Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Mbona unamatatizo sana yakuelewa ndugu???

Mohamed Said amesema balozi alilihutubia bunge la jamhuri, Mimi nimesema ni UONGO

Balozi aliteta na baadhi ya wabunge wa ccm katika kisemina elekezi kilichofanyika ukumbi wa pius msekwa pale Dodoma!

Hakulihutubia bunge, tofautisha mambo haya ndugu!
 
MOHAMED SAID,Umenikumbusha home! Mishikaki na mikate ya Matrani hotel ya Marehemu Nasibu ilikuwa maarufu sana! Watoto wa Mzee Nasibu wameacha biashara ya chakula kwa kufungua maduka! mikate ya Matrani ni mikate ya mchanganyiko wa nyama na mayai ya kienyeji! Kwa hapo Moshi Wachaga wanaipenda sana wakipata na mishikaki!any way ntaagiza toka New Nasibu Restaurant mtaa wa Sokoni bondeni na utapokea baada ya masaa 4 tu! tena tutakuwekea ndani ya jokofu maalum ndani ya basi ili mishikaki isishambuliwe na bacteria! Akina Jericko wakifika tu, kumbuka kupasha moto mishkaki na ntakuchanganyia na mikate ya Matrani ili jamaa zako watabaruk!Kuhusu kuagiza pipa la Juice ya bakhresa nakushauri pia agizia dramu la Coca Cola au Pepsi ili kama wageni wako wakivimbiwa wapate kucheua! haaa haaa!
 

ahsante kaka.tuendelee na mnakasha
 

Acha unafiki wewe leo hii tarehe 12/05/2013 ndiyo unajifanya kukemea hizo kauli Mohamed Said anatolewa maneno ya kejeli, matusi, dhihaka na maneno ya kifedhuri hata siku moja ujasema chochote.

Wewe kaa kimya waache wenyewe wapambane.
 

Yericko mbona huyu hamumfundishi adabu au mumesahau ule usemi wa wathungu "CHARITY BEGINS AT HOME"ondoeni uchafu kwanza kwenu kabla kwenda kwa jirani au kwasababu ni "home boy"
 

Ndugu kwa hiyo balozi aliteta na wabunge mpaka wakubali kupitisha sheria ya ugaidi?
 

Hata wewe una "shit list"?!

Maajabu hayajawahi kuisha kwenye huu uzi

Zali la Mentali isingekuwa lugha yake basi anaweza kuwa na umuhimu sana kwenye huu uzi na hata kuongea hayo lakini sio wewe.

Tunakusoma lakini usijejisikia vibaya
 
Last edited by a moderator:

Suala la mapinduzi ya Zanzibar tulishalitolea maelezo na kuelezea jinsi mapinduzi hayo yalivyopangwa kwenye ngazi ya East Africa yakifadhiliwa na Marekani wakati George Bush ndio Mkuu wa Mashushushu. Haya vilevile yalienda sambamba na mkakati wa kueneza Ukatoliki East Africa kama nilivyoelezea hapo awali. Sasa haya ya kutafuta legitimacy ya source ya mapinduzi yale nje ya mkakati ule mama wa Wamarekani na Wakatoliki kumtumia Nyerere na viongozi wengine wa East Africa kufanikisha hayo ni porojo ambazo huwezi kumlisha mtu mwenye akili zake timamu.
 

Ahali yangu naona umesahau Boko boko na mikate ya chila hapo ili lilete nakshi zaidi katika mnakasha huu.

Kweli jamvi hili ni tamu. nazidi kupata darsa kwa kila nyanja.

Ahsanteni wote
 
Kuambiwa usome ujifunze ndiyo dhihaka?

Wewe mbona unatufanyia dhihaka nyingi unatuita wafuta viatu wa Mohamed Said, wafia dini, akili za madrassa, Mapunguani, sisi mbona tupo kimya.

Wewe unatakiwa ujifunze.


Kabisa Kabisa,
Hivi hiko kitabu chake kweli kitauzika??
Anatia huruma sana...
 

Kadogoo,
Ahsante sana.

Mzee Nasib Siwa.
Wanae ni umri wangu.

Nikifika Moshi lazima nifike pale kwao kwenye barza.
 

Mzee MS; Salaam na heshima tele. Hizi za Ally Sykes na "his story" ni habari njema na zakupewa hongera. Binafsi nilishasema huko awali kuwa tuna tatizo kubwa sana la viongozi wetu wengi (na hata sisi wa kawaida) kuishi kwenye taasisi hadi kufikia mahali wakaondoka ama kwa kufa au kustaafu bila hata kujaribu kuandika "memoirs" zao. Sehemu nyingi sana duniani watu wanayafanya haya. Hii inakuwa ni historia ya kudumu kwao na pia wanazisaidia sana taasisi husika. Nimeona mnakasha umeshafika mpaka Marekani, vita zake na kina Powell. Lakini Powell aliandika memoirs zake. Leo hizo memoirs ndizo zinachangia sana kumsafisha na wimbi la lawama la wakati ule wa Bush. Kwa hiyo kama Ally kaandika pia kitabu (nitapenda kukisoma) ni faraja sana. Vivyo hivyo familia za akina Kawawa, Oscar Kambona, Bhoke Munanka, Rupia na wengineo ni juu yao kujitahidi kuandika wanayoyajua kama wao. Ma-shelfu bado yapo tupu. Kukosekana memoirs zako, always huzaa lawama za "kusahauliwa". Angalia hata nchi za karibu na kwetu viongozi (kina Museveni) wana historia ya kumbukumbu zao.

