Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar




Salam ndugu yangu Wickama,

Nashukuru sana kwa utafiti wako ulioufanya kuhusu kuvunjika kwa EAMWS.Ukipitia vizuri hiyo paper uliyopresent utaona kwa kiwango kikubwa ushiriki wa serikali ya MWL Nyerere katika kuhakikisha kwamba EAMWS inavunjika.Kama ulipitia kitabu cha Dr Njozi cha MWEMBE CHAI KILLINGS AND POLITICAL FUTURE OF TANZANIA utagundua kuwa paper yako inakubaliana kabisa na maelezo ya Dr Njozi akisimulia jinsi Usalama wa Taifa,Radio Tanzania chini ya David Wakati,na magezeti ya serikali chini ya mhariri mkuu Benjamin Mkapa yalivyofanya kazi za kuchochea kuvunjika kwa EAMWS.
Kuhusu kutenganisha siasa na dini hilo jambo haliwezekani,siku zote waislamu tu ndio wanaombiwa wanachanganya siasa na dini lakini tumeona kwenye kitabu cha Sivallon cha Kanisa katoliki na siasa za Tanzania ni jinsi gani kanisa katolilki limekuwa very active katika mambo ya siasa za nchi hii,lakini hatukuona hata askofu au padri mmoja akifukuzwa kwa kuchanganya siasa na dini.Mwaka 2010 tumeona vilevile kanisa likitoa election manifesto kwa waumini wake,sasa hii kama si siasa sijui ni kitu gani.
Ndugu yangu Wickama sisi waislamu hatuna kabisa ugomvi na ndugu zetu wa dini nyingine,sisi ugomvi wetu ni dhidi ya mfumo unaotukandamiza.Leo hii tupo mwezi wa nne tunajadiliana historia ya wanaharakati wa uhuru wa Tanganyika ambao kwa makusudi mfumo haukutaka juhudi zao zijulikane na watanzania.Sisi ambao tumezaliwa muda mrefu kidogo baada ya uhuru kwa kweli tulikuwa hatufahamu kabisa kama harakati za kuikomboa tanganyika zilianza tokea miaka ya 1929,na wala jina la Sykes hatukulipa uzito wowote.Alhamdulilahi sheikh Mohamed mwenyezi mungu amzidishie katutanua fikra na kutufanya tujue vingi sana kuhusu harakati za uhuru wa nchi yetu.


Amani iwe juu yenu.
 
Nguruvi kweli umetuchoka anyway sikukatalii ni mtazamo wako labda kwasababu sisi ni watu wa madrasa kwasababu kwenu mtu akisoma madrasa ni mjinga sanaaa dah safari ni ndefu
Manifestation of inferiority complex!
 


Tupo Pamoja Uthman...
Moh Said katusaidia kuyajua mengi na kuzid kuyatafiti...
 


Kama ni "half baked wasomi" bila shaka ungewapuuza na kwenda zako,cha kushangaza umehamishia hapa kwenye mjadala huu ndan ya miez minne kama sehemu yako ya kula,kuoga,kulala na kuamkia hapa hapa...
unaloliongea moyoni mwako linakusuta sana,ukweli ni vigumu sana kufifishwa kwa style ya kuupinga na kuukejeli...
 
Jasusi
Mbona picha niliyoipata kutoka kwenye simulizi za Mohamed Said ilikuwa kama vile maamuzi ya Rais Mwinyi yalikuwa yakifuata "alichotaka" mkatoliki Nyerere? Au hata Mzee Kitwana Kondo naye alikuwa mkatoliki?!¿¡?

Jasusi,
Ulitaka kujua habari za Chief Marealle na TANU.

Nakuwekea hiki kitu kutoka kitabu changu ''Uamuzi wa Busara:''

Historia ya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kama walivyoshiriki wananchi wa Kilimanjaro
haiwezi kamwe kukamilika bila ya kutaja jina la Yusuf Olotu au maarufu Yusuf Ngozi achilia mbali
mchango wake katika kuipa TANU ushindi katika Uchaguzi wa Kura Tatu.

Jina hili la Ngozi alilipata kwa kuwa alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya kuuza ngozi. Uchagga
ilikuwa chini ya utawala wa machifu waliokuwa wakijulikana kama Mangi.

Kupitia kumbukumbu za Yusuf Olotu ndipo kwa huzuni kubwa utakapokutana na mashujaa waliosahaulika
kama yeye mwenyewe, mashujaa wa kike na wa kiume na wazalendo kama marehemu Mama Bint Maalim,
Amina Kinabo, Halima Selengia, Juma Ngoma, Melkezedek Simon, Gabrieli Malaika na wengineo.

