Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Huwezi kuona kwamba maswali niliyoyauliza kwa Nguruvi3 yana logic ya hoja kwa sababu wewe uwezo wako wa kuelewa mambo ni mdogo sana. Nimekupima kwenye mijadala hii nakuona bado una akili za kitoto sana kwenye kujibu hoja za watu na huna uwezo wa kujibu kitu mpaka uwatumie hao kina Nguruvi3 wakusaidie. Sasa kama wewe huna uwezo mpaka usaidiwe utawezaje kuona kama majibu yangu yana logic au la?

Halafu mtu kama wewe unadai umeandika kuhusu ugaidi na uwezo huo wa kitoto uliouonyesha kwenye huu mnakasha?
 
Umesema vema sana Mohamed, na hakika ndicho watu wanachokitaka kuwa hiistoria iachwe kama ilivyo.

Abdul alikuwa na wakati na mambo yake kama ilivyokuwa kwa Nyerere. Kuanza kuwaweak watu hawa katika mizani ni kuleta ulinganifu wa chungwa na embe kitu kisichowezekana. Tena chungwa na embe ni karibu sana labda niseme ni kiazi na nanasi.

Abdul alikwenda vitani hadi Burma alikoanzisha ''TANU'' na wala hakuwahi kuwa msomi wa kiwango cha chuo kikuu.
Nyerere hakwenda vitani wala Burma, hakuwa mtoto wa mjini 'townmen'', alikuwa mwanasiasa msomi na mwenye maono.
Alikuwa na kipaji chake na kwa namna inayoacha alama ya yeye kutajwa kila siku miaka 14 baada ya kifo chake.

Umejaribu sana kufanya hivyo, eti Abdul ana akili na Nyerere ni debater mzuri. Ukaleta ulinganifu wa mambo kadha wa kadha huku ukijitahidi sana kumdunisha, kumdhalilisha na kumfarakanisha Nyerere ili nyota ya Abdul ing'ae.
Narudia hawa ni watu wenye viwango visivyofanana.

Endapo ungemjibu Mag3 maswali yake ya jana na juzi ungeweza kuona wapi unajikanganya. Hilo ukaona litaharibu kila kitu na umeamua kurukia hoja za spelling.

Historia ipo wewe ndiye unataka kuipindua. Ukweli ni kuwa Abdul Sykes alikuwepo, alikuwa katibu wa TAA na mambo mengi tu alishiriki. Nyerere alikuwepo ndiye alikuwa Rais wa kwanza wa TANU na Tanganyika huru.Ndiye alifanya transformation ya chama
Jaribio la kutaka kumfanya Abdul awe Rais wa Tanganyika linapingana sana na hoja yako ya leo.
Hakuwa na hatakuwa, tunamshukuru sana kwa machango wake.

Kuhusu mnakasha kuwa na matusi, aaah Mohamed ! Matusi umeyaona leo. Wewe ulimshangilia sana Zali la Mentali alipoanza kuporomosha mitusi. Wengine tukakaa pembeni maana ilm hiyo hatuna.

Iache nyuzi ijifunge yenyewe kwasababu matusi umeshangalia yalipoletwa hata sisi wengine tukahoji utu uzima ni dawa kumbe wakati mwingine inaweza kuwa utu uzima ni mghafala.
 
Mkuu Jasusi, kuna mambo mengi sana yameongelewa na yanayoonyesha jinsi gani imani zinavyowagawa Watanzania.

Lakini pia tumeona msimamo wa Nyerere anayetuhumiwa sana kuwa mkatoliki na kuhujumu imani nyingine, alivyofikia mahali pa kusema hatakwenda Jerusalem akipitia Israel! Kwa maana ya kuwa kwake utu ndio ulikuwa mbele zaidi ya watumia dini ambao waliingia kutaka kumlainisha kwa gia ya dini zao.

Inahitaji moyo mgumu sana kukataa hoja ambazo majibu yake hayahitaji hata darasa bali mantiki.

