Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Unaposhindwa kujibu hoja za unaowaita wafuata upepo hapo ndipo unapodhihirisha utoto wako kwenye mjadala. Ukikua utaacha. Kina nguruvi3 na Jasusi unaowategemea wameamua kuingia mitini kujibu hoja walizowekewa mezani kwao wamebaki kugona LIKE kwenye kujikanyaga kwako!!!!!!!!!!!! Wanakusubiri ukue!!!!!!!!!!!!!!
 
Mohamed, wewe ungekuwa unafaham itifaki ungaliweza kusimama katika JF na kusema balozi kahutubia bunge! Kama Yericko ataingia katika list ya vikaragosi nadhani atakukuta ukiwa umeshatangulia

Nguruvi3 be honest. Hivi kwenye hoja zote ulizoulizwa mpaka sasa hivi wewe na ambazo hujazijibu wewe umeamua kukomaa na hii hoja ya kitoto ya ama mtu kalihutubia bunge au kaliamrisha lifuate sheria ya ugaidi?
 
Nguruvi3 be honest. Hivi kwenye hoja zote ulizoulizwa mpaka sasa hivi wewe na ambazo hujazijibu wewe umeamua kukomaa na hii hoja ya kitoto ya ama mtu kalihutubia bunge au kaliamrisha lifuate sheria ya ugaidi?

Ndugu yangu.

Umekomaa kuwa unazohoja ambazo hazijajibiwa,

Zipo wapi?

Ukiona hoja haijajibiwa ujue sio hoja bali ni kihoja!

Sasa watu werevu huwa hatujibu vihoja, tuna ignore tu!

Kama unajiweza jibu yale ya akina Shariff Attas aliyoyakimbia Mohamed Said,

Lakini jibu kwa adabu ili tusonge mbele!
 
Uchafu alioufanya padre umeuona?

Nimeyaweka hayo pamoja ili kuwaamsha wapigania dini kwa pande zote kuwa wapiganie kwanza kusafisha madhaifu yao ya ndani kisha waje huku nje!

Ikiwa hujapenda hilo kulijua basi huo ni sehemu ya udhaifu wako mkuu!

Si ungeuweka na wa Nyerere?
 

Ndugu yangu. Utoto unajidhihirisha wazi kwenye swali lako. Umesahau kwamba mimi ndiye niliyekuambia kwamba Shariff alitumika tu kama subject wa kuelezea unafiki wa Nyerere kwa maana ya kwamba amejifanya hamjui baada ya mambo yake kumyookea na sio kwa sababu anastahili kuwa kwenye historia ya Uhuru wa Tanganyika? Nilitegemea ungejibu hilo swali lakini unarudi hapa na kunitaka nijibu suala la Shariff. Itabidi niige msemo wa Mzee Barubaru. Pole sana.
 
TUNAINGIA VITANI.

Powell na watu wengine miongoni mwa washiriki wake walikuwa wametumia masaa mengi na waandishi wa jarida la Times wakijaribu bila mafanikio kuwajulisha kwamba habari waliyoandika haikuwa ya kweli.

Lakini Powell na Armitage walifahamu nguvu iliyokuwepo Washington ambako kuibuka na kuanguka kwa umaafuru wa mtu ni jambo jepesi.

Tatizo lilikuwa kwamba msimamo huo wa habari hiyo ungeonekana kuwa ndiyo ukweli hata kama haikuwa hivyo. Tatizo kubwa zaidi lilikuwa kwamba habari hiyo kwa sehemu fulani ilikuwa ni kweli.

Powell alikuwa haanzishi sera mpya ya nchi za nje alikuwa akipangiwa majukumu ya kufanya na alikuwa akikabili migogoro midogo mmoja bada ya mwingine. Lakini kama alivyowahi kusema mara moja katika faragha, “ili kuweza kuendelea bila matatizo katika ngazi za juu lazima uwe mjanja katika mchezo wako.”

Alipokuwa mwenyekiti wa jopo la Wakuu katika jeshi aliwahi kuandika baadhi ya misemo aliyokuwa anaipenda zaidi na kuipenyeza chini ya kioo kilichokuwa juu ya deski lake katika makao makuu ya Wizara ya Ulinzi.