Hawa ndiyo mashujaa ambao kwa muda waliamua wasahau nguvu na utawala wa machifu wao na kujiweka
chini ya TANU.

Yusuf Ngozi alimfahamisha mwandishi kuwa ofisi ya CCM Wilaya, miaka michache iliyopita walimuandikia barua
kumuomba awape nyaraka zake zote za mwanzo kuhusu TANU na awaandikie historia ya jinsi chama kilivyoenezwa
Kilimanjaro na mchango wake binafsi.

Kazi hii aliifanya na akakabidhi nyaraka hizo kwa CCM.

Yusuf Ngozi alimfahamisha mwandishi kuwa alidokezwa kuwa nia ya zoezi hilo ilikuwa ni kuweka kumbukumbu za
mashujaa wa harakati za uhuru ili wapate kuenziwa na taifa na wale ambao hali zao za kimaisha si nzuri wasaidiwe
na chama.

Tuendelee na kisa chetu.

Baadhi ya machifu Uchaggani walikuwa katika Baraza la Kutunga Sheria na kwa ujumla wao walikuwa karibu na serikali
ya kikoloni kuliko walivyokuwa na wananchi wanaowaongoza.

Hali ya siasa katika Jimbo la Kaskazini ilikuwa ngumu na ya kukatisha tamaa.

Wakati TANU inakabiliwa na Kura Tatu mgogoro wa ardhi ya Wameru ulikuwa umemalizika kwa wananchi kudhulumiwa
haki yao.

Japhet Kirilo alikuwa tayari amerudi mikono mitupu kutoka Umoja wa Mataifa alikopeleka madai ya Wameru.

Kirilo hakuwa na chochote cha kuwaonyesha Watanganyika.
Ilikuwa Yusuf Ngozi ndiye aliyeweza kuifanya TANU iingie kwanza Moshi mjini kwa vishindo na kutoka hapo akaieneza vijijini.

Kupitia kumbukumbu za Mzee Yusuf Ngozi ndipo unapokutana na historia za awali kabisa za wanasiasa maarufu waliopata
majina na vyeo na wengine kuwa mawaziri katika Tanganyika huru.

Mfano wao ni Lucy Lameck, Enesmo Eliufoo na wengineo.

Ilikuwa ni Yusuf Ngozi pamoja na wazalendo wengine walioifanya TANU ishinde uchaguzi wa Kura Tatu mwaka 1958.

Yusuf Ngozi hakuwa na elimu bali alikuwa mwananchi wa kawaida aliyethamini utu wa Mwafrika na mtu aliyechukia dhulma
na fedheha ya kutawaliwa.

Kilimanjaro ilikuwa inasifika kwa kuwa na Waafrika waliokuwa na elimu ya juu kabisa katika Tanganyika.

Lakini wasomi hao walishughulishwa zaidi na maslahi yao binafsi. Wengi wao walikuja kujitokeza na kuingia chama cha TANU
mwaka 1958 katika uchaguzi wa Kura Tatu.
Wakati huo mambo yalikuwa shwari na Waingereza walikuwa wamesalimu amri.

Yusuf Ngozi labda kwa kuelewa mazingira ya Kilimanjaro alianza kujenga msingi wa TANU si kwa wanaume bali kwa akina mama.
Hiki ni kitu azizi sana katika historia ya kupigania uhuru.

Katika historia ya TANU sehemu ambazo chama kilipata nguvu kubwa sana ni zile sehemu ambazo kulikuwa na utamaduni wa
Kiswahili wa vyama vya akina mama kama hapo Moshi mjini, Dar es Salaam, Tanga, Lindi na kwingineko.

Yusuf Ngozi aliwahamasisha wanawake wa Moshi chini ya Mama bint Maalim kuipiga vita UTP hadi ikafa.
Wanawake wale walikuwa wakizikusanya kadi za UTP na kumpelekea Mzee Yusuf Ngozi kwenye ofisi ya TANU.

Yeye kama njia ya kuwakatisha tamaa na kuwapiga vita vya kisaikolojia UTP, alikuwa akichukua marundo kwa marundo ya
kadi za UTP na kumpelekea Rais wake Mohamed Badi kumhakikishia kuwa wananchi walikuwa hawakitaki tena chama chake cha
vibaraka.

Jasusi,
Je, umemuona Paramount Chief Marealle?

Nani umeowaona ''front line?''
 