Kuna kitu kimenigusa sana, nacho ni ile shule ya Temeke.
Hakika wale wanafanya kazi ya jamii na dini na kama ningelikuwa katika position ya serikali ningewasaidia kwa namna yoyote.Wao wanaangalia mayatima halafu wanawapa silaha ya kupambana na uyatima siku za usoni ''ILM'

Tena wamesoma mazingira na kugundua kuwa wanatakiwa wawaingize vijana wao katika dunia ya ushindani.
Kwamba kila mtu apate fursa ili kuweza kuweka level ya ushindani.

Ukimwangalia yule binti mdogo aliyekuwa anaongea, yeye mawazo yake ni kusoma afanikiwe ili aweze kuweka mkate mchana na jioni mezani kwa ndugu zake.

Focus yake ni kufanikiwa na tayari ameshaji tune kwasababu ameona kuwa uwezekano wa kuondokana na hali hiyo ni kwa kupitia kusoma ''nitasoma nipate kazi ninunue chakula.....''
Huyu birnit anahitaji kulindwa tu kwasababu tayari yupo ''fire'' na future yake.

Ndiyo maana kila siku huwa nasema tunahitaji watu wa kuibadili society in positive way.
Kwamba mtu anaweza ku-instill confidence kwa desparate people kama hao watoto walioondokewa na wazazi wao.

Sasa inapotokea vijana kama hao wakaambiwa mafanikio yao yatafifishwa na NECTA kwasababu ya majina au hijabu zao, huo ni upotoshaji wa hali ya juu sana na ni kuwavuruga kimawazo na kuwajengea dhana chafu sana vichwani mwao.

Sakina Datoo ni role model wa vijana wengi na wa aina na itikadi mbali mbali.
Nasema kuwa amejaribu sana na kwakweli vizuri sana kuandaa documentary hiyo.
Ukiangalia mpangilio unapata picha ya mtu aliyefanya homework yake vizuri.
Kuna mapungufu pengine katika maswali lakini hayo ni ya kibinadamu.

Sakina ana hijabu yake na Mwalim Saddika anahijabu yake wote wanaongelea mambo mazito yanayoigusa jamii.
Kwa wale mabinti pale Temeke nadhani yupo aliyesema ''nataka niwe kama Sakina'' hiyo ni motivation kwamba anaweza kuwa Sakina bila kuathiri imani au itikadi yake na akafanya vema tu.

Sasa ukitaka kuwapotosha vijana wale, wakalishe chini uwaambie kuwa kwavile wanavaa hijabu basi chuo chao kikuu kilichokuwa kijengwe mwaka 1968 (hata wengine baba zao hawajazaliwa) ndicho kitakuwa kikwazo kwao.

Bilal comprehensive wameweza kufanya hilo tena katika mazingira magumu.
Wanatoa lishe na elimu hapo hapo kwa kutambua kuwa bila lishe nzuri hakuna elimu.

Kwanini basi Mohamed asifikirie kuwa huenda tatizo la Kilwa nalo linahitaji approach nyingine?
Kwanini watu wasikae chini na kuangalia kulia na kushoto, bali waishie kutengeneza vitabu, CD za matusi na mikoba ya Ibadan kana kwamba hilo ndilo suluhisho la tatizo.

Nadhani video hii imeonyesha japo kwa kiwango fulani kile ninachokisema hapa kuwa tatizo na suluhu ipo ndani ya waislam na wala si katika Uislam au nje ya waislam. Ndivyo wanvyofanya Shia, Ismailia, Bohora n.k.

Sijui kwanini wengine wanasugua vichwa kujenga chuki, farki, uongo hata kubeba mikoba hadi Ibadan Kupitia Murtala Mohamed Airport tena mchana ili hali wanajua wazi kuwa suluhisho lipo mikononi mwa wadau na wala si mtu mwingine.

Hebu msikilize mama Saddika halafu wasikilize akina nani hii.
Utajua kuwa elimu siyo certificate ni jinsi gani unaitumia kukabiliana na mazingira yako.

Kwamba kama kuna mtu anadhani elimu ni ghali basi ajaribu ujinga na kwamba ni wakati wa kutenda si projo, tamthilia, hadithi ngano na mikoba ya Ibadan.

