Mkuu Jasusi, kuna mambo mengi sana yameongelewa na yanayoonyesha jinsi gani imani zinavyowagawa Watanzania.
Lakini pia tumeona msimamo wa Nyerere anayetuhumiwa sana kuwa mkatoliki na kuhujumu imani nyingine, alivyofikia mahali pa kusema hatakwenda Jerusalem akipitia Israel! Kwa maana ya kuwa kwake utu ndio ulikuwa mbele zaidi ya watumia dini ambao waliingia kutaka kumlainisha kwa gia ya dini zao.
Inahitaji moyo mgumu sana kukataa hoja ambazo majibu yake hayahitaji hata darasa bali mantiki.
Kuna kitu kimenigusa sana, nacho ni ile shule ya Temeke.
Hakika wale wanafanya kazi ya jamii na dini na kama ningelikuwa katika position ya serikali ningewasaidia kwa namna yoyote.Wao wanaangalia mayatima halafu wanawapa silaha ya kupambana na uyatima siku za usoni ''ILM'
Tena wamesoma mazingira na kugundua kuwa wanatakiwa wawaingize vijana wao katika dunia ya ushindani.
Kwamba kila mtu apate fursa ili kuweza kuweka level ya ushindani.
Ukimwangalia yule binti mdogo aliyekuwa anaongea, yeye mawazo yake ni kusoma afanikiwe ili aweze kuweka mkate mchana na jioni mezani kwa ndugu zake.
Focus yake ni kufanikiwa na tayari ameshaji tune kwasababu ameona kuwa uwezekano wa kuondokana na hali hiyo ni kwa kupitia kusoma ''nitasoma nipate kazi ninunue chakula.....''
Huyu birnit anahitaji kulindwa tu kwasababu tayari yupo ''fire'' na future yake.
Ndiyo maana kila siku huwa nasema tunahitaji watu wa kuibadili society in positive way.
Kwamba mtu anaweza ku-instill confidence kwa desparate people kama hao watoto walioondokewa na wazazi wao.
Sasa inapotokea vijana kama hao wakaambiwa mafanikio yao yatafifishwa na NECTA kwasababu ya majina au hijabu zao, huo ni upotoshaji wa hali ya juu sana na ni kuwavuruga kimawazo na kuwajengea dhana chafu sana vichwani mwao.
Sakina Datoo ni role model wa vijana wengi na wa aina na itikadi mbali mbali.
Nasema kuwa amejaribu sana na kwakweli vizuri sana kuandaa documentary hiyo.
Ukiangalia mpangilio unapata picha ya mtu aliyefanya homework yake vizuri.
Kuna mapungufu pengine katika maswali lakini hayo ni ya kibinadamu.
Sakina ana hijabu yake na Mwalim Saddika anahijabu yake wote wanaongelea mambo mazito yanayoigusa jamii.
Kwa wale mabinti pale Temeke nadhani yupo aliyesema ''nataka niwe kama Sakina'' hiyo ni motivation kwamba anaweza kuwa Sakina bila kuathiri imani au itikadi yake na akafanya vema tu.
Sasa ukitaka kuwapotosha vijana wale, wakalishe chini uwaambie kuwa kwavile wanavaa hijabu basi chuo chao kikuu kilichokuwa kijengwe mwaka 1968 (hata wengine baba zao hawajazaliwa) ndicho kitakuwa kikwazo kwao.
Bilal comprehensive wameweza kufanya hilo tena katika mazingira magumu.
Wanatoa lishe na elimu hapo hapo kwa kutambua kuwa bila lishe nzuri hakuna elimu.
Kwanini basi Mohamed asifikirie kuwa huenda tatizo la Kilwa nalo linahitaji approach nyingine?
Kwanini watu wasikae chini na kuangalia kulia na kushoto, bali waishie kutengeneza vitabu, CD za matusi na mikoba ya Ibadan kana kwamba hilo ndilo suluhisho la tatizo.
Nadhani video hii imeonyesha japo kwa kiwango fulani kile ninachokisema hapa kuwa tatizo na suluhu ipo ndani ya waislam na wala si katika Uislam au nje ya waislam. Ndivyo wanvyofanya Shia, Ismailia, Bohora n.k.
Sijui kwanini wengine wanasugua vichwa kujenga chuki, farki, uongo hata kubeba mikoba hadi Ibadan Kupitia Murtala Mohamed Airport tena mchana ili hali wanajua wazi kuwa suluhisho lipo mikononi mwa wadau na wala si mtu mwingine.
Hebu msikilize mama Saddika halafu wasikilize akina nani hii.
Utajua kuwa elimu siyo certificate ni jinsi gani unaitumia kukabiliana na mazingira yako.
Kwamba kama kuna mtu anadhani elimu ni ghali basi ajaribu ujinga na kwamba ni wakati wa kutenda si projo, tamthilia, hadithi ngano na mikoba ya Ibadan.
''It can be done play your part''