MS,

Unajua ukitaja moshi unanigusa huku kwetu nyumbani ati! naomba unijuzi huyu bwana Gabrieli malaika kama sijakosea ni yule aliekuja kuuguwa halafu akipita mitaa ya moshi kwa mbwembwe huku akiitusi Serikali ya mwalimu na mwenyewe mwalimu?
Ama kuhusu mzee Yusuf Ngozi huyu alikuwa maarufu sana hapa moshi lakini inasikitisha chama kilimsahau kabisa!
 
Hapa niwe mkweli 100%. Kama unatoka Tarime as i do, which i have noticed is an irritation to some, it is unwise to contribute here. Good Luck.
Wickama, naomba kutofautina na wewe kidogo.Iwe unatoka Tarime,Kyela, Marangu au Kashozi na uwe na imani au usiwe nayo unahaki kabisa ya kuchangia maoni yako bila kuingiliwa kwa namna yoyote.

Hakuna, narudia hakuna mwenye haki miliki ya imani ya mtu. Wala hakuna mteule aliyeletwa kuamua nani awe kundi gani.
Tumeona njama za makusudi za kuwagawa watu zinazofanywa na Mohamed Said.Alianza na ''sisi na wao''
Kahamia kwa wazee wa Dar es Salaam, halafu akawagawa Wamanyema, wanubi na Wazulu.

Badaye akaendelea kuwagawa, BAKWATA, Vibaraka n.k.
Kuendelea kukaa kimya au kukubali yaishe ni kumpa upper hand ya kulivuruga taifa achilia mbali waislam wenyewe.

Nina thamini sana mchango wako wa mawazo na kukuthamini kwasababu unasimamia kile kilicho sahihi kwa mtazamo wako na wala si kumeza au bendera fuata upepo.

Asiwepo wa kukutisha eti kwasababu unatoka Tarime.
Nimekupa mifano kuwa nimeishi Tarime na kwingine Tanzania.
Kote huko ni nyumbani kwangu kwasababu Tanzania ni yetu.

Ninashangaa sana hawa wanaosema kuhusu Utarime, eti ndio waislam wanaotaka kufanya daawa.
Hivi kweli kwa kauli hizi watu wa Tarime wanajisikiaje na je yule mwenye nia ya kuufuata uislam akisikia una mipaka na ''wenyewe'' anajisikiaje.

Haya ndio mambo baada ya miaka mingi watu wanalalamika idadi ya waislam inapungua.
Sasa kama hakuna watu wa kuwalingania kumejaa watu wanaodhani Uislam ni Dar na Zanzibar baadaye nini kinafuata.

Naomba urejee bandiko langu moja hapo nyuma. Nimesema Uislam ni dini inasimama kwa miongozo yake timilifu.
Uislam una waislam na waumini. Tatizo lipo kwa waislam kwasababu wengi hawauelewi uislam na miongoni mwao ni hao wanaosema umetoka Tarime.

Haiyumkini kuwa nao wakienda Saudia basi watasema hao wa Tanzania. Kwa upande mwingine ukiwauliza kwanini masuala ya Afghanistan yanawagusa watasema Uislam hauna mipaka. Sasa mpaka wa Tarime umetoka wapi!!!

Ni kujichanganya huku kunakofanywa na ''half baked'' ndiko kunaifanya dini ionekane kwa mtazamo tofauti.
Ukweli ni kuwa hiyo ni mitazamo ya watu na wala si dini ila dini inatumiwa kufikia malengo.

Mfano, utasikia kuwa Nyerere alinyima waislm fursa katika vitengo muhimu. Baada ya muda utasikia mkurugenzi wa anti corruption alikuwa Mwislam. Utasikia kunyimwa fursa lakini hutasikia akiongelewa mwalimu au bwana shamba.

Half baked ndiyo wanaivuruga kila jambo , kwamba wanaweza kutumia kalam zao in wrong way kuchanganya watu.
Big show anasema Nyerere asifiwe japo kidogo kwa kuliongelea suala la udini na ndiye kiongozi aliyewahi kufanya hivyo.
Njozi anasema Mkapa apewe credit kwasababu ndiye kiongozi pekee aliyefanya hivyo.

Gombesugu anasema Kitwana Kondo ndiye alikuwa anaongoza nchi kwa remote.
Mohamed anasema Mwinyi aliwekwa mfukoni na Nyerere.
Total chaos kwasababu kila mmoja anatumia kalamu yake kueleza namna inavyopaswa iwe si namna ilivyokuwa.
 