''It can be done play your part''
 
Suala la Shariff Attas na Mwalimu Nyerere kama unavyotaka kunisimulia,

Kwanza mimi naona ni ngano isiyo na mafaa kwenye historia ya Tanganyika.

Tujadili ya maana kwanza kisha hadithi za nani alimpa chumvi ama kiberiti zitafuata!
Hapo ndipo mnapokosea sana. Kisa cha Shariff Attas kimewekwa ili tupate mazingatio, kuwa Nyerere alikuwa na tabia ya kuwasahau wahisani wake. Wewe upo kwenye kupeana vitu. Kuwa makini kuelewa maudhui Sio kusoma Kama hadithi simulizi.
 
Mimi napendelea zaidi QASWIDA 😛out:
 
Hapo ndipo mnapokosea sana. Kisa cha Shariff Attas kimewekwa ili tupate mazingatio, kuwa Nyerere alikuwa na tabia ya kuwasahau wahisani wake. Wewe upo kwenye kupeana vitu. Kuwa makini kuelewa maudhui Sio kusoma Kama hadithi simulizi.

Nguvumoja,
Allah ana maajabu.

Hiki kisa cha Shariff Attas alikihadithia siku moja ilikuwa siku
ya Eid el Fitr nimekwenda na mmoja wa watoto wa Abdu Sykes
nyumbani kwake kumpa mkono wa Eid sasa tukakuta wazee wengi
maarufu wa Dar es Salaam wako pale wanakunywa chai.

Hiyo ni asubuhi baada ya kuswali Eid.

Haukupita muda wale wazee wakamtaka radhi shariff wakimwambia kuwa
wamealikwa Ikulu kufuturu na Rais Ali Hassan Mwinyi.

Haukupita muda ukumbi ukawa mtupu tumebaki sisi watatu.

Tukawa sasa tunamtania shariff huku tunamcheka kuwa yeye si lolote katika
watu maarufu wa Dar es Salaam kwa maana hata Ikulu haalikwi siku ya Eid
kunywa chai na rais.

Shariff Attas kwetu ni babu kwa hiyo tunamuogelea tupendavyo.
Yeye akawa anatucheka sisi anasema hatujui kitu.

Akasema, "Mimi kama Ikulu ningeingia kabla ya hawa bwana. Mimi Nyerere
anafika mji huu anajuana na Abdu Sykes mimi niko Sokoni Kariakoo. Nyerere
anakuja kwa Abdu mimi tumejuana pale. Alipoacha kazi na kuja kukaa kwa Abdu
ikawa muda mwingi tunakuwa sote pale na ikifika mchana wakati wa kula tukiongozana
mimi na yeye kwa miguu hadi Stanley Street nyumbani kwa Abdu kula chakula.
Tukafahamiana vizuri kipindi chote kile cha mapambano na Muingereza maana mambo
yote yakizunguka pale kwa Abdu...lakini rafiki yangu siku tulipoonana baada ya uhuru
pale TANU Office akaniuliza wapi tumekutana...alikuwa kanisahau. Mimi nikamjibu kuwa
hatajapata kujuana."

Huu ndiyo mkasa wa Shariff Attas na Nyerere.

Vipo visa na mikasa mingi ya uhuru mingine ya kuchekesha na mingine ya kuliza khasa
mtu akatokwa na machozi.
 
Yericko,
Pole sana.
Hao CIA wengine tumejuananao katika anga za kisomi na wametusikiza
katika mikutano ya kimataifa tukiwapa majibu ya dhulma zao.

Pentagon sijaalikwa lakini nimepita nje na nimeiona.
Ground Zero nimefika...

Wewe unataharuki leo na mambo hayo.
Mimi nimehadhir kwenye vyuo vyao kwa mwaliko wao.

Hivi una kipi wewe katika dunia hii ya wasomi uandike kitu
cha kuwastua Waamerika!

Au huwajui?
 

Mohamed Said,

Kisa hiki ni fundisho kubwa kwetu.
 
