Mzee Mohamed Said anayo meeengi ya kumfundisha huyo kijana pamoja na wengine wengi humu jamvini na nje ya jamvi. Lakini tunakosa uhondo huo kwa kuwa "Wanafunzi" wanafanya fujo darasani, hawampi mwalimu fursa ya kufundisha. Ukiwadadisi kwa nini wanafanya fujo? Wengi wao itakuwa wanataka Darsa lifundishe wanavyotaka wao kama walivyozoea kusikia na si vinginevyo.Kwa hiyo umekiri alichokisema Mohamed Said kule Ibadan kuwa balozi wa Marekani ndiyo aliwahotubia wabunge wa Tanzania wakapitisha sheria ya ugaidi.
Halafu Mohamed Said anavyokuambia pinda mgongo usome siyo dhihaka kiwango chako cha elimu bado.
Mohamed Said anakufundisha mengi sana.
Zali; Nakushukuru kwa majibu yako. Unayoyasema kuhusu kina Bush na Ukatoliki pia yanawezekana. Ila Bush sio Mkatoliki na Marekani sio a catholic country. Kwa CIA, nia ya kuiunganisha tanganyika na Zanzibar ilikuwa inainufaisha Marekani kuizuia Umma party (ikichukuliwa kama a communist party)isiwe na influence. Hata huyo mwandishi anapomhoji Babu anahoji jinsi gani Wakomunisti walimsadia. Hamu ya kuwakomoa wakomunisti wa zenj toka Marekani ilijitokeza pia walipopata fursa ya kumpigia Dr Salim kura ya veto asipate ukatibu mkuu wa UN, kwa kule yeye kuwa "rafiki" na China, japo bado ndio walikuwa wanawakomoa makomredi. Kwa hiyo hauko mbali na ukweli ukisema Marekani walitaka Zanzibar ithibitiwe. Kuwasilimisha Wazenj wote SIJUI. Sijalisoma.
Nachosema, ni kuwa angalia hizo silaha za hao askari wa Okello kwenye hiyo video, hizi sio bunduki za watu kuomba toka nchi nyingine kama Algeria. Na kama bunduki ni 850 kama video ya pili (hiyo ya rangi) inavyosema kuwa walipewa na Nyerere, haiwezekani Meli toka Algeria ilete bunduki 850 tena hizo nazoziona hapo.
Mi nadhani hii dhana ya kuwa kulikuwa na mapinduzi mengine yanasubiriwa (ya Afro-shiraz) na yangefanyika wiki moja kabla ya haya kina okello kama anavyo-eleza huyu mwandishi kwenye video ya kwanza huenda yakawa na ukweli. Aina hiyo ya mapinduzi ndio yangetumia silaha nzuri toka bara sio za kupora kituo cha polisi na magereza (sio hizi nazoona)na yangekuwa na kuratibiwa. Kwenye Kitabu cha Dr Ghassany sikumbuki kumsoma Okello akiwa Kipumbwi-Pangani kwenye mazoezi Iwe itakavyokuwa lakini ni dhahiri kuwa mshikamano kama jamii katika jumuiya hii ulishayumba hadi matatizo haya yanakuja.
Mzee Mohamed Said anayo meeengi ya kumfundisha huyo kijana pamoja na wengine wengi humu jamvini na nje ya jamvi. Lakini tunakosa uhondo huo kwa kuwa "Wanafunzi" wanafanya fujo darasani, hawampi mwalimu fursa ya kufundisha. Ukiwadadisi kwa nini wanafanya fujo? Wengi wao itakuwa wanataka Darsa lifundishe wanavyotaka wao kama walivyozoea kusikia na si vinginevyo.
Na wengine wana chuki binafsi tu. akisema fulani, hata Kama ni maneno ya kijinga, ni sawa, lakini fulani akisema...hawamuamini.
Hapo ndipo kwenye kasoro ingawa hawatathubutu kusema hivyo.
Wickama,
Nimekaa miaka mingi sana na Bwana Ally na katika kipindi hicho kila
nilipokuwa na nafasi nilikuwa ''nikimchokoza'' anieleze maisha yake na
mimi nikawa nachukua ''notes.''
Ana mengi kaniachia.
Zali la Mentali,
Me naona hili punching bag ungelipa nafasi kidogo lisije likapasuka na haya mapigo yako,
Lipumzishe na tuendelee na mengineyo,ukiamua kuendelea kulipiga piga mie sina neno,Ahalan wasa'lani...
