Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Wickama nakuwekea kipande hiki uweze tu kujua tulikoanzia na huyu Mohamed Said na ngano zake...

Hii ndiyo mihadhara ya hoja za nguvu aliyokuwa anayofanya Mohamed Said kutokana na eti utafiti wake wa miaka 15 hadi alipotinga ndani ya ukumbi huu na kuanza kupambana na nguvu za hoja za wana JF. Kuna watu walimeza hizi simulizi porojo mazima mazima na wanashangaa kweli tunapojitokeza watu kuupinga uongo na uchochezi wake! Walishamwamini kwani huko nyuma hakuwahi kuhojiwa hata siku moja! Mwaka 1963, chama cha siasa cha kidini AMNUT ilivunjika na ndio wengi wa wanachama wake walianza kutimkia EAMWS. Walioasi TANU kwa kumpinga Mwalimu walifanya hivyo miaka mitatu kabla ya uhuru, waliunda chama cha siasa cha kidini lakini walikataliwa na wazalendo.

Wickama nakuomba usome hicho kipande alichotoa Mohamed Said kwa utaratibu...hutashindwa kuelewa kwa nini akina gombesugu wanaandika wanayoyaandika. Wickama, tulianzia mbali, hayo ya laana ya ugonjwa wa Mwalimu yalisemwa sana na pacha wake Zali la Mentali ambaye kwa sasa ni ajabu haonekani! Nataka tu nikustue kidogo, si dini ni desturi za asili tu za watu...kuna wale utoto huuvaa kama shati hadi uzeeni...ndiyo, ndivyo walivyolelewa. Hawaoni taabu kuogea dimbwini na watoto, hawaoni taabu kukaa vibarazani na watoto kuwasengenya wasiokuwapo...babu kwa baba, baba kwa mtoto, mtoto kwa kwa mjukuu na mjukuu kwa mtukuu! Ndivyo walivyo...Dini ni kisingizio tu.
 

Mag3; Nashukuru sana. Nilikuwa napitia chapters za kitabu cha Dr. Hassan, hasa ile sehemu ya Sakura na mapinduzi ya Zanzibar. To my suprise, yule mzee Mkwawa anachoongelea ni wazenj waafrika kusukumwa na uzalendo wa kujikwamua na mateso na udhalilishaji kutoka kwa waarabu wa unguja na ndio wakajipanga kupitia mapinduzi. Ndipo anaeleza alivyoshiriki na jinsi walivyopata support toka bara (implying JKN) ku-organize vijana kupitia Pangani. Mzee Mkwawa anaeleza jinsi walivyopinduwa kwa kuanzia na silaha za kuwapora wazenj (askari). Hiki kisa hata Ali Muhsin alikisimulia hivyo. More importantly lakini pia anaiunganisha sana na jitihada za kizalendo kwa wazalendo na nia yao ya kulipa kisasi cha muda mrefu DHIDI YA WAARABU. Haongelei ku-attack UISLAM. Okello anaongelea kuuwa WAARABU hasemi kaua WAISLAMU. Yaelekea palinjengeka chuki ya kikabila. Hapa washikaji wanageuza stori, lengo ni kuua uislamu. Hamna anayesemea wahusiano mabaya kati ya waswahili na waarabu (kisa wote ni waislamu!!!!). Unakuja hilo linaloitwa "jeshi la wamakonde", Ajabu majina ya askari waliopata bahati ya kutajwa na Mzee Mkwawa wote ni waislamu. Walioenda kupindua zenj hivyo hivyo. Jamani, awali ilikuwa inawekwa utadhani hawa "makonde" ni wapagani, hawana dini. Hii ni internet age. Kila kitu ni kwenye keyboard. Kitabu ni hiki hapa.http://kwaheri.files.wordpress.com/2010/05/kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru.pdf

Ama kuhusu maradhi ya Nyerere hadi kufariki, frankly ni upuuzi na kutaka kugeuza direction ya debate. Lakini namsubiri Zali la Mentali ajibu maswali matano niliyompa. Nina orodha ya manabii waliougua na hata waliofariki kwa maradhi ya taratibu. Itabidi aniambie na aiambie JF kama hao wanabii pia walilaaniwa. Ni hasara ya taqwa yake na nimeshamtahadharisha. Maanake ubishi wa ushabiki huwa hasara.

Ama kuhusu eti kufariki huku mtu anatumia oksjeni machine kumaanisha marehemu kafa kilaana ni dalili kuwa muulizaji ana ufahamu mdogo sana, ni mjinga na ni msiba mkubwa katika dini hii ya kiislamu mtu kutunza na kusambaza mawazo ya kijinga kama haya. Kwa hiyo waliofariki kabla ya mashine hiyo kuanza kutumiwa ndiyo nini hukumu yao? Nina orodha ya viongozi mashuhuri wa KIISLAMU waliofariki huku wakiwa kwenye machine hiyo. Namsubiri huyu bwana kwa vile naona alikuwa ana hamu ya debate. Mimi nataka alete ushahidi wa maandishi sio porojo. Ndipo tutaelewa kuwa wapiga mbizi chini ya bahari, au wapandaji wa milima kama everest ambao wanatumia mitungi ya oksjeni ni Laanakum. Achilia wasafiri wa anga za juu.