Last edited by a moderator:
Cha kushangaza sana ni kuwa kuna baadhi ya watu humu na hata nje ya humu wao rejea zao ni matamshi ya Nyerere. Akisema huyu simjui basi kwao ndio uhalisia wenyewe huo ambapo sio kweli. Sasa kwa mfano huu wa Shariff Attas tunatakiwa tuamke na kutafakari upya maneno meeengi ya Nyerere.
 

Sioni sababu yakuganda hapa,

Kuhadhiri katika vyuo vyao si jambo laajabu,

Lakini nakueleza kuwa nimefika Pentagon kwaajili ya hiyo ngano yangu,

Nimeonana uso kwa uso na Bob Bequen, Mayers na waambata wengine ndani ya pentagon!

Maandishi yangu yamekuwa lulu kwao kiasi cha wao kuniomba haki shiriki kwa kukidurufu kwa lugha sita duniani kutoka lugha mama ya Kiswahili!

Haya sio mafanikio yangu bali ni waswahili wote ukiwemo wewe!
 

Mohamed Said

Wewe ni mwanazuoni na unajiita ni mwanahistoria,

Kisa hicho kina nguvu gani kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika?

Shariff Attas alishiriki vipi katika harakati za uhuru zenye nguvu ya kusimulia vizazi vyetu vya kesho?

Tusiweke porojo kwenye masuala nyeti ya nchi hii mkuu!
 
Ahsante MS kwa history unayotuweka hapa mengi tulikuwa hatuyajui lakini sasa tumeyaelewa japo kwa ufupi kwa hisani yako huyu shariff Attas alikuwa ananyadhifa gani ktk Taa au Tanu?
 

Yericko,

Hayo maswali yako machache hapo juu, inaashiria yakuwa kuna vitu huvijui. Na kwakuwa huvijui wewe au wenzio haina maana yakuwa havikutokea,havikufanyika au ati havina umuhimu kwenye Historia ya Tanganyika/Tanzania. Ndo maana ni muhimu kitaaluma umpe fursa Sheikh Mohammed ili akujuze. Halafu baada ya hapo ndipo tutayakinisha huo ukweli na kunyambua kwa kina kama hivyo vitu vina umuhimu wa kuwamo kwenye "Historia yetu".

Lakini unapomwandama Sheikh Mohammed kila kukicha yakuwa analeta porojo,huoni yakuwa unajipunja kwa usoyajua!?
 
Ndugu yangu Yericko sidhani kama ni busara sana kufurahia kwamba maandishi yako yamekuwa lulu kwa Wamarekani.
Hawa ndugu zetu ni mabeburu hawaoni tabu kutumia hila zozote kufikia malengo yao.Hawana rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.Tukikumbuka si zamani sana walimweka Mzee wetu Nelson Mandela katika list ya magaidi hatari,na wao wakashirikiana na makaburu kufanya madhila mengi kwa waafrika wenzetu.Mara tu baada ya makaburu kusalimu amri na Afrika kusini kuwa huru walibadilika na kurudi kumsifia sana Mzee wetu Madiba mpaka kumtaja kama kiongozi wa mfano duniani.

Usivutiwe sana na sifa zao ndugu yangu huenda wameona unafaa sana kwa sasa kueneza propoganda zao za ugaidi.




 
Ahsante MS kwa history unayotuweka hapa mengi tulikuwa hatuyajui lakini sasa tumeyaelewa japo kwa ufupi kwa hisani yako huyu shariff Attas alikuwa ananyadhifa gani ktk Taa au Tanu?

Isalia,
Shariff Attas hakuwa na wadhifa wowote katika TAA wala TANU ukitoa kuwa alikuwa mwanachama
na mmoja wa wanachama wa mwanzo katika TANU.

Yeye alikuwa dalali wa Soko la Kariakoo ambako Abdu Sykes ndiye alikuwa Market Master.
Hii ilikuwa 1950s kipindi cha mapinduzi katika TAA na wakati Abdu yuko katika pilika ya kuasisi TANU.

Lakini umuhimu wa Shariff Attas kwanza ni kuwa alikuwa mmoja wa wanamji na kubwa zaidi soko zima
lile likiendeshwa na watu maalum katika kila biashara.