Mohamed,Bila shaka rika lako ni Ali Nasibu, kwani nadhani ndie mkubwa ktk familia ya Mzee Nasibu, lakini Mzee Nasibu alikuwa na kaka ake akifanya kazi ofisi ya Tanu mkoani Kilimanjaro, alikuwa dereva wa miaka mingi ktk ofisi ya Tanu. Baadae Wazee wa Moshi hasa akina mama wakiongozwa na Marehemu Juma Ngoma, Mama Halima Selengia, Yusuf Ngozi na wengine walichangishana fedha nyumba hadi nyumba na kujenga ofisi kubwa na ya kisasa kwa ajili ya CCM! MS, amini usiamini ofisi hii sehemu kubwa ya fedha zimetolewa na akina Mama wa Kiswahili wauza vitumbua na mama ntilie!Baada ya kumtaja Mzee Nasibu siwa nimeamini kweli wewe mtoto wa Mjini! halafu kumbe watoto wa mjini mtandao wao si mdogo!Kadogoo,Ahsante sana.Mzee Nasib Siwa.Wanae ni umri wangu.Nikifika Moshi lazima nifike pale kwao kwenye barza.
Ni kweli kwamba suala la Marekani hasa lilikuwa ni Kuudhibiti Ukomunist. Lakini ajenda ya Bush ya Crusade dhidi ya Uaislamu inafahamika hivyo huwezi kutenganisha ajenda yake ya udini na ile ajenda mama ya kuudhibiti Ukomunist. Kama ni suala tu la kuudhibiti Ukomunist basi hata Muislamu wangeweza kumtumia kwani walishafanya hivyo sehemu nyingi tu including kumtumia Osama kule Afghanistan.
Wamarekani mpaka leo wameweka Plan B ya kuhakikisha kwamba Wazanzibari hawapati nchi yao kwa kutumia harakati zozote zile ziwe za kisiasa au vinginevyo. Dola la Urusi limeshaporomoka mda sasa. Kwa nini Plan B bado ipo na inafanya kazi mpaka leo kama sio suala la kuudhibiti Uislam?
Kama utataka mawazo na msimamo wangu kama mimi, kesho wakina Waryoba wakiweka kipengele cha kupiga kura kuhusu fate ya muungano uwe na uhakika nitawatema wa-zenj. Hii sio kwa sababu ya dini hapana. Ila kama wao wanaamini ndio njia iliyobaki ya kuwaletea masikizano na maendeleo, why NOT? Mashindano ya dini kuu mbili duniani (ukiristo na uislamu) yamepitia historia nyingi na ngumu na humu sio mahala pake. Unaweza ukaanza na kufika kwa wareno na wao walikaa 200 years mwambao huu wa afrika mashariki hadi zanzibar kuokolewa na wa-oman. Haya ya Plan B unayosema ni ya zama hizi za leo. Siasa hazina adui wa kudumu. Ni maslahi. Subiri utaona, Zipo dalili kuwa huenda mwambao wa zenj ukawa na mafuta, sasa kwa kuanzia zipo kelele tele 'jamani hatutaki mafuta kuwa suala la muungano'. Yaani kama vile huku tanganyika ni marufuku kupata mafuta. Sasa subiri uone kama wakuu hao unaowasema wataongelea Plan B zenj wakipata oil au wataongelea kupata mafuta kwenye jamhuri huru ya zenj. Refer case ya Savimbi na Angola. Walim-support for so many years, lakini ilipokuwa wazi kuwa sasa wanaweza kupata mafuta ya kule Cabinda and other parts? You will know how the war ended. Mimi navyoona (hapa na mimi ni mawazo yangu pia) Marekani (of course na nchi nyingi) hata vita zao ni masuala ya resources. Ingekuwa ni dini tuu basi leo Japan baada ya kumeza yale mabomu ya atomic, au Iraq, au Vietnam wote wangekuwa Protestant-Christians.
Hao kina Bush ndio kwanza wanahusishwa sana Freemasonry, Atheism, Bone and Skull society etc. Mwisho wa siku inakuwa kila mtu achague pa kupita. Nashukuru kwa majibu yako yana fikra nzuri.
Mzee Mwanakijiji,
Wapi mie nimekuambia Mohamed Said ndiyo wa kwanza kumtaja Sheikh Suleiman Takadir.
Nimecheka sana na maneno yako mpaka mtoto wangu kashangaa, wewe ulivyokuwa nyuma kufahamu historia ya Tanganyika unadhani wote kama wewe kwa taarifa yako vitabu vya histori ya Tanganyika nimevikuta nyumbani mzee wangu alikuanavyo ngoja nikutajie.
1. Macpherson Fergus, Kenneth Kaunda of Zambia.
2. Pratt Cranford, The Critical in Tanzania.
3. Hatch John, Two African Statesmen.
4. John Iliffe, A Modern history of Tanganyika.
5. Listowel Judith, The Making of Tanganyika.
Niambie wapi Listowel kamtaja Sheikh Takadir ndie mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Wazee wa TANU ambalo lilikuwa na wajumbe 170. Kama siyo Mohamed Said.
Wewe leo ndiyo umenunua vitabu AMAZON kuwasoma kina Listowel Judith, John Iliffe, haa haaa ha.
Vitabu vipo vingi bahati nzuri mzee wangu alikuwa anaeleza baadhi ya makosa ya vitabu vya Tanganyika.
