Julius Nyerere, lifelong learning and education. One of Africas most respected figures, Julius Nyerere (1922 1999) was a politician of principle and intelligence. Known as Mwalimu or teacher he had a vision of education and social action that was rich with possibility
Mkuu
Nguruvi3, ni hapo ndipo kwa mbali tunapata fursa ya kupima upeo wa baadhi ya watu tunaojadiliana nao humu...kuna hii picha inajaribu kujengwa ya kuwaweka kwenye mizani Mwalimu Nyerere na Abdulwahid Sykes! Inafika wakati hata kunatolewa hoja eti ya kuwapambanisha kwa vigezo vya akili, uwezo na sifa. Ziko hata porojo zinatolewa eti Abdulwahid Sykes alikuwa ana akili kiasi cha kupata pass ya juu ya "first class" katika mtihani wa darasa la kumi! Hii yote inafanyika katika harakati za kumjenga na kumweka kwenye kundi la wasomi wa wakati huo!
Nguruvi3. mtu kufika darasa la kumi miaka ya 1940s ilikuwa ni mafanikio ya kujivunia, siyo tu kwa mhusika bali kwa jamii yote iliyomzunguka hadi kwa shule na waalimu waliomwandaa toka awali. Mtihani wa darasa la kumi la wakati huo ulijulikana kama Territorial Exam ambao ulifanywa na nchi zote zilizokuwa chini ya himaya ya Waingereza...ulikuwa ni mtihani uliokuwa na heshima kuliko hata degree ya sasa inayopatikana nchini kwetu sasa hivi. Mtu aliyeweza kupata "first class" aligombewa kama kuku wanavyogombea mahindi na nafasi za kuendelea zilikuwa nje nje na hazikujali uraia, rangi, dini wala ukabila...ni akili ya mtu tu iliangaliwa.
Kumbukeni pia wakati huo, masomo ya sekondari hayakuwepo, ukishinda vizuri ni moja kwa moja Makerere na kwingineko...ndio maana akina Dr. Hamza Mwapachu, Chief Kidaha Makwaia, Dr. Vedasto Kyaruzi na wengine wengi waliweza kuendelea mbele kwa masomo ya juu bila ubaguzi wowote. Hakuna, narudia, hakuna namna mhitimu wa darasa la kumi aliyefuzu vizuri kama inavyodaiwa kwa Abdulwahid Sykes kupata "division one" angeweza kunyimwa hiyo nafasi na badala yake akapelekwa vitani, hakuna, wakoloni walijali sana elimu na hasa
intelligence ya mtu. Hata wale ambao hawakupasi vizuri kama inavyodaiwa kwa Abdul, walipata ajira nzuri tu katika utumishi sekalini.
Wanajamvi, lengo langu si kumdhalilisha mzee wetu Abdulwahid Sykes, lakini inafika mahala ukweli lazima utamalaki na hapa ni JF. Hata hivyo nakiri kuwa huenda ziko sababu maalum zilizomzuia Abdulwahid Sykes kuweza kuendelea na masomo ya juu zaidi...kama yupo anayeijua sababu hiyo naomba ajitokeze na sote bila shaka tutapima na kujiridhisha kwamba hapo kweli kulikuwa hamna namna. Kwenye miaka ya 1940s, jumla ya Watanganyika walioweza kumaliza darasa la kumi ilikuwa ndogo sana na aliyefaulu vizuri hakuhitaji kufanya jitihada zozote za binafsi kupata nafasi katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.