Kwa ajili hii palikuwa na fedha za kutosha kuingizwa katika harakati.
Sasa hapa ndipo unapomkuta Mshume Kiyate dalali wa samaki.

Mshume alihodhi biashara hii na alitajirika kiasi kuwa aliweza peke yake kujitolea kumuhudumia Nyerere kila
kitu hadi uhuru ulipopatikana.

Hata Nyerere alipomwambia Mzee Mshume kuwa sasa apumzike yeye atahudumiwa na serikali Mzee Mshume
alimgomea Nyerere akamwambia, "Mimi nataka wewe na wanao mle chakula changu na hicho cha serikali wape
wageni wako."

Yapo mengi ya hawa wapigania uhuru waliosahaulika.
In Sha Allah tutaambizana kila nafasi ikipatikana.

Unajua ile dua ya akina Jumbe Tambaza walomfanyia Nyerere yeye hakuwa wa kwanza katika viongozi wa TANU
kufanyiwa.

Ile dua wa kwanza kufanyiwa alikuwa Abdu Sykes.
Sijui kama wanajamvi wangependa kusikia mkasa huu.
 

Nguruvi3,

Kwa sababu umevunja ile "miadi yetu",adhaba yako ni mijeledi khamsa mia wa sitiini. Na italazim hiyo mijeledi uchapwe mbele ya hadhara pale kwenu Makorora. Na huo "mchozi" utageuka machozi!!

But in a serious note; Nguruvi3 haya mambo ya kumtafir roho yake mtu mzima mwenzio hayana maana na wala hayajengi ni kuzidi tu kuleta nakma na machafuko baina yetu.

Sheikh Mohammed,anajaribu mno kukuepuka na wala hakutaji asilan hilo jina lako. Sasa wewe kwanini hutumii busara na "ustaarabu" wa kwenu Kicheba ili kurahisisha mambo hapa jamvini!?

Jaribu kuchukua mfano wangu kiduchu;mimi ni mgeni saana hapa jamvini/JF lakini unaona hapa kashfa ninazopewa. Ni aghalab ati kunikuta nimemjibu Mwanaharasha yeyote,labda inaponilazim kumnyooshea mtu maneno kiduchu!

Tafadhali kuwa na stahamala na utumie staha ya kitaaluma unapotaka kuzungumzia na Sheikh Mohammed.

Shukran.
 

Huo ni sehemu ya mtazamo,

Lakini si kikwazo kwa walimwengu kufanya jambo likavutiwa na Amerika!

Huwezi kuacha kuiidarasisha dunia kwakuwa Amerika wameunga mkono kile ukifanyacho!
 

Ndugu

Katika michango yako ya mwanzo kwenye uzi huu nilikutazama na kukutafasiri kama mmoja wa wanazuoni na mbobevu wa fikra za nera!

Lakini kwa aina ya ujumbe unaochangia kadiri mjadala huu unavyosonga ndivyo unavyonipa picha ya watu wa aina ya "ndio mzee"

Sitaraji na siamini kamwe kwa msomi na anaesimamia elimu yake ataunga mkono hadithi ya Atass kuwa ni sehemu ya historia ya uhuru wa nchi hii!

Kwanza nikujuze kinyume na Mohame kuwa huyo aitwae Sharif Atass hakuwa na "URAFIKI" na Mwalimu Nyerere kiasi cha eti mwalimu aishi miaka yote akimuweka akilini!

Hivi haikuingii akilini kuwa Mwalimu angemuweka akilini Sharif kwa lipi?

Kwakupiga ngano wote pale Kariakoo?

Jiulize Sharif Atass ni nani kwa Nyerere mpaka kiwe kisa chakusimuliwa na kiwe sehemu ya historia ya uhuru?

Ndugu yangu jisimamie kama ulivyoingia mwanzoni usibebwe na hisia!

Mjadala huu ni mzito kwakuwa ili uuelewe inakubidi hisia zako za kidini uziweke kando jambo ambalo wachangiaji wengi limewashinda na wewe ukiwemo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…