Vipi wapajua kicheba?
Gombesugu alipomtaja sheikh Hemed Bin Jumaa alinikumbusha nyakati hizo akina sheikh Mwinyiatani wakiuunguruma pale muheza mjini. Jamani udongo unakula vitu!
Na usiseme!.Udongo unakula watu kweli
Masheikh wa Magila na Musoma wote wawajuwa lakini bado huwathamini michango yao.Kumbuka siku ardhi itakapotula na sisi.
 
Kunywa juisi ya miwa kwa maneno yako haya murua!.
 

Uthman,
Nilikusudia kutoa jibu hili kwa sahib yangu Wickama lakini
bandiko lake silioni.

Nataka niseme kitu katika hiyo google scholar.

Habari zote hizo za Sheikh Hassan bin Amir zimenakiliwa
kutoka moja ya mada zangu.

Kabla ya mie kutafiti historia ya Sheikh Hassan maadui zake
walikuwa wamefanikiwa kumfuta katika historia kama walivyofanya
kwa Abdu Sykes na wengine.

Mimi niliweza kukusanya habari zake baada ya kupewa nyaraka za
Bilal Rehani Waikela na kufanya mazungumzonae mwaka 1987
nyumbani kwake Tabora.

Yapo mengi lakini kwa sasa haya yanatosha.
 
Uthman,
Nilikusudia kutoa jibu hili kwa sahib yangu Wickama lakini
bandiko lake silioni.

....
Hizi ndio katika zile zohali za mjadala huu.Hata IE imekataa kusoma javascript za JF kwenye huu mnakasha.Ndio unaona wengi wanakuja na kutoka kimya kimya.Akina sisi tu ndio tumebaki.
Unadhani kutukana masheikh kunapita kimya kimya?.
 
Simulizi zako gombesugu zinafanana sana na za mzee wetu Mohamed. Haziwezi kuthibitika kwa namna yoyote ile. Mwalimu, Mzena na IGP Hamza wote marehemu. Kazi kwelikweli.
 

ndugu yangu UTHMAN,
Awali ya yote ni shukran kwa umakini wako wa kwenda na hoja. Hii natamani kila mmoja wetu angekuwa na mtiririko kama huu. Hii paper ni ya Dr Iddy Ziddy sio yangu. Nikiisoma naona kabisa kwa makusudi aliamua kuacha mapengo katika maelezo yake ya politics zilizomponza Sheikh na EAMWS. Lakini pia pengo kubwa sana ni kuwa hii ilikuwa ni Society ya East Africa. Katika hali ya kawaida kuvunjika kwa wing ya Tanzania kusingeimanisha a collapse pia kwenye nchi zingine. Hili swali nakumbuka Mr. Nguruvi aliliuliza somewhere kwenye hizi threads, sikujaaliwa kuona limejibiwa vipi.

Ni muhimu usijeelewa kuwa maoni yangu yalisema dini na siasa hapana. La hasha. Kwenye maoni nilichosema ni kuwa vile hii EAMWS ilikuwa taasisi kwa ajili ya waislamu kwenye nchi zote za afrika mashariki, kujihusisha actively na local politics za nchi moja nahisi haikuwa sawa. Hii ilitakiwa kuwa jukumu la smaller associations ndani ya nchi husika, na zilikuwapo. On a similar note sitatarajia kuona kwa mfano Jumuiya ya Makanisa ya Afrika Mashariki (kama ipo) ijihusishe actively na U-CCM na U-Chadema. Hii unayaachia makanisa madogo ya ndani kuogelea kwenye bahari yao. Maana yangu ilikuwa hiyo. Hapa tunaweza kutofautiana na sio tatizo. Shukran kwa maneno na lugha nzuri.
 

Kadogoo,
Yule alikuwa akiitwa Malekia ambae alikuwa akivaa sare za jeshi
nadhani ni huyu unaemkusudia.
 
Simulizi zako gombesugu zinafanana sana na za mzee wetu Mohamed. Haziwezi kuthibitika kwa namna yoyote ile. Mwalimu, Mzena na IGP Hamza wote marehemu. Kazi kwelikweli.

Wild Card,
Ikishakua ni historia usitegemee kuwakuta wahusika wa hai.
 