Nadhani sasa na haya ma-computer, it is even easier. Kawaida Hatakuja mwana-historia yeyote akayajua maisha yako na sababu za matendo yako kama wewe mwenyewe. Ni muhimu kutumia pumzi zako ukayaeleza ya muhimu kuliko aje mwingine kukusaidia. Yaani kama kweli atakusaidia.

Nadhani Ally ni wa kupongezwa. Natamani kama majenerali wetu hawa wangetuandikia maisha yao wakiwa katika harakati za Uganda, Msumbiji, Zimbabwe na kwingine. Hii inarudi pale pale kuwa sisi Watanzania tuna vitabu vichache sana duniani.
 
Ahali yangu naona umesahau Boko boko na mikate ya chila hapo ili lilete nakshi zaidi katika mnakasha huu.

Kweli jamvi hili ni tamu. nazidi kupata darsa kwa kila nyanja.

Ahsanteni wote


Barubaru,
Umejiponza.

Ukija In Sha Allah nitakuchukua kwa Muchacho Upanga
ukaonje mishkaki yake.

Sikujua kama wewe ni mshabiki wa mambo haya.
 

Wickama,
Nimekaa miaka mingi sana na Bwana Ally na katika kipindi hicho kila
nilipokuwa na nafasi nilikuwa ''nikimchokoza'' anieleze maisha yake na
mimi nikawa nachukua ''notes.''

Ana mengi kaniachia.
 

The Big Show,

Usizungumzie kuuzwa kwa kitabu kwa kuwa hakuna publisher
atakaegusa mauzauza hayo.

Kwa ajili hiyo basi hapatakuwa na kitabu wala kigazeti.


Inasikitisha sana kwa kweli,
Kwa maana anaonesha kweli yuko serious na anamaanisha kweli ana nia hiyo,
Tutajionea mengi sana kwenye uzi huu,
Yetu macho...
 

Zali; Nakushukuru kwa majibu yako. Unayoyasema kuhusu kina Bush na Ukatoliki pia yanawezekana. Ila Bush sio Mkatoliki na Marekani sio a catholic country. Kwa CIA, nia ya kuiunganisha tanganyika na Zanzibar ilikuwa inainufaisha Marekani kuizuia Umma party (ikichukuliwa kama a communist party)isiwe na influence. Hata huyo mwandishi anapomhoji Babu anahoji jinsi gani Wakomunisti walimsadia. Hamu ya kuwakomoa wakomunisti wa zenj toka Marekani ilijitokeza pia walipopata fursa ya kumpigia Dr Salim kura ya veto asipate ukatibu mkuu wa UN, kwa kule yeye kuwa "rafiki" na China, japo bado ndio walikuwa wanawakomoa makomredi. Kwa hiyo hauko mbali na ukweli ukisema Marekani walitaka Zanzibar ithibitiwe. Kuwasilimisha Wazenj wote SIJUI. Sijalisoma.

Nachosema, ni kuwa angalia hizo silaha za hao askari wa Okello kwenye hiyo video, hizi sio bunduki za watu kuomba toka nchi nyingine kama Algeria. Na kama bunduki ni 850 kama video ya pili (hiyo ya rangi) inavyosema kuwa walipewa na Nyerere, haiwezekani Meli toka Algeria ilete bunduki 850 tena hizo nazoziona hapo.

Mi nadhani hii dhana ya kuwa kulikuwa na mapinduzi mengine yanasubiriwa (ya Afro-shiraz) na yangefanyika wiki moja kabla ya haya kina okello kama anavyo-eleza huyu mwandishi kwenye video ya kwanza huenda yakawa na ukweli. Aina hiyo ya mapinduzi ndio yangetumia silaha nzuri toka bara sio za kupora kituo cha polisi na magereza (sio hizi nazoona)na yangekuwa na kuratibiwa. Kwenye Kitabu cha Dr Ghassany sikumbuki kumsoma Okello akiwa Kipumbwi-Pangani kwenye mazoezi Iwe itakavyokuwa lakini ni dhahiri kuwa mshikamano kama jamii katika jumuiya hii ulishayumba hadi matatizo haya yanakuja.
 
hivi kwa mfano hayo anayoyadai huyo ndugu zidi ya uislamu wakipewa yatawatoa hapo walipo?
 
Mohamed Said,

Huo "Mpini" wa Ally Sykes uliouweka ni hatari Ally Sykes kaongea maneno mazito sana tatizo unatoa kiduchu.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…