Zali na wengineo; Nawasalimuni. Leo nilipata nafasi kiduchu ya kuchungulia masuala ya JF. Haswa ilikuwa nafuatilia ile hoja yako ya Nyerere na Zanzibar. Nimepata hii mikanda pengine inaweza kusaidia kueleza kile nilichosema awali kuwa yaelekea kule visiwani walishachukiana kwa ukabila wao na sio udini wao. Ukiangalia huu mkanda wa kwanza utaona wazi kuwa kulikuwa na mapinduzi kama matatu yanasubiriwa (ndivyo mwandishi anavyosema; ya Afro-shirazi ambayo yangesaidiwa na kina Nyerere, ya Okello, na lingine hakutaja). Anaongeza kuwa Okello walipindua kama wiki moja kabla ya yale ya Afro-shiraz. Hii inajieleza kuwa ilibidi okelo kuvamia makao ya polisi na kupata bunduki walizoulia watu. Hii ni tofauti na silaha tunazosoma kuwa ziliombwa Algeria. Angalia hao askari mtaani aina ya silaha wanazo tembea nazo ni rifle kama zile za magereza wakati ule.
‫
Haya mapinduzi ya silaha za kupora hayawezi kuwa yale tena ya silaha za kutoka Algeria. Msikize Okello na Mungu wa Waafrika (huu ni Urangi). Sijui mchango wa viongozi wa Tanganyika katika mapinduzi haya kama unamsikiliza mwandishi wa habari vizuri.
Huu mkanda mwingine nao unaonyesha matukio hayo. Ila upo versions tofauti tofauti kwenye you-tube;
https://www.youtube.com/watch?v=fJmK_FL91vM
Lakini angalia hata mwandishi yupo kwenye dimbwi lile lile la ukabila. Ni barbaric Africans against arabs and MUSLIMS, yaani kama vile hao arabs sio moslems. Hapa kawapa waarabu daraja lao stahiki. Binafsi nina mashaka kiasi na huu wa pili kwa vile versions zake zote una rangi nzuri. Sina uhakika kama 1964 tayari color-videography ilikuwapo kiurahisi namna hiyo. Angalia hata shirika la habari liliwahoji kina Babu, Okelo, na Karume hawakuwa na color-videography (ule mkanda wa kwanza). Huu wa pili umechukuliwa na helikopta na ndege sindikizaji. Pia ukiivuta sana picha kwenye kaburi moja la jumla utagundua walioko ndani yake (yaani maiti) wengi wana balaghashia zao intact!!!! kiasi kuwa nasita kusema ni mkanda wa tukio halisia. Hata hivyo hilo sio la maana. La msingi ni kuwa mapinduzi haya yalichochewa na hisia za URANGI na tabaka. Dini iliwekwa kando. Hii chuki utaikuta pia kwenye kitabu cha Kwaheri uhuru......Ukisoma maelezo ya Mzee Mkwawa. Kwa hiyo kama Nyerere na viongozi wenzake wa Tanganyika walihusika ni katika hayo mapigano ya matabaka na Urangi kama walivyohusika Msumbiji, Namibia, Zimbabwe, South Africa na Sahara Magharibi (POLISARIO).
Shukran kwa majibu yako ya awali ambayo niseme ukweli hayakuwa na shari kama tulikotoka. Yale yote uliyosema ni mawazo yako binafsi hakuna tija ya kuulizana zaidi.
Salaam kwa Nguruvi, Ritz, Gombesugu, Mzee MS, Nanren, Son of Alaska, Nyambala, Mwanakiji, Kadogoo, Boko Haram.