Moja ya misemo hiyo ilikuwa “kamwe usiwaruhusu wakwambie kwamba unatapa tapa”.Rais Bush alikuwa akiwahutubia wanafunzi katika shule ya Emma E. Booker Elementary School huko Sarasota Florida wakati Rove alipomjulisha kwamba ndege moja ilikuwa imeubamiza Mnara wa Kaskazini wa kituo cha biashara cha kimataifa mwanzoni ilionekana kuwa tukio hilo lilikuwa ajali au labda kosa la rubani ambaye huenda alikuwa na mshitulo wa moyo, Bush alifikiri.

Alikuwa amekaa kwenye stulu darasani akiwa amevaa suti yenye rangi nyeusi shati la bluu na tai nyekundu, Ubao mdogo wa ukutani uliokuwa nyuma yake ulikuwa na maandishi yasemayo “ Kusoma kunaifanya nchi istawi”.

Andrew H. Card Jr mnadhimu wa Bush na msaidizi wa zamani wa Reagan na Bush mkubwa aliingia na kumnong’oneza rais huyo moja kwa moja sikioni mwake “ndege ya pili imeubamiza mnara wa pili, Marekani inashambuliwa”.

Picha ya hali iliyotokea wakati huo imebakia katika historia, mikono ya rais huyo ilikuwa imekunjwa juu ya miguu yake wakati anageuka kusikiliza maneno ya Card. Uso wake ukawa na sura tulivu kwa mbali japokuwa kulikuwa na mshituko pamoja na kuchanganyikiwa. Bush anakumbuka vizuri kabisa alivyokuwa, ‘nafikiri watu hawa wametangaza vita dhidi yetu, na nimeamua wakati huu kwamba tunaingia vitani.” Alisema Bush.

Bush aliamua kwamba alihitaji kuwaeleza wananchi wake mambo kadhaa.

Saa 3.30 asubuhi alitokea mbele ya kamera za televisheni katika kituo cha habari cha shule hiyo ya Booker ili kutoa taarifa yenyewe. “kwa nini niliyarudia maneno hayo hayo
labda huo ulikuwa ni mwangwi wa matukio ya nyuma” rais huyu alisema baadaye. “Sifahamu ni kwa nini nitakueleza ukweli kwamba hatukukaa kuyapanga maneno haya. Nilisimama na kujikuta nikiyasema. “Mlichokiona ndiyo hasa mimi mwenyewe nimeonyesha hulka yangu.” Msururu wa magari ya rais huyo kwa kasi ulielekea kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Sarasota Bradenton. Alichepuka haraka akipanda ngazi na kuingia katika chumba cha ofisi yake ya faragha ya ndege yake ya serikali ya Air Force
One. “hakikisheni mke wangu na mabinti zangu wanalindwa” hiyo ndiyo ilikuwa amri yake ya kwanza kwa maofisa wa vyombo vya upelelezi.

“Bwana Rais alisema mmoja wa maofisa hao kwa unyonge, “tunataka ukae haraka iwezekanavyo.” Bush alikaa kitini na kujifunga mikanda na ndege ikaanza kuondoka taratibu na muda si mrefu ikapaa angani kwa kasi.

Mke wa Rais huyo Laura Bush akiwa amevaa suti nyekundu na mikufu miwili ya mapambo ya lulu shingoni mwake alikuwa katika chumba cha Caucus katika jengo la Ofisi ya Seneti la Russe mjini Washingtoni akiwa tayari kutoa hoja kuhusu watoto kuanza elimu mapema mbele ya kamati ya Seneta Robert M. Kennedy mara wakapata habari kuhusu ajali hiyo na bibi Bush, Seneta Kennedy na watu wengine wakaondoka kupitia mlango wa pembeni. Baada ya maelekezo ya tukio hilo Bibi Bush alifanya juu chini kujituliza. Uso wake ulipauka mara moja machozi yakimlenga na midomo yake ikitetemeka kwa woga.

Kisha makao makuu ya jeshi la Marekani yakashambuliwa, na wapelelezi na polisi wa kamzingira. Walimweleza nia ya kumpeleka katika eneo lenye usalama. Kundi hilo mara moja likaondoka haraka. Saa 3.50 Bibi Bush alikuwa akisubiri watu wa kumsindikiza katika msongamano wa magari kutoka jengo la bunge la Seneti (Capito), ilichukua dadika 45 kumfikisha kwenye makao makuu yake na alipelekwa katika chumba cha mikutano cha Wood.