Mag3; huu ni ushahidi kuwa mtu akishaiachia akili yake kujua chuki pekee, Mwenyezi Mungu humnyima uwezo wa kuyatazama mambo kiupana. Huyu Mzee wa Sakura (Mkwawa) anaongelea makafara kama kushona paka macho (ushirikina) kutumika eti kuwapumbaza waarabu wakati wa mapinduzi ya zenj (pg 50-70). Kwenye hizi threads wanajizuia tu kusema JKN ndiye ali-supply hawa paka labda toka Butiama. Ndio culture ya waongo.

Somehow kuna persistent efforts za kuwatia hofu waislamu kuwa hawataendelea bila kuivunja taasisi kama BAKWATA. Katiba ya Jamhuri hii haitakazi ndoto. Washikaji, BAKWATA mtaiacha. Nyie Jitahidini ku-manage taasisi yenu (your EAMWS) MLIYOUNDA. Kwani lazima kila mtu awafate?
 

Wickama, ngoja nitengeneze swali la namna nyingine; ni nchi gani ambayo ina chombo kimoja tu cha Waislamu kutetea maslahi yao; chenye kuunganisha Waislamu wa Madhehebu yote? Misri? Iraq? wapi... kwanini ni Waislamu wa Tanzania tu wanatakiwa wawe chini ya chombo kimoja tu? Ukisoma hapo unaweza kuamini kabisa kuwa EAMWS ndiyo ilikuwa panacea ya matatizo yote ya Waislamu; ni kweli? Lakini mbona Aga Khan aliendelea kufanya kazi Tanzania (yeye ndiye aliyekuwa muasisi na mfadhili mkuu wa EAMWS. Kama Nyerere alikuwa na tatizo na Waislamu wa EAMWS (chini ya Aga Khan) kwanini Aga Khan aliendelea kufanya kazi nchini muda wote wa Nyerere na hata kuja karibu kila baada ya miaka michache na kukutana na Rais Nyerere? Au Aga Khan baada ya kuvunjwa EAMWS hakuwa tena Muislamu kwa sababu aliendelea kufanya kazi na Nyerere?

Ni maswali ya kuchokoza tu ndugu zetu ambao wanajaribu kuililia EAMWS... Hivi ile hospitali ya Aga Khan si imekuwepo nchini kwa muda mrefu sana? na shule ya Aga Khan nayo si bado ipo? WAkati shule binafsi zimetaifishwa si serikali ya Nyerere hiyo hiyo iliruhusu kujengwa kwa Shule ya Aga Khan mwaka 1967 ikiwa chini ya uongozi wa Waislamu wa Ismailiya?

Kwanini wanaozungumzia kuvunjwa kwa EAMWS hawazungumzii kabisa uhusiano wa Imam Aga Khan na serikali ya Tanzania chini ya Nyerere? Ni kweli Nyerere hakutaka Waislamu wasifanikiwe lakini bado akamruhusu Imam (kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu) kufanya kazi mbalimbali za maendeleo?

Unless of course, kina M. Said watuambie kuwa kina Aga Khan siyo Waislamu safi na hawamtambui Aga Khan kama Imam. Which... will bring us back to EAMWS.
 
Wickama, angalia hapo kwenye bold; yawezekana huyo unayemsubiri ni mwanamama!
 
Last edited by a moderator:
 
Wickama hicho kitabu cha Ghassany kimeelezea juu ya Usultani wa Witu?

Sijacheck-chote; Niliangalia zaidi kisa cha Sakura. Ila kama umeshadownload hiyo pdf form sasa tumia search terms kupata kila unachotaka kwa haraka
 
Wickama,
Ni Dr. Ghassany sio Hassan.

Mimi nilikuwa mtafiti msaidizi katika utafiti
wa kitabu hicho.
Mohammed,
Kuna tofauti gani kati ya Hassan (Kiswahili) na Ghassany (Kiarabu)? Isn't it the same name with a cultural alteration? Ndugu zetu Afrika magharibi wamezoea kuita Aminata. Waswahili tunaita Amina. Fatumata. Fatuma. etc
 
Zali la Mentali,

Unamkumbuka Mtanganyika/Mtanzania yeyote aliyewahi kuwa Rais/Mwenyekiti wa TANU taifa hili mbali na Mwalimu?

Rudia tena post yako uliyoniuliza kuhusu upuuzi wa kutaifisha shule wakati MOU ya Serikali na Kanisa inaendana kinyume na usanii huo wa kudai kusambaza elimu kwa watu walioikosa wakati wa ukoloni. Kuvunjwa kwa EAMW kunaendana na kuwanyima haki Waislamu kujiendeleza kimasomo nje ya mfumo Katoliki uliyodhamiria kuwabana kielimu kutumia MOU na mikakati mingine kama ilivyoainishwa na Hayati Kigoma Malima, n.k.