Nguruvi and Many others;
I have seen this many times. Katika kitu ambacho hakiwezi kuninyima usingizi hata siku moja ni INTIMIDATION tactics. Kila mtu hapa ana USERNAME na PASSWORD. Kwa hiari. Akileta hoja anaulizwa anajibu. Tena hapa JF tunapenda na ushahidi ili watu waupime wajifunze. Hakuna Mlemavu wa HOJA humu kiasi kuwa anahitaji askari wa kuwatisha wauliza HOJA au kupiga vuvuzela aaaaaaa YULE MWACHENI. Non-sense. How dare you uwaambia memmbers kuwa yule mwacheni wakati mwenyewe hana tatizo????? Hutaki tradition hii nenda Ilala weka Maspika watu wakusikie hadi jioni kalale. Hapa ni maswali na majibu. Ukitukana haina maana tuache kuuliza. Tukana, kama unapata thawabu kwa matusi basi zitumie siku hiyo ya hesabu. Jinsi wazazi wako walivyofika na kuishi pwani ndivyo na wa wengine walivyofika Tarime na kuishi. Wote huu ni mgongo wa ardhi. Location yako, haikupi ubora wowote, cha msingi taqwa. Usijedhani kwa vile unaishi Madina una ubora zaidi ya mwislamu wa West-kilimanjaro au Lubumbashi.

Kuna uungwana wa kuiga. Nitoe mfano; Barubaru ni mtu MUUNGWANA sana. Anapoona anaandamwa na maudhi yeye hutumia neno POLE SANA (soma threads zake). This is an indication ya maturity. Barubaru hatukani watu humu. Nina jirani yangu BIG SHOW, wenyewe tunajuana vimbwanga vyetu (Big Show, hujaniandikia; Kaa sawa upate Dawah......wewe; kitambo sasa, u-mzima weye? iam missing it already, hahahahaha). We enjoy them, mwisho tunacheka. No insults. Lakini mtu mzima anapotukana watu kwa kule walikotoka and by implication their color then akajiita ni muislamu mimi huwa namuona anaishi enzi za ujahiliya. Hana tofauti na makureishi waliombagua Billal (ra) kwa ule weusi wake. Mzee MS angetukana wangapi? Look at his language. Hata pale unapolazimika kumwambia mzee MS hapa sikubali, bado mnatengana kwa heshima. Kwani ulazima wa kumkubalia kila mtu hoja zake ni upi? Hii ndio maana kuitwa FORUM. You listen, you argue and you leave with your own conclusions. Aliyesema lazima ujue kila kitu ni nani? Hujui unasema hili sikulijua. Kwisha. Hailingani na kuleta matusi au kujaza masimulizi humu (no matter how sweet) ambayo hayana reference na wala huwezi kuya-verify kwa njia yoyote ile. Huku wewe unayaita facts, HOW.

Nguruvi, Hili la dini wala usilihofie. Mwenye kudhani yeye ndiye cream ya uislamu linamsaidia yeye tu. Ni yeye kama yeye. In summary ni kuwa hao mnaowaita humu JF wakina "Abu Jahal" ni kuwa wakiswagwa jehanam, wewe "Muungwana" mtoto wa Sharifu fulani hutapunguziwa maghorofa yako hata keyboard hutanyimwa, sasa vuvuzela za nini? Hapa ni hoja na majibu. Tena bila vitisho. Nice weekend.
 
..sasa unakuwa unawapa nguvu wale wanaougua ubaguzi na udini.

..mimi watu wa namna hiyo huwa nawalipizia heshima na lugha ya staha.

No dear; That was a joke. Iam here to stay (inshallah). I have already responded in Nguruvi's posting. Aiseeeee, JKN alikuwa na kazi kweli kweli. His mistakes notwithstanding, if what i occasionally read here belongs to that generation which directly served under him. Our Idols, the par-excellence workforce. Yet some are NOW putting such pathetic postings (quality), it is beginning to be clear to me why we are so much behind the likes of Kenya.
 

Nakubaliana na wewe ndiyo maana kuna nyakati nilisema gombesugu alikaribishwa na mbwembwe tukajua tumepata
mtoa hoja kumbe mshereheshaji, na kweli baada ya muda ndiyo hayo ya kuita watu habith, mashangingi, mara yule wa Tarime na story ndeefu hata huwezi kuokoteza hoja iliyosimama zaidi ya story za vijiweni.

Mtu anasema Meli ikawekwa Wanajeshi kutoka Zanzibar anasahau Ulinzi ni masuala ya Muungano, mara habari ya Wakubwa kunyang'anyana mabinti... Kifupi hizo ni story ambazo utazikuta vijiweni na nyingi tu.

Usipate shida Wickama, the man is extreemly hatred, na JF inasaidia si unaona anavyotema uchungu wake mwishowe atatulia.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…