Wewe unanichukulia poa unajidanganya ujiulizi kwa nini Ritz ameganda kwenye huu uzi muda mwingi kuna vitu najua vingi nimeadithiwa na Wazee wetu siyo kutoka kwa wazungu ambao nao wameadithiwa na wazee wetu, ambao wewe leo hii ndiyo unaanza kuwasoma na kutaka kuifahamisha mimi.
Endelea kusoma vitabu vyako.
Mohamed,Bila shaka rika lako ni Ali Nasibu, kwani nadhani ndie mkubwa ktk familia ya Mzee Nasibu, lakini Mzee Nasibu alikuwa na kaka ake akifanya kazi ofisi ya Tanu mkoani Kilimanjaro, alikuwa dereva wa miaka mingi ktk ofisi ya Tanu. Baadae Wazee wa Moshi hasa akina mama wakiongozwa na Marehemu Juma Ngoma, Mama Halima Selengia, Yusuf Ngozi na wengine walichangishana fedha nyumba hadi nyumba na kujenga ofisi kubwa na ya kisasa kwa ajili ya CCM! MS, amini usiamini ofisi hii sehemu kubwa ya fedha zimetolewa na akina Mama wa Kiswahili wauza vitumbua na mama ntilie!Baada ya kumtaja Mzee Nasibu siwa nimeamini kweli wewe mtoto wa Mjini! halafu kumbe watoto wa mjini mtandao wao si mdogo!
Ritz,
Judith Listowell amemtaja Takadir kama mwenyekiti wa kwanza wa baraza la wazee wa TANU.
Shukran Mzee MS; Leo unaongelea "kakuachia mengi". Binafsi ningependelea sana mtu aandike his own story kama ile ya Museveni "Sowing the Mustard Seed" (hopefully nimeitamka sawa) au vitabu vya Obama nk. Kina POwell, Clinton. Au hata vitabu vya fani husika basi, Lakini nenda kwenye vyuo vyetu, takriban vitabu vyote wanafunzi wanavyopewa kama references huwa waandishi ni wa nje. Nimesoma SUA, kitabu kimoja cha fani kama ya Veterinary, kwa sasa usishangae kuambiwa lipa 150,000, sijui fani zingine, ilimradi tuu mlango huu upo wazi na ni mara chache kukuta ma-professa wazawa wanaandika vitabu kulijaza soko hili. Sasa tabia hii ndio unaikuta karibu maafisa wote waandamizi wanastaafu bila hata kuandika memoirs zao (labda tatizo ni soko, au publishers hawataki sijui). Ni tatizo ambalo kila anayejaribu kulivuka sharti apewe nguvu na pongezi.
Judith Listowell, kamtaja Sheikh Takadir "Makarios" kijuu juu tu.
Mohamed Said ndiyo kaenda mbali zaidi kumuelezea Sheikh Takadir.
Vipi ameeleza ugomvi wake na Nyerere jinsi ulivyokuwa.
Ritz,
Katika historia ya TANU kuna mambo TANU yenyewe ilikuwa wanayaogopa
na hili limekuja kurithiwa na CCM.
Sheikh Suleiman Takadir anaogopwa kama vile anavyoogopwa Abdu Sykes.
TANU haikuipenda kueleza michango ya wazalendo hao.
Abdul Sykes anaogopwa na TANU?
Asingetajwa katika kitabu cha TANU cha Kivukoni
Wickama,
Kitabu cha Ally Sykes kipo.
Yeye hakushika kalamu kwa maana yake halisi lakini MS alikuwapo...na tape
yake na note book yake...
Nimejifunza kitu kimoja hawa ''celebrities'' ukitaka wafunguke wachukue kama
vile mko jamvini mnazungumza hapo utashangaa na hakika utastaajabu.
Lakini kwenye ''formal interview'' hupati kitu kizuri.
Miaka michache ilopita nilikuwa naandika maisha ya Sal Davis (Shariff Salim
Abdallah) kijana wa Kimombasa aliepiga muziki Ulaya katika 1960s.
''One on one'' hupati kitu lakini mkute barazani kisha mchokoze...
Utashangaa.
Wanajamvi hebu someni wenyewe haya siyo matusi.
gombesugu, THE BIG SHOW, Mohamed Said, Boko haram Kadogoo, Invisible, Buchanan, Yericko Nyerere,
Mkuu Wickama:
Nadharia nzima ya mapinduzi ya Zanzibar inabebwa na Okello,
Japokuwa inaelezwa kuwa Okello aliwazidi kete wahafidhina wa ASP ambao inaelezwa kuwa walishapanga kufanya mapinduzi wiki moja mbele ya yale ya Okello,
Mkanganyiko kwangu unakuja kutuama kwa Mzee Karume,
Je Karume alikuwa kwenye jeshi la Okello ama alikuwa kwenye kundi la mapinduzi la ya ASP ambayo yalipangwa kufanyika wiki moja mbele ya Okello?
Hebu tupeane elimu hapa mkuu!