Saa 4.51 ndipo vyombo vya usalama vilipoamua Kend kumficha katika Ofisi ya New Havana mtu mmoja aliyejuliakana kwa jina la Turquoise ambalo lilikuwa jina la siri la Barbar Bush Bint wa rais huyo aliyekuwa na umri wa miaka 19 akisoma huko . Twinkle jina jingine la siri la binti mwingine pacha wa Rais Bush. Akiwa anasoma Chuo kikuu cha Texas huko Austtin alipelekwa kufichwa katika Hotel ya Driskill dakika sita baadaye.

Ilikuwa saa 3.39 asubuhi ambapo ndege ya America Air lines Safari namba 77 aina ya Boeing 757 ilipobamizwa katika jengo la makao makuu ya jeshi la Marekani. Dakika tano baadaye aliweza kuwasiliana kwa simu na makamu wake wa rais Dick Cheney ambaye alikuwa amekimbizwa kutoka katika ofisi yake ya upande wa magharibi na maofisa wa usalama na kupelekwa katika kituo cha shughuli za Dharura cha Rais (Presidential Operations Center - POC) ambacho ni handaki maalum la dharura lililo chini ya viwanja vya Ikulu.


Kutoka

"Vita Dhidi ya Ugaidi"

Na Yericko Nyerere
 

Unajua kuchanganyikiwa sio lazima uokote makopo. Hivi post yako hii ina uhusiano gani na mnakasha wetu hapa?

Kama umeanza kutupa vipande vya kitabu chako kuhusu Ugaid, basi fungua mnakasha mwingine ili tumtendee haki Mzee Mohamed Said ambaye mada hii iliwekwa ili kumshambulia yeye kwa sababu tu ya kuelezea historia ya Tanganyika iliyopaswa kuandikwa.
 

Kuna sehemu nilikuambia kuwa mnakasha huu ni mkubwa kwako,

Nivigumu kuuelewa, jaribu kuwa msomaji tu!

Hujui tumetoka wapi, tumepita wapi, tupo wapi na tunaelekea wapi!

Machipuzi sahihi ya fikra nikujituliza nakuwa msomaji ama kuomba ufahamishwe kwa adabu!

Muulize Mohamed Said zile pepa za Ibadan aliziweka hapa za nini?

Atakujibu na kukufunda bwana mdogo!
 
Yericko sasa si bora uanzishe uzi mwingine?
Utupe hilo darsa lako la kucopy na kupaste?...
Lol..
 

Unajua Yericko sio lazima uufatilie mnakasha wote ili uweze ku assess logic ya mtiririko wa mahojiano. Hapa kuna maswali mengi tu hujayajibu. Unapoamua kurukia kwenye suala lingine kabla hujajibu maswali yaliyopo mbele yako, ndipo hapo dalili za kuchanganyikiwa zinapokuwa wazi.
 



Huna lolote,sisi tupo nawewe hapa tokea mwanzo wa page,anachokisema zali la mentali kipo sahihi kabisa,usikimbie hoja ya uchochez uliyoianzisha wewe mwenyewe kwa kutuwekea hizo copy n paste zako...
Kama umeshindwa,tangaza rasmi kisha tumpe fursa mpya Moh Said ya kuzid kumwaga historia hapa...
 

Kweli ni wazimu wa hali ya juuu sana...
Yan hata hajielewi anasimamia kitu gani huyu bwana mdogo yericko...
 

Ndugu zanguni

Leteni hizo hoja mnazodai "nimezikimbia"

Nipo tayari kuzijibu ilimradi ziwe ni hoja na sio vihoja!
 
Yericko naona umechoka sana. Nikuache kwa sasa. Tutaonana wakati mwingine.
 
Mojawapo ni kwamba uliweka kashfa za Padri na Sheikh wa Madrasa. Nikakuuliza na ya Nyerere vipi?

Heheee daah!

Dunia hii,

Utumwa mkubwa katika dunia ya leo ni ule wakukosa AKILI!

