kwa msisitizo:

Nyerere alishinda uchaguzi huo dhidi ya Abdulwahid kwa kura chache sana.

Huu ulikuwa ndiyo mwanzo wa Nyerere kujulikana katika siasa zaTanganyika.
Kuanzia siku ile historia ya Tanganyika ikabadilika na siasa zaTanganyika zikachukua sura nyingine kabisa.

Siasa zilichukua sura nyingine kwasababu walingia watu katika harakati ambao waligeuza mwelekeo kudai
haki kwavipaji vya kuhamasisha watu ambavyo Tanganyika ilikuwa haijapata kuona.

Hapa ndipo unapokutana na Titi Mohamed,
[1] Tatu bint Mzee, Said Chamwenyewe,[2] Sheikh Suleiman
Takadir,
[3] na wengine wengi lakini kwa bahati mbaya hawa wote historia imewasahau hawatajwi kabisa.
Nyerere mwenyewe kamwe hajazungumzia kuhusu uchaguzi huu au namna alivyokuja kuongoza TAA Dar es Salaam.

Kiasi cha karibusana alichofika kumhusisha Abdulwahid na historia yake kilikuwa katika ile hotuba ya mwaka
wa 1985 ya kuwaaga wazee Dar es Salaam, na kwa bahati mbaya Nyerere alipojaribu kumueleza Abdulwahid, a
lishindwa kwa kuwa kwa kauli yakealisema hakumbuki cheo alichokuwa akishika Abdulwahid katika TAA wakati
yeye Nyerere alipojiunga na chama mwaka 1952.

Hata hivyo gazeti la serikali, "DailyNews" lilijaribu kurekebisha historia kwa kutaja cheo cha Abdulwahid, ingawakwa
makosa, kwa kusema kuwa Nyerere alipojiunga na TAA makao makuu Abdulwahid alikuwa katibu.

Ukweli ni kuwa Nyerere alimkuta Abdulwahid akiwa rais wa TAA.
Nini sababu ya mparaganyiko huu?


[1]Titi Mohamed alianza kuhutubia mikutano ya TANU katika viwanja vya Mnazi Mmoja kabla
hajamjua Julius Nyerere aliingizwa TANU na Schneider Plantan.

[2]Said Chamwenyewe ndiye liyeitafutia TANU wanachama wa mwanzo kutoka Rufiji alikotumwa
na Abdulwahid Sykes Julai 1954
. Alitoka TANU baada ya kuhitilafiana na Nyerere kuhusu Kura Tatu akamuunga
mkono Zuberi Mtemvu katikaAfrican National Congress.

[3]Sheikh Suleiman Takadir alifukuzwa TANU kwa kumshutumu Nyerere kuwa uhuru ukipatikana
hatawatendea haki Waislam walioupigania uhuru wa Tanganyika. Sheikh Takadir ndiye aliekuwa
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU Dar es Salaam.

 
Una uhakika alihutubia Bunge? au unarudia alichosema Mohammed Said? Kulikuwa na kikao gani cha Bunge kinaendelea Mei 15, 2003?


Nafikiri kiswahili tu hapo kina mapungufu lakin kuzungumza na wabunge katika semina ina nguvu sana kuliko kulihutubia Bunge. Kwani katika semina unapewa nafasi ya kuuliza masuala na hata kujadiliana kitu ambacho katika kuhutubia upati nafasi hiyo ya kuulizana maswali na mtoa mada.

All in all alisema na wawakilishi wa wananchi katika kufanya lobbing ili muswada wake wa Ugaidi upite kilainiiii.

Poleni sana.
 
Safi sana kijana uliyezaliwa katika familia ya waislam safi wenye kumcha Allah! ukafundishwa kujenga kitu unachokiita hoja kwa kusoma hotuba kwa chuki zako na kufikia kutukana matusi matamu ya kiislamu ati mtu mwenye umri wa kumpita hata babu yako tena marhemu ati ni MNAFIKI au CHIZI. Mzee Mohamed angekuwa na chembe ya busara angekukemea mara moja kwamba huo si uislam!

Wewe unaifahamu dini yangu mimi? Nachangia kama Mtu mwenye usongo na nchi yake. Michango yangu humu haina uhusiano wowote ule na na isihusishwe na dini ya Kiislam au dini yoyote ile nyingine iwe ya Kikristo, kipagani, kienyeji, n.k. Hivyo si Mzee Mohamed au mtu wa dini nyingine yeyote yule atakayeweza kunisema kwa sababu michango yangu haihusu dini ya ya mtu yeyote yule.

Wewe ukikutana na chizi ambaye umri wake ni mkubwa kuliko babu yako utamwita nani? Anabakia kuwa chizi tu.
 
Wakati mwingine uwe unaandika kama mtu wa hadhi ya PhD. na wala sio mtu wa kawaida tu!unakuja na chuki zako badala ya uchambuzi wa kisomi! hebu basi tuletee hao wasiomi wakujiamini ambao Nyerere aliwatupa!
Wapo

Wapo wengi sana lakin ngoja nitakutajia wachache ambao umepata kuwasikia.
1. Mzee Edwin Mtei ( nimefanya nae kazi kwa ukaribu sana nikiwa wizara ya Fedha JMTz)
2. Dr (Engineer) Abdullah Salem Al-Harthy) huyu ni aucle wangu ni first Tz Engineer aliyegraduate Barmigham University 1960(Electrical) alikimbilia Oman
3. Mzee Kazibure (huyu aliwekwa kizuizini pale Kibaha Sec kama Mwalimu wakti alikuwa Mtaalamu wa masuala ya mawasiliano angani.


Na wengine wengi tu akina Osca kambona na wengine

 
Back
Top Bottom