Nimetoka kukuhitaji ujibu hoja kabla hujaniuliza masuali mengine kwenye post hiyo niliyokujibu punde kwa sababu sitaki mtumie usanii kujadiliana na mimi. Kama hamjanijibu hoja zangu za msingi, hamna haki ya kuniuliza masuali mengine kwa sababu maswali yoyote yale mtakayoniuliza sasa hivi tayari majibu yake yako kwenye hoja zangu nilizoziweka hapa.
 

Eti Zali la Mentali haonekani? Soma posts zangu za jana na leo sasa hivi ninazoziposts. WEWE NDIO UMEKIMBIA UWANJA KWA KUSHINDWA KUJIBU HATA HOJA MOJA NILIYOIWEKA MPAKA SASA HIVI. JINGA KABISA WEWE UANAYEKIMBIA KUJIBU HOJA ZA WANAUME WENZAKO (Kama kweli wewe si mwanaume). Mara nyingi nikiwepo humu, ninakuona chini ukiwa live lakini utasubiri mpaka nimeondoka ndipo uanze kuongea utumbo wako.

Sasa najibu utumbo wako uliyouweka hapo juu. Mpango wa kumsimika Nyerere ulitayarishwa na Ukatoliki kupitia wadau wenzake kama CIA (Marekani kama walivyojieleza wenyewe kwamba wanamtegemea Nyerere kusambaratisha Uislamu Zanzibar na wakaweka mpaka blan B kama Wazanzibar wakiyakataa mapinduzi yale haramu. Plan B hiyo ndiyo iliyompa Nyerere kiburi cha kuendelea kuwaua, kuwakandamiza na kuwadhalilisha Wazanzibar na Waislamu kwa ujumla wao alivyotaka na ndiyo inayowapa CCM uhalali bandia wa kuendeleza uuwaji, ukandamizaji na udhalilishaji wa Wazanzibar na Waislamu kwa ujumla wao mpaka leo), Uingereza (Kuleta makomandoo wa kurejesha utawala haramu wa Nyerere baada ya kukataliwa na Wazalendo wakati wa mapinduzi ya 1964) na Ukatoliki kupitia mfumo wao wa kutumia madicteta kuua na kukandamiza watu wasiokuwa Wakatoliki ili waeneze dini yao ambayo haiwezi kuenezwa kwa kutumia hoja bali nguvu.

Suala la Nyerere kuvunja EAMW limeeelezwa wazi kwamba ni maelekezo kutoka Kanisa Katoliki aliyopewa Nyerere baada ya Msimamizi wa Kanisa katika Ukanda wa Africa Mashariki kuwasilisha hofu yake kwa Papa kwamba EAMWS itawafanya Waislamu waendelee kielimu pamoja na mshikamano. Ndipo Nyerere alipopewa maelekeza kutoka Vatican kuhakikisha EAMW inavunjwa. Bila haya wao wana AMECEA ambayo ni taasisi ya Kikatoliki Africa Mashariki iliyojikita katika masuala ya kuwaendeleza Wakatoliki kielimu ukiachilia mbali TEC ya Tanzania. Na AMECEA haijaishia hapo, inaunganishwa hadi Vatican.
 
Barubaru, unanipa pole ya nini? mpe pole nduguyo Zali la mentali anayesema Nyerere ni CHIZI na kuiita hiyo ni hoja inayostahili kujibiwa!

Kwa hiyo kati ya ama UNAFIKI au UCHIZI wewe umechangua kumpa sifa ya UCHIZI si ndiyo? Hoja hii ilijengwa baada ya Nyerere kuamua kujiunga na TAA na kupanda ngazi kwenye chama hicho bila kujua viongozi wa chama hicho ni kina nani na chama kina malengo gani. Acha unazi wa kijinga na elezea kutoka kwenye nafsi yako ili tujue na wewe uko sawa au vipi. Mtu wa aina hiyo atakuwa mzima kweli? Mpaka sasa wakati haujajibu hili swali there is a very fine line between your misbehavior and his.
 
Uingereza (Kuleta makomandoo wa kurejesha utawala haramu wa Nyerere baada ya kukataliwa na Wazalendo wakati wa mapinduzi ya 1964)

Sikutaka kujibizana na huyu jamaa anajiita Zali la Mentali kwa sababu kwanza naona uelewaji wake wa masuala ni wa ajabu sana. Mfano ni hicho kipande nilichonukuu hapo juu kutoka kwa bandiko lake. Kwa hiyo ule uasi wa 1964 ulikuwa ni juhudi za wazalendo kukataa utawala haramu wa Nyerere? Hao wazalendo walikuwa ni akina nani? Na je, uasi uliofanyika wakati huo huo Kenya ulikuwa pia ni juhudi za wazalendo kuukataa utawala wa Kenyatta? Kwa sababu Waingereza vile vile walisaidia kuuzima ule uasi, lakini tofauti na Tanganyika, waliweka kambi za kudumu za kijeshi Kenya. Utajibizanaje na jitu la maoni kama haya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…