Ndugu zangu wanajamvi,

Hawa ndio watu ninaojadiliana nao hapa tangu jana,

Wanasema mimi nimekimbia hoja zao,

Lakini nilipoamua kusikiliza kilio chao wameniambia hoja zenyewe ndizo hizo hapo juu,

Siwalaum, bali nawasikitikia tu!

Ninawaomba endeleeni kutulia katika uzi huu kwakuwa dhamira yangu nikuwatoa kuzimu mlikowekwa na Mohamed Said
 
Ndugu zanguni

Leteni hizo hoja mnazodai "nimezikimbia"

Nipo tayari kuzijibu ilimradi ziwe ni hoja na sio vihoja!


1.kuhusu nasaba yako achana nayo,,

mimi nataka uanze na zile FIVE ESCAPE ROUTES ZILIZOKAA PENDING HADI SASA,,

gombesugu kawalalamikia sana mtolee majibu kimya hadi sasa,

Naomba tuanze na hizo kwanza,,

shukran
 
Ndugu zanguni

Leteni hizo hoja mnazodai "nimezikimbia"

Nipo tayari kuzijibu ilimradi ziwe ni hoja na sio vihoja!

Ndugu zangu Zali la Mentali,The Big Show,Mzee MS,Kadogoo,Ritz,Gombesugu huyu Yericko mpaka sasa hajamgundua"UBONDIA ANAUTAKA LAKINI ANAOGOPA MANUNDU"
 
Big show, nisetirike na nini wakati nipo katika list ya ''shit'' ya Mohamed Said? Ninyi mnaolirudisha hili jambo ndio mnaokusudia kumvunjia heshima Maalim. Uzuri wa JF ni rekodi na hapa naweka rekodi bila kusema neno.
Mzee Mwanakijiji[/B];6202686]Balozi wa Marekani hajawahi kuhutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano; niko tayari kusahihishwa. Lini Balozi Royall alihutubia Bunge la Tanzania? ili tupitie hansard.
Nguruvi3: Ndugu yangu yaani nilipatwa na mshutuko kusoma kuwa balozi wa Marekani aliwahi kuhutubia bunge. Afadhali umelileta.Mohamed Said, Balozi wa marekani alihutubia Bunge lini?
R;6205436Balozi Royall alihutubia bunge la Tanzania tarehe 15 May 2003
gombesugu;Ami,Nahisi pale umeona kuwaNguruvi3,anataka kutumia technicalities almurad awe hajakosea! Ahsanta Al Akhiy kwa kugundua hicho kitu na ku-highlightkwa haraka!ahaha!
Kadogoo;6206393 MZEE MWANAKIJIJI;Haya umepata jibu lako kuhusu Balozi wako! ndio ulitaka kusema nini vile

Ukisoma ni dhahiri kuwa waungwana walijaribu sana kumueleza Mohamed kuhusu itifaki za bunge.
Badala ya kuelewa, Mohamed Said kwa kudhani hapa ni mahala pa kumeza akaanza kashafa, jeuri, dhihaka, kejeli na tambo zake za kawaida.

Amethibitisha kuwa paper aliitoa Ibadan. Ni wazi alisafiri hadi huko akiwa na mkoba wake(Nimeshauriwa nisitumie ile terminology maarufu unless mtu aulize)

Akathibitisha kuwa balozi alihutubia tarehe hiyo hapo juu.
Ni wazi alikuwa si hakimu kiruka na alifanya utafiti mdogo tofauti nasisi tulioshindwa.

Akaeleza kuwa paper ya Ibadan ndiyo ilimfanya akamatwe!
leo tunajua hakukamatwa kwasababu hiyo kwavile balozi hakuhutubia bunge na hakukuwa na mzozo naye!

Angalia hapo chini orodha ya vijana waliojitoa kimacho macho kutetea upotoshaji wa Mohamed.
Hawa ni wale wachache sana walioko JF, kuna maelfu masikini ya wangu walimeza tu kwa kuogopa kuuliza maswali ili wasiwe hakimu kiruka.

Hili jambo limetokea miaka 10 iliyopita na lipo hivi, je yale ya nusu karne kuna nini ndani yake.
Sasa mnaonishambulia kuwa hili jambo limetolewa clarification, hiyo si kweli.
Limetolewa hukumu ambayo ni tarehe 15 may 2013 na Mohamed Said.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…